Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

PICHA MBALIMBALI ZA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA WALIOZIMIA UWANJANI

Shabiki mwananke wa Yanga akitolewa kwenda kupata huduma ya kwanza baada ya kuzimia alipokuwa akishagilia bao la pili dhidi ya watani wao wa jadi Simba katika mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3.



 Shabiki mwingine wa Yanga akiwa amezimia








 Wapenzi wa Yanga wakishangilioa


 Kikosi cha Yanga kilichopepetana na Simba


 Kikosi cha Simba kilichocheza na Yanga


 Yanga wakishangilia ushindi


 Shabiki wa Simba akiwa amezimia


NYUMBA ZA MCHEZAJI MRISHO NGASA ZANUSURIKA KUCHOMWA MOTO

Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa alikuwa amesema kuwa asipofunga goli ama kutoa pasi itakayo zaa goli zidi ya simba mechi ya jana basi angechoma moto nyumba zake tano .....Lakini simesalimika baada ya  kuwa mfungaji wa goli kati ya magoli matatu waliyo pata yanga .......Mechi hiyo simba na yanga walitoka droo ya 3-3

MWENYEKITI WA SHINDANO LA MISS UTALII "CHIPUNGAHELO" APEWA ONYO KALI KWA KUWADHALILISHA WASHIRIKI WA KIKE...

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limempa karipio kali Mwenyekiti wa shindano la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo(Pichani juu) kwa kosa la kudhalilisha baadhi ya washiriki na malalamiko kufanyiwa kazi na Baraza hilo.
                 
 


Karipio hilo lilitolewa baada ya Basata kupitia tathmini iliyohusisha vipande vya matukio yaliyorekodiwa (clips) na kujionea namna wasichana wanavyofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na Chipungahelo kwa kipindi cha kambi ya miezi mitatu.Katika hafla ya upitiaji wa clips hizo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Basata, Ilala, jijini Dar es Salaam mbele ya Chipungahelo, ilionekana wazi wasichana kukosa uangalizi walipokuwa kambini, hivyo kuwepo kwa matukio mbalimbali yasiyofaa.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa kitengo cha Sanaa wa Basata, Nsao Shaluwa alisema baada ya kupata malalamiko kuwa wasichana wanafanyiwa mambo yasiyofaa wakiwa kambini, waliamua kuutafuta ukweli na kujiridhisha shindano hilo lina ukakasi mwingi.

Alisema baada ya kukusanya baadhi ya matukio katika kuthibitisha hali halisi iliyopo kwenye shindanohilo, watapeleka vielelezo kwa Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana Michezo na Utamaduni ili Chipungahelo ajadiliwe kwa kosa la kudhalilisha warembo wa shindano hilo.Alisema kwa kukosa matroni, yaelezwa warembo walikuwa wakizurula kutwa nzima hadi usiku kwenye gari huku kukiwa hakuna ratiba ya chakula ya kueleweka huku wakifanyishwa mazoezi muda mrefu.

Mbali ya muda mrefu kuanzia saa 2 usiku hadi 9, pia walikuwa wakivaa viatu virefu, hivyo miguu kuvimba na wakati mwingine walikuwa wakichapwa makofi na kulazimishwa mapenzi.Aidha, Chipungahelo anakabiliwa na shutuma ya kuwaweka mabini washiriki kwa muda wa miezi mitatu tofauti na alivyoeleza Basata kuwa kambi ni ya wiki tatu.

Zaidi ya hapo, Chipungahelo alishindwa kutoa zawadi kwa washindi wala kifuta jasho kwa washiriki wengine huku mshindi wa mwaka 2013, akidaiwa kubebwa kwa hila.Shaluwa alisema baada ya malalamiko hayo kufikishwa kwao, waliamua kunyatia katika kambi yake iliyokuwa na warembo saba ambayo pia Chipungahelo aliwaficha.

Baada ya kuwahoji washiriki, walikiri kwamba walikuwa wakilala warembo saba, wengine watano katika chumba kimoja na wengine wakilala chini huku wakila mlo mmoja tena katika muda usiofaa.“Warembo wengi wamekiri walikuwa wakifanyishwa mazoezi kwa muda mrefu huku wakiwa wamevaa viatu virefu,“Tulikuwa tukifanyishwa mazoezi kuanzia saa mbili usiku hadi saa tisa, tuna njaa na tulipolalamika, baba alitutukana matuzi ya nguoni na kukashifu tupu zetu” mmoja wsa warembo alisema katika CD ya Basata.

Shaluwa anasema walipofika Ikondolelo ambako kulikuwa na kambi ya awali, walizungumza na warembo hao, lakini wakishindwa kusema ukweli mbele ya Chipungahelo.Alisema walipowapa karatasi kuandika kero zao, kila mtu aliandika jina na kusaini ambapo walieleza mengi yaliyorekodiwa na wadau kuoneshwa mwishoni mwa wiki mbele ya mwanasheria Ashura Mzava kutoka TAWLA.

Mzava alisema wazi kwa madudu yaliyopo kwenye shindano hilo, Chipungahelo anapaswa kushtakiwa kwa udhalilishaji.Kashfa nyingine ni kitendo cha Chipungahelo kutumia kiasi cha sh 200,000 ambazo zilitolewa na Mkuu wa Wilaya Tanga Mjini, Halima Dendego ili washiriki waende saloon kabla ya fainali.



“Baba ametunyanyasa sana hadi, ametumia pesa tuliyopewa na mama Halima Dendego, lakini hapohapo amekuwa akimpendelea mshiriki mwenzetu (jina tunalo), kwa vile alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi,” alisema mmoja wa washiriki na kuongeza:“Hata siku ile ya fainali, alipokuja mpambaji kutoka Sofia Record, alimuita na kumvalisha nguo nzuri pamoja na kumpamba tofauti na alivyovalisha washiriki wengine” wamesema washiriki hao.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi wa Sanaa kutoka Wizarani, Leah Kihimbi alisema atalifikisha kwa usahihi suala hilo katika ngazi ya juu akimtaka Chipungahelo ajitayarishe kwa maamuzi yoyote.Mshiriki pekee wa Miss Utalii 2013 aliyefika kwenye tahmini hiyo, ni Glory John aliyesema wazi shutuma zote zilizoelezwa na wenzake dhidi ya Cipungahelo ni kweli.

“Tulipokuwa tunakwenda Mikumi , tulilala Morogoro, Baba (Chipungahelo) aliniita akaniambia nipande juu katika chumba kimojawapo, nilipokwenda na kufungua mlango, nikakutana na moshi wa ajabu nikashindwa kuvumilia nikatoka.Akanifuata akinitaka nirudi chmbani mle, nikagoma, nilipowaeleza wenzangu, walinieleza nilielekea kunaswa kwenye mtego wake,” alisema Glory.

Naye Katibu Mtendaji BASATA Godfrey Mngereza alisema, hilo ni suala nyeti linalogusa jinsia ya kike, hivyo ni hatari kwa ustawi wa jamii.Kupitia tathmini hiyo ya aina yake, Basata itachunguza mazingira ya ushindi wa Miss Utalii mwaka 2013, ikibainika hakustahili, atavuliwa taji hilo ili iwe fundisho.

“Tabia hizi chafu zinatuchafua hata sisi BASATA tunaonekana hatufanyi kazi sasa ndio tutaanza na Miss Utalii na ikibidi kusiwe na shindano la aina yeyote kama mambo yenyewe ni kudhalilishana,” alisema Mngereza.Wadau wengine waliohudhuria tathmini hiyo ni kutoka TAMWA, TAWLA,TGNP,THAWE, Polisi Jamii, Polisi kutoka kituo cha Pangani Ilala, Dar es Salaam, Shirikisho la Sanaa na Ufundi, Binti Leo na wengineo.
Shaluwa alisema suala hilo litapelekwa ngazi za juu na vielelezo kuonesha wasichana wakieleza yanayotokea kambini pamoja na maoni ya wadau yaliyorekodiwa.

Akizungumnzia tuhuma dhidi yake, Chipungahelo alisema ni majungu yaliyopikwa na maadui zake ambao walimpandikizia makahaba kwa lengo la kuchafua taswira ya shindano hilo ili kummaliza, lakini aliomba radhi kwa dosari na mapungufu yaliyojitokeza na kuahidi kuwa hazitajirudia tena.
 

-MichuziBlog

MRISHO NGASSA WIKI IJAYO ANAOA MKE WA 5 KWA SIRI KUBWA NI BAADA YA KUCHANGIWA PESA YA KUWALIPA SIMBA


Mchezaji nyota aliyekuwa kwenye kifungo cha kutocheza mechi sita kisha kulipa faini ya shilingi milioni 45 kwa timu aliyokuwa anaichezea awali ya simba siku za hivi karibuni alitangaza kuwa mshabiki wake na wadau wamchangie pesa kwa ajili ya kufidia pesa aliyolipishwa na club ya simba ambayo kwa mujibu wa ngasa kuwa pesa hiyo ilitoka mfukoni mwake lakini kumbe wiki ijayo anaoa mke mwingine na kufuatiwa na bonge la sherehe.

Habari za uhakika zilizofika mezani  na kufanyiwa upepelezi wa hali ya juu zilisema kuwa mchezaji huyo sasa hivi yuko kwenye vikao cha siri kwa ajili yaa maandalizi ya kuoa msichana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la  Rebeka ambae alikuwa chuo cha CBE Mwanza.


Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa msichana huyo ameachishwa chuo na Ngasa na sasa hivi anaishi hapa mjini Dar na huenda wiki hii au ijayo wakafunga ndo” Habari ndo hiyo Ngasa anaoa lakini tukio hili analifanywa kwa siri kubwa sana hataki mtu yeyote ajue hata timu yake hapendi wafahamnu na ndio maana anafanya kwa siri kubwa” Alisema dada huyo
Ngasa ambae inadaiwa sasa hivi amekuwa akishikiria rekodi ya kufungua ndoa nyingi kuliko mchezaji yeyote na huyu mke wake huenda akawa wa wanne na hao ni wale wanaotambuana lakini inadaiwa bado kuna wengine pembeni ambao mchezaji huyo amewaongezea idadi.


Hata hivyo papalazi  alifanya juhudi za kumtafuta Ngasa kupitia simu yakeya kiganjani lakini kwa bahati mbaya lakini hata hivyo blog hii inawaahidi wasomaji wetu kuwa tutahakikisha tunazama kwenye sherehe hiyo hata kama ikifanywa kwa siri na tutaweletea picha za tukio zima zenye ushahidi wote.


source: Xdjayz

MTOTO WA NIYONZIMA AANGUKA SEBULENI NA KUFARIKI DUNIA WAKATI NYUMBA IKIUNGUA MOTO


               KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amepata msiba mkubwa baada ya mwanaye kuanguka na kufariki dunia wakati akicheza na wenzake.
Mtoto huyo wa Niyonzima, Akbar aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu, alianguka ghafla na kufariki dunia wakati akicheza na wenzake jijini Kampala, Uganda, mwanzoni mwa wiki hii.
“Mtoto wa Haruna ameanguka na kufariki dunia kule Uganda,” mtoa habari kutoka Kigali, Rwanda alilipasha Championi Ijumaa.
Gazeti hili liliamua kufuatilia ili kupata uhakika kuhusiana na tukio hilo na lilifika nyumbani kwa mchezaji huyo jijini Dar es Salaam na kumkuta mwanaye mwingine, Ramzey na mkewe.
Niyonzima raia wa Rwanda, alionekana kutopenda kulizungumzia kwa undani suala hilo.
“Ni kweli nimepata msiba wa mwanangu lakini nimekuwa na matatizo mengi yanayoniandama hadi nachanganyikiwa kwa kweli. Ningependa mniache kidogo,” alisema kiungo huyo kwa sauti ya taratibu.
Kweli Niyonzima ameandamwa na majanga kwa kuwa jana aliunguliwa na nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Magomeni Makuti jijini Dar.
Hivyo, gazeti hili likaendelea kufanya uchunguzi zaidi na kugundua mtoto huyo wa Niyonzima alikuwa akiishi na mama yake nchini Uganda.
“Tayari Haruna amempa nauli mdogo wake akashughulikie masuala ya msiba, yeye alikuwa na majukumu mengine lakini pia kama unavyoona, nyumba yake imeungua,” kilieleza chanzo kingine na kuendelea:
“Yule mtoto awali alikuwa Kigali lakini baadaye akahamia Kampala baada ya mama yake kupata kazi huko Uganda na walikuwa wakiishi huko.”
Niyonzima anaishi Magomeni Makuti jijini Dar pamoja mkewe na mwanaye Ramzey mwenye miaka takribani mitano.
Awali kulikuwa na taarifa za kuchanganya baada ya kusikika kuwa amepata msiba wa mwanaye, lakini ukweli si yule anayeishi naye jijini Dar ambaye anajulikana kwa rafiki zake na kwa mashabiki wengi wa soka nchini

Nyumba ya mchezaji wa yanga "Niyonzima" yaungua moto Dar

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima, amepatwa na tatizo kubwa baada ya nyumba yake kuungua moto jana asubuhi.
Niyonzima ambaye ni raia wa Rwanda, amejikuta katika wakati mgumu baada ya nyumba yake hiyo iliyopo eneo la Magomeni Makuti jijini Dar kuwaka moto ambao ulianza majira ya saa moja asubuhi na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwa sebuleni.
Mara baada ya kupata taarifa hizo, Championi Ijumaa lilifika katika eneo la tukio na kumkuta Niyonzima akiwa na majirani zake na mkewe, Nailah, wakiwa katika hali ya majonzi huku vitu ambavyo viliteketea na moto yakiwemo masofa, televisheni aina ya ‘flat screen’ vikiwa nje, vikionekana havitaweza kutumika tena kutokana na kuathiriwa na moto kwa asilimia 90.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Niyonzima alisema wakati moto huo ukianza, hakuwa anajua lolote, ambapo majirani zake ndiyo walioanza kuuona na kuamua kumuamsha, lakini tayari ulikuwa umeshateketeza karibu vitu vyote vilivyokuwa sebuleni, zikiwemo kompyuta zake mbili za ‘laptop’, ingawa walifanikiwa kuudhibiti kwa kutoingia katika vyumba vingine.
“Sebuleni hakuna tulichofanikiwa kuokoa, kila kitu kimeteketea na moto, kama mngekuta wakati unawaka, palikuwa hapapitiki kutokana na moto mkubwa ulioambatana na moshi mwingi, nashukuru hakuna aliyeumia zaidi ya hivi vitu vilivyoteketea.
“Nawashukuru sana majirani zangu, leo nimejua umuhimu wa kuishi vizuri na watu, niseme ukweli wamenisaidia sana katika kuudhibiti moto, kama isingekuwa wao, nisingeweza kufanya hivyo nikiwa mimi na mke wangu peke yetu, moto ulikuwa mkubwa sana,” alisema Niyonzima.
Aliongeza kuwa, bado hajajua hasara iliyopatikana na moto huo, ambapo sasa wanatafuta chanzo cha tatizo hilo, ingawa kwa haraka hali inaonyesha ni kutokana na hitilafu ya umeme.
-GLOBAL PUBLISHERS

RASHID MATUMLA AZUNGUMZA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI MDOGO WAKE KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ETHIPIA

 
Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake, Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.
“Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine,” alisema Matumla jana katika mahojiano na gazeti hili.Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na  maradhi alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla.
Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka.
“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
SOURCE: MWANANCHI

MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA "JOSEPH KANIKI" AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ETHIOPIA


Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya. 

Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
 

Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
 

Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
 

Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
 

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
 

Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu. 

Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
 

Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
 

“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.
 

“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda. 

“Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe.

 "Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
 

“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
 
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi

“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. 

"Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.
 

Shelukindo alisema wachezaji hao wapo mahabusu kwenye Kituo cha Polisi cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (Federal Police Crime Investigation) na hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa wamevaa.
 

Watanzania wengine kuachiwa leo

Shelukindo alisema kuna Watanzania wanne wanaotazamiwa kuachia leo baada ya kumaliza vifungo vyao baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
 

“Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya nyuma wao walikuwa wamemeza wakapasuliwa dawa zikatolewa na baadhi yao walifariki. Hata hivyo, wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka minne wanaweza kurudishwa Tanzania,” alisema Shelukindo.

-Mwananchi

UNYUMBA NDIO CHANZO CHA FRANCIS CHEKA KUMSHINDA BONDIA MMAREKANI


SIRI ya ushindi alioupata bondia maarufu nchini, Francis Cheka ‘SMG’ dhidi ya Mmarekani Phil Williams imefichuka baada ya mke wa bondia huyo kutoka Morogoro, Tosha Azenga kutoa la moyoni.
 
 Francis Cheka ‘SMG’ akiwa na mkewe Tosha Azenga.
Akizungumza katika mapokezi ya mumewe mwishoni mwa wiki iliyopita alipowasili mkoani hapa, Tosha alisema mumewe amekuwa akifanya vizuri kutokana na ukweli kwamba kila anapokaribia pambano huwa anamnyima unyumba.
“Siri ya mafanikio ya mume wangu ni kufanya mazoezi sana na zaidi ya yote anapokuwa na mchezo huwa simpi tendo la ndoa ambalo ni sumu kali ya mazoezi.
“Kwa mfano, gemu la juzi na yule Mmarekani, siku chache kabla sikumpa kabisa tendo la ndoa na yeye anakubaliana na mimi kwani anajua nafanya hivyo kwa nia njema, faida yake mmeiona,” alisema Tosha aliyemzalia Cheka mtoto mmoja wa kiume aitwaye Historia.

Tosha Azenga akiwa na mkanda wa mumewe.
Ushuhuda wa mwanamke huyo ulipongezwa na baadhi ya wadau hasa wanaojua madhara ya kufanya mazoezi sana kisha kuendekeza ngono kwani ni vitu viwili visivyochanganyika.
“Anachofanya ni sawa, huwezi kuwa unafanya mazoezi ya mpira au ngumi kisha ukitoka hapo unaenda kufanya mapenzi, wanaoendekeza hivyo ndiyo hao unasikia leo kafanya vizuri kesho kavurunda,” alisema Hassan Tolu wa Kihonda.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro aliyekuwepo kwenye mapokezi ya Cheka, Mhe. Saidi Amanzi alimpongeza ‘Mrs Cheka’ kwa uamuzi wake ambao umesababisha bondia huyo apeleke heshima nyumbani.
“Tumpongeze kwanza Cheka kwani licha ya yeye kuwa bondia na kuwachapa watu kila kukicha lakini muangalieni mkewe, hana alama yoyoye ya kichapo kwenye uso wake.
 
 Francis Cheka wakati akiwasili Morogoro baada ya kumtwanga Phil Williams kutoka Marekani.
“Pia nimpongeze mama huyu kwani alidai kwamba mumewe anapokuwa na pambano huwa hamgusi kabisa,” alisema mheshimiwa huyo na kushangiliwa na umati uliofurika kwenye mapokezi hayo.
Usiku wa Agosti 30, mwaka huu Cheka aliandika historia kama lilivyo jina la mwanaye kwa kumtwanga kwa pointi bondia Phil Williams kutoka Marekani na kutwaa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi la Dunia uzani wa Super Middle.
 

HUWEZI AMINI-HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MCHEZAJI MRISHO NGASA ,JIONEE MWENYEWE HAPA

Hakuna maslahi makubwa aliyopata Bukoba, zaidi alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza  kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga  vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu  zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari  nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado anategemea soka kama ajira yake, Ngassa amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada ya soka na katika mahojiano  wiki hii anasema anafanya biashara ya usafirishaji na kilimo.
    SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia  maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa
 kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa amerejea Jangwani,
 

                                         Ngassa akia na bibi na babu
                                          Ngassa katika kaburi la shangazi yake                                                        Ngassa na watoto wake

“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya
shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”. Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.    “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”. “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za >kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, hapo nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  biashara kubwa,”anasema Ngassa. 
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.  
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu
Nyumba nyingine ya Mwanza


Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,  ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana
 na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na
kutolewa CHAN.  Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoj uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa. Gari la Ngassa la MwanzaGari lingine la Ngassa

Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa  kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.  Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana  mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska nyota Tanzania.

BONDIA MASHUDU AUAWA KWA KISU WAKATI AKIGOMBELEZEA UGOMVI


BONDIA  maarufu Ramadhani Idd ‘Mashudu’ ameuawa kwa kuchomwa visu mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lililowaacha midomo wazi wakazi wa Mabibo Loyola, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam lilitokea saa sita usiku Julai 4, mwaka huu.

Imedaiwa kuwa, marehemu aliwakuta Jack Mchaki na mtu mwingine wakigombana, alipowaamulia wakamgeuzia kibao na kumchoma visu.

Waandishi wetu walifika eneo la tukio na kukutana na mashuhuda waliozungumza kwa sharti la kutoandika majina yao , mmoja alidai marehemu alikuwa anaangalia kanda za filamu katika banda moja maeneo hayo ghafla alifika Jack aliyelewa na kuanza kufanya fujo.

Shuhuda huyo alisema: “Kitendo kile hakikumfurahisha  kijana mwingine, hivyo wakaanza kupigana ndipo Mashudu akawaamua.”

Aliongeza kuwa, baada ya kuamuliwa mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwake akabadili nguo kisha akarudi tena na kumkuta Mashudu akiendelea kuangalia filamu, akaanzisha ugomvi tena na bondia huyo kumbe kiunoni alikuwa na kisu.


Walianza kupigana na baada ya kuona anazidiwa nguvu alichomoa kisu akamchoma Mashudu tumboni, kichwani na kumsababishia kuvuja damu nyingi kisha akatoweka.


Alisema walitafuta usafiri na kumpeleka majeruhi Hospitali ya Palestina Sinza, walipofika madaktari wakawaambia tatizo lake lilikuwa kubwa hivyo apelekwe Hospitali ya Mwananyamala.

“Tulipofika Mwananyamala alipopimwa na daktari Mashudu akathibitika kuwa amekata roho kutokana na kuvuja damu nyingi,” alisema shuhuda huyo.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

PICHA ZA MPAMBANO WA NGUMI WA ESTER BULAYA VS AUNT EZEKIEL

Aunt Ezekiel na Ester Bulaya wakizichapa ulingoni.Mhe. Ester Bulaya ndani ya ulingo.
clip_image002[6]Aunt Ezekiel akijiandaa kabla ya kuanza pambano dhidi ya Mbunge Ester Bulaya.clip_image002[8]Mbunge Ester Bulaya akikwepa ngumi iliyorushwa na Aunt Ezekiel (kushoto).clip_image002[10]Napo hapakupatikana mshindi..iliishia 5-5 kati ya Mbunge Ester Bulaya (kulia) na muigizaji Aunt Ezekiel

WABUNGE WA YANGA WAIFUNGA TIMU YA WABUNGE WA SIMBA KWA PENATI 4-3.....MATUKIO KATIKA PICHA

Mgeni wa rasmi wa tamasha la matumaini Raisi Jakaya Kikwete akiongozana na marefa kuingia uwanjani tayari kukagua timu za wabunge wa Simba na Yanga

Wimbo wa taifa

JK akisalimiana na timu ya wabunge wa Simba

Mgeni rasmi akisalimiana na upande wa wabunge wa Yanga 
Wabunge wa timu ya Yanga wwakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe kwa kuifunga timu ya wabunge wa Simba kwa penati 4-3.

Wabunge wa Yanga wakishangilia ushindi wao.
Yanga wakipokea kombe lao kutoka kwa Shigongo na Waziri Fenella Mukangara.
Eric Shigongo akiwa na kombe kabla ya kuwakabidhi Yanga.
Waziri Fenella Mukangara akimvisha medali refa wa mchezo.

Rais Kikwete akisaini mpira utakaotumika.
...Akiwakagua Yanga.
..Akiwakagua Simba.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Eric Shigongo, Waziri Fenella Mukangara, marefarii na manahodha wa Simba na Yanga.
Vikosi vya Simba na Yanga.
JK akipuliza kipenga.




Wabunge wa Yanga wakishangilia.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa