Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label msanii wa wiki. Show all posts
Showing posts with label msanii wa wiki. Show all posts

KUTANA NA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM "MILLAD AYO " FAHAMU MAISHA YAKE TOKA AMEZALIWA MPAKA SASA



Millard Afrael Ayo alizaliwa Arusha January 26 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Afrael Ayo ambae ni mmeru wa Akheri Tengeru, ni mfanyabiashara na mama Mary Ayo ni mwalimu.

Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Millard, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 12 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 16 mwaka 2002, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Patandi Primary School Tengeru, Akeri Secondary School na Mbezi beach high school..........

Wakati akisubiri majibu, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Millard arudishwe shule kuendelea na masomo ya sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa Millard kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule.

Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Gabriel aliekua Marekani aliporudi Tanzania na kumshawishi mama Millard amuache mtoto afanye kile anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Millard akapata nafasi ya kwenda kujiunga na East Africa Training Institute kusomea utangazaji na uandishi wa habari mwaka 2004.

Baada ya mwaka mmoja Millard alijiunga na TVZ Zanzibar kwa muda wa miezi mitano na akarejea Dar es salaam April 2005 kutafuta kazi baada ya hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza na masomo.

Alifanikiwa kupata kazi May 23 2005 kwenye kituo cha Wapo Radio 98.0 ambayo aliambiwa hatolipwa kwa sababu kanisa lililokua linamiliki radio hiyo halina pesa ila kwa sababu alikua na njaa ya maisha na kazi ilibidi aifanye kama ameajiriwa, kazi ilikua jumatatu mpaka jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi huku kazi yake kubwa aliyopangiwa ni kukusanya habari za bei za bidhaa na hali ya usafi kwenye masoko Dar es salaam, pia kwenda kitengo cha MOI Muhimbili hospitali kuchukua habari za majeruhi na vifo vya ajali mbalimbali.

Kutokana na jitihada hizo Millard alianza kulipwa shilingi elfu tano kwa wiki mwezi wa pili baada ya kazi hivyo akawa na mshahara wa elfu 20 kwa mwezi, mshahara ambao uliongezeka na kufikia elfu 20 kwa mwezi kwenye mwaka wa tatu na wa mwisho akiwa Wapo Radio.

Baada ya hapo Millard alijiunga na ITV/Radio One mwaka 2008 ambako alisikika kwenye vipindi mbalimbali lakini MILAZO 101 na habari za michezo ITV ndio vilimpa umaarufu mpaka November 2010 alipojiunga na Clouds FM/TV na kuanza kusikika kwenye kipindi cha AMPLIFAYA december 6 2010 na baadae kukabidhiwa CLOUDS FM Top 20 June 2013.

Mpaka sasa Millard Ayo ni mmiliki wa tuzo 4 ikiwemo ya Mtangazaji bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom Tanzania na African Stars, na moja ni ya heshima akiwa mwandishi pekee kutunukiwa kutoka kwenye familia ya Marehemu mwigizaji Steven Kanumba.

Kipindi cha AMPLIFAYA pamoja na website yake ya millardayo.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke.

Kitu ambacho watu wengi hawakifahamu, kipaji cha Millard Ayo kilionekana kwanza na aliyekua mtangazaji wa TBC1 Joseph Msami ambae kwa wakati huo ndio aliona uwezo wa Millard na kumshawishi boss wa Wapo radio kutoa ruhusa ya Millard kuingizwa studio kuwa mtangazaji na sio tena ripota.

Mtu wa pili ambae ndio alizidi kumnyanyua Millard kiutangazaji ni Godwin Gondwe ambae alimuona Millard toka akiwa Wapo Radio, kwanza ndio alikua mtu wa kwanza kumpa Millard dili la kurekodi tangazo la radio la bei kubwa 2007 toka ameanza utangazaji, lilikua la laki moja na nusu za Kitanzania na ndio ilikua pesa kubwa Millard kuwahi kulipwa kwa kazi ya mikono yake toka azaliwe, na ni pesa kubwa kuliko hata mshahara wake kwa mwezi wakati huo ambao ulikua shilingi elfu sitini.

Shukrani za pekee kwa Reginald Mengi, Joyce Muhavile, Julius Nyaisanga, Deogratius Rweyunga, Abdallah Mwaipaya na Isack Gamba ambao walikua kama wazazi/marafiki wakati Millard akiwa ITV, pamoja na kwamba kwa sasa hayupo ITV lakini urafiki wao haujaisha na Millard amekua balozi wao mzuri

Watu wengine waliomfikisha Millard hapa alipo kwa kiasi kikubwa ni Gardner G Habash ambae wakati Millard akiwa Wapo Radio alimsaidia sana kumpa nafasi ya kusikilizwa Clouds FM ambako alipata kazi ya kuanza na kipindi cha gospel lakini wiki hiyohiyo ndio akaitwa ITV, Reuben Ndege nae alicheza kwenye uwanja mkubwa zaidi kumsuka Millard Ayo alipojiunga na Clouds FM na alijaribu sana kumshawishi Millard kujiunga nao wakati akiwa Radio One, kiukweli siku zote amekua msaada mkubwa wakati wote na supporter mkubwa kwa Millard.

Sebastian Maganga ambae ni mkuu wa vipindi Clouds FM amekua msaada mkubwa sana kwa Millard Ayo, mshauri na hata ndugu ambae ni msikilizaji mzuri sana pale Millard anapozungumza nae na ndio alipendekeza Millard kuchukuliwa Radio One wakati huo.

Ruge Mutahaba amekua boss, kaka, mshkaji na mshauri wakati wote kwa Millard Ayo, kwa kiasi kikubwa pamoja na kwamba alitoa idhini ya Millard kujiunga na familia aliyokua anaipenda kwa zaidi ya miaka 10, amekua ni msaada mkubwa sana kwa Millard, kuna vitu vingi Millard alikua anasema hawezi lakini Ruge amempa neno na kumpa nguvu kwamba anaweza na ndio mafanikio ya Millard yameanza kuonekana hapo.

Big Boss Joseph Kusaga ambae ndio MD wa Clouds FM, nae amekua mshkaji, boss na kaka kwa Millard Ayo, nguvu ya neno lake kwamba ‘i’am proud of you’ pekee ndio linampa Millard Ayo nguvu kubwa ya kujituma zaidi na kutumia saa kadhaa kuandaa vipindi vyake siku zote na kujituma zaidi.

MFAHAMU FEZA KESSY AMBAYE NI MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA

Hii ni makala iliyoandikwa kwenye jarida la Mzuka  miezi kadhaa iliyopita yenye kichwa cha habari kisemacho ‘Feza Kessy arudi kwenye muziki, asema, ‘I am taking it very seriously’. Feza ni mmoja kati ya watanzania wawili wanaoiwakilisha Tanzania mwaka huu kwenye shindano la Big Brother Africa.
DSC_6900
Mawimbi ya vituo vya radio nchini Tanzania yako mbioni kuvamiwa na sauti mpya ya msichana anayejulikana zaidi katika fani ya umiss. Ni aliyekuwa Miss Dar City Centre na Miss Ilala mwala 2005, mrembo Feza Kessy. Ameamua kuingia kwenye muziki kwa asilimia mia moja na anasema muziki ulikuwa, na ni kila kitu kwake hata kabla ya kushiriki Miss Tanzania.  imefanya mahojiano exclusive na mama huyu wa mtoto mmoja kujua amejiandaaje kuingia kwenye soko gumu la muziki wa Tanzania. Anaanza kwa kuelezea kwanini ameamu kufanya muziki sasa na sio zamani.
“Basically condition ya nyumbani ilikuwa lazima nimalize shule. When I went for Miss Tanzania 2005 I was not really not of a miss miss, ilikuwa opportunity yangu mimi kushow my talent on music which I did na nikashinda a couple of talent shows. After that sasa my mom akasema ‘Okay if that is what you want to do, fanya’. Then nikaenda chuo England and I had a baby and ikawa ngumu kustart up a career na mtoto mdogo. So nilipomaliza nimerudi nina mtoto wangu ni mkubwa, I said this is my passion let me do it again.
Niliporudi nikaamua nianze tena because now my son ni mkubwa,now I can handle being a mother and my career naweza nika handle , so I decided this is time.”
Mtoto wako ana umri gani sasa hivi? Ana miaka mitatu na nusu, ambae ulimpatia huko huko England? Ndio, Manchester. Na mzungu ama na mwezetu? na mwenzetu (anacheka) Siyo Lucci lakini (anacheka tena) Hapana.
Siyo kwamba lucci alikushawishi kwa kiasi fulani ufanye muziki tena?
Not really, no, when I met Lucci sikumjua Lucci ni producer na yeye hakujua kama I have a passion ya kuimba we just met, I have known him for so long tangia……. Me I was born and raised in Arusha, so nilikuwa nilikuwa namjua tangu Arusha. So when we met as friends and started dating nilikuwa sijui he is a producer sababu tulikuwa hatujaonana miaka mingi, yeye alikuwa nje na mimi nilikuwa nje. But then obviously nika find out he is a producer na mimi naimba so we worked for some music together, it was a good combination, but sio kwamba yeye alinishawishi, No! I was already doing this na yeye pia he was doing his things.
Unaimba style gani? Unarap, unaimba R&B ama?
(Anacheka) Kila kitu!! I would say my music is afro pop, R&B, Soul and I rap kidogo.

Sasa hivi upo studio umeshafanya ngoma na Nash, bila shaka unarekodi nyimbo zingine, so lini tutegemee kuanza kumsikia Feza Kessy hewani?

End of November my first single hopefully………sijajua single itakuwa ipi, ipi kabisa but definitely my single ningependa iwe with a song that I did with Luchi, inaitwa ‘Strong Woman’. I am giving you an exclusive. Inaitwa strong woman it’s talking about just a strong woman kwenye society as Tanzania, as me being a single mother. And Luchi is a different producer compared na hawa producers wengine. It’s different music but at the same time is Tanzanian music on a different level. So I believe inaweza kuwa the perfect single for me to bring out late November.
DSC_6876
Kwanini unasema Luchi ni tofauti na maproducer wengine, naona kama unampendelea kwakuwa ni mzee!

(Anacheka) First of all sio mzee, he is my ex, hatupo pamoja, Ni washkaji, I respect him because he is very talented unajua just because he is my ex it doesn’t mean I don’t respect what he does. He is very talented, he is very different and another reason kwanini mpaka leo sijatoa any song cause nimerekodi a lot of things lakini ni ngumu kurelate producers, sio kwamba wanafanya kazi mbaya, it’s just a style that I’m doing inatofautiana, you know you go somewhere anakupa beat ambayo it’s not really me, sijui kama unanielewa!! When I am with Luchi or Lamar pia I can work with. Sio kwamba he is the best wherever but he is very talented.
Mpaka sasa umesharekodi ngoma ngapi? Na zote amefanya Luchi?
Four. Hapana nimefanya na Luchi nyimbo tatu. Hizo zingine zipo with different producers which I can’t mention now but ni wengine tofauti tofauti. Obviously Imma wa THT, I have Max who is also at THT I am also working with Max from Authentic studios, ni wengi.
Muziki kwako unauchukulia vipi? Unafanya for fun ama kazi?
Music has been my passion for a long time so sasa hivi nilivyosema I’m coming back into music… before kwa mfano like a few years back it was just talent, a hobby but now I am taking it very seriously, it’s my career right now, yaani that’s my job, my life, my everything, I expect that to feed me and my family so naichukulia kama a business venture, it’s very serious and because ni what I love to do.
Na unaamini kuwa muziki utakuletea chakula mezani?

Ohh yes naamini sana hivyo. My mon thinks I am crazy (anacheka). But it’s good to be crazy!!
DSC_6903
Hii tuseme ni kama coincidence kwasababu sasa hivi models wengi, former Miss Tanzania, tumeona Jini Kabula, (Mirian Jolwa) na Rashida Wanjara wana kundi lao nadhani ulishaliskia linaitwa Scorpion Girls na wengine wengine wanaofanya modeling wanaingia kufanya muziki, najua wewe pia wanaweza kusema hivyo kwamba ni mkumbo fulani hivi, unaweza kulizungumziaje hilo?
Kwanza mimi napenda kusema nilienda Miss Tanzania my passion was singing. Nilienda pale kuonesha talent yangu ya kuimba ili nionekane. So that was my aim kwasababu nilijaribu kwenda kwa different producers na nini, na kama unavyojua the game ni ngumu, it’s very hard, ikawa ngumu kwa mimi kubreakthrough to even get a producer who would work with me. Lakini wale watu wa miss walivyoniapproach mimi, to me was like I am beautiful let me use this opportunity to get what I want. Hiyo ndio ilikuwa plan yangu mimi na with this other girls sijui, I am not sure kwanini wameondoka from the miss kuja kwenye music industry, I don’t know.
Miaka mitano unajiona utakuwa wapi kimuziki?
I don’t know. But ukiuliza hata watu wangu wa karibu na my family they always say Feza dreams very big. When I was 17 nilikuwa nasema I’m gonna be Miss World, that’s what I was saying, it was just I dreamt big, hata kama it didn’t happen, I always dream big. Kwahiyo mimi hapa for now with my music I believe I can take Tanzania to another level. Naweza nikasimama with big artists, sijui Beyonce, Rihanna, that’s where I see myself kiukweli, and I am not gonna stop dreaming big, that’s me.
Unatamani kufanya collabo na wasanii gani hapa Tanzania na nje?
Tanzania I would like to do a collaboration with Mwana Falsafa, TID, Ngwea, kidogo niko oldschool. I still love the Ngwea, the Mwana FA, I still love Nurah I don’t where he is. Hawa wapya wapya I think it will be Ommy Dimpoz. Internationally, I would love to do a collaboration with……..Ohh my God this is difficult, Rihanna, Lauryn Hill… I am so oldschool Tony Braxton, these are the people ambao nimekuwa nikiwapenda when I was growing up.
DSC_6861
Unajua muziki kibongobongo ni mgumu kidogo yaani kuna challenge za hapa na pale, Djs hawapigi nyimbo mpaka uwahonge na vitu kama hivyo, wewe umejiandaa vipi, utakuwa na menejimenti ambayo itakuwa inafanya promotion ama utafanya mwenyewe?
Sina menejimenti, sina promotion, mimi I really depend on God to be quite honest. Unajua this music thing a lot of people wako talented, a lot of people wanafanya nice music lakini unakuta it’s not being played na nini, kiukweli hiyo namuachia Mungu. I believe kwamba if the product is good watu watasikia tu, I believe so. And that only happens ukiwa unaamini some higher powers kwasababu mimi siwezi kufanya chochote, it’s up to God, it’s up to people.
Unategemea kufanya video zako wapi sababu Tanzania kuna challenge kwamba video nyingi zinaishia kupigwa hapa hapa tu, na wewe una ndoto za kupenya zaidi, una mikakati gani kukivuka hicho kiunzi?
Really I think hapa hapa Tanzania we have people ambao wanaweza wakafanya video nzuri tu. I think problem inakuja kwenye payment. I think if we paid the production company hela inayoeleweka then would really give you something that’s nice. And not kuwasema wasanii lakini we are too cheap sometime. I don’t think ni lazima kusafiri kwenda Nairobi, South Africa wherever kufanya a good video, I think good video inatoka hapa hapa, it’s just creativity, it’s just finding the right production team cause vifaa vipo just that tunajaribu kucram na kufanya vitu vile vile, so ukiweka a little bit of creativity and the right production team we can have something really good from hapa hapa Tanzania, I believe that kiukweli. And honestly after that unajua siku hizi we don’t make use of social media inavyotakiwa.
If your product is really good somewhere someone ataiona tu, kwa mfano when you put it on YouTube wherever it will get there somehow ,somewhere. Halafu pia kuna another thing wasanii wa Tanzania tukiweza kuunite, I think kuna shida ya unity with the most artists in Tanzania kila mtu anataka kutoka kivyake, kila mtu anataka kumzidi mwenzake it’s fine but the competition that we have is not constructive.
Umetisha!!!
(Anacheka) Unajua that’s another thing when you believe in God and when you believe kwenye muda wake yeye things really work out. Kwa mfano ningeanza muziki nilivyokuwa ile 18 I don’t think ningeweza kuwa mimi, I don’t think ningeweza kugundua my style or what I want to do, I think I was too young to do that ndio maana this is the time, I believe this is the time cause najijua mimi ni nani najua Feza ni nani, najua Feza anaweza kwenda mpaka hapa, Feza hawezi kwenda mpaka hapa. So it’s just a beautiful thing to know who you are and what you want to do and that’s why naamini sana music can really feed me and my family because siingii kwenye muziki kusuasua.
Kwa mfano the last three months niko THT wananisaidia na vocal training, sio kwamba sijui kuimba but it’s because I want to go to another level sio tu unakaa unaenda studio unaimba, I am training my voice, I am working out, nakimbia beach kama kichaa(anacheka), so that mwisho wa siku when you see your product mtu akijaribu kucritisize anakosa hata kitu cha kuongea. I am not gonna leave kwamba uzuri wangu ndio unibebe kwenye video, I want it to be proper and I hope kwamba it will be good.

MSANII WA WIKI HII-'FAHAMU UTAJIRI ANAOMILIKI MWANA DADA LADY JAY DEE'

Achilia mbali hoja na mabishano ya juzikati kwenye mitandao ya kijamii kati yake na wanamuziki wengine wa muziki huo, zote ni changamoto za kimaisha. Haziepukiki. Siku zote mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe.
ALIKOTOKEA
Jide alianza kuimba kwenye Kwaya ya Kanisa la Kisabato, Magomeni, jijini Dar. Alipoingia kwenye Bongo Fleva  alianzia kwa kurap kabla ya kufanya usaili wa utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Clouds FM ambapo alitusua vyema na kuanza kutangaza. Hapo ndipo Watanzania wengi walipoanza kumsikia.
Kuelekea kuongeza ufundi na kulisaka soko la muziki, Jide alibadilika na kuanza kuimba RnB na ulipomkolea, aliamua kuachana na utangazaji na kujikita kwenye muziki peke yake.
Muziki ulikua, akafanikiwa kutoa  albamu kadhaa kabla ya kufikia hatua ya kumiliki bendi yake ya Machozi ambayo ilimuweka kwenye nafasi nzuri ya kutambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Heshima ikaongezeka na sasa ana kila kitu.
Kazi na dawa, safari nzuri ya maisha ya muziki isiyokuwa na skendo ilimpa heshima zaidi baada kufunga ndoa na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner Gabriel Fikirini Habash ‘Kapteiiini’.
Ndoa yao iliyodumu kwa takriban miaka nane sasa, pia ni chachu na fundisho kwa baadhi ya mastaa wanaochipukia kujifunza heshima ya ndoa.



Hili ni gari kwa ajili ya Bend yake inayojulikana kama Machozi Band





Hii ndo nyumba anayoishi mwanadada Lady Jay dee 





Hii ndo gari anayomiliki aina ni Super Murano 





Hu undo mgawa anaomiliki mwanadada lady Jay dee unaojulikana kama Nyumbani lounge 





Jide anajivunia kushinda Tuzo za Tanzania, Kilimanjaro Music (2004) kupitia kipengele cha Albamu Bora ya R&B (Binti), mwaka 2006 kupitia Tuzo za Pearl of Africa Music alizoshinda kama Mwanamuziki Bora wa Kike kutoka Tanzania.
Kama hiyo haitoshi, mwaka 2007, Jide alishinda Wimbo Bora wa kushirikiana (Hawajui) kupitia Tanzania Music Awards alioshirikiana na MwanaFA.

 Mwaka 2008, kupitia Tanzania Music Awards, Lady Jaydee alishinda Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike pamoja na za Pearl of Africa Music katika kipengele hichohicho, Kisima Music Awards (Wimbo Bora wa Mwaka) uitwao Anita alioshirikiana na Matonya.
Mwaka 2009, alishinda Tuzo za Tanzania Music (Wimbo Bora wa Mwaka), Anita kisha 2010 Tanzania Music Awards (Mwanamuziki Bora wa Kike), mwaka 2011 Mwanamuziki Bora wa Kike na Wimbo Bora wa Afrika (Nitafanya, aliomshirikisha Kidum kutoka Kenya na mwaka jana (Mwanamuziki Bora wa Kike).

Safari ya kibiashara haikuishia hapo, aliona kuna sababu ya kuanzisha kipindi chake cha runinga ambacho kina maudhui ya maisha yake halisi. Kinaitwa Diary ya Lady Jaydee kinachorushwa na runinga ya EATV. Kupitia hapo ameweza kupata faida mbili kwa wakati mmoja. Watu wengi wanazidi kumfuatilia (umaarufu unaongezeka), wakati huohuo anaingiza fedha kwa kukirusha kipindi hicho kinachodhaminiwa na kampuni kubwa ya simu za mikononi.

  Ishu nyingine ya chinichini kwamba mwanamuziki huyo anayetamba kwa sasa na wimbo wa Joto Hasira aliomshirikisha legend Profesa Jay, yuko mbioni kuanzisha kituo chake cha redio. Kama hivyo ndivyo, Lady Jaydee atakuwa ni mwanamuziki wa kwanza wa Bongo ambaye amethubutu kufanya makubwa ambayo kwa wasanii wengi itabaki kuwa ni ndoto kufikia.
Kwenye suala la kujitanua kibiashara ndiyo ilisababisha mwaka 2010 afikie makubaliano na Kampuni ya Mohamed Enterprises kuzalisha maji yenye nembo ya jina lake ingawa biashara hiyo haikudumu kwa muda mrefu. Hakukata tamaa, cheche zake kwenye ujasiriamali zilizaa matunda kwenye mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni, jijini Dar ambao unamuingizia mkwanja hadi sasa.
Heshima kwake ilizidi kuongezeka, taratibu alifanikiwa kujijenga katika maisha yake binafsi kama ujenzi wa nyumba yake ya kifahari iliyopo Kimara, Dar. Mali kama magari ya kutembelea, magari ya kazi zake za muziki havimpigi chenga.
Katika kuonesha muziki na ujasiriamali kwake vimevuka mipaka, ilifika wakati walishauriana na mumewe aachane na kazi ya utangazaji kwa muda ili aweze kusimamia miradi yao ambayo ilihitaji kutanuka zaidi jambo ambalo limefanikiwa.

MSANII WA WIKI:PICHA ZINAZOMTAMBULISHA BOB JUNIOR 'SHAROBARO PRESIDENT' NA FAMILIA YAKE


Unaonaje kuhusu kipengele hiki(msanii wa wiki)? TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI

MSANII WA WIKI:WAFAHAMU DADA WA WEMA SEPETU NA BAADHI YA WASIFU WAO



Kama kawaida wadau wa vituko vya mtaa kila wiki inatoa makala inayoelezea wasifu mbalimbali na taarifa nyingi kuhusu wasanii maarufu na vitu usivyo vijua kuhusu wasanii mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi leo katika msaanii wa wiki tunao wadada wa msanii maarufu WEMA SEPETU.Nao ni

1. TUNNU SEPETU... .... YEYE NI MAMA WA MTOTO MMOJA.. ANAISHI NCHINI MAREKANI.. TUNNU NI MPOLE.. ANAPENDA KUSIKILIZA.. ANAPENDA KUCHUKUA MUDA KABLA YA KUTOA MAAMUZI YA JAMBO ANALOPENDA.. NI MTAFUTAJI...
2.NURU SEPETU... NI MAMA WA WATOTO WATATU, AMEOLEWA NA ANAISHI DAR.  







3. SUNNA SEPETU: HUYU PIA ANAISHIA MAREKANI KWA KIPINDI KIREFU NA NI MCHESHI.
 
Wema katika muonekano wake mpya baaba yakunyoa nywele

MSANII WA WIKI:'MZEE YUSUF AFUNGUKIA UTAJIRI WAKE, SKENDO YA USHIRIKINA '

Wiki hii kwenye kolamu hii tunaye mfalme wa muziki wa Mwambao Bongo, Mzee Yusuf ambaye anafunguka juu ya utajiri wake na skendo ya ushirikina ambayo imekuwa ikielekezwa kwake.
Mzee Yusuf ni Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab ambayo aliianzisha rasmi mwaka 2006, maskani yake yakiwa jijini Dar.
Mzee Yusuf na kundi lake wamejipatia mafanikio makubwa katika medani ya muziki wa taarab na kurudisha hadhi ya muziki huo ulioanza kupoteza mvuto miaka ya 2000.
Funguka: Kwanza Mzee Yusuf unazungumziaje muziki wa taarab?
Mzee Yusuf: Zamani muziki wa taarab ulikuwa na mashabiki hasa kipindi kile cha ushindani wa marehemu Nasma Khamis na Hadija Kopa. Walijitahidi sana kuupandisha kwenye chati lakini baadaye ukapotea ila kwa sasa tumeweza kuwarudisha mashabiki wetu na muziki unapendwa Tanzania nzima, siyo Pwani pekee kama ilivyokuwa zamani.
Funguka: Inafahamika kuwa wewe ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio na utajiri mkubwa Bongo. Nini siri ya mafanikio yako?
Mzee Yusuf: Ni kweli mafanikio ya kundi langu yamekuwa yakiongezeka kwa kujipatia mashabiki kila kukicha. Umaarufu wake nao umekuwa ukiongezeka kila siku kwani sisi hatubagui mashabiki.
Huwa tunawafuata hadi Uswahilini kwa sababu ndiko kwenye mashabiki wengi ambao hawawezi kupanda teksi kuifuata bendi mjini. Wakati mwingine huwa tunapiga shoo za ‘ndondo’ (mtaani), harusi na sherehe mbalimbali za watu binafsi tena kwa gharama nafuu. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio yetu.
Funguka: Vipi kuhusu skendo ya ushirikina ambayo imekuwa ikielekezwa kwako?

Umati wa watu ikiwa katika moja ya show ya Mzee yusuph
Mzee Yusuf: Ushirikina upo sana hasa katika muziki wetu huu na tena ukiuendekeza basi utakutawala. Wengi wanaoamini kuwa hakuna mafanikio hadi kwenda kwa waganga huwa hawafanikiwi kabisa zaidi ya kuliwa fedha na waganga wa mjini na wengine wakishafanikiwa husahau maagano. Kwangu mimi hayo ni maneno tu, uchawi wetu ni kujituma katika kazi.
Funguka: Je, ulishawahi kwenda kwa sangoma?
Mzee Yusuf: Siwezi kusema uongo kuwa sijawahi kwenda kwa mganga, nilishawahi kwenda tena nakumbuka wakati nazindua bendi yangu ya Jahazi mwaka 2006 pale Travertine Hotel, Magomeni, Dar.
Nilikwenda kwa mganga mmoja hivi maarufu sana nikamwambia nahitaji watu wajae kwenye uzinduzi, akaniambia watakuja watu elfu moja, nikamwambia nataka watu mia saba tu kwa sababu bendi yangu bado changa.
Mganga aliniambia nimpe laki tatu, ukweli sikuwa nayo ilibidi niweke bondi tivii yangu. Baada ya wiki moja, yule mganga akaniuliza kama nimetangaza huo uzinduzi kwenye vyombo vya habari na kuweka matangazo ya barabarani, nikamjibu ndiyo ila nilijiuliza sana kwa nini aniulize wakati alinihakikishia kuwa shoo itakuwa nzuri?
Siku ya tukio ilikuwa balaa, kwanza mvua kubwa ilinyesha watu wakanyanyua viti kujikinga, watu tuliowategemea hawakuja, ukweli nilipata hasara ambayo sikuitegemea, nikagundua kuwa kwenye muziki hakuna uchawi

HAWA NDIO WACHUMBA NA WAKE WA WACHEZAJI MAARUFU WA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID

Hizi baadhi ya sababu kubwa za kwanini soka inajulikana kama ‘Beautiful Game’.
Miongoni mwa wachezaji bora kabisa duniani wanakutana kwenye mchezo wa leo usiku wa kombe la mabingwa wa Ulaya kati ya Man United na Real Madrid — lakini hata hivyo mchezo huo utahusisha warembo walio nyuma ya wachezaji wa timu hizo. Hapa ni superstars na superbabes tu!
Manchester United
Bouchra Elbali na Robin van Persie
Bouchra Elbali na Robin van Persie
Coleen Rooney na Wayne Rooney
Coleen Rooney na Wayne Rooney
Daniela Martins na Nani
Daniela Martins na Nani
DJ Sam Cooke na Chris Smalling
DJ Sam Cooke na Chris Smalling
Edurne Garcia Almagro na David de Gea
Edurne Garcia Almagro na David de Gea
Georgina Dorsett na Tom Cleverley
Georgina Dorsett na Tom Cleverley
Lety Sahagun na Javier Hernandez
Lety Sahagun na Javier Hernandez
Real Madrid
Aida Yéspica na Mesut Ozil
Aida Yéspica na Mesut Ozil
Caroline Celico na Kaka
Caroline Celico na Kaka
Irina Shayk na Cristiano Ronaldo
Irina Shayk na Cristiano Ronaldo
Lala Alvarez na Sergio Ramos
Lala Alvarez na Sergio Ramos
Lena Gercke na Sami Khedira
Lena Gercke na Sami Khedira
Sara na Casillas
Sara na Casillas
Soledad Fandiño na Gonzalo Higuain
Soledad Fandiño na Gonzalo Higuain

MATAJIRI 10 DUNIANI WANAONGOZA KUWA NA HELA NYINGI


Jarida la Forbes limetangaza majina ya mabilionea 1,426 duniani kwa mwaka 2013. Mfanyabiashara wa Mexico Carlos Slim ameendelea kukamata nafasi ya kwanza kwa mwaka wa nne mfululizo. Ingia ndani kusoma list nzima ya matajiri 10 duniani.
1. Carlos Slim Helu – Mexico

Net Worth: $73 billion (UP)
Source: telecom
Citizenship: Mexico
2. Bill Gates
bill-gates
Net worth: $67 billion (UP)
Source: Microsoft
Citizenship: U.S.A
3. Amancio Ortega
7_ortega
Net worth: $57 billion (UP)
Source: Zara
Citizenship: Spain
4. Warren Buffett
BUFFETT CREDIT
Net worth: $53.5 billion (UP)
Source: Berkshire Hathaway
Citizenship: U.S.A.
5. Larry Ellison
Larry-Ellison
Net worth: $43 billion (UP)
Source: Oracle
Citizenship: U.S.A.
6. Charles Koch | No. 6 David Koch
David-and-Charles-Koch-007
Net worth: $34 billion (UP)
Source: diversified
Citizenship: U.S.A.
8. Li Ka-shing
Li_Ka_Shing
Net worth: $31 billion (UP)
Source: diversified
Citizenship: Hong Kong
9. Liliane Bettencourt
230889-liliane-bettencourt-637x0-2
Net worth: $30 billion (UP)
Source: L’Oreal
Citizenship: France
No. 10 Bernard Arnault
bernard-arnault-france-1
Net worth: $29 billion (DOWN)
Source: LVMH
Citizenship: France
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa