Kama ulikua hujaangalia kipindi cha wema sepetu kinachorushwa EATV ..Basi ambatana nae hapa katika kipindi chake Katika Episode 1,Akielezea undani wa maisha yake juu ya yeye kurogwa,Maisha yake ya Mapenzi na mengineyo mengi.. ANGALIA HAPO CHINI...
Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo kwenye hii picha. Maana ya hii picha ni kwamba watu wengi wanafikiri kwamba muda wote Diamond yupo kwenye kichwa cha Wema, lakini yeye mwenyewe anasema kwamba muda wote anafikiria pesa. Unaionaje hiyo picha?
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa. Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane. “Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.
Mwingine aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji. Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.” Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu. Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha
Habari za chini ya kapeti zilitonya kuwa baada ya kuambiwa na kuoneshwa picha za Diamond akiwa kimahaba na Wema alikuja juu akidai kuwa hamtaki Wema kwa kuwa anamkubali zaidi Penniel Mungilwa ‘Penny’. Akizungumza nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar wikiendi iliyopita, bi’mkubwa huyo alisema kuwa kwa sasa hafahamu chochote kuhusu Diamond kurudiana na Wema zaidi ya kusikia kwa watu na kuona picha katika mitandao ya kijamii. “Kuhusu Nasibu (Diamond) kurudiana na Wema, nasikia tu na kuoneshwa picha namsubiri Nasibu arudi kisha nikae naye ndipo nitatoa tamko,” alisema mzazi huyo. Mapaparazi wa Ijumaa Wikienda kadiri walivyozidi kumchimba mama mkwe huyo wa Wema ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu tabia ya kubadilisha wanawake kama nguo, ikizingatiwa yeye ni mzazi haoni kama mwanaye anamfedhehesha alisema kuwa hayo ni maisha yake. “Hayo ni maisha yake na mwenyewe kwa kuwa ameshazoea kuonekana katika magazeti kila wakati mi niongee nini wakati ndiyo maisha aliyojiwekea,” alimalizia kusema.
Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja from KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.
Huko, Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny
Hivi karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not the easiest relationship I’ve ever had..but its the most intresting! When I’m down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend, my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love, Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika Penny.
Miaka ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye. Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani. So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho am happy with my man, am happy na watu wangu so am good mimi sina tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.
Story zilizopo ni juu ya msanii wa bongo Fleva Daimond anavyo endelea kuwachanganya wasichana wa kibongo na hii ni mpya kabisa baada ya Penny kuzidiwa pale alipoona picha muda mfupi uliopita kwenye mitandao ya kijamii, Kuwa Diamond na Wema wako wote kwa mara nyingine tena apo ndipo ikampelekea Dvj Penny kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospitali.
Let’s face this big elephant in the room…Diamond Platnumz na Wema Sepetu wana agenda ya siri. Naiita agenda ya siri kwakuwa kuna maswali makubwa mawili ambayo mimi na watu wengine wengi tunahisi Diamond anakificha kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu. Swali la kwanza ni Diamond na Wema wamerudiana tena? Jibu la swali hili lilitolewa juzi na Diamond mwenyewe: Kumekuwa na uvumi na habari nyingi sana mitandaoni na kwenye media tofauti… kwamba mimi na mwanadada Wema Sepetu tuna mahusiano ya kimapenzi, kitu ambacho sikweli na taarifa hizo ni za uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye account yangu ya instagram?..Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya mapenzi basi msizungumze ama kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na mbadilike, ina maana mnapenda kuona watu wanauadui… Ni muda wa kufanya kazi ili kulipa sifa na heshima taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo na faida..I real love my Penny,sijarudiana na Wema.” Baada ya Diamond kuandika hivyo, swali hilo likaanza kupotea. Lakini jana na leo swali hilo limekuja tena kwa kasi baada ya kuonekana picha mpya za Diamond na Wema Sepetu wakiwa pamoja katika nchi ya barani Asia ambayo bila shaka ni Malaysia ambako Diamond alikuwa ameenda kufanya show. Kwa picha hizo ni wazi, Diamond na Wema walienda pamoja. Picha za wapenzi hao wa zamani zimesambaa kwenye akaunti ya Instagram ya msichana anayejiita Chynabongo na sasa zimeshasambaa kama kila kona.
Baadaye Diamond naye akaweka picha moja kati ya hizo zilizowekwa na Chyna na kama kawaida yake akasema ni movie mpya inakuja.
“Katika moja ya muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii… #TEMPTATIONS …. STAY TUNED!!!! SOON!….#DayOne #Location #SomeWhere,” ameandika. Kufanya movie ni kisingizio nambari moja cha Diamond. Nikukumbushe kuwa kabla ya uhusiano wake na Penny kufahamika, ilileak picha yao wakionekana wakiwa wamelala, na wote kwa pamoja wakadai walikuwa location wakifanya movie mpya, ambayo hadi leo haijaingia sokoni... tutaingoja hadi miguu iingie tumboni. Kufanyika kwa movie ya Diamond na Wema si kitu kigeni kusikika kwani tangu mwaka jana kulikuwa na taarifa hizo na tayari ilidaiwa walikuwa wameshalipwa. Kama watu wengine, nashindwa kuamini kwa haraka kuwa picha hizi zina ukweli wowote kuhusu kisingizio cha Diamond kuwa hiyo ni movie. Hata hivyo hivi karibuni, Wema alisema ameandaa surprise kubwa kwa mashabiki wake, labda hii ndio yenyewe basi… “What more can I say other than thank ol my beloved fans for all da love nd support uve bin showing me nd naamini hamtoacha maana you guys are jus amazing…. kuna kitu nataka kufanya jus to show my appreciation… its a Surprise I wont tel… ila im sure y’all are gon die… nat die die, but y’all are gon b soooo happy… nawapenda mpaka basi…. thank y’all sooo much,” aliandika Wema kwenye Instagram. Kama Wema na Diamond hawajarudiana, basi wawili hawa wanajua kucheza vizuri na akili za watu na uwezo huo ndio umewafanya wasiwe na mpinzani katika kutafuta ‘publicity stunts’. Uwezo huo ndio umewafanya wawe mastaa wanaongoza kwa kutawala kwenye magazeti ya udaku. Picha hiyo ya Diamond na Wema imeshavutia comments zaidi ya 500 na like zaidi ya 2, 000 kwenye Instagram, na kwenye Facebook imepata comments zaidi ya 400 na likes zaidi ya 900 kwenye Facebook. I guess that what’s Diamond likes right? Confusing people’s minds.. and he is good at it. Na sasa tayari, Wema na Diamond wanatrend tena…kila website/blog leo ina habari yao.… mission accomplished. Okay, tunaisubiria Temptations kwa hamu kubwa lakini tusije kuisubiria kwa muda mrefu kama tunavyoendelea kuisubiria ile ya Diamond na Penny.
Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo.
Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…
Kupitia account yake ya instagram diamondplatnumz amepost moja ya picha zilizopo katika movie mpya aliyoshirikiana na mwanadada wema sepetu kuonyesha msisitizo ktk hilo diamond amesema haya:
diamondplatnumz: Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii... #TEMPTATIONS .... STAY TUNED!!!!SOON!....#DayOne #Location #SomeWhere
Mtaalamu wa miti shamba nchini ambae ni mwenyeji wa Tabora aliyejitambulisha kwa jina la Kamdege amesema kuwa anasikitishwa sana maumivu anayoyapata mtangazaji wa kituo cha DTV DVJ PENNY kwa sababu ya mwanamuziki Diamond, hivyo amemtaka mrembo huyo afike ofisini kwake mara moja ili ammalizie tatizo hilo.
Akiongea kwa njia ya simu [ 0788-844490 ], Kamdege amesema kuwa unyama na ukatili anaofanywa na msanii Diamond unaweza kukomeshwa endapo mmoja wa wasichana hao ataamua kufanya maamuzi magumu ya kuchukua kinyesi chake na kumpelekea ili amtulize.
Katika maelezo yake, mganga huyo alifafanua kwamba kinyesi hicho hakitatumika kumdhuru Diamond kwa namna yoyote ile, bali kitatumika kuituliza MAMBO yake na kumfanya aridhike na mwanamke mmoja huku wengine akiwaona mavi tu... Mwandishi wetu alitaka kujua maana ya kuwaona mavi tu ambapo mganga huyo alifafanua kama ifuatavyo: "Huo ni msemo tu, maana yake ni kwamba hatakaa atamani vya nje ambavyo ni VICHAFU.Sina maana ya kumfanya awachukie wasichana wengine".. "Naomba niweke wazi, dawa hii si kwa ajili ya Diamond tu.Ni kwa ajili ya mwanaume yoyote msaliti. Yaani akitengezwa, usaliti utabaki kuwa historia tu
Aidha mtaalamu huyo alijinadi kwamba anauwezo wa kutibu matatizo mengine ya kiafaya, kikazi, kwa wenye kesi mahakamani na wangependa kesi hizo zifutwe, kupandishwa vyeo nk.
ISHU ya wapenzi zilipendwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kurudiana inadaiwa kumtesa mpenzi wa sasa wa Diamond ambaye ni mtangazaji wa DTV, VJ Penniel Mungilwa ‘Penny’ hivyo kulazimika kukiri kuwa hajawahi kupitia wakati mgumu kama anaopitia sasa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Penny, mwanadada huyo amekuwa akikosa amani kila anaposikia habari za Wema kurudiana na Diamond hivyo kuwa katika wakati mgumu. “Watu wanapomwambia au kumuuliza Penny habari za Diamond kurudiana na Wema amekuwa akiumia sema tu watu hawajui,” kilisema chanzo hicho. Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuwa habari ya mjini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Penny alifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anachokifanya ni kuhakikisha anamshikilia staa huyo wa Bongo Fleva hadi hapo Mungu atakapoamua vingine. “Katika uhusiano niliowahi kuwa nao huu ni mgumu mno,” ilisomeka sehemu ya utetezi wa Penny aliouandika juu ya penzi lake na Diamond.
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Hakuishia hapo kwani aliendelea kujitetea kwa wadau wake ambao walimjibu kuwa kinachoonekana anamhofia Wema ambaye akikita penzi lake kwa Diamond, kwa ustaa wake, atamfanya mwanamuziki huyo kuendelea kuliweka juu jina lake. Katika maelezo yake, Penny alikiri kuwa mapenzi yanatesa lakini anaamini mateso hayo ni ya muda tu hivyo liwalo na liwe yeye anampenda Diamond. Wiki iliyopita, Wema na Diamond waliripotiwa wakidaiwa kurejesha upya penzi lao lililozimika mwaka jana, jambo ambalo lilimpa Penny wakati mgumu huku akieleza kuwa anachoamini ni kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa penzi hilo.
C.E.O wa kampuni yaEndless Fame Filmmaarufu kma Wema Sepetu ameonekana kuchukizwa na kitendo cha kuchafuliwa kwa jina lake katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini. Mapema asubuhi ya leo kupitia account yake ya Instagram mwanadada Wema alitupia picha ya gazeti hilo lililo mchafulia jina kwa kumuandika kuwa"Wema Kunyongwa China Awaomba Watanzania Wamuombee".Pia dakika chache zilizopita kupitia account yake hiyohiyo ya Instagram wema amefunguka zaidi kwa kitendo hicho cha kuchafuliwa jina na kuandika hivi ...
Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana.
Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri.
WEMA Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu. Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo.
DIAMOND Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla. Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua nyumba takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja kwenye akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia watu kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya muziki tu au kuna kingine. Madai ya jina la Diamond kutajwa katika saga hilo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri mara nyingi nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana kujihusisha na biashara hiyo nacho kilimponza. Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa jasho juani hivyo watu wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa amechumia juani na hajui chochote juu ya dawa hizo.
WEMA SEPETU Sikukuu kila mtu huwa anapenda kuisherekea kitofauti zaidi. Hivi ndivyo muigizaji Wema Sepetu aliamua kuisherekea kwa upande wake, alitumia muda wake wa sikukuu ya Eid kukaa pamoja na wazazi wake wote wawili na kusherekea pamoja nyumbani kwao ikiwa ni pamoja kupiga nao story nyingi.
Siku za hivi karibuni mwigizaji anayefanya vizuri kwasasa katika filamu nchini Niva Zubery amekuwa akiweka status zikimhusu mwigizaji mwenzake Wema Sepetu na baadhi ya mashabiki wa mastaa hao na wasomaji wetu kutaka kuupata ukweli kama mastaa hao ni wapenzi kwa siri au lah. "nyie swp hembu muulizeni Niva kama mtu wake kwasasa ni Wema coz status zake ni za kuchombeza kwa bibieee then kama wako close sana siku hizi, maskini kaka wa watu kaoza kwa wema tayariii !" alisema shabiki mmoja wa kike aliyekataa kutajwa jina lake. Status za Niva zinaonekana kama kuchombeza kitu flani kwa Wema kwa mujibu wa wasomaji walioitonya SWP. Baadhi ya status hizo za Niva katika facebook yake ni hizi hapa "Baaabaa eti wewe upo na wemaa? (Apana mwanangu) huku akiwa ameweka picha yake mwenyewe na ya mtoto anayedaiwa kuwa wake", nyingine iko hivi "Niva hanipokerei cm jamaani mwambieni basi kama nampigiaa mwambieeni nawaomba tafazalii" huku akiwa amepost picha ya Wema Sepetu akiwa ameweka simu sikioni". Status nyingine akiwa ameweka picha hiyo hapo chini wakiwa pamoja na Wema ilisomeka hivi "Etiiiiiii kama tunamuaa kuwa nanihiii na nanihiii itakuwa poa? basi nipe maoni yako ili nijue simmeshajua nilicho maanisha so nataka jibu ili nijue". Baadhi ya wachangiaji walimwambia Niva kuwa wakiwa wapenzi yeye na Wema watapendeza huku wengine wakimwambia kuwa Wema sio hadhi yake, wengine walimwambia ajaribu bahati yake kama tayari ameshamzimikia mrembo huyo. Ili kuupata ukweli kutoka kwa Niva mwenyewe kama baadhi ya wasomaji walivyotutumia ujumbe mwanzoni ilibidi kumtafuta Niva jana na kumueleza kila kitu na yeye alikataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema na alipoulizwa kama kweli sio wapenzi status zake zikionekana kwa mtu wa Wema si zinaweza kuzua tafrani? Niva alijibu kwa ufupi kwa kusema "hakuna kitu kama hicho kaka
KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake. Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu. Kabla ya kupandishwa kwa ‘pilato’, staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.
ANASWA AKIFUTURU Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.
MTITI KIDOGO Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.
WEMA AGEUKA MBOGO, ALALA SELO Baada askari kumfikia staa huyo, walimtaka kwenda naye kituo cha polisi kwa kutumia difenda walilofika nalo ambapo Wema alipinga na kugeuka mbogo kwa kudai kwamba hawezi kupanda difenda kutokana na hadhi yake.
Pamoja na askari kutaka kumpandisha kwa nguvu, staa huyo alipinga na ikakubaliwa apande gari lake aina ya Audi Q7 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari. Safari ikaishia Kituo cha Polisi cha Kawe ambako staa huyo aliandikisha maelezo na baada ya zoezi hilo akatupwa selo.
WEMA HAUOZI Kama lilivyo jina lake, wema hauozi, staa huyo alipata dhamana saa 5 za usiku baada ya kudhaminiwa na msanii mwenzake wa filamu, Kajala Masanja. Kajala aliwahi kutolewa katika mdomo wa jela na Wema siku za nyuma baada ya kukutwa na hatia na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar alipotakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 13 au kwenda jela, Wema alimlipia kiasi hicho cha fedha. WAPAMBE FULL SHANGWE Wapambe wa Wema waliokuwa wamejazana nje ya kituo hicho cha polisi, walilipuka kwa shangwe baada ya bosi wao kuchomolewa kutoka selo. Staa huyo aliondoka na gari lake lililokuwa likiendeshwa na meneja wa kampuni yake aitwaye Petit Man.
ATEMBEZWA KWA MIGUU Julai 17, asubuhi Wema alirudi kituoni hapo na kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashitaka yake. Katika hatua ya kushangaza, staa huyo alitembezwa kwa miguu umbali wa mita 200 kutoka kituo cha polisi hadi Mahakama ya Mwanzo ya Kawe. APANDISHWA KIZIMBANI Wema alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake na Mh. Hakimu, Bernice Ikanda na kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Kayumbu. Mbele ya hakimu, Wema alikana mashitaka na hakimu aliiahirisha kesi hiyo mpaka Julai 31, mwaka huu.
IKO SIKU WEMA ATAFUNGWA GEREZANI Kumbukumbu kutoka kwenye makabrasha yetu zinaonesha kuwa, mrembo huyo ni mtu wa majanga, mara kwa mara amekuwa akifikishwa polisi na mahakamani kutokana na ugomvi.
ALIVUNJA KIOO CHA GARI LA KANUMBA Mwaka 2009, Wema alidakwa na Polisi Kituo cha Magomeni na baadaye kupandishwa katika Mahakama ya Kinondoni, Dar kwa Hakimu Emilius Mchalu kwa kosa la kuvunja kioo cha gari la aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Marehemu Steven Kanumba chenye thamani ya shilingi milioni moja. Hata hivyo, Kanumba aliifuta kesi hiyo.
ALIMTISHIA MAISHA BOB JUNIOR Kama vile haitoshi, mwaka 2011, Wema huyohuyo alikamatwa na Polisi wa Oysterbay jijini Dar na kufikishwa Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kumtusi na kumtishia maisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rahem Nanji ‘Bob Junior’. Katika kesi hiyo, Hakimu Mariam Masamalo alimtia hatiani Wema kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi 40,000 ambapo alilipa fedha hizo. ALIMTUSI REHEMA FABIAN Aidha, mara baada ya Wema kuachiwa huru mahakamani hapo alikamatwa tena na polisi kwa kile kilichodaiwa kumtusi Miss Kiswahili 2008, Rehema Fabian. Wema alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar kwa maelezo zaidi.
ALIMTUKANA MSANII Aidha, Wema amewahi kulala kituo cha Polisi Oysterbay, Dar akiwa na mashoga zake, Kajala na Dida kwa madai ya kumshambulia mwigizaji mmoja wa Bongo, kwenye pati iliyofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar. Kesi hiyo iliisha kwa mazungumzo nje ya polisi.