Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label wema. Show all posts
Showing posts with label wema. Show all posts

HII NDIO KAULI YA KAJALA BAADA KUSADIKIKA KUPIGWA CHINI NA WEMA

“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika, mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha, au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper ni rafiki yangu”

MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA......



TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevujaKwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

 

MKOROGO WAMUAHARIBU WEMA SEPETU....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006..
Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....
 Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani....
Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni...
"Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo"...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar

Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huyo, mwandishi  wetu  alitinga  nyumbani  kwa  Wema  Sepetu  kufanya  naye  mahojiano  juu  ya jambo  hili
Alipofika  nyumbani  hapo, mwandishi  wetu  aligonga  geti  na  kufunguliwa  na  dada  mmoja  ambaye  alidai  kuwa  maadam Wema  alikuwa  amelala  na  kwamba  hawezi  kuamshwa mpaka  aamke  mwenyewe..

WEMA NA KAJALA WAMWAGANA.......

Wema katika pozi na Kajala.
Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.
SIKU KAMA HIZI
“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu?
“Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.
Wema akimlisha keki Kajala wakati wa sherehe ya kumkaribisha uraiani.
TATIZO NI WAPAMBE
“Hapo ndiyo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao.
“Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu.
“Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.
KUMBE ALIMKOSESHA DILI?
“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake.
“Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.
TATIZO MILIONI 13?
“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).
“Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?
SASA NI KUNUNIANA KWA KWENDA MBELE
“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.”
Baada ya kupata habari hizo,tulimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.
NYUMBANI KWA WEMA
Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.
MENEJA WAKE ANASEMAJE?
Hata hivyo, tulibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu.
“Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”
WEMA ANAUMWA NINI?
Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”
HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, tulimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema.
Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa