Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label sugu. Show all posts
Showing posts with label sugu. Show all posts

POLISI WASHINDWA KUMPANDISHA SUGU KIZIMBANI BAADA YA KUANZISHA VULUGU BUNGENI


JESHI la Polisi mkoani Dodoma limeshindwa kumpandisha kizimbani Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kwa madai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ alifunguliwa jalada na jeshi hilo Ijumaa iliyopita, akidaiwa kumjeruhi jichoni askari wa Bunge, Koplo Nikwisa Nkisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Wakili wake, Tundu Lissu, alisema kuwa hawakufikishwa mahakamani kama walivyotegemea kutokana na kuelezwa kuwa upelelzi haujakamilika.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa baada ya mteja wake kuripoti kituoni aliambiwa kwamba upelelezi huo ukikamilika wataitwa ili kupewa maelezo ya hatua gani inafuata.

Alisema kitendo hicho cha polisi kuwaita bila kukamilisha upelelezi wao ni kuwapotezea muda.

“Nashangaa ni kwanini tunaitwa, tuliambiwa tufike hapa, lakini tulipokuja hapa hakuna jambo lolote la maana tuliloambiwa, badala yake wanasema tuendelee na shughuli zetu upelelezi haujakamilika na baada ya wiki mbili watatuambia kinachoendelea.

“Yaani, haya mambo yanayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Naibu wa Spika, Job Ndugai, ni ya ajabu sana. Tumeitwa kutoka mbali kote kwa ajili ya kuja hapa kuambiwa kuwa upelelzi haujakamilika,” alisema.

Aliongeza kuwa Sugu alitoka Mbeya huku naye akitoka huko alikokuwa kwa ajili ya kuja Dodoma lakini hakuna jambo lolote limefanyika, na kuhoji ni kwanini wasingearifiwa hata kwa simu.

Lissu alisema kuwa atashanga kama jeshi hilo litapeleka kesi hiyo mahakamani kwani kosa lenyewe lilifanyikia bungeni.
“Nitashangaa kama jambo hili litapelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa kanuni, mbunge hatashitakiwa kwa jambo ambalo alilitenda akiwa katika maeneo ya Bunge.

“Mambo haya yalitokea tukiwa bungeni na huko kuna kinga ya mbunge. Mbunge akikosa anahukumiwa kwa mujibu wa kanuni, lakini kwa fikra na mashikinizo ya viongozi wa CCM wanataka kuvuruga na kufanya mambo kwa masilahi ya chama chao,” alisema.

Naye Sugu alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Ndugai ni cha kihuni na wala hakikuwa na misingi yoyote hadi kulazimisha askari wa Bunge kumpiga.

HIZI NDIZO PICHA ZA MKE WA MBUNGE WA CHADEMA SUGU AKIONESHA TATOO KIUNONI

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, ameshare picha zinazowaonesha akiwa na mwanae pamoja na mama wa mtoto wake huyo, Faiza Ally, waliamua kupark usafiri wao pembeni ya barabara na kufurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Kitonga, mkoani Iringa. Tazama picha zao.
946294_484823404924724_125451513_n
Sugu akifurahia mandhari ya Kitonga





















Sugu akifurahia mandhari ya Kitonga
Yohoooooo!!!
Yohoooooo!!!
Faiza na mwanae
Faiza na mwanae
935165_484821214924943_1643712272_n
Sugu na familia yake
Sugu na familia yake

chanzo:jambo tz

TAZAMA PICHA 15 ZA TIMBWILI LILILOTOKEA JANA SEPT 5 BUNGENI: SUGU KACHOMOKA NA MAIKI YA BUNGE, VIATU VYAMTOKA NA KUTOLEWA PEKUPEKU KAMA KIBAKA:

22

12

14


21

Ni vurugu ambazo zimetajwa kutokea kwa mara ya kwanza kwenye historia ya bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa mjadala wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba.

23


17
13
14
15

12
16
18
Add caption
24
20
19 
 

PICHA 3 ZA MH.SUGU AKIWA NA FAMILIA YAKE



SUGU AFIKISHWA MAHAKANI LEO NA HAKIMU AMFUTIA KESI YAKE YA KUMUITA WAZIRI MKUU "MH PINDA" MPUMBAVU

Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.
 
Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
 

HIZI NDIZO SABABU ZA KUACHIWA KWA MBUNGE WA CHADEMA JOSEPH MBILINYI a.ka SUGU BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUITA WAZIRI MKUU MPUMBAVU MJINI DODOMA.

KUHUSU Joseph Mbilinyi 'Sugu', Mbunge wa Mbeya Mjini. Ni kweli alikuwa polisi Dodoma, alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo:

1. Wakili wake, Tundu Lissu, amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini, maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bun

ge, wakati bunge likiendelea, kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu zinazotakiwa.

2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa hivyo.

3. Wakili wake (Tundu Lissu) kawauliza, nani mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda mwenyewe ? Majibu yalikuwa ya kigugumizi"

Wameondoka polisi kwa makubaliano ya kurudi kesho asubuhi.
Tumaini Makene.

SUGU APATA DHAMANA NI BAADA YA KUTIWA ROKAPU KUTOKANA NA KUMWITA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA "MPUMBAVU" MJINI DODOMA.

MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.

Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.

Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhoj
iwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.

Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.

Hivi karibu Sugu aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kwamba "Tanzania haijawai kuwa na Waziri Mkuu 'Mpumbavu' anayetoa tamko la kuchochea Jeshi la Polisi kupiga raia".

Habarimpya.com imemtafuta msemaji wa Jeshila Polisi Tanzania ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kukamatwa kwa Mbunge huyo kupitia simu yake ya mkononi lakini hakupatikana.

BREAKING NEWS:- SUGU AMEKAMATWA NA POLISI

Mbunge wa Mbeya Mjini Kupitia CHADEMA Mh. JOSEPH MBILINYI"SUGU" anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani
Dodoma kwa tuhuma za kumuita waziri mkuu mpumbavu.

"TANZANIA HAIJAWAHI KUPATA WAZIRI MKUU MPUMBAVU KAMA PINDA"....HAYA YA NDIO MATUSI YA SUGU KWA WAZIRI MKUU


Katika  hali  yakushangaza , mbunge  wa  mbeya  mjini  kwa  tiketi  ya  CHADEMA, mh.  SUGU  ameporomosha  tusi  zito  kwa  waziri  mkuu  wa  tanzania  ( mh. PINDA )  akidai  kuwa  Tanzania  haijawahi  kuwa  na  waziri mkuu   mpumbavu  kama  yeye.....

Tusi  la  Sugu  limekuja  baada  ya waziri  mkuu  kuwaruhusu  rasimi  polisi  kutumia  nguvu  ya  ziada   kuwadhibiti  wananchi  kwa  kuwashushia  kichapo  ili  wazitii  sheria.....

Hili  ndo  tusi  la  mbuge  wa  mbeya  kwa  waziri  mkuu...

SUGU (Mr.II) .AMTUKANA MWANAFA JUU YA SHOW YAKE...SOMA ALICHOANDIKA

 
Baada ya show ya mwana FA kusambaa kwenye mitandao juu ya kupwaya kwa washabiki kuhudhuria na show ya mwanadada komando lady jay dee kufurika ....Msanii wa Hiphop Joseph Mbilinyi a..k.a  MR II a.k.a SUGU..Amshambulia mwana FA kwenye mtandao wa face book .HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA
"..The finest???!!..The finest My Ass..."
angalia apo chini Post yake Katika mtandao wa facebook

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa