Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » MTOTO WA NIYONZIMA AANGUKA SEBULENI NA KUFARIKI DUNIA WAKATI NYUMBA IKIUNGUA MOTO

MTOTO WA NIYONZIMA AANGUKA SEBULENI NA KUFARIKI DUNIA WAKATI NYUMBA IKIUNGUA MOTO


               KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amepata msiba mkubwa baada ya mwanaye kuanguka na kufariki dunia wakati akicheza na wenzake.
Mtoto huyo wa Niyonzima, Akbar aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu, alianguka ghafla na kufariki dunia wakati akicheza na wenzake jijini Kampala, Uganda, mwanzoni mwa wiki hii.
“Mtoto wa Haruna ameanguka na kufariki dunia kule Uganda,” mtoa habari kutoka Kigali, Rwanda alilipasha Championi Ijumaa.
Gazeti hili liliamua kufuatilia ili kupata uhakika kuhusiana na tukio hilo na lilifika nyumbani kwa mchezaji huyo jijini Dar es Salaam na kumkuta mwanaye mwingine, Ramzey na mkewe.
Niyonzima raia wa Rwanda, alionekana kutopenda kulizungumzia kwa undani suala hilo.
“Ni kweli nimepata msiba wa mwanangu lakini nimekuwa na matatizo mengi yanayoniandama hadi nachanganyikiwa kwa kweli. Ningependa mniache kidogo,” alisema kiungo huyo kwa sauti ya taratibu.
Kweli Niyonzima ameandamwa na majanga kwa kuwa jana aliunguliwa na nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Magomeni Makuti jijini Dar.
Hivyo, gazeti hili likaendelea kufanya uchunguzi zaidi na kugundua mtoto huyo wa Niyonzima alikuwa akiishi na mama yake nchini Uganda.
“Tayari Haruna amempa nauli mdogo wake akashughulikie masuala ya msiba, yeye alikuwa na majukumu mengine lakini pia kama unavyoona, nyumba yake imeungua,” kilieleza chanzo kingine na kuendelea:
“Yule mtoto awali alikuwa Kigali lakini baadaye akahamia Kampala baada ya mama yake kupata kazi huko Uganda na walikuwa wakiishi huko.”
Niyonzima anaishi Magomeni Makuti jijini Dar pamoja mkewe na mwanaye Ramzey mwenye miaka takribani mitano.
Awali kulikuwa na taarifa za kuchanganya baada ya kusikika kuwa amepata msiba wa mwanaye, lakini ukweli si yule anayeishi naye jijini Dar ambaye anajulikana kwa rafiki zake na kwa mashabiki wengi wa soka nchini
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa