Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label msanii. Show all posts
Showing posts with label msanii. Show all posts

"NEY WA MITEGO HAPA HATOSAHAHU"-NISHA

Salma Jabu ‘Nisha’ amesema hata kama msanii Nay wa Mitego akiwa na mpenzi mwigine kwa sasa lakini anajivunia kupendwa na kijana huyo kwani alihangaika sana kumpata.
Akizungumza na paparazi wetu, Nisha alisema Nay alimfuatilia kwa kipindi kirefu na alimzungusha kama miaka miwili kabla hata hajawa staa.
“Nikivuta ile picha ya kumdengulia kiasi kile mpaka kuamua kumkubali, naamini alinipenda tu na hata kama hakunipenda lakini najivunia kwamba alihangaika kunipata,” alisema Nisha.
Wawili hao walidumu katika uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana na kila mmoja akichukua ‘hamsini zake’.

HUWEZI AMINI-HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MCHEZAJI MRISHO NGASA ,JIONEE MWENYEWE HAPA

Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza  kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga  vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu  zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari  nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado anategemea soka kama ajira yake, Ngassa amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada ya soka na katika mahojiano  wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.
    SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia  maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa
 kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa amerejea Jangwani,
 

                                         Ngassa akia na bibi na babu
                                          Ngassa katika kaburi la shangazi yake                                                        Ngassa na watoto wake

“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya
shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”. Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.    “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”. “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za >kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, hapo nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  biashara kubwa,”anasema Ngassa. 
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.  
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu
Nyumba nyingine ya Mwanza


Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,  ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana
 na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na
kutolewa CHAN.  Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoj uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa. Gari la Ngassa la MwanzaGari lingine la Ngassa

Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa  kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.  Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana  mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska nyota Tanzania.

"STRESS ZA MUZIKI ZINATUFANYA TUNYWE POMBE, TUVUTE BANGI NA MADAWA YA KULEVYA" -DUDU BAYA

“Mimi sina stress na game, kwanza mimi nina jina kubwa sana nina makampuni ya mbao Mambas Timber, huko mwanza, Mambas Entertainment na hii Mambas Pub nasonga mbele na maisha. Kwahiyo ningekuwa na stress ningekuwa kama hawa wasanii wenye stress ambao wanakunywa pombe, bangi na mwishowe wanakula madawa, unatakiwa uongee na Mungu akupe matumaini,” ameiambia Bongo5.
Amesema pia kuwa yeye ni professional kwenye uchoraji ramani za majengo na fundi.
“Nimejenga majumba mengi kwhaiyo nafanya mengi naweza kuwaajili baadhi ya wasanii ambao wamechoka na maisha.”

“Mimi sina stress na game, kwanza mimi nina jina kubwa sana nina makampuni ya mbao Mambas Timber, huko mwanza, Mambas Entertainment na hii Mambas Pub nasonga mbele na maisha. Kwahiyo ningekuwa na stress ningekuwa kama hawa wasanii wenye stress ambao wanakunywa pombe, bangi na mwishowe wanakula madawa, unatakiwa uongee na Mungu akupe matumaini,” ameiambia Bongo5.
Amesema pia kuwa yeye ni professional kwenye uchoraji ramani za majengo na fundi.
“Nimejenga majumba mengi kwhaiyo nafanya mengi naweza kuwaajili baadhi ya wasanii ambao wamechoka na maisha.”
- See more at: http://www.thechoicetz.com/2013/08/dudu-baya-stress-za-game-zinatufanya.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29#sthash.ENm9PwYU.dpuf
“Mimi sina stress na game, kwanza mimi nina jina kubwa sana nina makampuni ya mbao Mambas Timber, huko mwanza, Mambas Entertainment na hii Mambas Pub nasonga mbele na maisha. Kwahiyo ningekuwa na stress ningekuwa kama hawa wasanii wenye stress ambao wanakunywa pombe, bangi na mwishowe wanakula madawa, unatakiwa uongee na Mungu akupe matumaini,” ameiambia Bongo5.
Amesema pia kuwa yeye ni professional kwenye uchoraji ramani za majengo na fundi.
“Nimejenga majumba mengi kwhaiyo nafanya mengi naweza kuwaajili baadhi ya wasanii ambao wamechoka na maisha.”
- See more at: http://www.thechoicetz.com/2013/08/dudu-baya-stress-za-game-zinatufanya.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29#sthash.ENm9PwYU.dpuf
es Salaam wakidai kuwa hawataki Klabu ya British Legion of Tanganyika kuendesha shughuli zao katika eneo wanalodai ni lao kwa madai ya kuwepo kwa picha chafu na ulevi, sakata hilo limeibua mapya baada ya maaskofu kudai kuwa wamekashifiwa.



Baadhi ya picha za ufuska zilizopo katika klabu iliyopo ndani ya eneo la kanisa.

Maaskofu wa kanisa hilo, wamedai kukashifiwa na kudhalilishwa na Mwenyekiti wa Klabu, Abdul Mtiro Sisco kutokana na kiongozi huyo kuwaambia waandishi wa habari kuwa eneo la klabu yao linataka kuuzwa na kanisa kutokana na dhiki waliyonayo Wagiriki.

Mtiro alidai kwa waandishi wa habari kuwa kutokana na matatizo ya kiuchumi nchini kwao, Wagiriki hao wanataka kuliuza eneo hilo ili wapeleke fedha kwao.



Mwenyekiti wa Klabu, Abdul Mtiro Sisco.

“Wanadai kuwa hapa sisi tunafanya uhuni wakati watu wanaokuja hapa si wahuni…Hawa Wagiriki kwa sababu ya matatizo ya uchumi nchini kwao, wanataka kuuza eneo hili ili wawapelekee fedha ndugu zao…” alidai Mtiro.

Mtiro alidai klabu yao ipo hapo tangu mwaka 1970 kama British Legion of Tanganyika ambapo awali ilikuwa ni ya wanajeshi wa Uingereza lakini baadaye Waafrika wakaingia lakini ugomvi wao ulianza mwaka 1990 walipoambiwa watoke eneo hilo.

Kuhusu madai ya kuwepo picha za utupu ndani ya klabu hiyo, Mtiro alisema si kweli, hata hivyo, akasema kwamba hiyo ni klabu binafsi.

Habari zinasema kauli hiyo imewaudhi maaskofu wa kanisa hilo na kuwafanya kuwasiliana na wanasheria wao ili kuona jinsi ya kushughulikia hicho wanachodai kuwa ni kashfa kwao.




Baadhi ya viongozi wa kanisa.

Askofu mmoja wa kanisa hilo amesema hawakubaliani na madai ya Mtiro kwa sababu ndani ya klabu hiyo kulikuwa na picha za utupu na wanafanya biashara ya pombe eneo la kanisa.“Lengo letu sisi ni kuwafundisha watu wamfuate Mungu waende Mbinguni na tunaomba maeneo yote ya kanisa yaheshimiwe,” alisema askofu mmoja.

Wakati hayo yakiendelea, sakata la kugombea eneo hilo tayari limefikishwa Mahakama Kuu chini ya Jaji John Mgetta ambapo upande wa kanisa, Wakili Edward Chuwa amedai kuwa wamezuia kuingia wanachama wa klabu hiyo kwa sababu hawawajui na hakuna mahali panapoonesha wanachama ni akina nani.

Upande wa klabu ukiongozwa na Wakili Evod Mmanda katika kesi hiyo namba 178/2013, wamedai mbele ya jaji huyo kuwa kanisa lisiwepo katika eneo hilo na wanachama waruhusiwe kuingia katika klabu yao wakati shauri likiendelea kusikilizwa mpaka hapo mahakama itakapotoa uamuzi.

Jaji Mgetta alitembelea eneo hilo Jumanne iliyopita na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Agosti 21, mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza pingamizi lililowekwa na kanisa

Via GPL
- See more at: http://www.thechoicetz.com/2013/08/mapya-yaibuka-kuhusu-sakata-la-picha-za.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29#sthash.FEk6JC9U.dpuf

"NIMEKOMA SIVAI TENA HERENI MASIKIONI"-HEMEDI

Kutokana na kusikikia malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki, Hemedy ameamua kuwa mpole na kufuata kile watakacho.
“Kumekuwa na fight kubwa sana kati ya mimi na director wangu pale ninapokuwa na scene za ofisini nakuwa mbishi sana swala kuvaa hereni sasa nimepata ushauri kutoka kwa mashabiki wangu nimeona nikamshauri director wangu kuepuka kero ambazo hawazipendi mashabiki wangu. Nitakuwa mjinga nisipo wasikiliza mashabiki wangu,” PHD aliiambia Enewz ya EATV.

MONALISA AGOMA KUOLEWA TENA BAADA YA NDOA YAKE YA 5 KUVUNJIKA

Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....
Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....
"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?
"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa

ROSE NDAUKA LAIVU AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI

Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
 
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...
  Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui.

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...

"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho

-Habari  kwa  hisani ya KIU

VIDEO YA MABESTE NA LISA WAKIMTAMBULISHA MTOTO WAO "KENDRICK"

Hii ni video inayomuonesha rapper Mabeste akiwa na mchumba wake Lisa wakiongea kwa mara ya kwanza baada ya kupata mtoto wao wa kwanza jana, Kendrick. Kwenye video hii, Mabeste anasema wamempa jina hilo mtoto wao kwakuwa mama yake (Mabeste) anampenda sana rapper wa Marekani, Kendrick Lamar.



MSANII WA BONGO MOVIE "NATASHA" AOLEWA LEO JIJINI DAR...PICHA ZA MAANDALIZI


 
  Natasha akiwa  anawekwa gauni vizuri na mpambaji wa saluni ya Partners.
 
  Natasha akijiangalia kama yuko sawa.
  …Akitengenezwa vizuri na mtaalamu wa nywele kwenye saluni hiyo.
 
  …Akiendelea kupambwa vizuri.
 
  …Akiwa na mpambe wake Neema wakiwekwa vizuri.
 
  …Akiwa amepozi katika saluni hiyo.
 
  … Akiwa katika picha ya pozi na mpambe wake.
Muigizaji mkongwe wa tansia ya filamu hapa Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ leo hii amefunga ndoa  kwenye Kanisa la Mtakatifu  Joseph lilipo Posta jijini Dar na mume wake Alex Humbila .
Kabla ya kutinga kanisa kamera yetu ilimnasa Natasha katika suluni moja maarufu kwa kupamba mastaa mbalimbali hapa Bongo , Partners Wedding iliyopo Sinza  Mori akiwa anaandaliwa kwaajili ya kwenda kanisani. Kufunga ndoa

NYOTA YA ELIZABETH MICHAEL "LULU" YAANZA KUNG'AA ......SASA ACHUKUA TUZO YA MUIGIZAJI BORA WA KIKE


Zanzibar Filim Festival bado inaendelea na msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amejikuta mwenye furaha tele baada ya kushinda tuzo ya Best Actress in Swahili Film kupita movie ya Woman of Principles ya RJ Company. Movie hiyo ambayo imeigizwa na Ray,Nagris Mohamed na Lulu mwenyewe, ilifanya vizuri mwaka jana na ni ilipata nafasi ya kuingia kwenye tuzo hizi za ZIFF. ZIFF ni tamasha kubwa sana  Africa nzima huku likiwa kutanisha wadau mabalimbali wa filamu, inaonekana hii itakuwa ni kick ya Lulu kufunguka kimataifa zaidi baada ya kupata platform kama hii.
lulu
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa