Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label mapenzi. Show all posts
Showing posts with label mapenzi. Show all posts

KWA WANAWAKE: HIZI NDIZO MBINU ZA KUMTEKA AKILI MWANAUME WAKO..HAKUNA HAJA YA KUMWEKEA LIMBWATA..

WANAWAKE wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.

Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au night dress ndani huna kitu.

Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia zake. Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue tayari mwenzako alishafiria mbali zamani we huna habari.

Ni vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za mwanaume huyo mumeo kama inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya hivyo unamwathiri kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje waliowaweka waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia. 

Akiwa na ahadi na mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?

NB:
Nikisema mpe mumeo Hitaji lake sina maana Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai si Mume mwenye Busara huyo na wala hakutakii mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya Tendo la ndoa kinyume na maumbile.

MVUTIE MUMEO KWA MWENEKANO WAKO. 
https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTbMbChPtpJvGIFzCIElrXQ7i9Y2W-5W1Pn2ZI95DjaA2y-7zAHMvuto ni muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake wanaowavutia kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi yanayomvutia.


Sio vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga moja kama upo pamoja nae. Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka kwa kuona. Kwanini avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe unaweza kuvaa.

Wanawake jueni hili mnapokuwa karibu na waume zenu jianchieni Kwa mfano hakuna ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini akiwa amechoka, wakati unampotengea chakula ukavaa kanga moja au night dress. 

Unaweza kuona hilo ni jambo dogo lakini kisaikolojia utakuwa umefanya jambo kubwa. Hapo hata kama atakuwa ameudhiwa kazini atasahau na kukuona wewe mpenzi wake.

Usafi panga vitu vyako vya chumbani vizuri:

Jambo hili limekuwa lizizungumzwa sana hadi wengine wanasema mwanamke usafi.
Kisaikolojia mpangalio wa vitu ndani na hasa chumbani kama ni mbovu unaweza kuathiri hata tendo la ndoa. Kama chumba ni kichafu vitu havijapangwa vizuri kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi na hata kumfanya mwenzako achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani hakupendi.

Mwanamke tandika kitanda chako vizuri panga chumba chako tandika shuka nzuri. Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi nunua hiyo uwe unatandika. Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe chumba chako na hata wewe mwenyewe. 

Mazingira mazuri yatamfanya asisimke haraka kimapenzi anapokuwa na wewe na hata kuitamana nyumba yake na kurudi mapema nyumbani.

Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata kuchukia. 

Unaweza kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio mbovu wa chumba ndio sababu inayomfanya achukie.

Uwe msafi wa mwili:
http://i1174.photobucket.com/albums/r619/ameliavega003/Miss%20World%202012/russia.jpg
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni muhimu.
Niwakumbushe wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama mwanamke mchafu. Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi ukawa msafi. Oga vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato kidogo yanayomvutia mumeo. 


Sio lazima utumie gharama kubwa usafi wa kawaida unatosha na kupaka rotion kuna fanya ngozi ya mwanamke ikawa laini inayovutia wanaume wanapenda sana wanawake wenye ngozi laini yenye kuvutia inaleta msisimko mumeo anapokuwa anakuangalia mara kwa mara.

Wanawake wa nje hawana zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na mengine ndiyo wanayotumia kuwaweka waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa mganga hakuna atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi vitu vyako vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo kufikiria nje.

Kujiamini kwako iwe ni kwa sababu unajua ‘kumhendo’ mumeo kwa kumpa mapenzi ya kiwango cha juu, kumheshimu, mjali na kumpatia mambo ya msingi ambayo anastahili kuyapata kutoka kwako. Ukifanya hivyo utaifanya roho yake imsute kila anapotaka kukusaliti.

Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe kujiamini na wala huna sababu ya kujinadi kwa wenzako. Tambua kuwa kuna wanaofikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kwa kutoa ‘mtandao’ wakijua kuwa ni njia ya kuwashika waume zao kumbe wanajitafutia matatizo makubwa.

Wapo waliopoteza fedha zao nyingi kwa kwenda kwa waganga ili waume zao wasifurukute mbele zao lakini imekuwa kazi bure. Shituka leo, anza kutumia mbinu sahihi za kuishikilia ndoa yako na usijidanganye kwa kufanya mambo ambayo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Mwanamke aliyekamilika ni yule anayeuthamini mwili wake, sasa kwa nini leo hii ukubali ‘kumrukisha ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje ? Kwa nini utumie fedha zako kwenye kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe mwenyewe ni limbwata tosha ?.

KWA WAPENDANAO: FAHAMU HATUA TATU MUHIMU ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAPENZI...

WAPENZI na wanandoa wengi hivi leo wanapoingia kitandani tayari kwa kuianza safari ya kupeana haki zao za msingi hushindwa kufurahia tendo na hasa hali hii hujitokezwa kwa wanawake kwani mwanaume huwa na haraka iliyopitiliza! 

Mwanaume atamkumbatia na kumbusu mwanamke kwa muda mfupi na kabla hata hamasa ya mapenzi ya mwanamke ahaijashika hatama, atamwingilia na ndani ya dakika sekunde ama dakika zisizozidi 3, mwanamme hufika mshindo.

Katika hali ya kusikitisha baada ya mwanaume kujitosheleza hujongea pembeni bila kujali mwenza wake hajafika mwisho wa safari hali inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya tendo endapo tabia hiyo ya mwanaume itaendelea.

Kuna hatua tatu muhimu ambazo wapendanao wakizishika na kuzitekeleza ipasavyo basi watafanikiwa kujitosheleza kila wanapokutana na kwa hakika watakuwa miongoni mwa watu wachache wanaofurahia faragha kila wakutanapo!

Hatua ya kwanza ni kusameheana:
Wanandoa wengi hushindwa kupata raha ya mlo wa usiku kutokana na kushindwa kumaliza tofauti zao kabla ya giza halijaingia, mgogoro wowote baina ya wapendanao ni lazima umalizwe kabla ya kukutana kwa ajili ya mlo wa usiku. Hii husaidia kuondoa kinyongo miongoni mwao na kuwafanya mioyo yao igubikwe na upendo ambao humfanya ahamasike kunako majambo!Hivyo basi endapo unataka kufurahia mambo fulani hakikisha unamaliza tofauti, ombaneni msamaha na samehaneni kwa dhati kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia muwapo faragha kufurahia kile mnachokifanya kwa kuwa mtakuwa mmemalzia tofauti zenu.

Hatua ya pili ni michezo ya mahaba:
Mashamsham hunoga na kupamba moto kiasi cha kumfanya yoyote aliye kwenye uwanya wa raha kusahau kwa muda shida na matatizo yanayomuandama pale anapokutana an mtu anayeweza kumpagawisha kwa michezo ya mahaba kabla ya kuianza safari yenyewe!
Michezo hii husaidia kuamzsha hamasa na muhemko baina ya wapendanao, hivyo ili wapendanao waweze kufika mwisho wa safari pamoja na kila mmoja alidhike na udereva wa mwenzake uliowafikisha safari yao lazima watumiye muda wakutosha katika michozo yakimahaba!

Hata hivyo kila mmoja wenu anapaswa kuujua mwili wa mwenza wake. Mwili wa mwanaume ni rahisi kuuelewa kwani una sehemu moja kuu ambayo ni kama kiini cha muhemko na msisimko wa mapenzi. Sehemu hiyo ni uume. Hivyo endapo mwanamke yoyote atatumia muda wakutosha kuhangaika na sehemu hiyo basi mambo huwa safi kwa upande wa mwanaume.

Mwili wa mwanamke una shughuli pevu kubaini sehemu zenye ambazo huamsha hisia za mapenzi na ndiyo maana wanaume wengi hushindwa kuwafikisha mwisho wa safari wapenzi wao. Kiini cha hisia za mapenzi kwa mwanamke ziko kwenye kipegere G (namaanisha critoris wadu, haya ni mambo ya infenizimu tu). Kipegere G kipo nje ya uke ambapo wataalamu hudai kuwa kipo sentimita 4 kutioka ukeni.

Wanaume wengi wanaelewa hili lakini walio wengi wamegubikwa na imani potofu kuwa, kwa kuingiza kidole ukeni watafanikiwa kuinua hamasa ya za wenza wao kutaka kuanzisha safari jambo ambalo si kweli, kwani wanawake wengi hujisikia vibaya kuingizwa vidole ukeni kutokana na ukweli kwamba kucha zinabeba uchafu na bakteria wengi ambao huwasababishia kupata fangasi!

Hivyo basi, endapo wewe ni miongoni mwa wanaume waliokuwa wakiaminin dhana hii nataka nikujulishe kuwa, ukitaka kumpa msisimko uliotukuka mwenza wako usiangaike kuingiza kidole chote ukeni badala yake hakikisha unatumia kidole chako (hakikisha si kikavu) kucheza na sehemu ya nje ya uke ambapo utakutana na kipegere G na lips za ndani. Hata hivyo usisahamu kuhangaika na uke pia lakini hasa shughulika na sehemu za nje!

MUHIMU KUJUA: Mwanaume huahamasika kwa sekunde kadhaa lakini mwanamke humchukua takriban dakika 20 kuweza kuamsha hisia zake na kumfanya awe tayari kwa kuianza safari! Hivyo, mwanaume mwenye busara yaani asiye mbinafsi huakikisha anatumia muda wakutosha kumuuanda mwenza wake kabla ya kuanza safari! Hivyo mwanaume anapaswa kunza michezo ya mahaba kwa kuzingatia hatua tatu muhimu ambazo ni:-

Sehemu ya juu:

Wanume wengi kutokana ana haraka zao hukimbilia sehemu ya chini ya mwili wa mwanamke yaani kunako na kuanza ama kupapasa kwa kidole chake ama ulimi na baada ya sekunde chache huanza kumwingilia mwanamke, lakini mwanaume mwenye kumjali ampendaye na mwenye nia hasa yakumfikisha kwenye kilele cha raha huwa hana papara huhakikisha anamhagi na kumpiga mabusu sehemu ya juu ya mwili wake yaani mdomoni, shingoni, kwenye matiti, chuchu etc.

Hata hivyo, si wanawake wote wako sawa, kuna amabo hufurahia kutomaswa maziwa yao huku wengine wakichukizwa kutokana na sababu mbalimbali kwa mfano kama mwanaume ni mtu wamitungi ama mvuta sigara mara nyingi kinywa chake hutoa harufu mbaya hivyo huwa vigumu kwa mwanamke asiyependezewa na matumizi ya vitu hivyo kufurahia kupigwa denda!

Kimsingi mwanamke kama kweli unampenda mpenzi wako na unataka ufurahie majambozi anayokupa hakikisha unakuwa muwazi kwa kuanza na kumuonyesha sehemu zinazokupa hamasa ya kufanya mapenzi, si lazima ushike mkono wake na kuupeleka kunako hiyo sehemu!

Hakikisha pindi mwanaume anapokugusa sehemu inayokusisimua unamwonyesha wazi kuwa hapo unasikia utamu yaani kama miguno ilikuwa haitoki hakikisha inaanza toka, kama pumzi zilikuwa zatoka kawaida basi zianze toka isivyo kawaida, nachomaanisha hapa ni kuwa unapaswa kuonyesha umepagawa kwa raha unayopata basi kwa mwanaume aliye kamili hatasita kuishughulikia kikamilifu sehemu hiyo!

Sehemu ya chini:
Baada ya kumtomasa kiasi cha kutosha sehemu ya juu ya mwanamke, mwanamke huhitaji kutomaswa sehemu ya chini na hapa ndipo ambapo unaweza kuhisi anataka kuingilia mana huanza ama kujishikasiika sehemu za chini ama hukupeleka maeneo yake nyeti upate kumwingilia kwani huwa amehamasika na ili kujua kama amaehamasika basi uke wake huwa unamajimaji ambayo hutoka kwa ajili ya kulainisha nyia ya kupita uume.

Hata hivyo, ili mchezo uwe mtamu mwanaume anapaswa kuhakikisha anatumia dakika kadhaa kuuchezea uke na kufuatia kinena. Hapa ieleweke kuwa kuna wanawake baada ya mizuka kuwapanda hutokwa na majimaji mengi sehemu zao za siri hivyo endapo mwanaume ukikutana na hali hiyo usishutuke jua mzuka imempanda mpenzi wako tu na si vinginevyo!

Katika kuchezea sehemu zake za siri mwanaume anapaswa kujua kuwa kuna wanake wanapenda chezewa kinena pekee na wengine hupenda mwanaume atumie ulimi ama akidole chake (kisiwe kikavu) kuingiza ukeni huku kidole kingine kikitomasa kinena hali inayomsisimua mwanamke. Hivyo mwanamke anapaswa kuwa muwazi nini anapenda kufanyiwa!

Katika kipindi hiki mwanamke naye anatakiwa kutoa ushirikianao wa miguno na viuno vya hapa na pale kuashiria anapata raha na asisahau mptomasa mwanaume, lakini ikumbukwe kuwa mwanaume ana sehemu kuu moja inayomtia wazimu ambayo ni uume wake hivyo ni rahisi kwa mwanaume kufika mshindo hata kabla ya tendon a hapo ndipo tatizo huibuka kwani wengine baada ya tendo moja huwa hawana uwezo wakurudia mzunguko wa pili!

Nini mwanaume anapashwa kufanya sasa ili kuhakikisha hamalizi mzungoko haraka? Anapaswa kuwa muwazi kwa mwenza wake endapo mwenza wake atakuwa anamshika sehemu ambayo inamnyegesha sana na kumfanya ajisikie kumaliza biashara basi amueleze wazi kuwa aiache sehemu hiyo kwa muda ili uweze kudumu kunako majambozi!!

Hata siku moja msifanye mahaba kimya kimya! Simaanishi mpige mikelele hadi iwe kero kwa majirani na nk, elezenaneni kwa sauti za mahaba nini kila mmoja wenu anapenda mwenzi wake afanyiwe na mwenza wake.

Hatua ya tatu:
Kuingiliana kimwili
Mwanaume anapaswa kuahkikisha amasa za mapenzi za mwanamke zimeamka kabla ya kumwingilia. Wanaume wengi kutokana na papara hujikuta wanawaingilia wenza wao hata kabla hawajahamasika na hatimaye kumaliza tendo pasipo kuwafikisha kileleni na hili ni tatizo la kawaida kwa wapenzi wanaokutana kwa mara ya kwanza na has amwanamke akiwa na zile nataka sitaki yani atasumbuana na mwanaume weeeee na hatimaye hadi dume lifanikiwe kumwingilia kimwili inakuwa kama mbakano tu!

Hivyo basi, mwanaume unapaswa kujua kweli mpenzi wako yuko tayari kwa tendo la ndoa na utajua kwa kungalia kwanza mashavu ya uke wake kama yamekakamaa na kuongezeka ukubwa huku kinembe chake kikionyesha kukaza na mwanamke akifikia hali hii basi mwanaume huweza kuingiza uuume wake ambao umesimama kiurahisi kwani kuta za uke zitakuwa na ute unaoteleza huku uume nao ukiwa na ute unaotoka sehemu ya mbele kabisa hali inayowafanya wapendanao kufurahia tendo kwani hawataumizana !.

JE, PENZI LAKO LIMECHUJA, UNAJUA CHANZO...?? SOMA HAPA...


Leo nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.
Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo.
Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi  alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu, hali hiyo itabaki historia tu.
Hivi hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi wangu mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
Maneno kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio wengi wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini baada ya muda mambo hubadilika kabisa.
Sijajua ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa baadhi ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’ hujenga kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe tofauti vipi hawawezi kuachwa!
Labda nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye uhusiano wa kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila linalowezekana kulifanya penzi lenu lisichuje.
Wewe ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku ama kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza katika ndoo ya maji ya moto.
Hatukatai kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja hata siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini penzi lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo hayakwepeki kutokana na umri.
Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi wetu na kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.

JE UNATAMANI KUMUACHA MPENZI WAKO, KWA SABABU MOJA AU NYINGINE...?? CHUKUA MUONGOZO HUU..



Upo uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa. Kuna wengine hawa sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na kile kilichomo ndani ya nafsi zao.

Unaweza kujiuliza; Kwanini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na mwenzako? Iwe kirafiki au kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuwafanya wahusika kuamua.

Yawezekana uhusiano wako na mpenzi wako au rafiki yako wa jinsia tofauti unakutia hasara, au unakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii, au pengine uaminifu wako kazini. Mathalan, mpenzi wako anapokuwa anafahamika kuwa ni kahaba.

Inawezekana uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano, mwenzio ana nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote analokwambia. Pengine kutokana na hali hiyo umekuwa ukilazimika kufanya mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na maadili.

Lakini pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako. Mazingira yamebadilika, kwahiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua kwamba ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!

Naam, baadhi ya mahusiano, yawe ya kirafiki au kimapenzi, huwaweka katika wakati mgumu watu kiasi kwamba ni lazima mtu achukue hatua ili aweze kuishi kwa amani na furaha ya kweli. Hata hivyo, ikae akilini kwamba inauma mno kuachana na mtu unayempenda!

Kumaliza uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa namna yoyote. Kwa sababu hiyo unapaswa kujifunza njia sahihi ya kumaliza uhusiano wako na mwenzako inapobidi.

Kuna jamii inaweza kuthubutu kusema, unapochoshwa na mtu, mchukue uende naye mahali kisha umueleze kwa uwazi kuwa hutaki tena kujihusisha naye kwa sababu moja, mbili, tatu. Hata hivyo, hilo si jambo rahisi kwa wengi.

Badala ya kukubaliana na mtu ana kwa ana na kumweleza kuwa humhitaji tena, zipo njia za kirafiki na za kidiplomasia ambazo unaweza kuzitumia na kumaliza mambo bila kusababisha matatizo makubwa au madhara yoyote ya kisaikolojia.

WEKA SABABU ZAKO MEZANI!
Unapotaka kumbwaga rafiki yako au mpenzi wako ambaye hujampa ahadi yoyote ya kuishi naye katika ndoa, anza mchakato kwa kuweka bayana sababu zinazokufanya utake kuachana naye. Hakikisha kuwa sababu unazoziweka ni zile ambazo mpenzi wako huyo hatapata namna ya kuzipinga.

Zitengeneze sababu hizo kwa kuzingatia mtazamo wako mwenyewe, na si kwa mtazamo wa mpenzi au rafiki yako huyo, ili hatimaye kusiwe na sababu ya mwenzako huyo kudhani atajirekebisha ili aweze kuendelea kuwa na wewe.

Namna hii utakuwa unayaangalia zaidi maslahi yako mwenyewe na iwapo utalazimika kumweleza mwenzako ni kwa nini unataka kumaliza uhusiano wako na yeye, sababu zako hazitaonekana kama shambulio kwake yeye mwenyewe wala tabia yake.

USITHUBUTU KUWASILIANA NAYE!
Utakapaokuwa umeweka wazi sababu zako na kuziamini, weka mkakati kuwa hutaanzisha tena mawasiliano na mwenzako. Jiwekee msimamo kuwa hutampigia simu, wala kumtumia ujumbe wa simu, wala baruapepe na kadhalika, ila utajibu tu yeye atakapoanzisha.

Unapomwalika mtu au kumpigia simu au kumtumia ujumbe ni kama unamtia moyo na kumfanya aamini kuwa unampenda na kumjali. Kama mhusika ni mtu mwenye fahamu atashtuka kuwa jitihada zote anafanya yeye na wewe uko kimya. Akitafakari atagundua kuwa hauko naye tena.

AKIKWITA KATAA!
Iwapo kweli umedhamiria kumaliza uhusiano wako na mwenzako, jaribu kukataa mialiko anayokupa, mathalani kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana. Pia kama atasema atakufanyia jambo Fulani, kataa kiaina.

Fanya vivyo hivyo kwa matukio yote ya kijamii. Kataaa mialiko kwa njia ambayo hatkushtukia haraka kuwa humhitaji tena, bali aje kushtuka baadaye atakapojumlisha matukio.

Katika hatua za awali, hii itamaanisha kuwa utakosa kwenye matukio Fulani ambayo wewe mwenyewe ungependelea kuyahudhuria, lakini huna la kufanya, maana umeazimia kumaliza uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako.

Unapotaka kupeleka ujumbe kwa mpenzi wako kuwa hayuko tena moyoni mwako, lazima tu ujitoleee kupata hasara katika baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa huhitaji tena uhusiano wako na mwenzako.

KUOLEWA SIO KILA KITU DADA....VUTA SUBIRA

 
 
Ni mada ambayo imezaliwa kutoka katika mazungumzo na msomaji wangu kwa njia ya simu. Alinipigia na kuniomba ushauri juu ya tatizo lake, lakini katika maongezi yangu na yeye alionekana kuwa tayari kuendelea kuteswa, kuumizwa, kunyanyaswa katika uhusiano alionao, eti kwa sababu anaogopa kuishi bila mume.

Anataka kuolewa maana anaamini kwamba kutokuolewa ni nuksi! Masikini, alikuwa anawaza tofauti sana. Nilizungumza naye kwa muda mrefu, mwisho akaonekana kuingiwa na kitu fulani cha tofauti. Kilichobaki ni yeye kufanyia kazi ushauri niliompatia.

Hapa nimeona ni vyema kuandika, ili kwa rafiki zangu wengine wenye mtazamo kama wa dada yetu huyo, wabadilike. Naam! Ukimaliza kusoma hapa lazima utabadilika. Twende kwenye mazungumzo yangu na msomaji huyo, ambayo bila shaka yatakupa mwanga wa kuendelea na mada hii vyema.

Alisema yupo kwenye uhusiano na mwanamume ambaye kwake ni kero. Anaeleza kwamba, mpenzi wake huyo ana umri wa zaidi ya miaka 45 na yeye ana miaka 32, wakiwa katika uhusiano huo kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Hata hivyo, alisema tatizo kubwa linalouyumbisha uhusiano wao ni kitendo cha mwanamume huyo, kuwa na tabia za kuwatongoza wadogo zake ambao anaishi nao nyumbani kwake. Baada ya kero hizo kuzidi, dada huyo aliona ni bora kuachana naye. Akamweleza mwanamume huyo msimamo wake na kuachana.

Kilichomfaya anipigie simu ni juu ya jamaa huyo kumsumbua kila wakati, akitaka warudiane. Amekuwa akiomba msamaha na kuahidi kwamba hatarudia tena. Alisema, hii siyo mara yake ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akiwatongoza hata rafiki zake wa karibu na akishtukia mchezo, kazi yake imekuwa kuomba msamaha akiahidi kutorudia lakini baada ya muda, mambo yanakuwa vile vile!

Kinachomuuma zaidi ni kwamba, amejikuta akimpenda sana mwanamume huyo na anashindwa kumuondoa kichwani mwake. Nilizungumza naye juu ya tatizo lake, lakini niliona yawezekana kabisa kuna wengine wengi wenye tatizo kama hilo, lakini hawajui cha kufanya. rafiki zangu, hapa nitakupa njia madhubuti za kutumia ili uweze kukabiliana na tatizo hilo katika uhusiano wako.

Je, upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haishi kuwatongoza rafiki, ndugu au watu wako wa karibu? Hapa haijalishi jinsia, nazungumza na wake kwa waume. Dawa hii hapa...

ANABADILIKA?
Siku zote katika uhusiano wowote ule, suala la msamaha ni jema na lenye nafasi kubwa ya kuboresha uhusiano, lakini kabla ya kuchukua hatua ya kusamehe ni lazima ujiulize, anaweza kubadilika?

Hili linaweza kudhibitishwa na historia yake ya nyuma. Haiwezekani ikawa ndiyo mara yake ya kwanza kukosea, lazima atakuwa ameshakukosea mara nyingie huko nyuma.

Je, hili ni kosa lake la kwanza? Alivyokosea huko nyuma aliomba msamaha? Kama aliomba, alirudia tena? Maana kama mtu anakosea kosa lile lile zaidi ya mara tatu na anaomba msamaha akiahidi kubadilika na habadiliki, ujue kwamba si rahisi kubadilika tena!

Lazima ujiridhishe kwamba ni kweli atabadilika na hatarudia tena. Kama nilivyosema hapo juu, utapata ukweli huu kupitia historia yake ya nyuma.

LINGANISHA UMRI NA MAKOSA
Rafiki zangu, kuna aina ya makosa fulani, ukishavuka umri fulani unakuwa huwezi kuyafanya tena, kwa mfano, kesi za kwenda disko na demu mwingine, kwa mwanaume wa miaka 45 huwezi kuzisikia tena.

Sasa hata katika hili, lazima uangalie umri wake kama unafanana na kosa lake. Unajua, kuna tabia nyingine hubadilishwa na wapenzi na nyingine ni za kuzaliwa ambazo kwa hakika huwezi kufanya mabadiliko.

Suala la kubadilisha wapenzi, linaonekana kuwa fasheni zaidi kwa vijana, lakini kama umri wake umeshasonga na bado akawa na tabia hizo, ujue kwamba hiyo ni tabia yake ya asili ambayo haibadilishiki!

Mwanaume wa miaka 52 bado unakimbikizana na vitoto vidogo, lazima kuna tatizo. Wataalamu wa Saikolojia ya Uhusiano na Mapenzi wanaamini wanaume wenye uwezo wa kuwa na familia bora na kuisimamia vyema ni wale wenye zaidi ya miaka 35, kwamba atakuwa ameshapitia mambo mengi na sasa anatamani kuwa baba tu!

Fungua ubongo wako, msimamizi wa familia hawezi kuwa malaya, anatakiwa awe mwenye kujiheshimu. Huyu anafaaa? Wa nini? Akili kichwani mwako.

NI WA MAISHA?
Lakini pia, kabla hujachukua uamuzi wa kuachana naye, lazima ujiulize swali hilo hapo juu, ni mwenzi sahihi wa maisha yako yote? Lazima awe na sifa zitakazomfanya apewe kofia ya mwenzi sahihi.
Tuliona jinsi msomaji aliyewasiliana nami, akiomba ushauri, jinsi ambavyo alikuwa akiteswa na mtazamo wa kwamba kuolewa ni kila kitu, hivyo kujikuta akiwa tayari kuendelea kuteswa na mwanamume wake ambaye ana tabia za ovyo ili kutetea kuolewa!
Sasa tuendelee na vipengele vilivyosalia...

KUTOKUOLEWA NI NUSKI?
Moyo unatudanganya sana rafiki zangu, lakini kumekuwa na mawazo mengine ya kitumwa yanayotawala hisia zetu bila kujua. Eti mtu anafikiria kwamba, kukaa bila kuolewa ni nuksi! Unajua kinachotokea? Anakubali kuwa na mwanaume yoyote hata kama ana matatizo, ili awe ameondoa nuksi.

Kama una mtazamo huo, futa. Jipe moyo dada yangu, huna nuksi. Tulia, pima mambo, kisha panga maisha yako ya baadaye. Kama mumeo yupo basi yupo tu, ni siku ya kukutana tu, ndiyo haijafika.

UNAFIKIRI HUVUTII?
Huu ni mtazamo tasa uliopo vichwani mwa wanawake wengi, hawajiamini. Wanadhani wao si wazuri au hawavutii, kwahiyo wanapokuwa na mwanaume, wanahisi kama wamebahatika tu, hivyo hawataki kuachia bahati hiyo! Huko ni kujidaganya.

Wapo wanaoshinda kwenye vioo wakijitazama na kuhakikisha kama kweli ni wazuri, kwa bahati mbaya vioo huwapa majibu tofauti kidogo...kwamba si wazuri kiivyo! Halafu kuna hizi filamu na video za wasanii wa Kizazi Kipya, basi kutwa nzima mwanamke anashinda akijifananisha na msanii fulani kwenye sinema.

Akiona aina ya wanawake wanaosalitiwa kwenye ndoa za kwenye hadithi za sinema au nyimbo za wasanii husika, hujifananisha nao! Si kweli. Wewe ni mwanamke mzuri, ambaye unapendeza kwa mwanaume wako atakayekupenda. Si rahisi kupendwa na kila mtu. Unaweza kuambiwa na mpenzi wako anakupenda, lakini mtu mwingine akashangaa, kwanini mwenzi wako anakupenda!

Kila mtu ana mzuri wake jamani. Hata hivyo, ili uwe mzuri ni lazima kwanza uanze kwa kujikubali wewe mwenyewe. Kwamba wewe ni bora, unavutia na umeumbwa kipekee. Unajua ukianza kuwaza hivyo, hata tembea yako itakuwa ya kike na kujiamini, utavaa vizuri na kujipamba sawasawa. Utavutia zaidi ya unavyofikiria.

KUOLEWA SI KILA KITU!
Kitu kibaya kingine kinachofikiriwa na baadhi ya wanawake ni kwamba kuolewa ni kila kitu! Mwanamke akishaolewa anakuwa amemaliza kila kitu. Hili si wazo baya sana, maana heshima ya mwanamke ni kuolewa.

Lakini vipi kama utaolewa na mwanamume ambaye si sahihi, akutese, akutukane, akupige, akusimange na kukufanyia kila aina ya vitu vibaya? Si utakuwa mwanzo wa kuharibu maisha yako?

Heshima ya ndoa ni kuishi kwa amani na furaha, hapo utakuwa umekamilisha kipengele hicho sawia. Kama kijisehemu hicho hapo juu kinavyosema, ni bora kuandaa maisha yako mwenyewe, uwe na uhakika na kesho yako, ukiweka malengo na kuyatimiza taratibu, ili uwe mwanamke bora. Kuwa mwanamke bora ni mwanzo wa kuelekea kuwa MKE BORA.

RUHUSU MAUMIVU MARA MOJA
Inawezekana kichwani mwako kuna mambo mengi, likiwemo la mapenzi ya dhati kwa mwanamume wako, lakini tayari amepoteza sifa za kuwa mume sahihi, uendelee kuwa naye? Hata kama unampenda sana, moyo unakusisitizia hivyo, lakini tayari taa nyekundu inawaka mbele yako.

Fanya maamuzi, bora uruhusu maumivu mara moja halafu ufurahi milele, maana kukubali machozi ya mara moja na kuachana na mtu ambaye ni kikwazo kwako, kutafungua mlango wa aliye bora kuingia. Utaonekana vipi kama hutoki nje?

KUANZA UPYA SI UJINGA
Kuanza upya si ujinga! Hakuna uwendawazimu wowote katika kuanza upya hasa unapogundua kwamba kuna makosa uliyoyafanya. Inaaminika kwamba anayekubali kukosea na kutaka kuanza upya, huwa bora zaidi katika hicho anachorudia, maana tayari anakuwa ameshajua kosa lake.

UMENIPATA?
Naamini umeelewa mada na una kitu cha kufanya. Ni bora uelewe na uanze kupiga hatua ya kuanza maisha mapya yenye mtazamo mpya. Nina hakika utakuwa umefungua ukurasa mpya wa maisha yako ya uhusiano ukiwa na furaha na nguvu mpya. Wewe ulikuwepo kabla ya mapenzi, kwa nini yakutese? Yatawale!

Mapenzi yana wigo mpana yatizamwe kwa jicho la tatu
KAMA ilivyo ada tumekutana tena kwenye kona yetu, kwa uwezo wa Karima nina imani mu wazima wa afya njema. Siku zote sitaki kupiga porojo zaidi ya kuweka mada mezani ili kila mmoja aisome.

Kumekuwa na uwezo mdogo wa watu kufikiri mapenzi ni nini na muonekano wa mapenzi uko vipi. Leo nimelenga kwenye upungufu mkubwa katika utengenezaji wa filamu zetu zinazohusu mapenzi.

Wengi wanaamini kunyonya midomo ndiyo kuwakilisha mapenzi, mtu kukaa nusu utupu kitandani au bafuni, watakuwa wametimiza lengo lao hilo.

Ndiyo maana maandalizi ya mapenzi au muonekano wa mwanamke kwa mpenzi wake huwa jambo la siri lisilotakiwa mwingine alione. Naweza nisiwalaumu waandaaji kwa vile ni uwezo wa ufahamu kuhusu mapenzi yana mtazamo gani mbele ya jamii.

Nimekuwa mfuatiliaji wa filamu nyingi za mapenzi, ndani na nje ya nchi na kuangalia maigizo ya maudhui hayo yanawakilishwaje. Je, haya mapenzi tunayoigiza ndiyo tunapaswa kuishi ndani ya familia zetu?

Inawezekana wengi hawaelewi maigizo yanayoonekana mbele ya jamii huwa kivuli cha maisha tunayoishi, mengi yakiwa yanalenga kuelimisha jamii na si kupotosha.
Pia yanazingatia utamaduni wa nchi yetu husika, lakini kwa baadhi ya waigizaji wetu nina imani kabisa ni uwezo mdogo wa kukifahamu kile unachokifanya kwa kuamini wapo sahihi na hawataki kujifunza.

Siku zote usipotaka kujifunza na kubadilika utajiona unakwenda mbele na mwisho wake utakuwa unapiga ‘maktaimu’ na kupoteza nguvu zako.
Sitaki kuhamia sana katika uwezo wa waandaaji wa maigizo ila nataka nitoe elimu ya mapenzi ambayo huenda itakufumbua macho zaidi na kuvaa uhusika ambao utaangaliwa na rika zote.

Katika maigizo hayo kuna aina nyingi ya kuwakilisha mapenzi ya wawili na si lazima mlale kitandani mkiwa nusu utupu, kunyonyana ndimi au kushikana maeneo ya aibu ambayo anatakiwa kuyagusa mtu wako tena mkiwa faragha.

Kumbuka mwanadamu ameumbwa kwa matamanio hasa kiumbe wa kike, kuna sehemu anatakiwa kuguswa na mpenzi wake tena kumuandaa kwa ajili ya tendo wkiwa faragha.

Unapocheza filamu ya mapenzi halafu mnyonyanye ndimi tena kwa kurudia zaidi ya mara tatu, inakuwa si sawa kwa vile kuna siku mzazi wa mmoja ama wahusika wote ataona mchezo ule pengine na akiwa na familia, kisha amuone mwanaye katika tukio lile.

Nasema haya kutokana na baadhi ya watu kushindwa kuwapa ruhusa wake au marafiki zao wa kike kwenda kushiriki kwenye tasnia hiyo kutokana na kile kinachofanyika huko.

Hebu tuangalie picha za nje za mapenzi hata za Kinigeria kama My love, True Love, Real Love, na za nje kama La Muja, Timeless nyingine kadhaa za Kihindi ambazo zinatazamwa kwenye ulimwengu wa filamu za mapenzi, huwezi kuona uchafu kama unaofanywa na baadhi ya waigizaji wa Tanzania na kwingineko.
Hisia unazitekaje kwa mpenzi wako?
NAAMINI rafiki zangu wote mtakuwa wazima wa afya njema, kama mimi na mpo tayari kuanza darasa hili jipya baada ya kumaliza somo lililopita last week. Karibuni tujifunze pamoja na ninaomba utayari wako ili uweze kuingiza kitu kipya ubongoni mwako.

Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kwamba, mapenzi ni furaha na kama upo kwenye uhusiano ambao una mateso na kila aina ya matatizo, basi ujue kwamba haupo sahihi. Hakuna masimango kwenye mapenzi, kunyanyasana na maumivu.

Tafsiri hasa ya mapenzi ni upendo, sasa kama ndivyo, si sahihi kuwa kwenye upendo, halafu chuki inachanganyika ndani yake. Hayo niliyoyataja hapo juu, mama yake ni chuki! Ndugu zangu, nirejee kusema tena kwamba uwanja wa huba ni mpana sana na unahitaji elimu kila wakati.

Wakati naandika mada hii ofisini, nilipata ugeni wa dharura. Nilipigiwa simu kutoka Mapokezi na kuelezwa kwamba nina wageni muhimu sana wanaonihitaji. Niliacha kwanza kuandaa mada hii na kuagiza waingizwe kwenye chumba cha mahojiano, kisha nikaenda.

Walikuwa wasichana wawili, ambao walionekana kuwa ni marafiki. Kwa kawaida huwa nakutana na wasomaji wangu (kwa mambo ya ushauri) kila Jumapili kwa kuweka ahadi maalumu, hivyo ujio wao haukunifanya nihisi kwamba walikuwa na shida ya mambo ya mapenzi.

Kwa haraka nikajua kwamba walikuwa na mambo mengine ya kihabari, lakini nilipowauliza, wakasema kwamba mmoja wao alitaka kuzungumza nami kwa kuwa alikuwa na hali mbaya sana katika uhusiano wake. Nikawapa utaratibu kuwa waje kuniona Jumapili (keshokutwa).

Pamoja na kuwapa utaratibu huo, waliomba sana kuzungumza nami kwa vile, mmoja wao alikuwa na tatizo kubwa. Haikuwezekana, nikamshauri nimpatie namba yangu maalumu ambayo angenipigia kwa muda niliompangia, hapo akasema: “Simu? Sawa, lakini tatizo ni kwamba ukinipigia atapokea... (mpenzi/mchumba/mume wake) simu yangu amei-divert kwake. Mh!

Anyway, nitakupigia huo muda.”
Tukaachana kwa ahadi kwamba angenipigia siku hiyo kwa muda ambao tulikubaliana.

TUNAJIFUNZA NINI?
Pamoja na kwamba sikuweza kuzungumza naye chochote mpaka naandika mada hii, niligundua mengi sana kutoka kwa dada yule ambaye kwa haraka nilimkadiria kuwa na umri kati ya miaka 22-28.

Ni msichana mrembo kwa kumtazama, lakini uso wake umepoteza matumaini. Anaonekana yupo kwenye uhusiano ambao kwake ni mateso. Nathubutu kusema kwamba, inawezekana kabisa yupo kwenye mapenzi ya utumwa.

rafiki zangu, inapofikia hatua mpenzi wako hakuamini kiasi kwamba ana-divert simu yako kwake, ujue hapo kuna tatizo. Niliagana na dada huyo nikimpa matumaini makubwa kwamba, tatizo lake lingeisha kwa kuwa hakuna kisicho na dawa.

Nilimwambia: “Samahani nashindwa kuongea na wewe sasa hivi kwa kuwa ni nje ya utaratibu, lakini pia nina majukumu mengi yanayonisubiri, ila nakuhakikishia tatizo lako limefika mwisho. Kwa kuwa umeonana na mimi, amini masaibu yako yameshapata dawa!”

Nashukuru aliondoka akitabasamu kidogo. Nilikuwa na matarajio makubwa ya kumpa dawa ya tatizo lake. Wiki ijayo nitawaletea mrejesho. Rafiki zangu, niliona hili liwe kama utangulizi wa somo letu.

HISIA NI NINI HASA?
Katika tafsiri ya kawaida hisia ni neno linalotokana na hisi, fikiri, buni. Kwenye uwanja wa mapenzi linanyambulishwa tofauti kabisa. Huku linajulikana kama mshawasha, mhemko, miliki n.k.

Kwa kifupi, hakuna tafsiri ya moja kwa moja ya neno hilo, lakini limebeba ile hali ya mwenzi kuwa na hamu, mapenzi, uhitaji zaidi kwa mwenzake. Ndiyo maana mtu anaweza akauliza, “Nitawezaje kuteka hisia za mpenzi wangu?”
Bila shaka tupo pamoja.

UNAZITEKAJE?
Hapo ndipo kwenye tatizo kwa watu wengi walio kwenye uhusiano. Wapo wasioweza kabisa kuteka hisia za wapenzi wao. Hawajui mbinu za kufanya hivyo. Rafiki zangu, suala la kumfanya mpenzi wako akupende, awe na hamu na wewe, akufikirie, asiwaze kukusaliti lipo mikononi mwako.

Ni kazi yako. Hapo unaanza na kujua ni mambo gani ambayo hayapendi na yapi anayapenda. Kujua jambo hilo, unakuwa unaelekea kwenye kuelewa namna ya kumaliza kabisa tatizo hilo.
Kuna ambao wapo kwenye uhusiano, halafu wanashangaa ghafla wapenzi wao wamebadilika.

Wanakuwa wakali bila sababu, wakorofi, hawana hamu ya kukutana nao faragha na mengine. Umewahi kujiuliza kwa nini? Jibu ni rahisi sana, AMEPOTEZA HISIA KWAKO!
Kama ndivyo, kazi ipo mikononi mwako ya kurejesha hisia hizo kama zamani. Yapo mambo mengi ambayo natakiwa kuzungumza na wewe kuhusu namna ya kurejesha hisia za mwenzi wako kwako. Ni rahisi sana, wiki ijayo nitakuletea.

Kitu kikubwa rafiki yangu, ninachotaka kukuacha nacho ni kwamba, matatizo mengi kwenye uhusiano husababishwa na kupoteza hisia. Mchunguze mpenzi wako, siku hizi anakukaripia? Anakusimanga? Hakusikilizi?

Anakudharau? Hapendi kukushirikisha kwenye mambo yake? Kama una matatizo haya ujue chanzo chake ni kupoteza hisia. Kazi yangu mimi ni kurejesha amani katika uhusiano wako.

JE NGONO NI KIPIMO CHA MAPENZI YA DHATI...? TUSOME PAMOJA TUELEWE

 

Wanaume wengi wanatumia kigezo hiki kama kuthibitisha au kudhihirisha mapenzi ya dhati. Utamsikia mwingine anasema: “Sasa kama hutaki kufanya mapenzi na mimi, utakuwa hunipendi.”


Kwa sababu wanawake nao wanaogopa kuachwa au wanatamani ndoa, kwa kuamini kwamba tendo hilo ni kila kitu wanajikuta wakikubali; sasa hapo inategemea, mwisho unaweza kuwa mzuri au mbaya!

MAPENZI NI NINI HASA?
Kila mmoja anaweza kuwa na maana yake, lakini kimsingi mapenzi hayana maana ya moja kwa moja! Kwa ujumla mapenzi ni hisia zenye msisimko wa pendo la dhati zinazotoka moyoni mwa mmoja kwenda kwa mwingine.

Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja watahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo.

Tafsiri hii nimewahi kuitaja mara kadhaa katika makala zangu, kama wewe ni mdau wa kona hii utakuwa unakumbuka, kama ndiyo kwanza unasoma hapa, basi si vibaya maana utakuwa umeingiza kitu kichwani mwako.

Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi sawasawa. Wapo wanaofikiria mapenzi ni ngono au ngono ni sehemu ya mapenzi. Hawa nitapingana napo kwa nguvu zangu zote.



HAKUNA ugonjwa mbaya kama utumwa wa fikra. Yaani uwezo wako wa kufikiria kuwa mikononi mwa mtu. Kwa maneno mengine naweza kusema kwamba, kukubaliana na jambo ambalo huna uhakika nalo, lakini kwa sababu wengi wanaamini na wewe unafuata mkumbo bila kuangalia athari zake.

Eti wakifanya mapenzi na wapenzi wao, ndiyo wataonesha kuwa wanawapenda! Ni sahihi kweli? Si sawa...

Msichana ambaye ameutunza usichana wake kwa miaka 22, auharibu kwa mtu mwenye tamaa zake halafu amuache? Nasema hapana...ni afadhali uendelee kuvumilia mpaka kwenye ndoa. Kwanza hakuna uvumilivu hapo; uvumilie nini wakati hujawahi kujaribu?

Heshima ya usichana wako ni zawadi nzuri sana kwa mwanaume ambaye ameitambua thamani yako na kuamua kufunga na wewe ndoa. Huyo ndiye anayestahili. Ikiwa utaamua kwa hiyari yako kutoa penzi, ni wewe tu, lakini isiwe kwa sababu ya kuonesha mapenzi.

LAZIMA NGONO?

Hakuna ulazima, wala faragha si kiashirio cha mapenzi ya dhati. Ngono ni kitu kingine na mapenzi ni kitu kingine. Hivi ni vitu viwili ambavyo havina uhusiano wowote. Asitokee mtu akakudanganya kwamba kwa kutoa penzi ndipo utaonesha unavyompenda. Si kweli. Kimsingi ngono huja baada ya tamaa kuingia kati ya wawili wanaopendana.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa, ukawa na tamaa ya kufanya ngono na mtu hata kama huna mapenzi katika moyo wako. Kimsingi suala la kufanya ngono siyo kithibitisho cha kuonesha mapenzi ya dhati.

Baadhi ya walio katika uhusiano, hudanyanywa na kipengele hiki. Utakuta msichana anaambiwa na ‘boyfriend’ wake kwamba ili aoneshe kuwa anampenda basi lazima akubali kufanya naye ngono.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kufanya hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa penzi hilo kuyeyuka! Ni kweli ni rahisi kuachwa kwenye mataa hasa kama mhusika alikuwa ameshikwa na tamaa badala ya mapenzi ya dhati.

MUDA GANI NI SAHIHI?

Kimsingi suala la kufanya mapenzi halina kanuni, hakuna muda maalum wa kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wako mpya. Ngono ni hisia tu, tena basi huwa bora zaidi kama hisia hizo zikaja kwa wakati mmoja kati yako na huyo unayempenda.

Wataalam wa saikolojia ya mapenzi, wanashauri wapenzi wasishiriki tendo hilo mpaka pale watapokuwa wamefahamiana kiasi cha kutosha juu ya tabia zao na historia waliizopitia. Pamoja na hayo, suala la ngono halikwepeki ikiwa mtaruhusu kukutana sehemu tulivu mkiwa wawili.

Jambo la msingi ni kutulia na kujipanga, msifanye ngono kama sehemu ya mapenzi. Tambua kuwa ngono ni kitu kingine na mapenzi ni kitu kingine. Hata kama mtakuwa mmeamua kushiriki kitendo hicho, mfahamu kuwa mnastarehesha nafsi zenu tu na siyo kuoneshana mapenzi ya dhati.

TATIZO LIKO WAPI?

Tafiti mbalimbali za wataalam wa mambo ya uhusiano, zinaonesha kuwa wengi walio katika uhusiano huwa hawawezi kuvumilia kuendelea kuwepo katika uhusiano bila ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, tafiti hizo za uhakika zinaeleza kuwa baada ya wapenzi kufanya ngono, ile hamu ya kuendelea kuwa pamoja hupungua!

Hiyo husababishwa na dharau za kimaumbile na kujihakikishia kuwa hakuna kitu asichokijua kwa patna wake. Wengi hulia baada ya kujikuta wakiingia katika mkumbo huu. Hebu jiulize, kama anakupenda, kwa nini ang’ang’anie kufanya mapenzi haraka?

Wewe ni wake na huenda mna ndoto za kuishi pamoja siku moja, kwa nini asivumilie mpaka wakati huo? Akitaka anaweza kuvumilia na kufaidi mambo hayo mkiwa katika ndoa.

NINI BADALA YA NGONO?

Yapo mambo mengi sana ya kufanya badala ya ngono, huna sababu ya kutoa kipaumbele kwenye ngono wakati kuna vitu vingine vingi unavyoweza kuvifanya na kuyafanya mapenzi yenu yakaendelea kudumu kila siku.

Mnaweza kukaa sehemu nzuri yenye utulivu kwa ajili kupanga maisha yenu ya baadaye. Epukeni sehemu zenye vificho, ambazo zinaweza kuwapa vishawishi vya kufanya mapenzi. Lakini pia, kutoka pamoja mitoko maalum hususan wikiendi hunogesha zaidi mapenzi.

Hata hivyo, kutumiana zawadi ni njia nyingine ambayo inaweza kunogesha penzi lenu na kuweka mambo ya ngono pembeni. Amini usiamini rafiki yangu, suala la faragha si muhimu sana katika uhusiano hasa unapokuwa mchanga. Mkifikia uamuzi huu ni lazima wote wawili mjadiliane na kufikia muafaka kabla ya kukimbilia, mwishowe ukaingia kwenye majuto. 

MAMBO MANNE YA KUFANYA KWA MPENZI WAKO ILI AKUOE HARAKA

Hoja kubwa ya msingi leo ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba, hapa tunazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.
Leo nazungumzia juu ya wewe ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa unaitaka. Unajua cha kufanya? Soma hapa chini mambo ya kufanya ili mpenzi uliyenaye akuoe haraka...

1.EPUKA MAKUNDI MABAYA
Mwanaume anapenda kuwa na mke mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya ‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.
Lakini yawezekana, jamaa alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa mbali na makundi ya wanawake hatari! 

2. ZINGATIA MAVAZI YAKO
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo, mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu anapenda nini na nini anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo. Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi, lakini swali la msingi, mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim anaona sehemu zako za faragha hadharani?
Ukiachana na chaguo la mwenzi wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue! Jisitiri vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili wako ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.

3. JIPE MOYO
Hili nilishawahi kulizungumza sana katika mada zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya kuolewa au watahangaika sana lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
Mwingine anajinyima mwenyewe nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.
Unaitengeneza kwa misingi ya kwanza, kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo baadaye.
Iko hivi, ukianza kujishusha mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani moyoni, hapo sasa ni mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa mtindo huo.
4. ACHA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi. Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia kumfanya jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake yanaweza kumpa picha tofauti.

Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu

FANYA HAYA KUMNASA MPENZI ALIYE NA MPENZI WAKE

Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.

Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.


Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.

Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.

Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.

Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.

Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?

Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.

Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.

Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.

Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.

Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.

Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.

Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.

Urafiki ni poa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.

Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

 

Mambo ya kuzingatia unapomtumia mpenzi wako zawadi



Nazungumzia ishu ya wapenzi kununuliana zawadi. Hapa sizungumzii zawadi ambazo wengi wetu tumekuwa tukinunuliana siku za Sikukuu kama vile Iddi, Krismasi, Valentine na nyinginezo bali namaanisha zawadi nje ya siku hizo.Kumtumia mwenzi wako zawadi ni kati ya mambo ambayo humfanya afurahie uhusiano wake na wewe. Hata hivyo, hakuna zawadi za moja kwa moja ambazo ni rasmi kwa ajili ya wapenzi lakini ni vyema ukamtumia zawadi kulingana na mapenzi yake zaidi.Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi mwenzi wako, unaweza kujua zawadi gani ni nzuri zaidi kwake au anayopendelea kuliko aina nyingine.Wiki hii nimechambua aina kuu za zawadi ambazo ukimtumia mpenzi wako utamteka hisia zake na ataona unamjali.MavaziMavazi ni kati ya zawadi ambazo zitamfanya mpenzi wako azidi kukupenda na kuwa karibu zaidi na wewe. Aina ya nguo ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ni zile ambazo unaamini atavutiwa nazo au zile ambazo zitampendeza na kumfanya aonekane nadhifu.Hata hivyo, zipo aina za mavazi ambazo zimependekezwa zaidi kwa ajili ya wenzi kutumiana wanapokuwa mbali na hata wanapokuwa karibu.
Kama wewe ni mwanamke unataka kumtumia mpenzi wako wa kiume, mavazi yafuatayo yanafaa zaidi. Saa nzuri ya mkononi, nguo za ndani, lakini lazima uzingatie rangi ya bluu, bluu bahari au nyeupe kimsingi zisiwe za rangi zinazoficha uchafu.
Zingine ni fulana za ndani ‘singlendi’, fulana, mkanda wa suruali, simu ya mkononi, vitambaa vya jasho n.k. Hakikisha katika zawadi hizo, unaambatanisha na manukato mazuri hasa yale ambayo unajua atayapenda.Haishauriwi kumtumia suruali au shati kwa sababu inaweza kuwa kubwa au ndogo, hivyo kupunguza ladha ya zawadi hasa kama atakuwa ameipenda sana.
Zawadi za aina hiyo, unaweza kumpa mwenzi wako ofa ya kwenda kuchagua moja kwa moja dukani lakini kama unajua saizi yake na una uhakika akivaa atapendeza, ruksa kumnunulia vitu hivyo na tena utakapopatia saizi yake vizuri ataamini uko makini naye na unampenda kwa dhati.
Kama wewe ni mwanaume na unataka kumtumia mpenzi wako wa kike zawadi, lazima uwe makini sana! Mavazi yaliyopendekezwa hapa ni pamoja na batiki (gauni, blauzi na sketi, blauzi yenyewe n.k), hereni, bangili, mkufu, simu ya mkononi, saa ya mkononi, nguo za ndani (kulingana na mapendekezo yake, kwa jinsi umjuavyo), sidiria, viatu n.k.Kama umesoma vizuri utaona mwanamke anaweza kununuliwa vitu vingi zaidi (hasa nguo) tofauti na mwanaume. Hii inatokana na aina za mavazi na saizi zao kukaririka kirahisi zaidi au kutokuwa na saizi ya moja kwa moja. Mathalan, batiki, sketi na blauzi na vinginevyo. Kama kawaida, mavazi haya, ambatanisha na manukato mazuri, hasa yale ambayo ndiyo anayopendelea mpenzi wako.Maua pia ni kati ya zawadi zinazopendekezwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi. Maua ni mazuri sana kwa mwezi aliye mbali, lakini ni vyema kuzingatia na umbali uliopo kati yenu, kwani maua huweza kusinyaa kabla ya kumfikia (hasa kama ukimtumia yale halisi, kwani ndiyo haswa mazuri).
Hata hivyo, zipo zawadi nyingine ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kwa kuangalia vitu anavyovipenda sana.Hii ni njia pekee ya kuonesha ubunifu wako na jinsi unavyomjali hata akiwa mbali kwa kumtumia vitu ambavyo huwa anavipenda lakini alipo hawezi kuvipata! Mathalan, mpenzi wako anapenda sana zabibu lakini amekwenda mkoa ambao vitu hivyo havipatikani kwa urahisi, hii ni nafasi yako kumtumia.Mathalan unajua kabisa anapenda sana kusoma vitabu lakini sehemu aliyopo hawezi kupata, basi nunua majarida, magazeti na matoleo yote ambayo hajayapata kisha mtumie, hakika utakuwa umemfurahisha sana na kumfanya afurahi kupata vitu hivyo. Kwa leo naomba niishie hapo, lengo ni kukufahamisha kwamba zawadi ni kitu muhimu sana katika kuliboresha penzi lenu. Kwanza mpenzi wako aamini kwamba unampenda lakini pia unamjali.

Nazungumzia ishu ya wapenzi kununuliana zawadi. Hapa sizungumzii zawadi ambazo wengi wetu tumekuwa tukinunuliana siku za Sikukuu kama vile Iddi, Krismasi, Valentine na nyinginezo bali namaanisha zawadi nje ya siku hizo.
Kumtumia mwenzi wako zawadi ni kati ya mambo ambayo humfanya afurahie uhusiano wake na wewe. Hata hivyo, hakuna zawadi za moja kwa moja ambazo ni rasmi kwa ajili ya wapenzi lakini ni vyema ukamtumia zawadi kulingana na mapenzi yake zaidi.
Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi mwenzi wako, unaweza kujua zawadi gani ni nzuri zaidi kwake au anayopendelea kuliko aina nyingine.
Wiki hii nimechambua aina kuu za zawadi ambazo ukimtumia mpenzi wako utamteka hisia zake na ataona unamjali.
Mavazi
Mavazi ni kati ya zawadi ambazo zitamfanya mpenzi wako azidi kukupenda na kuwa karibu zaidi na wewe.
Aina ya nguo ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ni zile ambazo unaamini atavutiwa nazo au zile ambazo zitampendeza na kumfanya aonekane nadhifu.Hata hivyo, zipo aina za mavazi ambazo zimependekezwa zaidi kwa ajili ya wenzi kutumiana wanapokuwa mbali na hata wanapokuwa karibu.

Kama wewe ni mwanamke unataka kumtumia mpenzi wako wa kiume, mavazi yafuatayo yanafaa zaidi. Saa nzuri ya mkononi, nguo za ndani, lakini lazima uzingatie rangi ya bluu, bluu bahari au nyeupe kimsingi zisiwe za rangi zinazoficha uchafu.

Zingine ni fulana za ndani ‘singlendi’, fulana, mkanda wa suruali, simu ya mkononi, vitambaa vya jasho n.k. Hakikisha katika zawadi hizo, unaambatanisha na manukato mazuri hasa yale ambayo unajua atayapenda.
Haishauriwi kumtumia suruali au shati kwa sababu inaweza kuwa kubwa au ndogo, hivyo kupunguza ladha ya zawadi hasa kama atakuwa ameipenda sana.

Zawadi za aina hiyo, unaweza kumpa mwenzi wako ofa ya kwenda kuchagua moja kwa moja dukani lakini kama unajua saizi yake na una uhakika akivaa atapendeza, ruksa kumnunulia vitu hivyo na tena utakapopatia saizi yake vizuri ataamini uko makini naye na unampenda kwa dhati.

Kama wewe ni mwanaume na unataka kumtumia mpenzi wako wa kike zawadi, lazima uwe makini sana! Mavazi yaliyopendekezwa hapa ni pamoja na batiki (gauni, blauzi na sketi, blauzi yenyewe n.k), hereni, bangili, mkufu, simu ya mkononi, saa ya mkononi, nguo za ndani (kulingana na mapendekezo yake, kwa jinsi umjuavyo), sidiria, viatu n.k.
Kama umesoma vizuri utaona mwanamke anaweza kununuliwa vitu vingi zaidi (hasa nguo) tofauti na mwanaume. Hii inatokana na aina za mavazi na saizi zao kukaririka kirahisi zaidi au kutokuwa na saizi ya moja kwa moja. Mathalan, batiki, sketi na blauzi na vinginevyo. Kama kawaida, mavazi haya, ambatanisha na manukato mazuri, hasa yale ambayo ndiyo anayopendelea mpenzi wako.
Maua pia ni kati ya zawadi zinazopendekezwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi. Maua ni mazuri sana kwa mwezi aliye mbali, lakini ni vyema kuzingatia na umbali uliopo kati yenu, kwani maua huweza kusinyaa kabla ya kumfikia (hasa kama ukimtumia yale halisi, kwani ndiyo haswa mazuri).

Hata hivyo, zipo zawadi nyingine ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kwa kuangalia vitu anavyovipenda sana.
Hii ni njia pekee ya kuonesha ubunifu wako na jinsi unavyomjali hata akiwa mbali kwa kumtumia vitu ambavyo huwa anavipenda lakini alipo hawezi kuvipata!
Mathalan, mpenzi wako anapenda sana zabibu lakini amekwenda mkoa ambao vitu hivyo havipatikani kwa urahisi, hii ni nafasi yako kumtumia.
Mathalan unajua kabisa anapenda sana kusoma vitabu lakini sehemu aliyopo hawezi kupata, basi nunua majarida, magazeti na matoleo yote ambayo hajayapata kisha mtumie, hakika utakuwa umemfurahisha sana na kumfanya afurahi kupata vitu hivyo.
Kwa leo naomba niishie hapo, lengo ni kukufahamisha kwamba zawadi ni kitu muhimu sana katika kuliboresha penzi lenu. Kwanza mpenzi wako aamini kwamba unampenda lakini pia unamjali.

NINI TOFAUTI KATI YA KUFIKA KILELE NA KUKOJOA MKOJO KWA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA


Mimi ni mwanamke wa miaka 30 tatizo kubwa linalonitatiza ni kuwa wakati wa kungonoka na mr. Nitajuaje kama nami pia nimekojoa?? huwa napata mtihani mkubwa sana sijui kama nishawahi "kukojoa" au la!
Kuna siku nyingine huwa napata raha up to the maximum yaani hadi nalia machozi kabisa sasa sijui huwa huko ndio "nakojoa" kwenyewe au ni mautamu tu?
Jawabu:
Utamu unaousikia to the maximum ndio kufika kileleni kwenyewe au unaweza kusema kukojoa japokuwa hutoi maji mengi kama baadhi ya wanawake, Ikiwa unasikia huo utamu, ukalia na kupiga kelele na kuhisi umajimaji umekuzidi ukeni na kutotaka kuendelea kwa muda yaani unakuwa too relaxed huku misuli ya uke ikimwenyua-mwenyua(kubana na kuachia) basi ujue umekojoa yaani umefikia mwisho wa safari...


Kuhisi kutaka kukojoa-Sehemu kubwa ya wachangiaji wamefananisha au kulinganisha hisia za kutaka kufika kileleni na zile za kuhisi kutaka kukojoa. Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa lakini kama wewe ni mwanamke ambae hujawahi ufika kileleni na hujui hisia za utamu wa ngono ni wazi kuwa utadhani hisia hizo za kutaka kukojoa (mkojo wa kawaida yaani empting your bladder) ndio kufika kileleni kwenyewe lakini sio.


Baadhi ya wanwake huwa wanahisi hisia hizo za kutaka kukojoa mara tu uume unapoingia na hapo ndio huwa wanadhani kuwa huo ndio utamu wa Ngono unaopatikana kwa kusuguliwa kipele G, vilevile wapo ambao wanapata hisia hizo tendo likiendelea kwamuda mrefu na kudhania sasa wanafikia mshindo na kuachi makojo (kwa kawaida).....hufurahia wakihisi "nafuu" lakini unapofika kileleni au kukojoa kutokana na utamu wa ngono husikii "relief" (nafuu) kama ile ya ku-empty bladder, unasikia utamu wa hali ya juu yaani unaweza kutamani mchezo uendee tena na tena na wakati huo huo utahisi uke wako ukimwenyua mwenyua yaani kama unafunga na kuachia(kama unavyokaza misuli ya uke) which huwezi kufanya hivyo unapokojoa.....

Unajua wakati mwingine ngono ya kuingiliana (uume ndani ya uke) huwa ina-irritates the bladder(kifuko cha mkojo) na kukufanya wewe uhisi kutaka kukojoa kila unapofanya ngono nitakushauri ukamuona"Gynecologist" ili kuhakikisha kuwa huna tatizo la kitibabu ambalo linaweza kabisa kuwa Saratani au inawezekana una tatizo linaitwa Orgasmic dysfunction kwamba hujawahi kupata Kilele kwa namna yeyote ile (kama nilivyosema awali) hivyo basi upata hisia za kutaka kukojoa na unaweza kufurahia hisia hizo ukidhani ndio unafika kileleni lakini sio kilele bali kibofu chako kimejaa au kimesumbuliwa na kusababisha hisia hizo.


UNATONGOZWA OVYO NA WANAUME...? DAWA NDIO HII

http://clutchmag.s3.amazonaws.com/wp-content/uploads/2012/10/Black-Woman-Exercising1.jpg 
Leo nimeona nizungumze juu ya tabia ya baadhi ya wanawake kutongozwa hovyo. Kiukweli ni tabia ambayo inakera. Kila ukipita huku unaitwa, ukienda kule unaitwa, hili tatizo lipo kwa wanawake wengi hasa wa mijini.
Kiukweli hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunapoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwatomasa tomasa sehemu zao nyeti bila ridhaa yao. Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao.

Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao. Hata hivyo, ili kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye.

Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana! Hizi hapa chini baadhi ya njia muhimu za kukabiliana na tatizo hilo la kusumbuliwa hivyo na wanaume.

MAVAZI YAKO YAKOJE?
Wanawake wengi sana hukosea katika suala zima la uvaaji. Baadhi yao hupendelea kuvaa mavazi yanayoonesha maungo yao kiasi cha baadhi ya wanaume kuwachukulia kuwa ni machangudoa.

Ni kweli kwamba mavazi ya mtu hayawezi kumfanya akaingizwa katika kundi la watu fulani na pia kila mtu anao uhuru wa kuchagua avaeje lakini, kwa uhalisia mwanamke asiyeujali mwili wake kwa kuvaa nguo zisizokuwa na heshima, asitarajie kuuepuka usumbufu wa wanaume wapenda ngono. Ni lazima watamtongoza na wakati mwingine kumfanyia vitendo vya kumdhalilisha.

Hivi mwanamke kuvaa ‘kitop’ na suruali inayobana huku ikionesha shepu ya sehemu zako nyeti kisha kukatiza mbele za wanaume kutakuwa kunamaanisha nini kama siyo kujitangaza kwao? Hivi kwa mavazi hayo utakuwa na tofauti gani na wale wanaoijiuza kule Ohio?

Ifike wakati uondokane na ulimbukeni wa kwenda na wakati hasa kwa wewe mwanamke ambaye umeolewa ama una mpenzi wako. Vaa mavazi ya heshima kila unapokwenda.

Mavazi yanayoonesha maungo yako yavae ukiwa na mpenzi wako chumbani. Naamini kwa kuvaa hivyo, kidogo utakuwa unapunguza ile kasi ya wanaume wakware kukusumbua.

TABIA ZAKO VIPI?
Baadhi ya wanawake acha wasumbuliwe kwani tabia zao huwafanya wasiheshimike mbele ya jamii na kuonekana kwamba ni jalala. Unakuta mwanamke anapita mbele za wanaume kisha anatembea kwa kujishebedua huku akitingisha maungo yake makusudi, hapo unatarajia nini?

Achilia mbali hilo, wapo baadhi ya wanawake ambao ni rahisi kuchukuliwa na wanaume. Yaani hawawezi kusema hapana! Ukiwa na tabia hiyo tambua kuwa, kila mwanaume mkware atataka kuweka mhuri wake mwilini mwako.

USITANIANE NA WANAUME!
Wanawake wengine ni wa ajabu sana. Unamkuta anajenga ukaribu sana na baadhi ya wanaume na kufikia hatua ya kutaniana nao katika mambo ambayo mwishowe huwa kutongozana.

Mwanamke aliyeolewa ama mwenye mpenzi wake hatakiwi kujenga ukaribu sana na wanaume wa pembeni. Unapopita maskani wamekaa wavulana, wasalimie kisha chukua hamsini zako, utani wa kijinga epukana nao kwani mwishoni watakutongoza na ukionesha kuchukia watadai walikuwa wanakutania kumbe wako ‘sirias’.

MWAMBIE MPENZI WAKO
Sishauri kila mwanaume atakayekuchomekea umwambie mpenzi wako. Nasema hivyo kwa kuwa, natambua itageuka kero kwa mwenza wako. Ila sasa wapo wanaume ambao ni ving’ang’anizi. Unamweleza kuwa una mpenzi wako lakini hakuelewi ni vema ukamtaarifu mumeo ili akae akijua.

Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya. Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza!

Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.

Wanaume wa siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.

Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala, kwamba kila mtu anaweza kumchezea. Naamini msimamo huo pamoja na mambo hayo niliyoyataja hapo juu unaweza kuepukana na usumbufu huo kutoka kwa wanaume.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa