Showing posts with label diamond. Show all posts
Showing posts with label diamond. Show all posts
JE WAJUA KWA NINI DIAMOND NI TAJIRI NA MZEE GURUMO NI MASIKINI...?? SOMA HII MAKALA HAPA..
MWAKA 2005 nilikuwa nikipanda daladala na Naseeb Abdul (Diamond) katika kituo cha Shule Tandale Magharibi jijini Dar es Salaam. Wakati huo, sikuwa hata na wazo kwamba atakuja kuwa mtu maarufu katika muziki hata kushughulisha watu kutaka kujua zaidi kuhusu maisha yake.
Baada ya hapo nikaanza kuona wimbo wake wa kwanza kwenye video, ‘Nenda Kamwambie’ kilikuwa kibao kizuri kilichompa umaarufu, ndipo alipoanza kunivutia kusikiliza nyimbo zake. Baada ya video ile sikumuona tena kituoni kama ada yetu, nikaanza kusikia anaendesha gari aina ya Toyota Celica.
Kutoka mwaka 2006 mpaka sasa ni mfululizo wa mafanikio aliyoendelea kuyapata kijana huyu aliyezaliwa Septemba 28, 1988 mpaka kuwa mwanamuziki wa kwanza Tanzania kulipwa pesa nyingi kutokana na shughuli hiyo.
Kutokana na utafiti uliofanywa na tovuti inayozungumzia masuala ya vijana inasemekena ‘Diamond Platnamz’ anapata kiasi cha Sh Mil 16 kwa matamasha mawili anayofanya katika mwezi.
Mbali ya mikataba minono aliyoingia na makampuni mbalimbali yanayonufaika kwa taswira ama sauti ya mwanamuziki huyo kijana, Diamond anaingiza fedha nyingi kila anaposafiri nje ya Tanzania na bara la Afrika kufanya matamasha ya muziki.
Mbali ya mikataba minono aliyoingia na makampuni mbalimbali yanayonufaika kwa taswira ama sauti ya mwanamuziki huyo kijana, Diamond anaingiza fedha nyingi kila anaposafiri nje ya Tanzania na bara la Afrika kufanya matamasha ya muziki.
Wakati Diamond, ambaye hajatimiza hata miaka kumi kwenye tasnia ya muziki kuna mtu mmoja anaitwa Muhidini Gurumo, amejishughulisha na muziki kwa takriban miaka 45 lakini kila alipokutana na swali hili kutoka kwa wanahabari kuwa kwa kipindi chote hicho muziki umemsaidia nini, jibu lake ni: “Bado hakuna ninachoweza kujivunia kupitia muziki, hali ya maisha ni ngumu.”
Gurumo ambaye alizaliwa 1940 alianza muziki mwaka 1959 akiwa na bendi ya Kilimanjaro Chacha Band. Sasa ni takriban miaka 45, umri wa baba mwenye wajukuu lakini alichofanikiwa ni kujenga nyumba mbili na kupata shamba moja. Gari lenyewe alizawadiwa na Diamond mwaka huu baada ya kulalamika sana kwenye vyombo vya habari.
Nini Tatizo
Maalim Gurumo (Kamanda), analalamika kuwa wanamuziki wa kizazi kipya wanasifiwa sana na vyombo vya habari. Akisisitiza kuwa hawana ubunifu, nyimbo zao hazina athari katika jamii na hudumu chini ya mwaka mmoja zinapoteza taswira.
Lakini amesahau kuwa wanamuziki wa sasa wengi wamejiajiri, kipindi hicho bendi nyingi zilimilikiwa na kampuni, taasisi ama mtu ambaye anapenda sanaa hiyo ya muziki.
Lakini sasa wanamuziki wameamka, wanajimiliki wenyewe pesa wanazopata zinaingia mifukoni mwao.
Mathalan tangu Diamond aanze kuimba ameshaingia zaidi ya mikataba kumi tofauti ambayo ilimnufaisha yeye kama Diamond, matamasha yake yanamnufaisha yeye, kikundi anachomiliki anakilipa kiasi wanachokubaliana kutokana na uwezo wa mwanakikundi.
Mwaka jana, 2012, Diamond aliingia mkataba na kampuni ya I-View Studios wa kusimamia kazi zake zote kwa miaka miwili. Huu ni mkataba ambao umemjengea heshima kubwa sana. Ingawa kiasi cha malipo kilifanywa siri lakini inaonekana ni mkataba mnono.
Kampuni nyingine ya One Touch, ilifunga naye mkataba wa kuwa wasemaji wake. Yaani kila anachotaka kufanya ama kuzungumza kwenye jamii, ikiwa kuna kampuni inataka kufanya naye mazungumzo ya kibiashara, One Touch Company ndio watakaofanya kazi hiyo.
Hilo tu linamfanya Diamond awe na uwezo mkubwa wa kupata fedha kutokana na muziki. Mara nyingine msanii anashindwa kujua thamani yake, anaweza kutaja kiasi kidogo cha fedha katika ‘dili’ kubwa. Lakini kwa kupata mtu wa kukusimamia kwenye mazungumzo ya kifedha lazima uwe tajiri.
Aidha, bendi ambazo Maalim Gurumo amehama kutokana na sababu za kimaslahi hazipungui kumi, alianza na Kilimanjaro Chacha Band, Kilwa Jazz Band, NUTA Jazz Band, Mlimani Park, Safari Sound Ochestra, Rufiji Jazz, na nyingine nyingi kabla ya kumalizia muziki kwenye bendi kongwe ya Msondo Ngoma Music Band.
Kote huko alizunguka kwa kutumia kichwa kitupu kujadili thamani ya sauti yake, hakuwa na mshauri wa masuala ya muziki ambaye atamwambia kutokana na thamani yako usikubali kuhama bendi hii ili kuenda bendi nyingine bila kupewa kiasi fulani cha fedha.
Aliweza kuitwa baa akawa anakunywa bia na nyama choma huku anajadili mustakabali wa maisha yake na mkurugenzi wa bendi pinzani na anayofanyia kazi.
Katika mazungumzo yake na wanahabari Maalim Gurumo aliwahi kutamka kuwa anatamani siku zirudi nyuma ili anufaike na muziki wake. Lakini nakataa, hata awe vipi kutokana na mfumo anaoutumia hawezi kuwa tajiri kama Diamond.
Leo hii, Maalim Gurumo akiandaa tamasha na kuingiza Sh Mil 50, basi atakachoambulia ni asilimia 10 ya mapato ambayo ni Sh Mil 5, ambacho kitakuwa ni kiasi kikubwa kuwahi kukipata kwa tamasha moja tangu aanze kuimba.
Lakini siku hiyohiyo Diamond akialikwa katika tamasha hilo la Gurumo ataondoka na Sh Mil 8 taslimu bila kupungua senti. Bado tofauti ipo kubwa.
Aidha, mbali ya mapato ya stejini lakini Diamond ana mikataba minono na makampuni ya simu ambayo yanatumia nyimbo zake kama miito ya simu, ana mkataba mwingine mnono na kampuni ya Vodacom, ana mkataba na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola hata kufikia kujiita Coke Boy.
Tukiwakusanya wanamuziki wa zamani kuanzia Mbaraka Mwinshehe mpaka kufikia Maalim Gurumo, bado hawawezi kufikia mafanikio ya muda mfupi aliyoyapata kijana mdogo Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye hata ladha ya ndoa hajaionja kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Wakati Gurumo akijisifia nyumba mbili alizojenga kwa tamu, Diamond ana nyumba zaidi ya mbili ambapo moja amemjengea mama yake yenye thamani inayofikia zaidi ya Sh Mil 50.
Pengine Gurumo ni mwanamuziki bora zaidi kuliko Diamond lakini mwenziye amemzidi kwenye ujanja wa kutafuta fedha
-muhariri wa gazeti la Raia Mwema
JOKATE AFICHUA MAZITO....MH!
KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.
DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;
DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;
Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).
Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.
PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?
Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.
PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?
Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.
‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.
KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.
‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.
KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.
Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?
Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.
Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.
ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?
Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.
Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.
HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?
Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…
Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...
Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?
Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.
Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.
SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.
Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?
Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.
ZAWADI
Ijumaa Wikienda: Kati ya Diamond na Hasheem nani zaidi kwa zawadi?
Jokate: Naona sasa unataka kumkasirisha Diamond!
Ijumaa Wikienda: Tangu ulipoachana na Diamond una zaidi ya mwaka. Je, huna mpenzi mwingine?
Jokate: Nipo singo au unanishauri nani ananifaa?
Ijumaa Wikienda: Siwezi kuingia kwenye moyo wako wakati umesisitiza kuwa unampenda Hasheem!
Jokate: Yap…nilimpenda na ninampenda sana.
MWANA-FA VIPI?
Ijumaa Wikienda: Mbali na Hasheem, Diamond na huyo jamaa wa zamani, vipi kuhusu habari za wewe kutoka na mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana-FA’?
Jokate: Afadhali mnisaidie kwa sababu sijui hicho kitu kilianzia wapi. Ni uzushi tu uliosambazwa na mtu mmoja.
-Gazeti la ijumaa wikienda via Gpl
PICHA ZA DIAMOND ALIVYO WAPAGAWISHA WATU WA CHINA..
Wakati ile movie ya Temptation iliozua Gumzo Jijini iliyowakutanisha tena Msanii wa muziki Diamond na Mcheza Filamu Wa Tanzania Wema Sepetu ambao waliwahi kuwa wapenzi ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Diamond Na Wema Week End Hii diamond Amekua na Show Ya kukata na shoka huko Guangzhou huku baadhi ya washabiki wakijiuliza mbona hawamuoni Maddam
Mkumbuke kuwa Maddam Na Diamond walikutana Hongkong na kwamba tayari Maddam amesharejea nchini, Labda show hiyo ni muendelezo wa Temptation ambayo location yake kuwa inaonekana kuwa Nje ya Nchi.Cheki picha za show hiyo:-
WEMA AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIAMOND...!! SOMA HAPA...
Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo kwenye hii picha. Maana ya hii picha ni kwamba watu wengi wanafikiri kwamba muda wote Diamond yupo kwenye kichwa cha Wema, lakini yeye mwenyewe anasema kwamba muda wote anafikiria pesa. Unaionaje hiyo
picha?
WADAU WAPITISHA NDOA YA WEMA SEPETU NA DIAMOND....
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.
Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha
WEMA AENDELAEA KUTOKOMEZA PENZI LA DIAMOND NA PENY...TAZAMA PICHA ALIYOPOST WEMA INSTAGRAM AKIWA AMEVAA VIATU VYA DIAMOND NA USIBITISHO WA VIDEO YA DIAMOND AKIWA AMEVAA VIATU IVYO NCHINI CHINA
Takribani week sasa habari kubwa kuhusu mastaa Bongo ni story ya Diamond na Wema ,kurudiana
ambapo habari hizo bado ni tata kutokana na wahusika wote kutosema chochote kuhusu mahusiano yao.
ingawa kuna viashiria vingi vinavyozidisha utata wa mahusiano ya wawili hawa waliowah kuwa wapenzi zamani.
Wakati wakiendelea kutuchanganya ,kama unakumbuka tuliweka video ya diamond akikatiza ndani ya mitaa ya China akiwa amevaa nguo nyeusi na viatu vyeupe
Wema nae alipost picha Ikionyesha amevaa viatu kama alivyoonekana amevaa Diamond,utata siyo??
tazama picha na video kisha u judge mwenyewe.
Diamond aliponda PENZI la Penny na Wema Sepetu na kudai ni la UONGO.....Kama vipi, wamwache maana hana njaa ya penzi

Diamond Platnumz hataki kusikia cha Team Wema wala cha Team Penny, wote anawaona wale wale tu wenye mapenzi ya uongo na kama vipi wamuache maana hana njaa ya penzi.
Staa huyo wa bongo fleva ambaye bado yupo nchini China, ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akimpongeza ndugu yake kwa kupata mtoto.

Naye Wema Sepetu jana amerejea Dar akitokea Hong Kong ambako alikuwa kwenye mapumziko ya muda ambako alikutana na Diamond kukumbushia penzi lao.
TAZAMA DIAMOND PLATNUMZ AKIIMBA TEMPTATION YA P SQUARE KWENYE PROJECT YA COKE STUDIO AFRIKA...KATISHA SANA
Mtu wangu hii ni video ambayo Diamond ame-perform wimbo wa Temptation wa P Square kwenye project ya Coke Studio Africa. Diamond ameimba sehemu kubwa ya wimbo huu akiwa na live band pamoja na back ya msanii HHP.Chukua time yako kuiangalia hapa
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
MAMA DIAMOND AINGILIA PENZI LA DIAMOND, WEMA
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akizungumza nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.
Akizungumza nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii.
“Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo.
Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake.
“Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.
HIVI NDIVYO DIAMOND ALIVYOKUTANA NA WEMA HONG KONG....MAMBO YOTE SASA HADHARANI..
Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny
Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not the easiest relationship I’ve ever had..but its the most intresting! When I’m down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye. Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho am happy with my man, am happy na watu wangu so am good mimi sina tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.
<<INGIA HAPA KUCHEKI PICHA ZAO WAKIWA HON'GKONG WAKIFANYA YAO>>
<<INGIA HAPA KUCHEKI PICHA ZAO WAKIWA HON'GKONG WAKIFANYA YAO>>
PENNY MAHUTUTI NI BAADA YA KUONA PICHA ZA DIAMOND NA WEMA SEPETU
"DIAMOND NA WEMA SEPETU WAMERUDIANA...." NI MOVIE KWELI AMA....?
Let’s face this big elephant in the room…Diamond Platnumz na Wema Sepetu wana agenda ya siri. Naiita agenda ya siri kwakuwa kuna maswali makubwa mawili ambayo mimi na watu wengine wengi tunahisi Diamond anakificha kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu.
Swali la kwanza ni Diamond na Wema wamerudiana tena? Jibu la swali hili lilitolewa juzi na Diamond mwenyewe:
Kumekuwa na uvumi na habari nyingi sana mitandaoni na kwenye media tofauti… kwamba mimi na mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya kimapenzi, kitu ambacho sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye account yangu ya instagram?..Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya mapenzi basi msizungumze ama kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na mbadilike, ina maana mnapenda kuona watu wanauadui… Ni muda wa kufanya kazi ili kulipa sifa na heshima taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo na faida..I real love my Penny,sijarudiana na Wema.”
Baada ya Diamond kuandika hivyo, swali hilo likaanza kupotea.
Lakini jana na leo swali hilo limekuja tena kwa kasi baada ya kuonekana picha mpya za Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja katika nchi ya barani Asia ambayo bila shaka ni Malaysia ambako Diamond alikuwa ameenda kufanya show. Kwa picha hizo ni wazi, Diamond na Wema walienda pamoja. Picha za wapenzi hao wa zamani zimesambaa kwenye akaunti ya Instagram ya msichana anayejiita Chynabongo na sasa zimeshasambaa kama kila kona.
Baadaye Diamond naye akaweka picha moja kati ya hizo zilizowekwa na Chyna na kama kawaida yake akasema ni movie mpya inakuja.

“Katika moja ya muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii… #TEMPTATIONS …. STAY TUNED!!!! SOON!….#DayOne #Location #SomeWhere,” ameandika.
Kufanya movie ni kisingizio nambari moja cha Diamond. Nikukumbushe kuwa kabla ya uhusiano wake na Penny kufahamika, ilileak picha yao wakionekana wakiwa wamelala, na wote kwa pamoja wakadai walikuwa location wakifanya movie mpya, ambayo hadi leo haijaingia sokoni... tutaingoja hadi miguu iingie tumboni.
Kufanyika kwa movie ya Diamond na Wema si kitu kigeni kusikika kwani tangu mwaka jana kulikuwa na taarifa hizo na tayari ilidaiwa walikuwa wameshalipwa. Kama watu wengine, nashindwa kuamini kwa haraka kuwa picha hizi zina ukweli wowote kuhusu kisingizio cha Diamond kuwa hiyo ni movie. Hata hivyo hivi karibuni, Wema alisema ameandaa surprise kubwa kwa mashabiki wake, labda hii ndio yenyewe basi…
“What more can I say other than thank ol my beloved fans for all da love nd support uve bin showing me nd naamini hamtoacha maana you guys are jus amazing…. kuna kitu nataka kufanya jus to show my appreciation… its a Surprise I wont tel… ila im sure y’all are gon die… nat die die, but y’all are gon b soooo happy… nawapenda mpaka basi…. thank y’all sooo much,” aliandika Wema kwenye Instagram.
Kama Wema na Diamond hawajarudiana, basi wawili hawa wanajua kucheza vizuri na akili za watu na uwezo huo ndio umewafanya wasiwe na mpinzani katika kutafuta ‘publicity stunts’. Uwezo huo ndio umewafanya wawe mastaa wanaongoza kwa kutawala kwenye magazeti ya udaku.
Picha hiyo ya Diamond na Wema imeshavutia comments zaidi ya 500 na like zaidi ya 2, 000 kwenye Instagram, na kwenye Facebook imepata comments zaidi ya 400 na likes zaidi ya 900 kwenye Facebook. I guess that what’s Diamond likes right? Confusing people’s minds.. and he is good at it. Na sasa tayari, Wema na Diamond wanatrend tena…kila website/blog leo ina habari yao.… mission accomplished.
Okay, tunaisubiria Temptations kwa hamu kubwa lakini tusije kuisubiria kwa muda mrefu kama tunavyoendelea kuisubiria ile ya Diamond na Penny.
SIO SIRI TENA KUHUSU MAHUSIANO YA DIAMOND NA WEMA SEPETU....PICHA NNE WAKIFANYA YA KWAO MALAYSIA
Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo.
Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…
Kupitia account yake ya instagram diamondplatnumz amepost moja ya picha zilizopo katika movie mpya aliyoshirikiana na mwanadada wema sepetu kuonyesha msisitizo ktk hilo diamond amesema haya:
diamondplatnumz: Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii... #TEMPTATIONS .... STAY TUNED!!!! SOON!....#DayOne #Location #SomeWhere

Mganga wa Kienyeji asema yuko tayari kumsaidia Penny asiachwe na Diamond...Amtaka ampelekee KINYESI chake ili kumaliza tatizo

Mtaalamu wa miti shamba nchini ambae ni mwenyeji wa Tabora aliyejitambulisha kwa jina la Kamdege amesema kuwa anasikitishwa sana maumivu anayoyapata mtangazaji wa kituo cha DTV DVJ PENNY kwa sababu ya mwanamuziki Diamond, hivyo amemtaka mrembo huyo afike ofisini kwake mara moja ili ammalizie tatizo hilo.
Akiongea kwa njia ya simu [ 0788-844490 ], Kamdege amesema kuwa unyama na ukatili anaofanywa na msanii Diamond unaweza kukomeshwa endapo mmoja wa wasichana hao ataamua kufanya maamuzi magumu ya kuchukua kinyesi chake na kumpelekea ili amtulize.
Katika maelezo yake, mganga huyo alifafanua kwamba kinyesi hicho hakitatumika kumdhuru Diamond kwa namna yoyote ile, bali kitatumika kuituliza MAMBO yake na kumfanya aridhike na mwanamke mmoja huku wengine akiwaona mavi tu...
Mwandishi wetu alitaka kujua maana ya kuwaona mavi tu ambapo mganga huyo alifafanua kama ifuatavyo:
"Huo ni msemo tu, maana yake ni kwamba hatakaa atamani vya nje ambavyo ni VICHAFU.Sina maana ya kumfanya awachukie wasichana wengine"..
"Naomba niweke wazi, dawa hii si kwa ajili ya Diamond tu.Ni kwa ajili ya mwanaume yoyote msaliti. Yaani akitengezwa, usaliti utabaki kuwa historia tu
Mwandishi wetu alitaka kujua maana ya kuwaona mavi tu ambapo mganga huyo alifafanua kama ifuatavyo:
"Huo ni msemo tu, maana yake ni kwamba hatakaa atamani vya nje ambavyo ni VICHAFU.Sina maana ya kumfanya awachukie wasichana wengine"..
"Naomba niweke wazi, dawa hii si kwa ajili ya Diamond tu.Ni kwa ajili ya mwanaume yoyote msaliti. Yaani akitengezwa, usaliti utabaki kuwa historia tu
Aidha mtaalamu huyo alijinadi kwamba anauwezo wa kutibu matatizo mengine ya kiafaya, kikazi, kwa wenye kesi mahakamani na wangependa kesi hizo zifutwe, kupandishwa vyeo nk.