Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » WEMA NDANI BIFU NA BONGO MOVIE....WANATAKA KUMPOTEZA KWENYE TASNIA YA FILAMU

WEMA NDANI BIFU NA BONGO MOVIE....WANATAKA KUMPOTEZA KWENYE TASNIA YA FILAMU

HIVI sasa kuna vita inayofukuta chini kwa chini kati ya watayarishaji wakubwa kutoka kundi kubwa la Bongo Movie linaloitwa Big Five, vita hiyo ambayo watafiti wa mambo bado hawajaelewa sababu inayoleta uhasama kati ya watayarishaji hao na mwanadada huyo mwenye makeke mjini, kundi hilo limepanga kumpoteza kabisa Wema katika tasnia ya filamu.
.Moja ya sababu kubwa ambayo imezua ugomvi huo ambao pengine hawataki kabisa ujulikane ni sababu ya Wema kufungua kampuni yake ya uzalishaji wa filamu ya Endless fame film ambayo pengine imeonekana kuja kisasa zaidi na kuweza kutoa ajira hata kabla ya kuwa na kazi nyingi za kufanya za filamu.
Moja ya chanzo chetu cha habari nimeitaarifu FC kuwa takribani mwezi kumekuwa na vikao kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Wema anapotea katika utayarishaji wa filamu na kumtaka afanye kazi nyingine tofauti na filamu kwani ni kikwazo kwao, hivi karibuni mmoja ya watayarishaji wakubwa ambaye hataki jina lake litajwe alinena kwa kwa kusema.
Wema Sepetu akiwa na Richie katika ofisi yake.
“Pengine watu wanaweza kutafsiri vibaya si Wema pekee yake tu ambaye amekuwa ni tatizo kubwa katika tasnia ya filamu, hawa dada zetu bwana wanatuangusha sana kwani wao wakiandaa filamu zao hawatumii pesa za mitaji yao, wanawezeshwa na jamaa zao, lakini wakifika sokoni kwa sababu hawana uchungu nazo wanauza bei ya kutupa,”anadai mdau huyo.
Awali ilikuwa ni kama utani ambao kila aliyesikia hakujua kama inaweza kufikia hapo ilipo sasa, Wema mwenyewe haoni kama ni tatizo kuwa na kampuni ya Production na kuzalisha kazi zake, lakini mwenyewe anaona ni moja kati ya kuongeza ajira wala haoni kama ni mshindani.
Mwenyewe anahisi pengine kuwa na msimamo inaweza ikawa ni njia mojawapo ya kumjengea maadui, kwani mara nyingi watayarishaji wengi wanawapangia waigizaji fedha ya kuwalipa na si waigizaji kujenga thamani yao kama ambavyo yeye anafanya, kutaja malipo kulingana na hadhi yake..

JB akiwa na Wema Sepetu
Inasemekana kuwa mtayarishaji ambaye anataka kufanya kazi na Wema lazima amlipe milioni kumi ikiwa sambamba na kampuni yake kurekodi kazi sababu kubwa ikiwa ni hana imani na kampuni zingine kuhusu ubora wa uzalishaji wa filamu katika kulinda kazi yake ni bora kutumia vijana wake.
Tutakujulisha kila hatua ya sakata hilo linaloweza kudumaza tasnia kama si kuvuruga, lakini pia ni wakati wa shirikisho la filamu kuweka vigezo vya uuzaji wa filamu kulingana na ubora uliopo.
    
CHANZO : FILAMU CENTRAL                                                  
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa