Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label Funguka. Show all posts
Showing posts with label Funguka. Show all posts

MTAZAMO WAKO:HIVI UNADHANI NI NANI HAKUSTAHILI KUPATA TUZO JANA NA NANI ALISTAHILI LAKINI HAKUPATA ?...KWENYE TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS

KUANGALIA WALIOCHUKUA TUZO BOFYA >>HAPA<<
UNADHANI NI NANI HAKUSTAHILI KUPATA TUZO JANA NA NANI ALISTAHILI LAKINI HAKUPATA ?

FUNGUKA:ISHU YA DIAMOND KUBAKI NA MAREHEMU BI KIDUDE KUNYONYA NYOTA ZA BI KIDUDE





Baada ya msiba wa Bi Kidude kumalizika, hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ alibaki peke yake na mwili wa marehemu chumbani kwa ajili ya kuchota nyota ya Bi. Kidude.
Ustadh akimchambua Diamond
Leo tunaye Dr Salum Mkumba ambaye ataeleza kwa kirefu tafsiri ya kitendo alichokifanya Diamond.
Funguka: Dr Mkumba asalam aleikum,
Dr Mkumba: Waaleikum salaam, ahsanteni nashukuru. Mimi leo nina jambo ninataka niliweke sawa.
Funguka: Liweke sawa, sisi pamoja na wasomaji wetu tunakusikiliza.
Dr Mkumba: Nataka kuweka sawa juu ya suala la nyota, mtu akifariki huwa anakwenda na nyota yake sasa nimeshangaa kusikia Diamond alikwenda kuchukua nyota ya marehemu.
Funguka: Sasa Diamond alipobaki peke yake chumbani na mwili wa marehemu ilikuwa ina maana gani?
Dr Mkumba: Pale alikuwa anajaribu kujisafisha tu katika jamii, hakuna cha ziada.
Funguka: Unaposema anajisafisha, kwani amechafuka?
Dr Mkumba: Eee! Kwani hujui? Amenaswa na mke wa mtu hotelini, skendo za wanawake tofauti zimekuwa zikimtafuna kila kukicha.
Funguka: Unaposema alikuwa anajisafisha una kitu gani cha kushika mkononi?
Dr Mkumba: Surat Nnajimi Sura ya 39 imezungumza kwa kirefu ila tafsiri yake ipo hivi; hakuna anachokichuma mwanadamu kwa marehemu ila marehemu anategemea kuombewa dua na mtu mzima.
Funguka: Kwa hiyo ina maana vile alivyofanya Diamond ni kazi bure?
Dr Mkumba: Nakwambia hakuna cha maana zaidi ya kujisafisha.
Funguka: Sasa una mshauri nini Diamond?
Dr Mkumba: Amrudie mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada ya kweli.
Funguka: Vipi kuhusu suala la kujenga msikiti ambalo Diamond alitangaza kuwa ana mpango huo?
Dr Mkumba: Hapo ndiyo kabisa, ajenge tu lakini haisaidii kitu sababu ukijenga nyumba ya ibada inatakiwa utumie fedha ambazo umezipata kihalali katika njia safi.
Funguka: Kwani fedha zake hajazichuma kwa njia safi?
Dr Mkumba: Kiimani yetu ya Kiislam muziki siyo halali hivyo fedha anayoipata kwenye muziki haiwezi kuwa halali.
Funguka: Tunashukuru, karibu tena siku nyingine.
Dr Mkumba: Haya Ishallah!

FUNGUKA:FAHAMU MENGI KUHUSU CATHY


Wiki mbili zilizopita tulimleta kwenu mwigizaji na mcheza filamu za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambaye mlimuuliza maswali hivyo wiki hii anajibu na kufafanua kile mlichohitaji kujua kuhusu maisha yake, shuka nayo.
NINI SIRI YA KUDUMU KWENYE NDOA?
Dada Cathy samahani, naomba unipe siri ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka kumi. Juma Ramadhani, Moro, 0716110028
CATHY: Siri kubwa ni uvumilivu tu kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika. Nilimsoma mume wangu naye akanisoma hivyo tunajuana vyema.

PONGEZI
Hongera sana kwa uigizaji wako kwani unatufundisha sisi wanajamii kiujumla. Prosper Mallya, 0658565860
CATHY: Nashukuru sana Mungu akubariki.

KAZI NYINGINE?
Tofauti na kucheza filamu unajishughulisha na nini? Ivody, Iringa, 0764608330
CATHY: Mimi ni mjasiriamali.

SIMU YA KICHINA?
Tunakuona kama simu ya Kichina ambayo haidumu mbona hutoi filamu hata watu hawakushirikishi au umeishiwa swaga? Msomaji, 0754021962
CATHY: Umechelewa sana, tafuta muvi zangu madukani zipo nyingi sana za kwangu mwenyewe na za kushirikishwa.

HISTORIA
Dada Cathy nataka kujua historia yako kwa ufupi. Ester, Morogoro, 0654502305
CATHY: Mimi ni mtoto wa saba kati ya watoto 12 tuliozaliwa katika familia yetu, nina watoto watatu, kabila langu ni Mpare wa Lembeni, Kilimanjaro na sanaa nilianza mwaka 1997.

PONGEZI
Hongera dada Cathy kwa kazi yako nzuri nakufahamu tangu enzi za Mambo Hayo hadi sasa kwenye filamu hauna skendo kama mastaa wengine, upo juu dada kaza buti. Maimuna  Dammbaya, Dar, 0658878793
CATHY: Nashukuru sana.

NDUGU YAKE
Eti dada Cathy ni kweli una undugu na mke wa Championi Keko? Natamani kuwa kama wewe. Msomaji, 0719058681
CATHY: Ni ndugu yangu tumetoka sehemu moja, kuhusu kuwa kama mimi nitafute.

USHAURI
Cathy ni mwanamke unayejiamini, hujivuni na unampenda kila mtu ila tunaomba ujikite zaidi kwenye filamu. Aggrey, Dar, 0712316278
CATHY: Asante kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi.

IDADI YA WATOTO
Dada Cathy nataka kujua una watoto wangapi? Baby Fay, Handeni, 0772274232
CATHY: Nina watoto watatu.


WATOTO WAKE?
Eti Jamila na Sophia ni watoto wako? Jamila, Kisarawe, 0716093981
CATHY: Ni watoto wa rafiki yangu ninawapenda na wao wananipenda sana kama mama yao.

ANAMUELEZEA
Cathy nimesoma na wewe jina lako unaitwa Lina John, tulisoma Shule ya Kaili uliacha darasa la tano ukakimbilia Tanga, sijui huko aliendelea au la mko mapacha mwenzako anaitwa Lilian. Celine, 0753485724
CATHY: Umekosea kidogo, mimi nilihamia Tanga nikiwa darasa la saba ambapo nilienda kuanza tena darasa la sita, ni kweli tuko mapacha.
KABLA YA SANAA
Kwa kawaida watu wengi maarufu kabla ya kupata umaarufu kupitia kazi fulani huwa kuna kitu ambacho walikuwa wakifanya. Wewe je, ulikuwa ukifanya kazi gani?  Andrew Peter, Dar, 0717570873
CATHY: Nimefanya kazi nyingi sana kama biashara, mfanyakazi kwenye maduka ya watu na saluni na huko kote nilikuwa nahangaika kutafuta maisha.

HUYU ANAMFAHAMU SANA
Nakufahamu Cathy Issaya, kwenu ni Lembeni, Mwanga, una dada yako anaitwa Rozi ndugu zako ni kina Naomi na baba mkubwa wako ni Mzee Kivatiro. Msomaji, 0755699959
CATHY: Kweli unanifahamu.

FUNGUKA:KAULI YA UWOYA BAADA YA KUFUMWA AKILA URODA NA DIAMOND

Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.
Ndikumana, alianguka na kuzimia, asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma magazeti  yaliyoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya, aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe, aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani ndiye aliyemsababishia majanga yote.
Hivi sasa, Ndiku yupo Rwanda, alitimka nchini baada ya kusoma habari ya Uwoya na Diamond kunaswa hotelini, ila kabla ya kuondoka, alitamka rasmi kuvunjika kwa ndoa yao.
Habari ya kuvunjika kwa ndoa, ilitoka kwa Uwoya mwenyewe ambaye alimweleza mwandishi wetu siku Ijumaa Wikienda, lilipodondosha ‘jiwe’ hilo mtaani. Uwoya alisema: “Na ndoa yenyewe imevunjika asubuhi ya leo, kila kitu kimeharibika.”
KWELI ANAJUTA KUMFAHAMU DIAMOND
Uzungumzaji na hata sauti, ni dhahiri Uwoya hataki tena kumsikia Diamond, kutokana na ukweli kuwa ‘brazameni’ huyo, amemharibia kila kitu, ikiwemo kuipeleka kaburini ndoa yao.
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Uwoya na mwandishi wetu;
MWANDISHI: Habari za kazi?
UWOYA: Salama tu.
MWANDISHI: Vipi shemeji yetu hajambo?
UWOYA: Shemeji gani? (anatukana) mume wangu ameniacha kisa stori ya Diamond.
MWANDISHI: Duh, imekuwaje tena jamani?
UWOYA: Alipoona stori ya mimi kuwa hotelini na Diamond, aliumia sana. Akaanguka na kuzimia.
MWANDISHI: Shida ilikuwa habari ya Diamond au mgogoro ndani ya ndoa?
UWOYA: Alipoona ile habari kwenye gazeti alianguka ghafla, akazimia kisha alipozinduka akarudi kwao. Ameamua kuniacha sijui kama atanirudia.
MWANDISHI: Pole sana, kwa hiyo familia yako inasemaje kuhusu hilo?
UWOYA: Familia yangu imenitenga kwa sasa.
MWANDISHI: Pole sana Uwoya.
UWOYA: Haina haja. Andikeni tu, mume wangu amenitosa rasmi.
MWANDISHI: Kwani amekupa talaka ndugu? Maana ndoa haiwezi kuharibika kirahisi.
UWOYA: Mimi na wewe hatutaniani, nakwambia ndoa yangu haipo tena.
MWANDISHI: Lakini shemeji yetu anakupenda sana.
UWOYA: Unataka kuandika hayo? Ukweli familia yangu haitaki kabisa kusikia habari za Diamond.
MWANDISHI: Kwani magazeti ya Global hayajasaidia kurejea kwa ndoa yako?
UWOYA: Mliandika habari nzuri ya ndoa yetu, tukarudiana, mlinisaidia sana na familia ilifurahi kuona hayo kwa wakati huo.
MWANDISHI: Sasa nani wa kulaumiwa juu ya ndoa yako?
UWOYA: Mimi niko ‘siriaz’, nimeachwa.
MWANDISHI: Ok, asante ndugu.
UWOYA: Asante, Mungu atawalipia tu.
KUHUSU DIAMOND NA UWOYA
Machi 25, mwaka huu, Diamond na Uwoya, walinaswa na kamera  kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
  huku tukiwa na ushahidi wa kutosha jinsi Diamond na Uwoya, walivyolala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, wakiingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
PICHA ZIPO CHINI

















KWA HABARI JINSI WALIVYONASWA NA DIAMOND >>BOFYA HAPA<<
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa