Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label bongo movie. Show all posts
Showing posts with label bongo movie. Show all posts

"WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"-WASTARA JUMA

Sura ya mauzo kunako gemu la filamu za Kibongo, Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.

“Kweli ninaumia sana kwa sababu ninakaa na kujiuliza hawa wanaume walikuwa wanasubiri mume wangu afariki dunia ndiyo wanitongoze?
“Kusema kweli inanishangaza, hata watu ambao sikuwadhania kabisa eti nao wananitaka, watu wajue kwa sasa sipo tayari kuwa na mwanaume.
“Sitaki kukurupuka kwa sababu naweza nikaingia kwenye shimo la taka kwani jamii itanikimbia kutokana na kunuka, natamani kumpata mwanaume anayefanana na mume wangu kitabia.
“Uvumilivu wangu na uzuri ulitokana na kutunzwa siyo aje mtu anayetaka nikavumilie shida, hilo sitaki litokee, namuomba Mungu sana,” alisema Wastara.
Kwa upande mwingine, staa huyo alisema kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu kutokana na upweke na kama angekuwa hana watoto, angeomba afe akapumzike kwani faraja yake kubwa ilikuwa ni Sajuki lakini baada ya kutwaliwa na Mungu watoto ndiyo wamechukua nafasi hiyo.
Wastara aliwaomba watu wote wakimuona wasioneshe huzuni kwani ndiyo anaumia zaidi badala yake wawe na furaha kwani tangu aliporudi kutoka Uarabuni mawazo ya marehemu Sajuki yamekuwa yakimrudia mara kwa mara kutokana na kukutana na stori na maswali yaleyale.
Baadaye, tuliwasiliana na Wastara na kumuuliza kama miongoni mwa wanaomtaka kimapenzi wapo wafanyakazi wa Global Publishers kwani ni miongoni mwa waliomsaidia ambapo alijibu kuwa hawahusiki.
“Jamani Global hamhusiki nilimaanisha mtu mmojammoja na wenyewe pia siyo wote ni baadhi yao,” alisema.
Wastara alifiwa na mumewe Sajuki Januari 2, mwaka huu baada ya kumuuguza kwa muda mrefu.

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO WA MZEE MAGARI "DAR RAHA"

http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/07/cd-8.jpg

"SERENGETI BOYZ WANATOA PENZI ZITO"-JACKLINE WOLPER

 
Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu...

Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati  kwani mapenzi yao ni ya  chumbani tu...


" Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake , alafu mtu mzima, ni  lazmia  ukose  penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi ...


"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..

“Wanaume wengi wenye  pesa zao huniona  nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
 
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.

Wolper  anadai kuwa  kuna watu ambao huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine....
 
Jack Wolper anasema wao si malaika , wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.

HATIMAYE NATASHA AFUNDWA.." MASTAA WAKATA MAUNO ILE MBAYA "



Baadhi ya waalikwa wakijiachia pamoja na Natasha (kushoto) wakati wa sherehe hiyo.

HUKU siku za kufunga ndoa zikihesabika, mkongwe kwenye filamu za Kibongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ amefanyiwa sherehe ya kufundwa kabla ya kwenda kwa mumewe ambayo huko mitaani inajulikana zaidi kwa jina la singo.Shughuli hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Tandika Maghorofani, Dar ambapo iliandaliwa na shostito wa Natasha aliyejulikana kwa jina moja la Nuru.

APEWA SOMO
Natasha aliwekwa ndani kwa muda wa saa moja akipewa somo la ndoa na watu maalumu walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo kabla ya kutoka nje kuungana na wageni waalikwa.


Alipotoka nje, alikutana na waalikwa ambapo kati yao ni mastaa mbalimbali Bongo kisha wakaungana kwenye zoezi zima la kucheza ngoma.
KIASILI ZAIDI
Waalikwa walipata nafasi ya kupakwa urembo mbalimbali wa kiasili usoni na kuifanya hafla hiyo iwe ya kipekee kutokana na vivutio hivyo.
Baada ya yote hayo kukamilika, msafara wa kuelekea nyumbani kwa Natasha, Yombo ulianza huku ngoma zikiendelea kupigwa na mastaa mbalimbali wakikata mauno ndani ya gari.


Akizungumzia shughuli hiyo, Natasha alisema: “Nashukuru sana jamani kwa kupita hatua hii ya kwanza kuelekea kwenye ndoa yangu. Siwezi kuacha kumshukuru zaidi rafiki yangu Nuru kwa kunifanikishia.”

KAMPUNI YA STEPS YANOGESHA TUZO ZA BONGO MOVIE....MATUKIO KATIKA PICHA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stevin JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala

Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji


Msanii Stiv Nyerere akipokea Tuzo

Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI

Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake

Add caption

Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado

Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.vitukovyamtaa.blogspot.com

Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo






Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.vitukovyamtaa.blogspot.com

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baazi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya steps Picha nawww.vitukovyamtaa.blogspot.com

MPIGA PICHA mOHAMED aralakia  ZA KAVA MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO

:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike

Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya

na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'

Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu

mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano,Hussein Ramadhani Mkiety,'Sharo Milionea'

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa