Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label skendo mastaa. Show all posts
Showing posts with label skendo mastaa. Show all posts

HUU NDIO MSIKITI ANAO UJENGA MZEE MAJUTO NYUMBANI KWAKE....ANGALIA PICHA HAPA

Ni kitu kizuri kuona binadamu yeyote anapojisogeza karibu zaidi na Mungu, mwigizaji/mchekeshaji staa wa Tanzania ambae kwa sas


Katika kijiji kipya atakachohamia siku kadhaa zijazo huko Tanga, Mzee huyu ameamua kujenga msikiti mdogo mpya wa matofali ya cement ambao atautumia kuswali pamoja na watu wengine ambapo mwanzoni alikua amejenga huo wa udongo hapo juu lakini akabadili mawazo hata kabla ya kuanza kuutumia, sasa anajenga wa kisasa zaidi.
 

DOGO JANJA AFUKUZWA RASMI MTANASHATI ENTERTINMENT...TABIA MBAYA NDIO CHANZO

Msanii mdogo aliyewahi kutamba katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefukuzwa rasmi Mtanashati Entertinment, Taarifa zilizofikia dawati letu la habari zinasema Dogo Janja amefukuzwa na Ostazi Juma Na Musoma baada ya kushindwana kitabia, Hapo awali Dogo Janja aliwahi kuwa mwanakundi la Tip Top Connection lililo chini ya uongozi wa Madee hata hivyo alifukuzwa na kurudi kwao Arusha ambapo Ustazi Juma Na Musoma alimfuata na na kumuweka kundini huku akimuhudumia katika kila jambo ambalo alitakiwa kupata kama
mtoto na mwanamuziki pia. Lakini Leo imefika tamati ya Ostazi Juma na kuamua kumuacha Dogo Janja aende zake.



Vile vile kutoka katika kundi hilo la Mtanashati Kuna nyimbo mpya ya msanii PNC inayokuja hivi karibuni, ni Bonge moja la track linakwenda kwa jina la HABARI YA MJINI, nyimbo hii itayoachiwa hvi karibuni itakuja pamoja na video kali. Jiandae kwa nyimbo kali kutoka kwa PNC


KWELI BONGO FLEVA INALIPA TENA SANA, HEBU CHEKI PICHA ZA GARI MPYA ALIYONUNUA OMMY DIMPOZ


107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
106
105
104
103
2
1


DIAMOND AAMBO WASHABIKI WAKE WAPIGE PICHA WAKIWA KATIKA POZI KAMA ZAKE...CHEKI PICHA ZA MASHABIKI 11 WAKIWA KATIKA POZI KAMA ZA DIAMOND


 Kama unafatilia habari za mastaa wa Marekani utafahamu kuwa hii issue alishawahi kufanya rapper Nicki Minaj wa Young Money, Aliomba mashabiki watume picha wakiwa wamevalia mavazi kama yake na pozi zaki Nicki Minaj, Well Bongo Super Star Diamond amefanya yake kwenye instagram.
Picha zaidi ziko hapa.











VIDEO YA KIPINDI CHA WEMA SEPETU EPISODE 1 KINACHORUSHWA EATV...KAMA HUJAKIONA ANGALIA HAPA

 
Kama ulikua hujaangalia kipindi cha wema sepetu kinachorushwa EATV ..Basi ambatana nae hapa katika kipindi chake Katika Episode 1,Akielezea undani wa maisha yake juu ya yeye kurogwa,Maisha yake ya Mapenzi na mengineyo mengi..
ANGALIA HAPO CHINI...

ANGALIA VIDEO YA LULU AKIELEZEA MAISHA YA JELA NA IDADI YA WANAUME WALIOMTONGOZA MPAKA SASA NA MENGINEYO




HUYU NDIYE WINTA WA JUMBA LA DHAHABU ALIYENUSURIKA KUUWAWA KWA RISASI

 LICHA ya kipaji cha kuzaliwa alichoanza kukionyesha tangu akiwa kinda wakati akisoma Shule ya Msingi Mgulani, msanii Angel John Komba 'Winta' anakiri kuwapenda na kuvutiwa kupita kiasi na Genevieve Nnaji wa Nigeria na Yvonne Cherly 'Monalisa' kulichangia kuingia kwake katika fani ya uigizaji.
Winta, mmoja wa waigizaji wa kike mahiri nchini aliyetamba na kazi mbalimbali kama tamthilia na filamu anasema nyota hao walikuwa wakimkosha kila alipoziona kazi zao na kuapa kuwa ni lazima na yeye aje kuwa staa kama wao.

"Nnaji na Monalisa ndiyo walinipa mzuka wa kujibidiisha katika sanaa ya uigizaji kwani walinikosha na mpaka sasa navutiwa nao," anasema.
Anasema kabla ya kuvutiwa na umahiri wa wanadada hao alikuwa amejikita kwenye sanaa ya kupiga na kucheza ngoma enzi akiwa darasa la sita na kuendelea hata alipojiunga na Sakhafa Sekondari ambapo tayari alishaanza kuigiza.
Hata hivyo anasema kujitosa kwake rasmi katika uigizaji, ilikuwa mwaka 2001 alipokutana na Jumanne Kihangale 'Mr Chuz' anayemtaja kama mmoja wa watu asiyoweza kuwasahau kwa alivyomsaidia kufika mahali alipo sasa na kuwa miongoni mwa waasisi wa kundi maarufu ya uigizaji la Fukuto Arts Professional.
"Kiukweli nilitumbukia rasmi kwenye uigizaji mwaka 2001 nikiwa miongoni mwa waasisi wa kundi la Fukuto na kazi ya kwanza kuicheza ilikuwa ni igizo lililokimbiza nchini la Jumba la Dhahabu na mingine iliyokuja baadaye kabla ya kuhamia kwenye filamu kwa kucheza kazi mbalimbali zilizonipaisha ndani na nje ya nchi," anasema.
Mrembo huyo anayeishabiki Simba na mabingwa watetezi wa England klabu ya  Manchester United, anasema tangu ameingia kwenye fani hiyo anashukuru amepata mafanikio mengi ya kujivunia baadhi hapendi yaanikwe gazetini.
Winta anadai mbali na manufaa ya kiuchumi, sanaa imemfanya afahamiane na watu wengi na kupata rafiki na kutembea sehemu mbalimbali.
"Nashukuru sanaa imenisaidia kwa mambo mengi ya kujivunia, japo sijaridhika kwa vile ndoto zangu ni kuja kumiliki kampuni binafsi itakayozalisha na kusambaza kazi zangu na za wasanii wenzangu," anasema.

MKASA
Kisura huyo anayependa kula ugali kwa mlenda na dagaa mchele wa kukaangwa, anasema sanaa ya Tanzania imezidi kupiga hatua kubwa kulinganisha na siku za nyuma japo anadai wizi na unyonyaji unawafanya wasanii washindwe kunufaika.
Anasema, lazima serikali na mamlaka zinazosimamia fani hiyo kutoa makucha yake ili kuwabana wanyonyaji na wezi wa kazi za wasanii ili kuinua maisha ya wasanii tofauti na sasa wengi wao wakiishi maskini tofauti na jasho lao.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJdCcnivEBcqU6BF4zu8ZgFoqzKfutW-kKi-asqor7dX3Rsa5y-_Ub6D1SrSzarGwdp1Q7njlOrjSeOzvKSm6lNql4iUstyixqC6Cq5EwwODd4JZ8fnTLPGnzaDWcP3efufYusZZ94BfE/s400/winterwebMsanii Winta katika pozi

 Pia anataka watengeneze miundo mbinu itakayowasaidia chipukizi kuendeleza vipaji vyao ili kusaidia kuondoa tatizo la ajira sambamba na serikali kuvuna pato kupitia fani hiyo.
Juu ya tukio la furaha, Winta anasema ni siku alipojaliwa kujifungua mtoto wa kiume aliyenaye, huku akidai hawezi kuusahau mkasa uliowahi kumkuta hivi karibuni alipokuwa na rafikize 'wakila bata' na kubadilishana mawazo baa.
Anasema akiwa na wenzake hawana hili wala lile, ghafla Pub waliyokuwepo (jina limehifadhiwa) ilivamiwa na majambazi ambao waliwamrisha wateja wote kulala na yeye kwa ubishi alikurupuka ili kukimbia na kufyatuliwa risasi iliyomkosakosa sentimita chache na kwa kiwewe alijikuta akitumbukia kwenye mtaro wa maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi.
Winta anasema kila anapolikumbuka tukio hilo la kusalimika kufa kwa risasi na jinsi alivyokoga uchafu huo hukosa raha.
"Siwezi kulisahau tukio hilo kwa jinsi nilivyonusurika kifo cha risasi na kutumbukia kwenye mtaro wa kinyesi, yaani ilikuwa balaa. Ila nashukuru  Mungu aliinusuru roho yangu," anasema.
Winta ambaye hajaolewa japo ana mtoto mmoja, anasema hakuna msanii wa kiume anayemkuna nchini kama mkongwe Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto.
"Huyu mzee noma, hana mpinzani na anajua kitu anachokifanya katika fani," anasema mwanadada huyo anayejikubali mwenyewe kwa uwezo alionao.

ALIPOTOKAAngel John Komba 'Winta' alizaliwa mwaka 1982 katika hospitali ya Temeke, Dar es Salaam kabla ya kuanza Shule ya Msingi Mgulani kabla ya kujiunga na Sakhafa Sekondari ambapo tayari alishaanza kujishughulisha na sanaa akicheza, kupiga ngoma na kuigiza.
Winta anayependa kunywa Fanta Passion na Castle Light, baada ya kumaliza shule alitumbukia rasmi kwenye sanaa hiyo akianzia kundi la Fukuto Arts Professional na kutamba nalo na tamthilia kadhaa kabla ya kuangukia kwenye filamu.
Baadhi ya filamu alizoigiza mwanadada huyo anayependa kutumia muda wa ziada kuangalia 'muvi' kuchati na kusoma vitabu na magazeti ni pamoja na 'Shock' aliyoigiza na marehemu Steven Kanumba, 'I Hate My Birthday', 'Pigo la Yatima', 'Kovu la Laana' na nyingine.

Winta akiwa na marehemu Kanumba walipokuwa wakiigiza filamu ya The Shock
Winta anayewataka wasanii wenzake kutegemea vipaji walivyonavyo na kuvitumikia kwa ufanisi badala ya kujihusisha na skendo au vitendo vya ushirikiana.
"Hakuna siri kwa sasa wasanii wanaendekeza sana mambo ya kishirikiana kwa kushinda kupishana kwa waganga ili kuroga na kutembelea nyota za wenzao, ila ukweli mtu anayejiamini na kutegemea kipaji hawezi kufanya upuuzi huo ambao hausaidii zaidi ya kujidhalilisha," anasema.
Mwanadada huyo anayemshukuru mno Mr Chuz na watu wengine waliomsaidia kwa namna moja au nyingine kufika alipo, anaiomba jamii iwachukulie wasanii kama watu wengine na pale wanapokosea wasiwahukumu wote au kuwaona watu wa ajabu kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika.
"Pia watuunge mkono kwa kununua kazi zetu sambamba na kutusaidia kupambana na maharamia kwa kuacha kununua kazi feki badala yake wazinunue kazi halisi ili tuweze kuendelea kuwapa burudani," anasema.

WARIDI ALIA NA MAADILI KATIKA FILIMU ZA KIBONGO..

Muigizaji wa siku nyingi Anna Costantine maarufu kama Waridi ambaye alitamba sana mwishoni mwa miaka ya tisini amesema kuwa maadili ya kitanzania na kiafrika yameshuka sana katika filamu zetu mpaka ni aibu kutokana na kuiga sana uzungu ambao hata wazungu wenyewe hawafanyi hasa kwa waigizaji wa kike. Akizungumza na Mwananchi Waridi alisema "maadili yameshuka, hatuendani na maadili ya mwafrika, wanaiga sana umagharibi, tunaiga mpaka inakuwa aibu, hata wazungu hawafanyi hivyo"
Waridi ambaye alitamba enzi hizo na kina Monalisa, JB, Bishanga na Aisha alipoulizwa kuwa anategemea kurudi lini katika filamu alisema "mwanzoni mwa mwaka ujao nitarejea, nimejipanga vilivyo, ni lazima nifanye vizuri, nina kipaji, nimesomea kazi hii(chuo cha sanaa Bagamoyo), pia nina karama ya uigizaji, nitarudi kwa kasi, nitatingisha kama awali"

HUYU NDIYE BABA YQKE MADEE AMBAYE NI DEREVA TAXI...MFAHAMU ZAIDI HAPA

 
Baba mzazi wa Madee Ally Selengia ambae ana zaidi ya 50 sasa hivi lakini bado anaonekana kijana na hata mambo yake mengine ni ya ujana ujana, anayo mpaka a.k.a ya ‘Mwakitoki hoi’ ambayo Madee amekua akisikika akimrusha kwenye nyimbo zake.

Ni mzazi ambae kazi yake kwa zaidi ya miaka 20 ni kuendesha Taxi jijini Dar es salaam kama unavyomuona kwenye picha akiwa na Taxi anayoimiliki, ni biashara ambayo ndio imemuwezesha kuwasomesha kina Madee na kuilea familia kwa miaka yote.
Anasema kwa miaka kadhaa hata mpaka sasa hivi, nyumbani kwake analea baadhi ya Wasanii ambao ni marafiki zake Madee, kwa sababu wanafanya muziki na Madee imebidi akubali hali halisi ya maisha ya mwanae ambapo toka miaka hiyo amewalea watu kama kina MB Dogg yani kama watoto wake, chakula kinapikwa pamoja wanakula na kulala kama familia.
Baba Madee anasema yeye ndio alikua mtu wa kwanza kumkataza Madee kufanya muziki miaka hiyo kwa sababu hakuona faida yake ila kwa sasa ameiona na mpaka amemruhusu mdogo wake Madee wa mwisho kufanya muziki pia mwingine kuwa producer wa video.
Ni shabiki mkubwa wa Madee na anasikiliza sana nyimbo zake na hata kutokea kwenye video, faida mojawapo aliyoiona kutokana na muziki wa Madee, ni nyumba aliyowajengea kama Wazazi na nyumba nyingine Madee aliyoijenga kwa ajili ya kuishi yeye.
Moja kati ya Matukio asiyoyasahau Baba Madee ni pale ugomvi wa Madee na Ney wa Mitego ulivyopamba moto zaidi ya miaka kumi iliyopita, kuna kipindi Ney wa Mitego alikwenda nyumbani kwa kina Madee na kuweka kambi karibu na nyumba yao na kuanza kuimba nyimbo za kumtukana Madee.
Tukio jingine analolikumbuka kuhusu Madee ni siku ambayo kundi la Ney wa Mitego lilikwenda nyumbani kwao huku likimkimbiza Madee spidi kwamba ni mwizi, Madee alipokimbilia nyumbani ndani ilibidi mama yake atoke kusawazisha na ndio ikawa siku ya mama yake kubaki na alama ya kudumu usoni baada ya mmoja kati ya waliokuwemo kwenye kundi la Ney wa Mitego kurusha chupa iliyompiga usoni.
Uhusiano kati ya Madee na Ney wa Mitego uko vizuri sasa hivi na wamekua marafiki na hata wakati mwingine Ney akitaka kutoa single ni lazima ammtumie Ney ili asikilize kwanza mfano ni wimbo wa ‘Salamu zao’ ambao unapata airtime kubwa kwenye radio sasa hivi.

-milardayo.

EXCLUSIVE:VIDEO YA JOKETI AKIFUNGUKA JUU YA MAHUSIANO YAKE YEYE NA DIAMOND NA HASHIMU THABITI



JOKATE AFICHUA MAZITO....MH!

KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.

Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.

DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;
Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.

PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?
Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.

‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.

KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?
Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.

DIAMOND ALIMTIBULIA
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.

ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?

Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.

Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.

HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?

Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…
Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...

Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?
Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.

SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.

Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?
Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.

ZAWADI
Ijumaa Wikienda: Kati ya Diamond na Hasheem nani zaidi kwa zawadi?
Jokate: Naona sasa unataka kumkasirisha Diamond!
Ijumaa Wikienda: Tangu ulipoachana na Diamond una zaidi ya mwaka. Je, huna mpenzi mwingine?

Jokate: Nipo singo au unanishauri nani ananifaa?
Ijumaa Wikienda: Siwezi kuingia kwenye moyo wako wakati umesisitiza kuwa unampenda Hasheem!
Jokate: Yap…nilimpenda na ninampenda sana.

MWANA-FA VIPI?
Ijumaa Wikienda: Mbali na Hasheem, Diamond na huyo jamaa wa zamani, vipi kuhusu habari za wewe kutoka na mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana-FA’?

Jokate: Afadhali mnisaidie kwa sababu sijui hicho kitu kilianzia wapi. Ni uzushi tu uliosambazwa na mtu mmoja.

-Gazeti la ijumaa wikienda via Gpl

SALAMU ZA LULU KWA WANA YANGA WOTE...BASI SAWA

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa