Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

KASHFA...MBUNGE WA CCM MWENYE MIAKA 60 AFUNGA NDOA NA KIJANA MDOGO(KINDA)...

 Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60). 
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.
Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI CHATANGAZA KUMSHITAKI ZITTO KABWE KWA KUTANGAZA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE


HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
 
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.

Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.
 
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
 
Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.
 
Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.

 Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
 
“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.
 
Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.
 
Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.

CCM WAMSALITI KIKWETE..WADAI KWAMBA WAKO TAYARI BUNGE LIVUNJWE NA UCHAGUZI UFANYIKE KABLA YA 2015


HOFU kubwa imetanda ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), juu ya upatikanaji wa katiba mpya, hasa baada ya Rais Jakaya Kikwete kusaini muswada ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.
 
Mkutano kati ya Rais Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni uliofanyika Ikulu Oktoba 15, 2013 umeongeza mpasuko ulioanza kujitokeza baina ya makada wa CCM na wapinzani.

Katika mkutano huo, rais na viongozi wa upinzani waliafikiana vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.
 
Walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
 
Awali kabla ya mkutano huo, makada wa CCM wakiwamo mawaziri kadhaa waliweka wazi kuwa milango ya Ikulu imeshafungwa kwa wapinzani kuzungumzia suala hilo, lakini Rais Kikwete alipotangaza kukutana nao iliwaweka njia panda.
 
Tanzania Daima  limedokezwa kuwa baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakimshutumu Rais Kikwete kwa kuwabembeleza wapinzani huku akikiumiza chama chake.
 
Hoja wanayoijenga ni kuwa Rais Kikwete anataka kujijengea kitu cha kukumbukwa, hasa katika suala la katiba mpya bila kujali athari zinazokipata chama chake.
 
Makada hao wanaweka bayana kuwa hali hiyo itakiacha chama katika wakati mgumu wa kukabiliana na wapinzani wanaoonekana kuimarika kadiri siku zinavyoyoyoma.
 
Baadhi ya wabunge wa CCM wanamuona Kikwete kama msaliti kwa wabunge wake waliopitisha muswada huo, ambao sasa ni Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba, ukiwa na upungufu ulioainishwa na wapinzani.
 
Mmoja wa watu waliohudhuria mazungumzo ya Ikulu anasema rais aliridhia marekebisho hayo na alibainisha kuwa yajikite katika masuala kadhaa, likiwamo suala la Tume ya Warioba kuwapo kwenye Bunge Maalumu la Katiba, marekebisho katika suala la uteuzi wa wajumbe 166 ili idadi iongezeke na hoja ya Zanzibar kushirikishwa kabla ya muswada wa sheria ya kura za maoni kuanza.
 
Tayari Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alishatoa tamko kuwashangaa wabunge wa CCM kwa kupotosha kifungu kilichokuwa kinasema Tume ya Mabadiliko ya Katiba itavunjwa na rais mara tu baada ya kuwasilisha rasimu kwenye Bunge Maalumu la Katiba, msimamo ambao unaungwa mkono na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala (CCM).
 
Mbunge huyo katika andiko lake alilolisambaza katika vyombo vya habari, anakiri kuwa moja ya upungufu alioubaini katika muswada ule ambao sasa ni sheria, ni kuiua Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya mchakato kufikia mwisho.
 
“Kiukweli, lina mantiki ndani yake. Tukiwa kwenye Bunge la Katiba hakutakuwa na serikali, sasa ni nani atakayejibu na kuweka sawa hoja za wabunge? Hili kwa kweli wabunge tuliopitisha muswada ule hatukuliona vizuri,” alisema Kigwangala.

Wakati Kigwangala akiona upungufu huo, Naibu Spika Job Ndugai,  anajitetea  kuwa haoni udharura wa suala hilo kurejeshwa bungeni.
 
Ndugai amebeza suala la urejeshwaji wa sheria hiyo bungeni, akihoji kuwa suala hilo halina udharura.
 
“Ni ishu gani hasa ambayo wapinzani walienda kumwona rais ambayo inahitaji udharura huo? Je, kanuni za Bunge zinaruhusu suala hilo?” alihoji Ndugai.
 
Akizungumza na mwandishi  wetu wiki hii, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Bunge ni muhimili tofauti. 

Wabunge kama wataona kuna kitu cha kubadilisha watabadilisha, lakini wakiona hakuna cha kubadilisha itabaki ilivyo.
 
Kauli hiyo imeungwa mkono jana na Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, ambaye alinukuliwa na gazeti moja nchini , akisema: “Serikali haikusudii kufanya marekebisho yoyote kwenye Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba iliyosainiwa na Rais Kikwete hivi karibuni.”
 
Mmoja wa wabunge wa CCM aliyehojiwa na mwandishi wetu  na kutoa msimamo wake baada ya rais kusaini muswada kuwa sheria ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Hamad Yusuf Massauni, ambaye sasa ni Mbunge wa Kikwajuni.
 
“Mimi ningekuwa rais nisingepoteza muda kuongea na wapinzani, na hata kama sheria hii itarejeshwa bungeni, sioni sehemu yoyote ya kufanyia marekebisho, iwe ya kuondoa koma wala kuweka nukta,” alisema.
 
Kabla ya muswada huo kusainiwa kuwa sheria, Nape alinukuliwa  akisema: “Hofu yangu ni kuwa rais asiposaini muswada huo, ataingia katika mgogoro kikatiba, itabidi arejeshe muswada bungeni aeleze kwanini hajasaini, na ukirejeshwa bungeni wabunge wa CCM wakakataa kufanya mabadiliko, rais angelazimika kuvunja Bunge.
 
Aliongeza kuwa: “Mimi ninaona afadhali rais asaini muswada huu ili kama kuna upungufu uwekwe mezani kama ilivyokuwa mwanzo, ila nakubali kabisa mzee Warioba ana hoja katika suala la kutovunjwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kabla ya kutetea rasimu mbele ya Bunge Maalumu la Katiba.”
 
Alisema wabunge wa CCM ni asilimia 74 ya wabunge wote, hivyo wakishikilia hoja ya kutobadilisha jambo lolote katika muswada huo baada ya kurejeshewa na rais, matokeo yake ni kuvunjwa kwa Bunge na nchi kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015.
 
Nape alisema CCM haiko tayari kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015, hivyo akawataka wanaopinga na kuunga mkono hoja hizo watumie busara na hekima kufikia maridhiano yatakayolijenga taifa.
 
Alisema kuwa muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwanzo nao ulipitishwa ukiwa na kasoro mwaka 2011, lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo walienda kwa rais wakajadiliana wakakubaliwa, na kwamba viongozi wa CCM walilazimika kwenda Dodoma kuwaeleza wabunge msimamo wa Rais Kikwete na kuwashawishi waukubali.
 
“Tulipoona kuna hoja tulilazimika kwenda Dodoma kuwaomba wabunge wetu wakubali hoja za CHADEMA ili marekebisho yafanyike, ingawa suala hilo lilifanyika kwa taabu sana, sasa zamu hii wabunge wa CCM wanaweza wasikubali hoja za wapinzani, na likiendelea vile rais atalazimika kuvunja Bunge, hili suala limetuweka pabaya sana CCM, sijui hatima yetu,” alisema.
 
Tanzania Daima , limedokezwa kuwa iwapo serikali itaridhia marekebisho yaliyotajwa na wapinzani, mvutano mkubwa utazuka bungeni kati ya washindi na washindwa.
 
Jambo hilo linadaiwa halitakubaliwa na wabunge wa CCM ambao mara kwa mara wamekuwa wakishutumiwa kupitisha mambo kwa kuangalia zaidi masilahi ya chama kuliko taifa.
 
Kumekuwa na mipango ya CCM kumuandaa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, kuwa Spika wa Bunge la Katiba.
 
Inadaiwa Chenge ndiye atakayebeba jukumu la kudhibiti baadhi ya hoja zinazopingwa na CCM zilizotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba.
 
Miongoni mwa mambo yaliyomo ndani ya rasimu ya katiba ni serikali tatu.

-Tanzania daima

VIDEO YA RAIS KIKWETE AKIONGEA NA VIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANIA...NA HUU NDIO MUAFAKA ULIOFIKIWA JUU YA KATIBA MPYA

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitikadi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliitishwa na Rais Kikwete ili kuondoa sintofahamu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Septemba na Bunge lilipokutana mjini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana jioni ilisema katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.
Pia Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.
“Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini,” iliongeza taarifa hiyo.
Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Isaack Cheyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema. Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao waliambatana na wenyeviti wao ni Mohamed Mnyaa na Julius Mtatiro wa CUF, Tundu Lissu na John Mnyika wa Chadema na Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.
Vicheko Ikulu
Vicheko na bashasha vyatawala Ikulu
Ilikuwa fursa kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi hao baada ya kipindi cha miezi miwili cha kurushiana maneno baina ya viongozi wa Bunge, Serikali, CCM waliokuwa wakivutana na viongozi wa vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi.
Kama mtu yeyote angeulizwa kutabiri katika tukio lililotokea jana lingetokea basi angekuwa na wakati mgumu kutokana na ukali wa maneno na malumbano katika kipindi chote baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge wa Septemba.
Rais Kikwete alionekana mwenye furaha tele wakati alipokutana na viongozi wa vyama hivyo na kivutio zaidi ilikuwa pale alipokutana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu.
Viongozi hao walisalimiana huku wote wakitabasamu na kuashiria kuwa waliamua kuweka tofauti zao pembeni na kuangalia masilahi ya nchi.
Kumbuka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Septemba, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa yeye hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Rais Kikwete alikaririwa akisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu, huku akisisitiza kuwa mbunge huyo alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alipinga tuhuma hizo na kusisitiza Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) bila ya ridhaa yao.
Chikawe, Wassira na Lukuvi ndani
Mawaziri watatu, ambao walitetea kwa nguvu kupitishwa kwa muswada ule ndani na nje ya Bunge walihudhuria mazungumzo hayo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira walikuwemo kwenye mazungumzo ya jana.
Mawaziri hawa kwa nyakati tofauti walitetea kuwa mchakato wa muswada ule haukuwa na matatizo yeyote na kushikilia kuwa lazima Rais lazima asaini muswada kwani ulikuwa umepitishwa kihalali na Bunge.
Pia walikuwa wameshikilia kuwa safari hii kulikuwa hakuna mambo ya mazungumzo kati ya Rais na upinzani.

Chanzo cha sintofahamu
Wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.
Katika hatua nyingine, taarifa kutoka Ikulu zilisema kwamba Rais Kikwete alisaini muswada huo tangu Oktoba 10 mwaka huu siku ambayo wapinzani walipanga kufanya maandamano nchi nzima.
Katika mahojiano na Mwananchi jana jioni, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema muswada huo tayari ulikwishasainiwa na Rais na kama kuna marekebisho yatafanywa.
Mwananchi ilimtafuta Rweyemamu baada ya kusikia akithibitisha kusainiwa kwa muswada huo katika mahojiano na BBC Idhaa ya Kiswahili jana.
Akizungumza na Mwananchi Rweyemamu alisema, “Rais ameshasaini tangu Oktoba 10, unajua kulikuwa hakuna tatizo lolote kuhusu muswada huu kwa sababu ulifuata taratibu zote bungeni.”
Rweyemamu alisema kuwa awali Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais atakutana na wapinzani, pia atausaini muswada huo.
“Muswada umepitishwa bungeni na yeye amekamilisha kazi kwa kuusaini ili kuwa sheria. Alipokutana na wapinzani leo (jana) amewaeleza hilo na wameridhika” alisema Rweyemamu.
 CHEKI VIDEO HAPO CHINI....

MBUNGE MBARONI KWA WIZI WA GARI ...

Makalla anamtuhumu Ngonyani a.k.a Profesa Maji Marefu kuwa alichukua gari lake aina ya BMW X5 kisha akatokomea nalo kisha akawa anampigia simu hapokei na hata akimtumia SMS hajibu.
Kutokana na malalamiko hayo, hivi sasa Maji Marefu anasakwa na polisi wa Kituo cha Kati (Central), Dar es Salaam, tuhuma zikiwa ni wizi wa kuaminiwa, shauri lipo kwenye kitabu cha ripoti za polisi (Report Book ‘RB’) kwa namba CD/RB/13336/2013.
NYEUPE NA NYEUSI YA TUHUMA ZENYEWE
Nyeupe na nyeusi (black and white) ya tuhuma hizo, inawekwa wazi na ‘sosi’ wetu ambaye aliliibia siri kwamba sakata kati ya Maji Marefu na Makalla lilianza tangu Julai, mwaka huu wakati waheshimiwa hao walipokuwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

“Maji Marefu aliomba gari la Makalla ili alitumie kwa mizunguko ya siku moja tu lakini hakurudisha,” kilisema chanzo chetu. “Mgogoro mkubwa ulianza kuibuka kuanzia hapo na mpaka leo waheshimiwa hao hawazungumzi kwa salamu wala kutakiana heri.”
Chanzo chetu kiliendelea kusema: “Siku ya kwanza tu ilipopita, Makalla alimpigia simu Maji Marefu akawa hapokei, akimtumia SMS hajibu. Kwa kifupi Makalla alipoteza mawasiliano na Maji Marefu lakini aliendelea kusubiri kwa sababu anajua ni mtu wake.”
Habari zaidi zinasema kuwa kilipita kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja bila ya Makalla kumpata Maji Marefu kwenye simu lakini walikutana katika Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioketi kati ya Agosti 27 hadi Septemba 13, mwaka huu, Dodoma.
“Walipokutana Makalla alimuuliza Maji Marefu gari lake lipo wapi? Maji Marefu alimjibu alilikabidhi Lamada Hotel, Dar es Salaam,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza: “Unajua makabidhiano ya lile gari yalifanyika Lamada Hotel, kwamba angelirudisha baadaye lakini ikawa kimya.
“Hata hivyo, Makalla aliona siyo kesi kubwa, akafuatilia Lamada Hotel, menejimenti ya hoteli hiyo ilijibu kuwa gari hilo halijapelekwa pale. Vilevile baada ya kuzungumza siku hiyo, Maji Marefu alitoweka na bungeni hakuonekana tena.
“Baada ya kupata majibu hayo kutoka kwa Profesa Maji Marefu na Lamada, Makalla alifungua mashitaka Central, akidai kuibiwa gari lake na Maji Marefu.”
MAKALLA AFUNGUKA
Makalla ambaye ni Mbunge wa Mvomero (CCM) alipozungumza na mwandishi wetu alikubali kila kitu kisha akafunguka: “Niliomba polisi wanisaidie maana kwa hali iliyokuwepo ni kama nilikuwa nimeshatapeliwa. Vilevile niliripoti kwa Kamanda Mohamed Mpinga (mkuu wa kikosi cha usalama  barabarani) ili naye awaambie vijana wake wanisaidie kunitafutia gari langu.

“Nilimpa alama zote, rangi na namba za usajili. Oktoba Mosi, mwaka huu, ikiwa ni karibu miezi mitatu imepita tangu nimpe gari, polisi Tanga waliliona gari langu likiwa linaendeshwa na mheshimiwa Ngonyani (Maji Marefu) kwenye msafara wa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
“Nilimtumia SMS kumwambia kuwa gari langu ameonekana nalo katika msafara wa makamu wa rais. Polisi Tanga walitaka kumkamata lakini nikaomba aachwe kwanza, kukamatwa katika msafara wa makamu wa rais angeona amedhalilishwa.
“Nilimuomba baada ya msafara akalikabidhi gari kwa RPC Tanga kwa sababu linatafutwa na polisi. Akaniambia hawezi kulipeleka polisi kwa sababu tulikabidhiana vizuri. Nikamwambia sitaki kwa sababu alikuwa ananizungusha sana kunirudishia gari langu, mara aseme amelipeleka Lamada kumbe bado analo na wakati huohuo hapokei simu wala hajibu SMS zangu.”
USHAHIDI WA SMS
MAKALLA: “Mhe. pamoja na kutopokea simu na kutojibu meseji zangu, nakujulisha leo Oktoba Mosi, umeonekana na gari langu kwenye msafara wa makamu wa rais. Polisi walitaka wakukamate nikashauri wasubiri umalize mkutano. Kwa meseji hii naomba kesho asubuhi ukakabidhi gari langu kwa RPC Tanga, bila kukosa. Utamkuta ndugu Rajabu alipokee gari hilo baada ya ukaguzi mbele ya RPC.”

MAJI MAREFU: “Sawa nimekuelewa, yote ni makosa yangu na hii ni mali yako ila gari hatukupeana polisi, ungeniambia ulipo nikuletee.”
MAKALLA: “Sitaki umenizungusha sana, nilikukabidhi kwa heshima lakini umegeuka adui, hupokei simu huu ni mwezi wa tatu.”
MAJI MAREFU: “Ok nitafanya hivyo.”
MAKALLA ANAENDELEA
“Hakupeleka gari kwa RPC Tanga kama nilivyomtaka. Zilipita kama siku tatu, ndipo mtu mmoja akaenda kulitelekeza gari langu Lamada Hotel usiku. Walinzi walimuuliza yule mtu aliyetekeleza lile gari kwa nini anaacha gari na anakimbia? Hakujibu, akarukia kwenye pikipiki ambayo ilikuwa inalifuata lile gari kwa nyuma kisha akatoweka.
“Uongozi wa Lamada baada ya kuliona gari langu walinipigia simu, wakanijulisha nami nikapiga simu polisi, wakaenda kulichukua. Mpaka sasa gari lipo polisi central, wanasubiri kumkamata Mhe. Ngonyani ili kesi iendelee mbele.”
KAZI YA UWAZI
 baada ya kuzungumza na Makalla, lilikwenda kufanya upekuzi wake central na kubaini kwamba kesi hiyi ipo na madai yapo kama yalivyoelezwa.

Baada ya hapo, mwandishi wetu alimpigia simu Maji Marefu ambaye alipokea akiwa Nairobi, Kenya, na aliposomewa tuhuma dhidi yake, alijibu: “Subiri nirudi Dar, nitaeleza kila kitu.” Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Kuna madai kwamba ulichukua gari la Mheshimiwa Makalla, umekaa nalo miezi mitatu, kipindi chote hicho simu ulikuwa hupokei wala hujibu SMS zake.
MAJI MAREFU: Siyo kweli.
MWANDISHI: Labda ukweli ni upi.
MAJI MAREFU: Labda kwa sababu sipo Dar, nisubiri nirudi tutakaa tuzungumze.
MWANDISHI: Ungeniambia kwa kifupi tu ni kwa nini Makalla akushitaki, maana hii kesi ipo polisi, RB ipo na unatafutwa kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa.
MAJI MAREFU: Polisi wananitafuta mimi?
MWANDISHI: Ndiyo wanakutafuta wewe.
MAJI MAREFU: Kwa vile nipo Nairobi na wewe upo Dar, naomba usubiri tukutane kwanza ndipo nitaweza kueleza ukweli halafu ndipo mtaamua kuendelea mbele.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, swali lingine wewe una ugomvi na Mheshimiwa Makalla?
MAJI MAREFU: Aah, ndiyo nikasema tukikutana ndiyo italeta picha nzuri. Kama natafutwa au kuna tukio lolote nitaeleza.
MWANDISHI: Sawa mheshimiwa, basi nijibu swali hili, wewe una ugomvi na Makalla?
MAJI MAREFU: Sina ugomvi naye.
MWANDISHI: Sasa kwa nini akushtaki kwa wizi wa gari lake?
MAREFU: Naomba tukutane nikirudi nitaongea tu.
MWANDISHI: Inasemekana hilo gari uliwahi kumwambia Makalla kwamba uliliacha Lamada Hotel lakini baadaye ukaonekana nalo kwenye msafara wa makamu wa rais Tanga. Hili limekaaje?
MAJI MAREFU: Mimi nina magari zaidi ya 15, nitakupeleka uone kama mimi nina shida ya gari. Nyumbani kwangu kuna magari ya kila aina.
MWANDISHI: Ni kweli Makalla alikukabidhi gari?
MAJI MAREFU: Subiri nirudi Dar nitaongelea hilo.
MWANDISHI: Nijibu tu hilo moja tu, alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Kwani yeye anasema nilimnyang’anya au alinipa?
MWANDISHI: Anasema alikupa.
MAJI MAREFU: Sasa subiri nirudi nitaeleza ukweli wangu.
MWANDISHI: Kwani mheshimiwa inashindikana nini kunijibu swali hili moja tu? Alikupa au hakukupa?
MAJI MAREFU: Ukweli mtaupata nikisharudi Dar.

POLISI NAKO
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alipoulizwa kuhusu kesi hiyo, kwanza alisema hajapata taarifa yoyote kuhusu sakata hilo mpaka afuatilie.

Siku iliyofuata, Kova alipigiwa tena simu akaulizwa kuhusu sakata hilo, akajibu: “Kuna mtu  alinipigia simu jana kuhusu hii kesi, unajua mimi ni kamishna, hii kesi ni ndogo na siyo kila kesi lazima nijibu mimi.

-Gazeti la uwazi Via Gpl

LEO NI NYERERE DAY...HII NDIO HISTORIA YAKE..


WAKATI taifa linaadhimisha miaka 14 ya kifo cha mwasisi wa taifa, na rais wa kwanza wa Tanzania, kizazi kinahitaji kujua Nyerere alikuwa mtu gani na alianzia wapi.

Katika makala haya,vituko vya mtaa blog  itaangazia sehemu tu ya historia ya mwalimu Nyerere .Nia yetu ni kutaka kumuezi na kujikumbusha.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa mmoja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.

 Alipokuwa mtoto,  Nyerere alichunga mifugo ya babake. Katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila kitu, mapadre wa Kanisa katoliki waliona akili yake na nia yake nzuri ya kutaka kujifunza , wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.

Akiwa katika Chuo cha Makerere,Nyerere alianzisha  tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia aliamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu, Nyerere alirudi Tabora nakuanza  kufundisha  shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s). Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza , akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi...

Kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari).

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika.

Nyerere alikuwa kiungo muhimu  sana   katika  muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.

Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong'atuka na kumwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.

Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa za Tanzania hadi kifo chake.

Baada ya kustaafu kazi ya ukuu wanchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi.

Pamoja na hayo,Nyerere  alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation", mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama

Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara, baadae alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.

Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia).

Mafanikio na kasoro
Kitendo kikubwa ambacho  Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka ni kuchanganya ardhi ya Zanzibar na Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi leo upo.

Mengine ni Kujenga umoja wa kitaifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitadhidi Nduli Idi Amin Dada wa Uganda.

Watu walimuita mwalimu kuwa ni mwanamapinduzi wa afrika, kiongoizi wa bara nzima kutokana na nia yake ya kutaka kila Mwafrika kuwa huru na kuwa na amani.

Mwalimu pia alifanikiwa kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo)

Kutofanikiwa kwake

Kitu ambacho kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara nyingi ni juu ya kutofanikiwa kwa nia yake ya kuanzisha siasa za Kijamaa. Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976.

Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani rais  Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.

Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumuaga juu ya siasa yake kiuchumi :  “Nimefeli.Tukubali hivyo.”

Alikosolewa pia
Kutokana na hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa , Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya uchumi wa Tanzania, pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo wao yanazitamani siasa hizo.

Mbali  na  hayo,  kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa wakristo.

Kutangazwa mwenye Heri
Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.

Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu. Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu.

Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu Justine Samba.

Alikuwa mwanamichezo

Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wanchi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo.

Alianzisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama alicheza bao nyumbani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.

Kutokana na maisha yake aliyoishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini  kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Taifa linamkumbuka kwa hayo na mengine mengi ambayo aliyafanya, ameacha machapisho mengi ambayo pia yamekuwa hazina ya maarifa kwa watanzania.

ZITTO KABWE ATAJA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE ...


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analipwa sh milioni 384 kwa mwaka, sawa na sh milioni 32 kwa mwezi pasipo kukatwa kodi.

Hii ni mara ya pili kwa Zitto kutangaza hadharani mishahara ya viongozi wakuu wa serikali, akiwa ameanza na ule wa Waziri Mkuu, aliyesema analipwa takribani sh milioni 26 kwa mwezi.
 
Akiwahutubia wananchi mjini Igunga jana, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema kuwa sababu ya kutaka mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ijulikane, ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
 
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanacholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi, bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho jambo alilosema kuwa linaweza kutumiwa na wajanja kuendelea kuinyonya nchi.
 
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa sh 220,000 kwa mwezi akikatwa kodi, huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi licha ya kuhudumiwa kila kitu na serikali.
 
Aliongeza kuwa katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara pamoja na malipo mengine, huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupurupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
 
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk. Willibrod Slaa akiwa rais na akataka kupunguza mshahara wake, kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka serikalini,” alisema Zitto.
 
Akiwa katika Kata ya Choma, Zitto alikagua kilichokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba cha Giner ambacho kimeacha kufanya kazi tangu mwaka 1998.
 
Alisema kufa kwa viwanda vingi vya uzalishaji nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, akidai kuwa alishindwa kutofautisha suala la uwekezaji na biashara huru.
 
“Ni serikali ya Mkapa ndiyo ilitufikisha hapa katika kupotea kwa viwanda nchini, wao walidhani biashara huru ni kuwapa wawekezaji viwanda vyetu na serikali kujiweka pembeni, sasa nchi imebaki kutegemea uchumi wa uchuuzi badala ya uzalishaji,” alisema.
 
Alisema sera ya uwekezaji katika Serikali ya CCM ilichukuliwa kama fursa ya viongozi wa chama hicho kujinufaisha na mali za serikali pasipo kujua wataendeleza vipi.
 
Zitto alisisitiza kuwa kila mara CHADEMA imekuwa ikisisitiza bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji wa pamba kwenda nje kama malighafi, na badala yake wakitaka viwanda vifufuliwe kwa ajili ya kutoa ajira kwa Watanzania.
 
Alirejea kusisitiza sera ya hifadhi ya jamii kwa wakulima akisema imefikia wakati serikali kupitia SSRA ione umuhimu na ulazima wa kuhakikisha wanaongeza Watanzania wenye hifadhi ya jamii kwa kuanza mfumo maalumu wa hifadhi ya jamii kwa wakulima (Supplementary scheme for social security to small holder farmers).
 
“Ninapendekeza serikali ichangie nusu kwa nusu na mkulima ili kuvutia uwekaji akiba katika nchi na kuwa na sera ya uwekezaji katika maeneo yatakayomwinua mkulima kama miundombinu ya umwagiliaji, mikopo nafuu kwa wakulima kwenye pembejeo na nyumba na bima ya afya.
 
“Nimezungumzia umuhimu wa uwazi katika matumizi ya fedha za umma ikiwemo malipo ya watumishi na viongozi wa umma. Nimewaeleza wananchi wa Nzega kuwa siku ya Jumanne kamati yangu ya Hesebu za Serikali (PAC) itaanza kukagua mahesabu ya vyama vya siasa nchini,” alisema.
 
Zitto alisema vyama vya siasa vinatumia fedha za umma takribani sh bilioni 20 kila mwaka kama ruzuku, kwamba ni haki ya wananchi kujua fedha zinatumika namna gani.
 
Alisema kuwa wananchi wa Nzega wana changamoto nyingi sana. Kwamba wakulima wa pamba walipewa madawa feki ya kuua wadudu, michango ya hovyo hovyo ni mingi mno na unyanyasi wa wana-CHADEMA ni mkubwa vijijini. 

-Tanzania  Daima

WAMILIKI WA MAGAZETI YA MTANZANIA, MWANANCHI WAONYWA....JUU YA KUTANGAZA KUWA WAMEMALIZA ADHABU YAO YA KUFUNGIWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Idara ya Habari – MAELEZO, inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba Mheshiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo amepokea maombi kutoka kwa wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi na Mtanzania wakiomba kupunguziwa adhabu au kusamehewa adhabu wanazozitumikia kuanzia 27 Septemba, 2013.

Wakati Mheshiwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo anatafakari maombi hayo, amesikitishwa kuona kwamba magazeti haya mawili yamekiuka masharti ya adhabu walizopewa.

Wamiliki wa Gazeti la Mtanzania baada ya kufungiwa wameamua kuligeuza gazeti la kila wiki la RAI kuwa la kila siku bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti. Kwa mujibu wa ratiba ,gazeti la RAI linapaswa kutoka kila siku ya Alhamisi.

Wamiliki wa gazeti la Mwananchi nao wameendelea kuchapisha gazeti hilo katika mtandao kinyume na agizo la kufungiwa.

Serikali inawataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuwa na utamaduni wa kutii sheria za vyombo vya habari zinazotumika wakati huu. Hivyo serikali kwa mara nyingine tena inawataka wamiliki wa Gazeti la MTANZANIA, kuzingatia ratiba yao ya kutoa gazeti lao kila siku ya ALHAMISI.

Aidha, serikali inawataka wamiliki wa Gazeti la Mwananchi kuacha mara moja kuchapisha gazeti lao katika mtandao kama amri ya kufungiwa ilivyoanisha.
Imetolewa na,
Idara ya Habari – MAELEZO
10 Oktoba, 2013

BIBI TITI ALIVYOMWAGA FEDHA KUMUUA NYERERE

Bibi Titi Mohamed.                 JUMAMOSI Agosti 1, 1970 Mahakama Kuu ya Tanzania iliambiwa na mkurugenzi wa mashitaka jinsi Bibi Titi Mohamed alivyogharamia mapinduzi ya kumuua Julius Nyerere na kuiangusha serikali yake.
Mahakama iliambiwa kuwa Bibi Titi katika siku isiyojulikana aliitisha mkutano na katika kikao hicho, Michael Kamaliza alimshauri mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Leballo aende London kwa Oscar Kambona kumwomba atume fedha zaidi ili kufanikisha mpango wao wa mapinduzi.
Kamaliza alimtaka Chipaka amwandikie barua Kambona na kumtumia noti ya shilingi 10/- ili Kambona aitie saini ije isaidie katika kuwashawishi wabunge na baadhi ya mawaziri kumuunga mkono Kambona.
Noti hiyo pia ilikuwa isaidie katika kuchangisha fedha za mapinduzi na kuwashawishi watumishi wa TANU na NUTA kuipinga serikali.
Mkurugenzi wa mashitaka alisema; “Kamaliza alimwambia Leballo kuwa hakukuwa na shaka wafanyakazi wa Tanzania wangeliunga mkono mpango wa mapinduzi kwa sababu Rais alikuwa amemwondoa (Kamaliza) kutoka NUTA kinyume cha matakwa ya wafanyakazi.
“Leballo alikutana na Bibi Titi nyumbani kwake tarehe Juni 23 na mama huyo alimweleza alikuwa amekwenda Nairobi kwa muda wa siku nne na kwamba alimpigia simu Kambona kutoka Nairobi na kumtaka atume shilingi milioni moja (1,000,000/-) kwa ajili ya mapinduzi katika muda wa wiki mbili.
“Titi akampa Leballo shilingi 400/- na kusema kwamba alikuwa amepokea shilingi 2,000/- kutoka kwa Kambona, 1,000/- za Chacha kwa matumizi madogo madogo. Titi alimwambia Leballo atampa shilingi 600/- baada ya siku chache na alifanya vile tarehe 26, Juni”. Fedha hizo zilitolewa mahakamani kama ushahidi kamili.
“Tarehe 28 Juni, Chacha alipanga kukutana na Leballo tarehe 30 Juni ili amjulishe Leballo kwa Meja Herman.
“Chacha na Luteni Kanali Marwa walikwenda nyumbani kwa Leballo tarehe 30 Juni saa 3 usiku. Chacha na Leballo walikwenda katika chumba cha kulala na kumwacha Luteni Kanali Marwa sebuleni.
“Huko chumbani Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa tayari kuipindua serikali kama angelipwa shilingi 20,000,000 na akamtaka Leballo amwambie Kambona atume fedha hizo kwa haraka.
“Leballo na Chacha walikutana tena tarehe 3 Julai huko makao makuu ya Jeshi kwa maombi ya Chacha. Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa amesikitishwa na ukawiaji wa fedha.
Akamtaka Leballo aende huko Lugalo barracks katika bwalo la maafisa ambapo Kapteni Lifa Chipaka atamtambulisha kwa Meja Herman.
“Leballo alikwenda kule, akamkuta Kapteni Lifa anamsubiri. Kapteni Lifa alimwambia Leballo kwamba hakuwa anamwamini Meja Herman katika mpango wa mapinduzi kwa sababu alikuwa chotara kutoka Iringa na kwamba yeye angempa orodha ya maofisa ikiwa pamoja na jina la mtu mmoja kutoka kisiwani. Kutoka kwenye orodha hiyo mtu wa kuongoza mapinduzi angechaguliwa. Baadaye Kapteni Lifa alimfahamisha Leballo kwa Meja Herman.
“Baada ya mkutano huo Leballo alionana na John Chipaka na Kamaliza wakiwa pamoja katika ofisi ya shirika la wafanyakazi la NUTA. Wote walizungumza na kumtaka Leballo aende London kwa Kambona kumtaka atume fedha zaidi.
“Kama saa kumi na robo alasiri siku hiyo Leballo aliitwa tena kwenye ofisi hiyo. Aliwenda na kumkuta Kamaliza peke yake. Kamaliza alimwambia kwamba alikuwa amemtuma mtu mmoja kwa Kambona “U That” akalete fedha.
“Kamaliza akamwambia Leballo kwamba yeye alipendelea Meja Herman aongoze mapinduzi kuliko Chacha”.
Washitakiwa saba ambao wamekana mashitaka matatu ya uhaini na moja kuficha siri ya uhaini ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Bibi Titi Mohammed, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga.

MZEE MAJUTO ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE 2015, NI WAPI NA KWA CHAMA GANI? BOFYA HAPA

MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametangaza nia yake ya kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Akihojiwa na kituo cha Clouds FM, Mzee Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60, alisema Mungu akimjalia atajitosa kwenye ubunge jimboni humo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kiu hiyo imechochewa na mafanikio ya wasanii waliojitosa kwenye siasa na kufanya vyema.
Mzee Majuto alisema, uzoefu alionao katika kuishi kwake mjini Tanga itamwezesha kuwatatulia kero na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wenzake iwapo Mungu atamjalia katika kusudio lake.
Kadhalika Muigizaji, ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu nchini, Yekonia Watson 'Amani' amesema matarajio yake miaka michache ijayo ni kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge kabla ya kuangalia nafasi ya juu zaidi kwa maana Rais.
Akizungumza na MICHARAZO jioni, Watson alisema anaamini ana uwezo na kipawa cha uongozi hivyo anaweka mambo sawa kabla ya kujitosa jumla kwenye duru hilo, japo yeye hakuweka bayana atajitosa kupitia chama gani.
"Kwa sasa ni mapema mno, ila nitaanzia Ubunge kisha kuangalia nafasi ya juu, ila muhimu Mungu anipe uhai na umri wa kufanikisha hilo," alisema mkali huyo anayejiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Uwanja wa Vita' aliyoigiza na wasanii kadhaa nyota akiwamo Irene Uwoya.

MKE WA WAZIRI WA ZANZIBAR ATAPELIWA NA VIJANA WALIOJIFANYA WAGANGA NA WALIOTAKA KUMTAJIRI KWA NJIA YA MIZIMU...STORI KAMILI ILIKUAJE NI HAPA



Wapigaji wanazidi kuiteka nchi, uthubutu wa vitendo vya uporaji kwa njia za udanganyifu umeshika kasi na sasa hivi umepiga hodi kwa mke wa waziri wa zamani.
Ikupa Mwakanjuki, mke wa waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Brigedia Adam Mwakanjuki, ametapeliwa shilingi milioni 280.
Waliomtapeli Ikupa ni vijana wanne ambao inadaiwa ni matapeli wazoefu jijini Dar es Salaam na kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania, wakitumia ‘triki’ ya uganga wa kienyeji.
Vijana hao wakijifanya waganga wa kienyeji, walimfuata Ikupa na kumwambia kwamba wangeweza kumfanya atajirike zaidi kwa njia za mizimu.
Watuhumiwa wote wanne wa utapeli huo wameshakamatwa lakini tumepata majina ya wawili, wa kwanza akifahamika zaidi kwa jina la Silver na mwingine ni Mwang’ombe ambaye picha yake inaonekana ukurasa wa kwanza.
Chanzo chetu kilisema kuwa baada ya mwanamke huyo kupewa maneno ya ulaghai, aliingilika lakini akawa hana fedha ambazo ‘waganga’ hao walizihitaji.
“Mama aliposema hana fedha, wale matapeli walimwambia anazo mali ambazo anaweza kuuza na kupata kiasi cha fedha kinachohitajika,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Mama alisema analo shamba, wakamshawishi auze. Mama naye sijui aliwekewa nini, akawa anafanya kila kitu kutokana na maelekezo ya wale matapeli.

“Kweli aliuza shamba lakini fedha zote alikabidhi kwa wale matapeli. Siku zikapita, haoni mabadiliko yoyote, ghafla akamuona Mwang’ombe anaendesha gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado.
“Hapo ndiyo akashtuka, Mwang’ombe bila woga, akarudi tena kwa mama akamwambia zinahitajika fedha nyingine kwa ajili ya sadaka kwa yatima.
“Akiwa na wenzake, wakamshawishi auze shamba lingine zipatikane japo shilingi milioni 100 ili maisha yaanze kubadilika kwa kasi. Hapo ndipo akatushirikisha ndugu, tukagundua huo ni utapeli. Tukaamua kulifikisha hili suala kwenye vyombo vya sheria.”
Habari zaidi zinasema kuwa Ikupa kwa ushawishi wa ndugu zake, alifikisha malalamiko yake mpaka makao makuu ya jeshi la polisi na inadaiwa kuwa IGP Said Mwema aliagiza ma-RPC wote kufanya juu chini na kuwaweka nguvuni watuhumiwa.
“Hii ishu ni ya juu, sisi tumetumwa tuwakamate, tukishafanikiwa tutawakabidhi watuhumiwa kwa maofisa upelelezi makao makuu,” mmoja wa maofisa wa jeshi la polisi Kinondoni, alilinong’oneza .
Septemba 18, mwaka huu, saa 8 usiku, Mwang’ombe bila kujua kama yupo mtegoni, alipaki Prado lake lenye namba za usajili T940 CLX, Corner Bar, Sinza Afrika Sana, Dar es Salaam.
Alipopaki hapo, alichagua kiti ili apate ‘kuzila bata zake’ lakini eneo hilo, alikuwepo kaka mdogo wa Ikupa ambaye alitoa taarifa polisi na mara moja, gari lake likazingirwa kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Mabatini.
Uwazi lilikuwepo wakati Mwang’ombe anakamatwa Corner Bar na lilipofuatilia, liligundua kwamba mtuhumiwa huyo alimtaja Silver kwamba naye ni mhusika.
Oparesheni ikitekelezwa na maofisa upelelezi makao makuu, ilifanikisha kukamatwa kwa Silver eneo la Kimara Baruti, usiku huohuo na siku iliyofuata, watuhumiwa wengine wawili walitiwa nguvuni kisha shauri likarejeshwa Oysterbay kwa utekelezaji wa mkondo wa kisheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura, alilithibitishia  kwamba tukio hilo lipo mezani kwake.
“Tupo kwenye uchunguzi, kuna vitu tunakamilisha halafu baadaye tutafanya mawasiliano na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili kwenda mahakamani,” alisema Wambura.
Ikupa alipopigiwa simu, alipokea mtu wake wa karibu ambaye alisema: “Kama mama atataka kuzungumza na wewe atakupigia.”
Baada ya hapo hakupokea tena simu.
Utapeli kwa njia za uganga, mitandao ya simu, katika mashine za fedha (ATM) na kadhalika, umekuwa ukishika kasi nchini ingawa jeshi la polisi limekuwa likijipambanua kwamba linashughulikia kwa nguvu kubwa.

HIVI NDIVYO MKUU WA WILAYA YA MBULU ALIVYOWAPIGIA WANANCHI MAGOTI...SOMA HAPA UJUE NINI SABABU



Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .

Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
 
 

Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.

“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya kuonyesha upendo na kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi wawadhibiti, lakini sioni sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala. Ndiyo maana nikaona bora nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu mbele yao,”alisema Choya na kuongeza:

“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kwa lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka Mungu mbele nina imani tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia kwenye mkumbo wa Syria na Misri”

Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga magoti mbeye ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Haydom.

Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali waliyokuwa nayo.

Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji hicho kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.

Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema tena: “Unasema utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba msamaha mkuu huyo wa wilaya

MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA YAFUNGIWA

Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti. Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake hakiwezi kupitisaha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.

Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.

Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.

Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.

Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.

Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 Septemba, 2013,.

Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.

Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Imetolewa na

MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

KUNDI LA KIGAIDI LA AL QAEDA YAITISHIA TANZANIA...YAJIPANGA KUISHAMBULIA MUDA WOWOTE


*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi

 
WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.

Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.

“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.

Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.

“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.

“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.

“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” alisema.

Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.

Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.

Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.

Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.

“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.

“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.

-Mtanzania
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa