Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label tanzania. Show all posts
Showing posts with label tanzania. Show all posts

MSICHANA WA MIAKA 10 WA KIKATILI NA MWILI WAKE KUTUPWA CHOONI


MKAZI wa Kijiji cha Msanzi wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa , Festus Sungura (37) anadaiwa kumuua kikatili msichana Janeth Mwanandenje (10) na kisha kutumbukiza mwili wake ndani ya shimo la choo.

Inadaiwa choo hicho kilikuwa kikitumiwa na mkewe waliyetengana naye na lengo lilikuwa aweze kukamatwa na kufungwa kwa kosa la mauaji. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 
Alibainisha kuwa lilitokea Oktoba 18 mwaka huu saa 11 katika Kijiji cha Katuka Kata na Tarafa ya Matai wilayani Kalambo.
 
Mwaruanda alidai Oktoba 13 mwaka huu saa mbili usiku Janeth (marehemu) alikwenda kwenye ukumbi uliokuwa ukionesha mikanda ya video katika Kijiji cha Msanzi na hakurudi tena nyumbani kwao hadi mwili wake ulipogunduliwa ndani ya shimo la choo, kijiji jirani cha Katuka .
Inadaiwa siku iliyofuata, baba mzazi wa marehemu huyo aitwaye Mussa Mwanandeje , alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Matai ya kupotea kwa binti yake huyo.
 
Kwa mujibu wa Mwaruanda, Oktoba 18 mwaka huu jirani wa wazazi wa marehemu huyo katika Kijiji cha Msanzi, aitwaye Festus Sungura (37), alikwenda Kijiji cha Katuka, ambacho ni jirani na kijiji cha Msanzi.
 
Alikwenda kumfuata mkewe Rosemary Arusha, ambaye alirudi kwao kijijini hapo baada ya kugombana na mumewe huyo miezi kadhaa iliyopita.
 
Baada ya Sungura kufika Katuka, alikutana na binti yake aitwaye Digna Sungura (15), ambapo alimhoji iwapo mama yake mzazi ( mke wa Sungura) akifungwa, kwa kuwa anamchukia yeye baba yake, ataenda kuishi kwa nani? Binti yake huyo, alimjibu kuwa ataishi na bibi yake kijijini hapo Katuka.
 
Ndipo Sungura alipomwagiza binti yake huyo, akamwambie mama yake atoe miti mitatu, iliyowekwa juu ya shimo la choo wanachotumia, waone alichofakifanya yeye.
 
Mama ya binti huyo, alitoa taarifa kwa viongozi wa kijiji hicho cha Katuka, ambapo kwa kushirikiana na wakazi wengine, walitoa miti chooni hapo na kuuona mwili wa marehemu uliotumbukizwa humo.
 
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi wa shauri lake utakapokamilika.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI CHATANGAZA KUMSHITAKI ZITTO KABWE KWA KUTANGAZA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE


HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
 
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.

Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.
 
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
 
Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.
 
Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.

 Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
 
“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.
 
Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.
 
Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.

VIGOGO WA TANZANIA WALIOFICHA FEDHA KIASI CHA SH323.4 BILIONI NCHINI USWISI KUCHUNGUZWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA EURODAD, MHE ZITTO KABWE KUONGOZA UCHUNGUZI HUO..


WAKATI ikisubiriwa ripoti ya uchunguzi wa Tume Maalumu iliyoundwa kwa Azimio la Bunge kuchunguza kashfa ya vigogo walioficha Sh323.4 bilioni katika benki nchini Uswisi, Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo (Eurodad), leo linaanza kuwachunguza walioficha mabilioni hayo ya fedha nchini humo.
Kazi hiyo ya uchunguzi inaanza leo hadi Novemba 5, mwaka huu, ambapo pamoja na mambo mengine watafanya ziara ya uchunguzi kuhusu masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya.
Uchunguzi huo utafanywa na jopo la wataalamu waliobobea katika masuala ya kodi na maendeleo na wataongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa bungeni kwa hoja binafsi ya Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, mwishoni mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Kufuatia hoja hiyo, Bunge chini ya Spika Anne Makinda liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo bungeni.
Ripoti ya Tume hiyo iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana, ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, mpaka sasa tayari imewahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Muda wa tume hiyo kufanya uchunguzi unakamilika mwezi huu na inatarajiwa katika mkutano ujao wa Bunge unaoanza Oktoba 29 mjini Dodoma, itawasilisha ripoti hiyo.
Taarifa zilizolifikia Mwananchi Jumapili na kuthibitishwa na Zitto jana jioni zilieleza kuwa Eurodad ambao ni mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali 48 kutoka nchi 19 za Ulaya, yanayojihusisha na masuala ya kufuatilia madeni ya nchi zinazoendelea, kwa muda sasa umekuwa ukipambana na watu wanaokwepa kulipa kodi.
“Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kesho Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswisi na maofisa wa benki mbalimbali na asasi za kiserikali zilizopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Geneva.
“Zitto pia atahudhuria mkutano wa Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za kimataifa ili kuzuia unyonywaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na kampuni kubwa za kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo. 
-MWANANCHI

CCM WAMSALITI KIKWETE..WADAI KWAMBA WAKO TAYARI BUNGE LIVUNJWE NA UCHAGUZI UFANYIKE KABLA YA 2015


HOFU kubwa imetanda ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), juu ya upatikanaji wa katiba mpya, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kusaini muswada ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.
 
Mkutano kati ya Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni uliofanyika Ikulu Oktoba 15, 2013 umeongeza mpasuko ulioanza kujitokeza baina ya makada wa CCM na wapinzani.

Katika mkutano huo, rais na viongozi wa upinzani waliafikiana vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.
 
Walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
 
Awali kabla ya mkutano huo, makada wa CCM wakiwamo mawaziri kadhaa waliweka wazi kuwa milango ya Ikulu imeshafungwa kwa wapinzani kuzungumzia suala hilo, lakini Rais Kikwete alipotangaza kukutana nao iliwaweka njia panda.
 
Tanzania Daima  limedokezwa kuwa baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakimshutumu Rais Kikwete kwa kuwabembeleza wapinzani huku akikiumiza chama chake.
 
Hoja wanayoijenga ni kuwa Rais Kikwete anataka kujijengea kitu cha kukumbukwa, hasa katika suala la katiba mpya bila kujali athari zinazokipata chama chake.
 
Makada hao wanaweka bayana kuwa hali hiyo itakiacha chama katika wakati mgumu wa kukabiliana na wapinzani wanaoonekana kuimarika kadiri siku zinavyoyoyoma.
 
Baadhi ya wabunge wa CCM wanamuona Kikwete kama msaliti kwa wabunge wake waliopitisha muswada huo, ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba, ukiwa na upungufu ulioainishwa na wapinzani.
 
Mmoja wa watu waliohudhuria mazungumzo ya Ikulu anasema rais aliridhia marekebisho hayo na alibainisha kuwa yajikite katika masuala kadhaa, likiwamo suala la Tume ya Warioba kuwapo kwenye Bunge Maalumu la Katiba, marekebisho katika suala la uteuzi wa wajumbe 166 ili idadi iongezeke na hoja ya Zanzibar kushirikishwa kabla ya muswada wa sheria ya kura za maoni kuanza.
 
Tayari Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alishatoa tamko kuwashangaa wabunge wa CCM kwa kupotosha kifungu kilichokuwa kinasema Tume ya Mabadiliko ya Katiba itavunjwa na rais mara tu baada ya kuwasilisha rasimu kwenye Bunge Maalumu la Katiba, msimamo ambao unaungwa mkono na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala (CCM).
 
Mbunge huyo katika andiko lake alilolisambaza katika vyombo vya habari, anakiri kuwa moja ya upungufu alioubaini katika muswada ule ambao sasa ni sheria, ni kuiua Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya mchakato kufikia mwisho.
 
“Kiukweli, lina mantiki ndani yake. Tukiwa kwenye Bunge la Katiba hakutakuwa na serikali, sasa ni nani atakayejibu na kuweka sawa hoja za wabunge? Hili kwa kweli wabunge tuliopitisha muswada ule hatukuliona vizuri,” alisema Kigwangala.

Wakati Kigwangala akiona upungufu huo, Naibu Spika Job Ndugai,  anajitetea  kuwa haoni udharura wa suala hilo kurejeshwa bungeni.
 
Ndugai amebeza suala la urejeshwaji wa sheria hiyo bungeni, akihoji kuwa suala hilo halina udharura.
 
“Ni ishu gani hasa ambayo wapinzani walienda kumwona rais ambayo inahitaji udharura huo? Je, kanuni za Bunge zinaruhusu suala hilo?” alihoji Ndugai.
 
Akizungumza na mwandishi  wetu wiki hii, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Bunge ni muhimili tofauti. 

Wabunge kama wataona kuna kitu cha kubadilisha watabadilisha, lakini wakiona hakuna cha kubadilisha itabaki ilivyo.
 
Kauli hiyo imeungwa mkono jana na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, ambaye alinukuliwa na gazeti moja nchini , akisema: “Serikali haikusudii kufanya marekebisho yoyote kwenye Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba iliyosainiwa na Rais Kikwete hivi karibuni.”
 
Mmoja wa wabunge wa CCM aliyehojiwa na mwandishi wetu  na kutoa msimamo wake baada ya rais kusaini muswada kuwa sheria ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Hamad Yusuf Massauni, ambaye sasa ni Mbunge wa Kikwajuni.
 
“Mimi ningekuwa rais nisingepoteza muda kuongea na wapinzani, na hata kama sheria hii itarejeshwa bungeni, sioni sehemu yoyote ya kufanyia marekebisho, iwe ya kuondoa koma wala kuweka nukta,” alisema.
 
Kabla ya muswada huo kusainiwa kuwa sheria, Nape alinukuliwa  akisema: “Hofu yangu ni kuwa rais asiposaini muswada huo, ataingia katika mgogoro kikatiba, itabidi arejeshe muswada bungeni aeleze kwanini hajasaini, na ukirejeshwa bungeni wabunge wa CCM wakakataa kufanya mabadiliko, rais angelazimika kuvunja Bunge.
 
Aliongeza kuwa: “Mimi ninaona afadhali rais asaini muswada huu ili kama kuna upungufu uwekwe mezani kama ilivyokuwa mwanzo, ila nakubali kabisa mzee Warioba ana hoja katika suala la kutovunjwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya kutetea rasimu mbele ya Bunge Maalumu la Katiba.”
 
Alisema wabunge wa CCM ni asilimia 74 ya wabunge wote, hivyo wakishikilia hoja ya kutobadilisha jambo lolote katika muswada huo baada ya kurejeshewa na rais, matokeo yake ni kuvunjwa kwa Bunge na nchi kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015.
 
Nape alisema CCM haiko tayari kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015, hivyo akawataka wanaopinga na kuunga mkono hoja hizo watumie busara na hekima kufikia maridhiano yatakayolijenga taifa.
 
Alisema kuwa muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwanzo nao ulipitishwa ukiwa na kasoro mwaka 2011, lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo walienda kwa rais wakajadiliana wakakubaliwa, na kwamba viongozi wa CCM walilazimika kwenda Dodoma kuwaeleza wabunge msimamo wa Rais Kikwete na kuwashawishi waukubali.
 
“Tulipoona kuna hoja tulilazimika kwenda Dodoma kuwaomba wabunge wetu wakubali hoja za CHADEMA ili marekebisho yafanyike, ingawa suala hilo lilifanyika kwa taabu sana, sasa zamu hii wabunge wa CCM wanaweza wasikubali hoja za wapinzani, na likiendelea vile rais atalazimika kuvunja Bunge, hili suala limetuweka pabaya sana CCM, sijui hatima yetu,” alisema.
 
Tanzania Daima , limedokezwa kuwa iwapo serikali itaridhia marekebisho yaliyotajwa na wapinzani, mvutano mkubwa utazuka bungeni kati ya washindi na washindwa.
 
Jambo hilo linadaiwa halitakubaliwa na wabunge wa CCM ambao mara kwa mara wamekuwa wakishutumiwa kupitisha mambo kwa kuangalia zaidi masilahi ya chama kuliko taifa.
 
Kumekuwa na mipango ya CCM kumuandaa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa Spika wa Bunge la Katiba.
 
Inadaiwa Chenge ndiye atakayebeba jukumu la kudhibiti baadhi ya hoja zinazopingwa na CCM zilizotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba.
 
Miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya rasimu ya katiba ni serikali tatu.

-Tanzania daima

MAUAJI YA KUTISHA MKOANI MBEYA.....AUAWA KWA KUKATWA KICHWA KISHA KUTUPWA

Mwili wa Marehemu Seba ukiwa umefunikwa na branketi

SEBA ERNEST MWAKASULA[45] ameuawa  kwa kukatwa kichwani na  tumboni na vitu vyenye ncha kali  na mtu au watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake.

Mke wa marehemu JOYCE DANIEL[39]amesema waliagana na marehemu majira saa mbili usiku akimtaarifu kuwa asubuhi ya octoba 19 mwaka huu atasafiri kuelekea Wilaya ya CHUNYA kwa ajili ya kujenga makaburi.

Aidha imedaiwa baada ya kutoka nyumbani kwa mke mdogo marehemu alipita kilabuni ambapo watu kadhaa walimwona marehemu akipata viburudisho.

Baadhi ya majirani wamesema kuwa hawakusikia sauti yoyote ya mtu kuomba msaada ingawa ni karibu na makazi ya watu hali inayosadikika mauaji kufanywa eneo jingine na mwili kutupwa karibu na nyumbani kwake

Mwenyekiti wa kijiji cha NSONYANGA ASUMILE MTAWA amesema alipata taarifa kutoka kwa mtendaji wa kijiji ambapo walifika eneo la tukio na kukuta marehemu amekatwa kichwani na utumbo ukiwa nje.

Diwani wa kata ya Mahongole BROWN MWAKIBETE amesema kuwa kitendo kilichofanywa na wauaji hao ni cha kinyama ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi li watuhumiwa wakamatwe ili kujibu tuhuma za mauaji.

Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kutoa wito kwa mtu au watu wanaowafahamu wliohusika na tukio hilo watoe taarifa polisi il wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

WANAFUNZI WAWILI WA KIKE WA SHULE YA SEKONDARI BUNJU WAFA MAJI WAKATI WAKIOGELEA BAHARINI..

Wanafunzi wawili wa kike mkoani Dar es Salaam wamefariki dunia baada ya kuzama wakati wakiogelea baharini.

Wanafunzi hao wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Wasichana ya Bunju, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, walifariki dunia juzi wakati wakisherehekea kumaliza mitihani yao ya kujiunga na kidato cha tatu.

Tukio hilo lilitokea katika ufukwe wa Ununio katika manispaa hiyo, baada ya marehemu pamoja na wanafunzi wenzao kufika huko kwa ajili ya kuogelea ikiwa ni sehemu ya kushangilia baada ya kumaliza mitihani.

Shuhuda wa tukio hilo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema aliwaona polisi wakifika eneo hilo kuchukua miili ya watoto hao baada ya ajali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliofariki kuwa ni Clara Emanuel na Salama Mohamed, ambao alisema walikuwa wanasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Bunju.

Alisema wanafunzi hao baada ya kufika katika ufukwe huo wakiwa na wenzao, walianza kuogelea, lakini walizidiwa na maji na kuzama na kwamba, waliopolewa na mvuvi wa samaki wakiwa wamekufa.

Kamanda Wambura alisema baada ya mvuvi huyo kuwaopoa baharini, alikwenda kutoa taarifa polisi na kwamba, askari walifika eneo hilo na kuwachukua marehemu na kwenda kuwahifadhi katika Hospitali ya Mwananyamala.

Alisema wazazi wa marehemu wameshapatikana kufuatia jitihada za kuwatafuta zilizofanywa na polisi.

UKATILI: MUME AMKATA MIGUU MKEWE KWA PANGA MARA BAADA YA KUCHELEWA KUMFUNGULIA MLANGO HUKO TARIME..


Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku  na  hivyo  kumfanya  aamini  kuwa  alikuwa  na  mwanaume  mwingine  ndani.

Akisimulia mkasa huo huku  akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.
 
"Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia.Akaaza  kunifokea  kwamba  nilikuwa  na  mwanaume  mwingine  ndani , baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema Ghati.


Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa  nini kinafuata , alifikiri  kuwa  ni  mambo ya wanaume tu, pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.
 
" Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.
 
Wakati anafanyiwa ukatili huo alipiga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.
 
"Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa" alieleza .
 
Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.
 
Hata hivyo siku moja  baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu za wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa , Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.
 
" Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha nii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema Kamugisha kwa nija ya simu

HII NI HATARI SANA..MASHARTI KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA 'MAGAIDI' WA MTWARA YAANIKWA HADHARANI..

Wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu kikundi cha vijana 11 wanaoshikiliwa Polisi baada ya kukutwa wakifanya mazoezi ya kivita porini, mwandishi amebaini kuwa kikundi hicho kilikuwa na masharti ya kusajili wanachama.

Kikundi hicho ndio kilichokamatwa msituni na vifaa mbalimbali zikiwemo CD za mauaji ya Osama Bin Laden, Mauaji ya Idd Amini, Kuandaa Jeshi, Zindukeni Zanzibar, al Shabaab na Mogadishu Sniper.
CD na DVD walizokamatwa nazo wakizitumia kufanya mazoezi

Pia walikutwa na DVD player moja, mashine ya umeme wa jua wati 30, mapanga mawili, visu viwili, tochi moja, betri ya pikipiki, simu tano za viganjani, vyombo vya chakula, jiko la mkaa na jiko la mafuta ya taa.

Vingine ni taa ya chemli, baskeli tatu, ndoo nne za maji, unga wa mahindi kilo 50, mbaazi kiroba kimoja cha kilo 50, mahindi viroba vitatu vyenye uzito wa kilo 150, virago vya kulalia na mfuko wa kijani unaosadikika ni wa kijeshi wenye nembo ya nanga ya meli, yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.

Miongoni mwa masharti ya kujiunga na kikundi hicho, yametajwa kuwa ni pamoja na mwanachama kufarakana na familia yake, ili kuonesha utayari wa kutumikia kikundi hicho.

Mwandishi alifika katika kitongoji cha Mwambo, karibu na mlima wa Mwakyolongo uliokuwa ukitumika kwa ajili ya mafunzo hayo na kukutana na mtoa taarifa aliyefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Mtoa taarifa huyo alimtaja mmoja wa vijana (jina limehifadhiwa), ambaye aliachana na mke wake na mwingine ambaye alikataa maonyo ya wazazi wake, na kuwataka wazazi hao kama hawamruhusu ajiunge, bora wamwachie radhi.

Mtuhumiwa Said Mawazo, anadaiwa aligombana na familia yake baada ya kutakiwa na wazazi wake kuacha kushirikiana na watu hao ambapo aliwaambia afadhali atengane na familia yake na sio kuacha kikundi hicho.

Mama mlezi wa kijana huyo, Fatuma Abdalah, alimwambia mwandishi kwamba kijana wao alikataa kusikiliza ushauri wa mtu yeyote na alikuwa tayari kugombana na yeyote aliyejaribu kumzuia au aliyejaribu kuhoji jambo lolote kuhusu kikundi hicho.

“Mimi na baba yake tulijaribu kumkalisha na kumwambia asijihusishe na kikundi hicho, lakini majibu aliyotupa yalitushangaza na hata alidiriki kusema kuwa heri apewe radhi lakini hawezi kuacha kikundi hicho ambacho najua kilijificha kwenye kivuli cha dini,” alidai Fatuma.

Mama huyo alisema hawana namna zaidi ya kuachia sheria ichukue mkondo wake endapo watabainika kujihusisha na mafunzo ya kijeshi, kwani walikuwa wanahatarisha na kuvuruga usalama wa nchi, ingawa vijana hao hawakujua jambo lililokuwa limejificha nyuma yao.

Katika hatua nyingine, walimu wawili wa Shule ya Msimgi Likokona, katika Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, wameongezwa katika idadi ya watuhumiwa wa kikundi hicho.

Mwandishi alifika kijijini hapo na kuwakuta walimu hao wakiwa stendi ya basi wakienda katika Kituo cha Polisi Nanyumbu, ambako waliitwa kwa ajili ya mahojiano.

Ingawa walimu hao Cheka Salum na Abilah Seleman hawakutaka kuzungumza chohote walipokutana na gazeti hili wakiwa njiani kwenda kituo cha Polisi, lakini Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Salum Omary, alikiri kuwataarifu kuwa wanatakiwa Polisi.

Taarifa kutoka katika kituo hicho, zilibainisha kuwa walimu hao baada kufika kituoni hapo, walihojiwa kisha wakawekwa chini ya ulinzi ambapo Oktoba 12 mwaka huu, walisafirishwa kwenda Mtwara mjini kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Zelothe Steven alipopigiwa simu, alisema polisi inaendelea na upelelezi na ukikamilika, atatoa taarifa kamili.

VIDEO YA RAIS KIKWETE AKIONGEA NA VIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANIA...NA HUU NDIO MUAFAKA ULIOFIKIWA JUU YA KATIBA MPYA

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitikadi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliitishwa na Rais Kikwete ili kuondoa sintofahamu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Septemba na Bunge lilipokutana mjini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana jioni ilisema katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.
Pia Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
“Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini,” iliongeza taarifa hiyo.
Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Isaack Cheyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema. Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao waliambatana na wenyeviti wao ni Mohamed Mnyaa na Julius Mtatiro wa CUF, Tundu Lissu na John Mnyika wa Chadema na Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.
Vicheko Ikulu
Vicheko na bashasha vyatawala Ikulu
Ilikuwa fursa kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi hao baada ya kipindi cha miezi miwili cha kurushiana maneno baina ya viongozi wa Bunge, Serikali, CCM waliokuwa wakivutana na viongozi wa vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi.
Kama mtu yeyote angeulizwa kutabiri katika tukio lililotokea jana lingetokea basi angekuwa na wakati mgumu kutokana na ukali wa maneno na malumbano katika kipindi chote baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge wa Septemba.
Rais Kikwete alionekana mwenye furaha tele wakati alipokutana na viongozi wa vyama hivyo na kivutio zaidi ilikuwa pale alipokutana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu.
Viongozi hao walisalimiana huku wote wakitabasamu na kuashiria kuwa waliamua kuweka tofauti zao pembeni na kuangalia masilahi ya nchi.
Kumbuka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Septemba, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa yeye hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Rais Kikwete alikaririwa akisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu, huku akisisitiza kuwa mbunge huyo alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alipinga tuhuma hizo na kusisitiza Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) bila ya ridhaa yao.
Chikawe, Wassira na Lukuvi ndani
Mawaziri watatu, ambao walitetea kwa nguvu kupitishwa kwa muswada ule ndani na nje ya Bunge walihudhuria mazungumzo hayo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira walikuwemo kwenye mazungumzo ya jana.
Mawaziri hawa kwa nyakati tofauti walitetea kuwa mchakato wa muswada ule haukuwa na matatizo yeyote na kushikilia kuwa lazima Rais lazima asaini muswada kwani ulikuwa umepitishwa kihalali na Bunge.
Pia walikuwa wameshikilia kuwa safari hii kulikuwa hakuna mambo ya mazungumzo kati ya Rais na upinzani.

Chanzo cha sintofahamu
Wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.
Katika hatua nyingine, taarifa kutoka Ikulu zilisema kwamba Rais Kikwete alisaini muswada huo tangu Oktoba 10 mwaka huu siku ambayo wapinzani walipanga kufanya maandamano nchi nzima.
Katika mahojiano na Mwananchi jana jioni, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema muswada huo tayari ulikwishasainiwa na Rais na kama kuna marekebisho yatafanywa.
Mwananchi ilimtafuta Rweyemamu baada ya kusikia akithibitisha kusainiwa kwa muswada huo katika mahojiano na BBC Idhaa ya Kiswahili jana.
Akizungumza na Mwananchi Rweyemamu alisema, “Rais ameshasaini tangu Oktoba 10, unajua kulikuwa hakuna tatizo lolote kuhusu muswada huu kwa sababu ulifuata taratibu zote bungeni.”
Rweyemamu alisema kuwa awali Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais atakutana na wapinzani, pia atausaini muswada huo.
“Muswada umepitishwa bungeni na yeye amekamilisha kazi kwa kuusaini ili kuwa sheria. Alipokutana na wapinzani leo (jana) amewaeleza hilo na wameridhika” alisema Rweyemamu.
 CHEKI VIDEO HAPO CHINI....

MBUNGE MBARONI KWA WIZI WA GARI ...

Makalla anamtuhumu Ngonyani a.k.a Profesa Maji Marefu kuwa alichukua gari lake aina ya BMW X5 kisha akatokomea nalo kisha akawa anampigia simu hapokei na hata akimtumia SMS hajibu.
Kutokana na malalamiko hayo, hivi sasa Maji Marefu anasakwa na polisi wa Kituo cha Kati (Central), Dar es Salaam, tuhuma zikiwa ni wizi wa kuaminiwa, shauri lipo kwenye kitabu cha ripoti za polisi (Report Book ‘RB’) kwa namba CD/RB/13336/2013.
NYEUPE NA NYEUSI YA TUHUMA ZENYEWE
Nyeupe na nyeusi (black and white) ya tuhuma hizo, inawekwa wazi na ‘sosi’ wetu ambaye aliliibia siri kwamba sakata kati ya Maji Marefu na Makalla lilianza tangu Julai, mwaka huu wakati waheshimiwa hao walipokuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

“Maji Marefu aliomba gari la Makalla ili alitumie kwa mizunguko ya siku moja tu lakini hakurudisha,” kilisema chanzo chetu. “Mgogoro mkubwa ulianza kuibuka kuanzia hapo na mpaka leo waheshimiwa hao hawazungumzi kwa salamu wala kutakiana heri.”
Chanzo chetu kiliendelea kusema: “Siku ya kwanza tu ilipopita, Makalla alimpigia simu Maji Marefu akawa hapokei, akimtumia SMS hajibu. Kwa kifupi Makalla alipoteza mawasiliano na Maji Marefu lakini aliendelea kusubiri kwa sababu anajua ni mtu wake.”
Habari zaidi zinasema kuwa kilipita kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja bila ya Makalla kumpata Maji Marefu kwenye simu lakini walikutana katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioketi kati ya Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu, Dodoma.
“Walipokutana Makalla alimuuliza Maji Marefu gari lake lipo wapi? Maji Marefu alimjibu alilikabidhi Lamada Hotel, Dar es Salaam,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza: “Unajua makabidhiano ya lile gari yalifanyika Lamada Hotel, kwamba angelirudisha baadaye lakini ikawa kimya.
“Hata hivyo, Makalla aliona siyo kesi kubwa, akafuatilia Lamada Hotel, menejimenti ya hoteli hiyo ilijibu kuwa gari hilo halijapelekwa pale. Vilevile baada ya kuzungumza siku hiyo, Maji Marefu alitoweka na bungeni hakuonekana tena.
“Baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa Profesa Maji Marefu na Lamada, Makalla alifungua mashitaka Central, akidai kuibiwa gari lake na Maji Marefu.”
MAKALLA AFUNGUKA
Makalla ambaye ni Mbunge wa Mvomero (CCM) alipozungumza na mwandishi wetu alikubali kila kitu kisha akafunguka: “Niliomba polisi wanisaidie maana kwa hali iliyokuwepo ni kama nilikuwa nimeshatapeliwa. Vilevile niliripoti kwa Kamanda Mohamed Mpinga (mkuu wa kikosi cha usalama  barabarani) ili naye awaambie vijana wake wanisaidie kunitafutia gari langu.

“Nilimpa alama zote, rangi na namba za usajili. Oktoba Mosi, mwaka huu, ikiwa ni karibu miezi mitatu imepita tangu nimpe gari, polisi Tanga waliliona gari langu likiwa linaendeshwa na mheshimiwa Ngonyani (Maji Marefu) kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
“Nilimtumia SMS kumwambia kuwa gari langu ameonekana nalo katika msafara wa makamu wa rais. Polisi Tanga walitaka kumkamata lakini nikaomba aachwe kwanza, kukamatwa katika msafara wa makamu wa rais angeona amedhalilishwa.
“Nilimuomba baada ya msafara akalikabidhi gari kwa RPC Tanga kwa sababu linatafutwa na polisi. Akaniambia hawezi kulipeleka polisi kwa sababu tulikabidhiana vizuri. Nikamwambia sitaki kwa sababu alikuwa ananizungusha sana kunirudishia gari langu, mara aseme amelipeleka Lamada kumbe bado analo na wakati huohuo hapokei simu wala hajibu SMS zangu.”
USHAHIDI WA SMS
MAKALLA: “Mhe. pamoja na kutopokea simu na kutojibu meseji zangu, nakujulisha leo Oktoba Mosi, umeonekana na gari langu kwenye msafara wa makamu wa rais. Polisi walitaka wakukamate nikashauri wasubiri umalize mkutano. Kwa meseji hii naomba kesho asubuhi ukakabidhi gari langu kwa RPC Tanga, bila kukosa. Utamkuta ndugu Rajabu alipokee gari hilo baada ya ukaguzi mbele ya RPC.”

MAJI MAREFU: “Sawa nimekuelewa, yote ni makosa yangu na hii ni mali yako ila gari hatukupeana polisi, ungeniambia ulipo nikuletee.”
MAKALLA: “Sitaki umenizungusha sana, nilikukabidhi kwa heshima lakini umegeuka adui, hupokei simu huu ni mwezi wa tatu.”
MAJI MAREFU: “Ok nitafanya hivyo.”
MAKALLA ANAENDELEA
“Hakupeleka gari kwa RPC Tanga kama nilivyomtaka. Zilipita kama siku tatu, ndipo mtu mmoja akaenda kulitelekeza gari langu Lamada Hotel usiku. Walinzi walimuuliza yule mtu aliyetekeleza lile gari kwa nini anaacha gari na anakimbia? Hakujibu, akarukia kwenye pikipiki ambayo ilikuwa inalifuata lile gari kwa nyuma kisha akatoweka.
“Uongozi wa Lamada baada ya kuliona gari langu walinipigia simu, wakanijulisha nami nikapiga simu polisi, wakaenda kulichukua. Mpaka sasa gari lipo polisi central, wanasubiri kumkamata Mhe. Ngonyani ili kesi iendelee mbele.”
KAZI YA UWAZI
 baada ya kuzungumza na Makalla, lilikwenda kufanya upekuzi wake central na kubaini kwamba kesi hiyi ipo na madai yapo kama yalivyoelezwa.

Baada ya hapo, mwandishi wetu alimpigia simu Maji Marefu ambaye alipokea akiwa Nairobi, Kenya, na aliposomewa tuhuma dhidi yake, alijibu: “Subiri nirudi Dar, nitaeleza kila kitu.” Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Kuna madai kwamba ulichukua gari la Mheshimiwa Makalla, umekaa nalo miezi mitatu, kipindi chote hicho simu ulikuwa hupokei wala hujibu SMS zake.
MAJI MAREFU: Siyo kweli.
MWANDISHI: Labda ukweli ni upi.
MAJI MAREFU: Labda kwa sababu sipo Dar, nisubiri nirudi tutakaa tuzungumze.
MWANDISHI: Ungeniambia kwa kifupi tu ni kwa nini Makalla akushitaki, maana hii kesi ipo polisi, RB ipo na unatafutwa kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa.
MAJI MAREFU: Polisi wananitafuta mimi?
MWANDISHI: Ndiyo wanakutafuta wewe.
MAJI MAREFU: Kwa vile nipo Nairobi na wewe upo Dar, naomba usubiri tukutane kwanza ndipo nitaweza kueleza ukweli halafu ndipo mtaamua kuendelea mbele.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, swali lingine wewe una ugomvi na Mheshimiwa Makalla?
MAJI MAREFU: Aah, ndiyo nikasema tukikutana ndiyo italeta picha nzuri. Kama natafutwa au kuna tukio lolote nitaeleza.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, basi nijibu swali hili, wewe una ugomvi na Makalla?
MAJI MAREFU: Sina ugomvi naye.
MWANDISHI: Sasa kwa nini akushtaki kwa wizi wa gari lake?
MAREFU: Naomba tukutane nikirudi nitaongea tu.
MWANDISHI: Inasemekana hilo gari uliwahi kumwambia Makalla kwamba uliliacha Lamada Hotel lakini baadaye ukaonekana nalo kwenye msafara wa makamu wa rais Tanga. Hili limekaaje?
MAJI MAREFU: Mimi nina magari zaidi ya 15, nitakupeleka uone kama mimi nina shida ya gari. Nyumbani kwangu kuna magari ya kila aina.
MWANDISHI: Ni kweli Makalla alikukabidhi gari?
MAJI MAREFU: Subiri nirudi Dar nitaongelea hilo.
MWANDISHI: Nijibu tu hilo moja tu, alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Kwani yeye anasema nilimnyang’anya au alinipa?
MWANDISHI: Anasema alikupa.
MAJI MAREFU: Sasa subiri nirudi nitaeleza ukweli wangu.
MWANDISHI: Kwani mheshimiwa inashindikana nini kunijibu swali hili moja tu? Alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Ukweli mtaupata nikisharudi Dar.

POLISI NAKO
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, kwanza alisema hajapata taarifa yoyote kuhusu sakata hilo mpaka afuatilie.

Siku iliyofuata, Kova alipigiwa tena simu akaulizwa kuhusu sakata hilo, akajibu: “Kuna mtu  alinipigia simu jana kuhusu hii kesi, unajua mimi ni kamishna, hii kesi ni ndogo na siyo kila kesi lazima nijibu mimi.

-Gazeti la uwazi Via Gpl

SAKATA LA KUFICHUA WAINGIZA MADAWA YA KULEVYA CHINA.....WABONGO NCHINI CHINA WAHENYESHWASAKATA

Taifa la China halina mzaha mbele ya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kwa kutambua kwamba wanaohusika zaidi ni Waafrika, sasa hivi kila mja mwenye ngozi nyeusi aliyepo nchini humo, anapewa msoto wa nguvu.
Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe vyao, barabarani na kadhalika, kote huko wanapewa msoto wa guvu kwa kile kinachoelezwa kuwa Wachina hawana imani tena na Watanzania na Waafrika kwa jumla ama wanaoishi nchini humo au hata wale wanaoingia na kutoka.
“Wazungu wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni Mtanzania anayeishi China kwa sasa.
Aliongeza: “Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito. Kwa vile wanajua Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.
 
  “Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa. Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.

“Kila anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo halali, anafunguliwa mashtaka. Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan, nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu wakikamatwa.
“Kote hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine, akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na kugundulika siyo madawa ya kulevya.”
Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana.
Imebainishwa zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.
Risasi Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.

KINACHOWAPONZA NI HIKI

Kwa mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la kisigino.
Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.
“Punda ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari sana. Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.
“Vilevile ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana. Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi Guangzhou, China.

CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA

Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012, iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.
Amnesty International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za kunyonga watu bila mafanikio.
Shirika hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.

BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA

Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu hapa. Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

BAADA YA TANZANIA KUWAFUKUZA WANYARWANDA...SERIKALI YA RWANDA IMEAPA KUTOWAFUKUZA WATANZANIA


Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda amesema kamwe hawatawafukuza Watanzania wanaoingia na kutoka nchini Rwanda kwa shughuli mbalimbali kwani tupo ndani ya shirikisho la Afrika Mashariki na hata kihistoria Rwanda haijawahi kuwa na tatizo na Tanzania.

Akizungumzia sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.

Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.

Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k

HII NDO KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU SHEIKH PONDA KUPIGWA NA RISASI MOROGORO

 
Kupitia mtandao wa facebook...Mh zitto kabwe alisema haya juu sheihh ponda kupigwa risasi..
Na nukuhu "Habari zinazidi changanya ,Napata taarifa kwamba sheikh ponda ni mzima ila ana majeraha makubwa ya risasi alizopigwa na polisi.Kwa hali yeyote ile ninazidi kushauri kwamba haya ni majaribu na kuna haja ya kuwa watulivu sana.Kitendo cha polisi kutumia risasi za moto dhidi ya raia ni kitendo cha kulaaniwa sana".Mwisho wa kunukuu.


HIKI NDICHO KILICHOANDIKA KWENYE ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK
 

MAPYA YAIBUKA: POLISI WAHAHA KUWAINGIZA DK. SLAA, MBOWE KWENYE KESI ZA UGAIDI

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya maofisa wa polisi na makachero wao wamekuwa wanatumia vibaya majina ya viongozi wakuu wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama kisingizio cha kupika kesi za ugaidi dhidi ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika tukio la hivi karibuni, makada wa CHADEMA waliokuwa rumande wakikabiliwa na mashitaka ya ugaidi, ambayo hatimaye yalifutwa na mahakama, wametoboa siri kuwa miongoni mwa majina yaliyotumiwa na baadhi ya polisi na makachero waliowatesa ni ya Rais Jakaya Kikwete; na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wiki hii, makada hao - Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Rajabu Kihawa, Seif Magesa na Henry Kileo, wamesema pia kuwa njama hizo za polisi na makachero wao, zililenga kuwalazimisha vijana hao wawahusishe viongozi wakuu wa CHADEMA (hasa Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa) na ugaidi na utesaji watu ambao umekuwa unaendelea.

Wengine ambao polisi walitaka watajwe ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.

Hata hivyo, vijana hao wanasema waligoma kuwahusisha, hata baada ya kuteswa kikatili.

Makada hao wanadai kwamba mateso waliyopata yaliratibiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi, Advocate Nyombi na afande Pasua.

Mmoja wa makada hao, Kihawa, aliyekamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Dodoma, anadai kuwa alipokuwa anahojiwa, alilazimishwa aseme kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wanahusika na utekaji na tindikali.

Akiendelea kusimulia mkasa huo, Kihawa alisema kuwa baada ya kauli hiyo, aliingizwa katika chumba namba 114, ghorofa ya pili, chenye kamera nyingi katika moja ya hoteli maarufu Mjini Dodoma (jina tunalihifadhi kwa sasa) akavuliwa nguo zote, akakalishwa kwenye chupa ya soda kisha akapigwa sana.

“Nilipoteza fahamu lakini nilipozinduka nilikuta nimevalishwa nguo, na nimekalishwa kwenye kiti na kuwekewa chakula karibu,” anasema, na kuongeza kuwa hakula chakula hicho, lakini alipotoka nje ya chumba hicho, kwenye ukumbi wa hoteli, aliwakuta vijana waliofukuzwa CHADEMA, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba na Habib Mchange wakinywa na kula.

“Walinikejeli sana, wakasema wanashangilia ushindi,” alisema.

Kutoka pale nilichukuliwa na Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, akaniingiza chumbani akadai anampigia simu Waziri Simba, akamwambia, “mama, huyu kijana ninaye hapa. Ungeongea naye ili akubali kulegeza msimamo, au umpigie mwanao Jakaya anipigie, pengine atabadili msimamo wake kama tulivyokuwa tumekubaliana awali.”

Kihawa anadai kuwa mtu huyo aliyedaiwa kuwa Waziri Simba alimjibu Shibuda kuwa asingeweza kuzungumza yeye kwa kuwa alikuwa hajisikii vema, ila kwa suala la kuongea na Rais Kikwete, atafutwe Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba, ili awaunganishe Shibuda na rais.

Kwa mujibu wa Kihawa, baada ya kupewa ushauri huo, Shibuda alijibu: “Mwigulu ni mropokaji, hawezi kuingizwa katika mkakati huu; na Kinana ni mgumu kuingilika katika suala hili.”

Anasema alisikia mazungumzo yao kwenye loud speaker ya simu ya Shibuda, na baada ya kukata simu Shibuda alimwambia kuwa alikuwa anazungumza na Simba, ambaye alidai ni ‘mama mdogo wa Kikwete.’

Kihawa anasema wakati anahojiwa hayo hapo hotelini, maofisa wa polisi walisimama kwa mbali wakimsubiri.

Wengine waliokuwapo wakishuhudia mahojiano hayo ni Meya wa Ilemela, Henry Matata na aliyekuwa Diwani wa Igoma, Adam Chagulani. Matata na Chagulani walishavuliwa uanachama na CHADEMA.

Wahusika walipohojiwa na Tanzania Daima jana, kila mmoja alikuwa na kauli yake kama ifuatavyo:

Tanzania Daima Jumapili: Afande Nyombi, vijana waliokuwa wametuhumiwa kwa kesi ya ugaidi kule Tabora, wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa ukiwalazimisha wawataje viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?

Advocate Nyombi: Mimi si msemaji wa Jeshi la Polisi, siwezi kusema chochote.

Tanzania Daima Jumapili: Msemaji atajuaje kama mliwatesa watu wakati wa mahojiano? Mbona huku ni kumwonea msemaji wa Jeshi la Polisi kusemea kila kitu hata mambo ambayo askari fulani ametenda kwa utashi wake?

Advocate Nyombi: Nimekwambia mtafute, msemaji katika hayo yote. Mimi siwezi kuongelea suala hilo, nakutakia Idd Mubaraka njema.

Tanzania Daima Jumapili: Afande Pasua, vijana waliotuhumiwa katika kesi ya ugaidi kule Tabora wamekutaja wewe kuwa ulishiriki kuwatesa, ukiwalazimisha wataje viongozi wa CHADEMA kuwa walishiriki kutenda ugaidi na utekaji. Unatoa ufafanuzi gani?

Afande Pasua: Kwani wewe uko wapi?

Tanzania Daima Jumapili: Nipo Dar es Salaam, hapa ofisini.

Afande Pasua: Njoo ofisini tuongee tuyaweke sawa unayouliza. Umesema unatoka gazeti gani?

Tanzania Daima Jumapili: Nimekwambia Tanzania Daima.

Afande Pasua: Mashtaka hayo kwanza yalikuwa ya serikali, mimi sifanyi kazi ya kubahatisha, mpigie msemaji wa Jeshi la Polisi mimi si msemaji. Alikata simu.

Henry Matata

Tanzania Daima Jumapili: Mstahiki Meya, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wanadai walihojiwa mbele yako Dodoma. Je, unafahamu nini kuhusu suala hili?

Matata: Kijana Rajab Kihawa ndio namfahamu. Huyu alikuwa mfanyakazi wangu, ila tangu aache kufanya kazi hapa sijaonana naye. Lakini mimi nina ugomvi na wafanyakazi wote wa gazeti lenu na gazeti lenu. Nisingependa kuongea na nyie. Tangu nifukuzwe CHADEMA gazeti lenu linaongeza chumvi habari zinazonihusu. Mimi si meya kwa kura za CHADEMA. CHADEMA walinifukuza, CCM wakaona nafaa, wakanipa kura nikawa meya.

Tanzania Daima Jumapili: Ulikutana na Rajab Dodoma hotelini?

Matata: Nimekwambia sitaki kuongea na gazeti lenu.

bi Mheshimiwa, vijana waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi wamekutaja kuwa ulikuwepo wakati wanahojiwa Dodoma. Je, una kauli gani kwa yao hii?

Chagulani: Mimi nilikuwa Dodoma mwezi wa nne lakini nilikuwa Kondoa kwa ajili ya uhamisho wa mke wangu. Hayo unayonieleza siyajui.

Waziri Simba hakupokea simu, na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu lolote.

Msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Senso, alipoulizwa kama jeshi ndilo linawatuma polisi kutesa watu wakati linawahoji, alisema: “Mhalifu asitafute huruma ya jamii kwa kuzushia jeshi kwa uhalifu alioutenda yeye, na endapo ikibainika anasingizia uongo na hilo ni kosa pia, kwani Jeshi la Polisi linafuata taratibu za sheria.”

Shibuda alipoulizwa jinsi alivyohusika katika sakata hilo alisema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa alikuwa Agha Khan Hospitali akihangaikia mgonjwa wake.

“Niacheni kwa sasa kwa kuwa nahitaji utulivu wa akili niweze kushughulikia afya ya mgonjwa wangu. Nadhani hata kama ni wewe sijui katika mazingira kama haya ungeweza kweli kuongea?” alisema.

Msemaji wa Ikulu, Salva Rweyemamu, alipopigiwa simu kuulizwa ikiwa wanayo taarifa ya watu wanaotumia vibaya jina la rais katika matukio ya kihalifu aliomba jambo lolote linalohusiana na kazi, lisubiri kwa kuwa alikuwa katika mapumziko ya sikukuu.

“Ndugu yangu, unajua leo ni sikukuu na ni usiku, nitafute wakati mwingine, maana siwezi kuzungumzia mambo ya watu wa CHADEMA muda huu. Niache nipumzike kidogo halafu tuwasiliane siku ya kazi,” alisema

Source:Mtanzania Daima

WALIMU WALIOMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR WARUDISHWA UINGEREZA...VYOMBA VYA HABARI UINGEREZA VYALAANI VIKALI

Baba wa mmoja wa wasichana wa Uingereza wajeruhiwa vibaya katika shambulio la tindikali mjini Zanzibar amefichua majeraha ya binti yake huyo kwamba 'ya kutisha mno' na 'kuliko inavyodhaniwa'.

Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye miaka 18, waliwasili nchini Uingereza jana mchana pale ndege ilipotua kwenye Uwanja wa RAF Northolt. Haraka wakasafirishwa kwenda hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa, huku wakisindikizwa na jamaa zao.

Baba wa Katie, Jeremy Gee, alielezea machungu ya familia hiyo baada ya picha ya kwanza ya majeraha hayo ya moto yaliyompata mmoja wa wasichana hao kuwekwa hadharani.

Alisema: "Picha hizo nilizoziona hakika ni za kutisha mno.

"Kiwango cha kuungua ni zaidi ya unavyoweza kudhani."


Wasichana hao wote wa Uingereza wamepata majeraha makubwa ya moto pale tindikali ilivyomwagwa kwenye nyuso zao wakati wakitembea kwenda kwenye mgahawa mmoja katika kisiwa chenye waumini wengi wa Kiislamu cha Zanzibar.

Lilikuwa shambulio la tatu kwao katika kipindi walichokaa kwenye kisiwa hicho.

Polisi wamebainisha kwamba watuhumiwa watano walikamatwa juzi Alhamisi na mapema jana asubuhi kwenye eneo la Mji Mkongwe, ambako Kirstie Trup na Katie Gee walishambuliwa, ofisa wa ngazi ya juu alieleza.

Na donge nono la Pauni za Uingereza 4,000 limetangazwa na polisi Zanzibar kwa yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa shambulio hilo, kwa mujibu wa BBC.

Polisi pia imetoa hati ya kukamatwa kwa Mhubiri wa Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, kwa hisia kwamba mafundisho yake yanaweza kuwa yanachochea mashambulio ya tindikali.

Marafiki wa wasichana hao wamehisi huenda walishambuliwa kwakuwa ni Wayahudi, na polisi wa kisiwani humo walisema wanataka kuzungumza na mhubiri huyo wa Kiislamu ambaye anawezekana kuwa alichochea shambulio hilo.


Wakiwasili ndani ya gari aina ya Audi jeusi kwenye uwanja wa ndege wa jeshi jana asubuhi mama wa Katie aliyeguswa mno, Nicky aliweka bayana mateso ya familia hiyo.

Akizungumza wakati wakikaribia kuingiwa uwanjani hapo alisema: "Nimejawa na hofu. Imekuwa mateso makubwa kwa familia zetu. Ninafurahi kwamba amerejea nyumbani. Ninataka kuingia ndani na kumwona.

"Tulizungumza asubuhi hii na alisema yuko salama. Sifahamu kabisa kinachoendelea.

"Siwezi kusema zaidi sababu tunatakiwa kuingia ndani na kuwaona wote."

Wafanyakazi wawili kutoka magari ya wagonjwa ya St John waliwasili kwenye makao makuu ya jeshi ya Middlesex, ambako pia hupokea ndege binafsi, majira ya Saa 4 asubuhi jana.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa