Showing posts with label mtaa kwa mtaa. Show all posts
Showing posts with label mtaa kwa mtaa. Show all posts
TAZAMA PICHA ZA JUKWAA LA FIESTA DAR LINAVYOTENGENEZW
MUUZA CHIPS AMTEKA MTOTO TANDALE DAR...ATOKOME BILA KUJUA ANAENDA KUMFANYIA NINI MTOTO HUYO
MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie.
Mama mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’.Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi.
Mtuhumiwa wa utekaji.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa kuwa mtekaji ambaye alishaacha kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka muda mrefu na binti yao na hakukuwa na dalili za kurejea.Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani.
Baba mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.
Inadaiwa kuwa katika mawasiliano hayo, mtekaji alikataa katakata ombi la kumtaka amrudishe mtoto wao na kutaka apewe kiasi cha shilingi milioni 6 ili kutekeleza jambo hilo ingawa baadaye ilibainika jamaa huyo alikuwa Gairo mkoani Morogoro.Wazazi hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji alishtukia na kukimbia.
AIBU...!! MUME NA MKE WA MTU WANASWA LIVE GESTI WAKINGONOKA BUGURUNI-SOKONI...
Live: Mume wa mtu, Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema baada ya kunaswa gesti saa 7 usiku.
Wawili hao walinaswa hivi karibuni kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue Roze maeneo ya Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.
Habari zilizopenyezwa katika timu yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya leseni yake ya biashara kwa kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu hufanya biashara ya kuuza miili yao katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa baa hiyo huwahifadhi machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono ikifanyika mchana kweupe na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na kukomesha biashara ya madanguro jijini, vijana wa OFM walitinga ndani ya baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!

Wakati huohuo, kijana mwingine wa OFM aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya baa hiyo ili kupeleleza bei zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei kwa kuwa alikuwa na changudoa kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na wengine waliokuwa wanatoka nje ya eneo hilo.
TAARIFA POLISI
Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya oparesheni hiyo.

Ilipotimia usiku wa manane, ndipo zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu kuingia ndani ya baa hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya gesti.
Akiwa ndani, paparazi huyo alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani huku akitoa ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi kufanyika tu.
KAZI IKAANZA
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa ndani ya gesti hiyo.
Katika pekuapekua hiyo ndipo mume huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa mtu huku wote wakiomba msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
Katika kurusharusha miguu, mwanaume huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
“Chondechonde mimi nina ndoa na familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu. Naombeni tuyamalize kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa polisi, utetezi ambao haukumsaidia.
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
Katika mahojiano huku kondom zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
“Hatujazitumia sisi hizi, tumezikuta humuhumu chumbani. Lakini nawaombeni sana, msinipeleke polisi nina ndoa yangu. Naombeni mnisamehe kwa sababu mume wangu atanirarua. Ninyi wenyewe mnajua ndoa ilivyo ngumu, tafadhali naomba mnisitiri,” alisikika mwanamke huyo.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.
Pamoja na kuomba sana, polisi hao waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi mwao.
Mbali na hao, oparesheni hiyo pia ilimtia nguvuni meneja wa eneo hilo, Emmanuel Mpinge, ambao wote kwa pamoja walifikishwa kituoni na kufunguliwa kesi yenye namba BUG/RB/13114/2013 - KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA 19/10/2013.
MSICHANA WA MIAKA 10 WA KIKATILI NA MWILI WAKE KUTUPWA CHOONI

MKAZI wa Kijiji cha Msanzi wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa , Festus Sungura (37) anadaiwa kumuua kikatili msichana Janeth Mwanandenje (10) na kisha kutumbukiza mwili wake ndani ya shimo la choo.
Inadaiwa choo hicho kilikuwa kikitumiwa na mkewe waliyetengana naye na lengo lilikuwa aweze kukamatwa na kufungwa kwa kosa la mauaji. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alibainisha kuwa lilitokea Oktoba 18 mwaka huu saa 11 katika Kijiji cha Katuka Kata na Tarafa ya Matai wilayani Kalambo.
Mwaruanda alidai Oktoba 13 mwaka huu saa mbili usiku Janeth (marehemu) alikwenda kwenye ukumbi uliokuwa ukionesha mikanda ya video katika Kijiji cha Msanzi na hakurudi tena nyumbani kwao hadi mwili wake ulipogunduliwa ndani ya shimo la choo, kijiji jirani cha Katuka .
Inadaiwa siku iliyofuata, baba mzazi wa marehemu huyo aitwaye Mussa Mwanandeje , alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Matai ya kupotea kwa binti yake huyo.
Kwa mujibu wa Mwaruanda, Oktoba 18 mwaka huu jirani wa wazazi wa marehemu huyo katika Kijiji cha Msanzi, aitwaye Festus Sungura (37), alikwenda Kijiji cha Katuka, ambacho ni jirani na kijiji cha Msanzi.
Alikwenda kumfuata mkewe Rosemary Arusha, ambaye alirudi kwao kijijini hapo baada ya kugombana na mumewe huyo miezi kadhaa iliyopita.
Baada ya Sungura kufika Katuka, alikutana na binti yake aitwaye Digna Sungura (15), ambapo alimhoji iwapo mama yake mzazi ( mke wa Sungura) akifungwa, kwa kuwa anamchukia yeye baba yake, ataenda kuishi kwa nani? Binti yake huyo, alimjibu kuwa ataishi na bibi yake kijijini hapo Katuka.
Ndipo Sungura alipomwagiza binti yake huyo, akamwambie mama yake atoe miti mitatu, iliyowekwa juu ya shimo la choo wanachotumia, waone alichofakifanya yeye.
Mama ya binti huyo, alitoa taarifa kwa viongozi wa kijiji hicho cha Katuka, ambapo kwa kushirikiana na wakazi wengine, walitoa miti chooni hapo na kuuona mwili wa marehemu uliotumbukizwa humo.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani upelelezi wa shauri lake utakapokamilika.
KANISA LAVAMIWA JIJINI MWANZA..MUHUMINI MMOJA AUWAWA NA WENGINE KUJERUHIWA,CHEKI PICHA
Wananchi wakiwa wakitafakari nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza.
----------
Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza , Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya uchomaji moto Makanisa.
Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki kwa wakazi wa jiji la Mwanza.Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi na ni mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao.
Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio hilo na akaiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.
BAADA YA ZITTO KUANIKA MSHAHARA WA RAIS KIKWETE..HII PIA NI BAADHI YA MISHAHARA YA MARAIS WENGINE DUNIANI..
WAKATI RAISI WA TANZANIA AKITIA KIBINDONI ZAIDI YA MILIONI 384 KWA MWAKA,HII HAPA CHINI NI BAADHI YA MISHAHARA KWA MARAISI WENGINE, WENGIWAO WANATULETEA MISAADA YA MAENDELEO.
Nchini Marekani, mshahara wa rais unajulikana tangu mwaka 1789 kiongozi wa nchi hiyo alipokuwa analipwa Dola 25,000 kwa mwaka.
Kuanzia 2001 hadi sasa, Rais wa Marekani analipwa Dola 400,000 (Sh 640 milioni) kwa mwaka, sawa na Sh 53.3 milioni kwa mwezi.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma analipwa Randi 2 ,917 038 sawa na zaidi ya Sh400 milioni za Kitanzania kwa mwaka, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Sh475 milioni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Sh338 milioni, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Sh277 milioni na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba Sh226 milioni kwa mwaka.
Wengine na malipo wanayopata kwa mwaka ni Marais wa Urusi, Vladimir Putin, Sh174 milioni, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia Sh137 milioni, Michael Satta wa Zambia, Sh126 milioni, Rais wa Angola, Jose dos Santos Sh91 milioni, Rais wa Lesotho, Profesa Pakalitha Mosisili Sh88 milioni, Armando Guebuza wa Msumbiji, Sh84 milioni na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping Sh60 milioni.
Wengine ni Rais wa India, Pranab Mukherjee Sh49 milioni, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Sh27 milioni, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Mothlanthe Sh331 milioni, Waziri Mkuu wa Namibia, Nahas Angula Sh160 milioni, huku Baba Mtakatifu wa Kanisa la Romani Catholic, Papa Benedict XVI akifanya kazi bila kulipwa mshahara.
MAAJABU YA MKOA WA MBEYA..!AUWAWA KWA WIZI WA KUKU WATATU, KUKU ALIYEIBIWA ATAGA YAI PEMBENI YA MWILI WA MAREHEMU
| Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa napolisi |
| Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu. |
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
|
WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.
Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.
Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.
Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Alisema mtuhumiwa huyo baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Aidha Baada mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea wa kuwabaini watu waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.
-Mbeya yetu
TAZAMA PICHA ZA WANANCHI WALIVYOJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA JULIUS NYAISANGA
Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu
Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara
Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders muda huu
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakisubiria Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kabla haujasafirishwa kupelekwa Kwao Tarime Mkoani Mara.
MAITI YAFUKULIWA, YAKATWA KICHWA...CHEKI PICHA ZA UFUKUAJI
UTATA umezidi kutanda miongozi mwa wakazi wa mji wa Geita, baada ya watu wasiojulikana kufukua kaburi kwenye makaburi ya Mtaa wa Elimu Nyantorotoro kisha kukata kichwa cha maiti iliyokuwemo na kuondoka nacho kwenda kusikojulikana usiku wa Oktoba 13, mwaka huu.
Watu hao baada ya kufukua kaburi hilo walipasua jeneza na baadaye kutoa kichwa cha maiti hiyo ya mwanaume ambaye utata umejitokeza kwani jina la marehemu halijafahamika kwani waliotenda unyama huo waliondoka na msalaba wenye jina lake na waliliacha kaburi wazi bila kulifukia.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Elimu Nyankumbu, Hassan Malima, tukio hilo liligunduliwa saa tatu asubuhi na watu walioenda eneo hilo kuchimba kaburi baada ya kutokea msiba kwa Mchungaji Mtafuteni Mihana wa Kanisa la Pefa aliyefiwa na mtoto wake, Rabeka (28).
“Tulipofika katika eneo hilo kuangalia sehemu ya kuchimba kaburi kwa ajili ya huyo marehemu, mtoto wa mchungaji ndipo tukaona hilo kaburi likiwa limefukuliwa,tulipolisogelea tukashuhudia maiti ikiwa imekatwa kichwa,” alisema mwenyekiti huyo.
Uongozi wa mtaa huo baada ya kupata taarifa za tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina, walitoa taarifa na polisi walifika eneo la tukio wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita, OCD Bwire.
Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifukua kaburi hilo na kulitoa jeneza ili kutambua jinsia ya maiti hiyo ambapo baada ya Dk. Alex Makomba kufanya uchunguzi iligundulika ilikuwa ya mwanaume.
Naye Mchungaji Mtafuteni alisema tukio hilo ni la imani za kishirikiana kutokana na baadhi ya wananchi kuamini kutumia njia hiyo wakiamini kuwa wanaweza kufanikiwa katika maisha yao.
“Watu wamekosa imani ya Mungu, wanadiriki kuchukua viungo vya watu waliokufa na kuzikwa,hivyo nawaomba watu kuachana na imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mungu pekee watafanikiwa,” alisema Mchungaji Mtafuteni.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, ACP Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Tukio hilo nina taarifa nalo na jeshi la polisi linaendelea kufanyia uchunguzi, wahusika wakipatikana watafikishwa mahakamani,” alisema.

KIJANA ALIJINYONGA, AKAFA, AKAZIKWA LAKINI…AFUFUKA!
HOFU imezidi kutanda kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kufuatia matukio ya watu waliofariki dunia na kuzikwa miaka iliyopita kuibuka wakiwa hai.
Mgonda Thomas (22), aliyefariki dunia kwa kujinyonga Mei 28, mwaka jana na kuzikwa siku iliyofuata, Ijumaa iliyopita aliibukia karibu na mlango wa nyumbani kwao akiwa hai.
Tukio hilo ambalo bado la moto, lilijiri katika Kijiji cha Rumasa, Kata ya Buseresere, wilayani Chato mkoani Geita.
Kwa mujibu wa chanzo, majirani ndiyo waliomshuhudia Mgonda akitembea barabarani saa tisa alasiri hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyumba hiyo huku nguo zake zikiwa zimechakaa.
Baba mzazi wa kijana huyo, mzee Thomas Msalaba (60) akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema majirani hao ndiyo waliomtaarifu kwamba mwanaye Mgonda alikuwa barabarani.
“Niliondoka kwenda kumshuhudia kama kweli ni mwanangu. Nilipofika, nilimchunguza kwa umakini sana na kubaini alikuwa yeye.
“Alama kubwa iliyokuwa kwenye mwili wa mwanangu ni kovu kwenye mkono wake wa kushoto lililotokana na kuungua moto, pia sura yake ilifanana sana na mama yake,” alisema mzee huyo.
Naye mama mzazi wa Mgonda, Martha Kitobelo alimthibitishia paparazi wetu kuwa kijana huyo ni mwanaye kweli.
Familia hiyo ilisema Mgonda alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba aliyoifunga juu ya mti wa mwembe hatua chache kutoka nyumbani kwao. Haikujulikana chanzo cha kujinyonga.
Mzee Msalaba alisema kuwa, baada ya Mgonda kufariki dunia alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao na siku ya tatu ndugu walianua matanga.
Kufuatia hali ya Mgonda kuwa ya mawengemawenge na kushindwa kuzungumza, wazazi wake walimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji wa eneo hilo aitwaye Juma Tabiho.
Mganga huyo alisema kijana huyo hakufa bali alichukuliwa msukule na maiti waliyoizika ilikuwa kiini macho.
Hata hivyo, katika tukio hilo Jeshi la Polisi Wilaya ya Chato likiongozwa na Mrakibu wa Polisi Wilaya, OCD Leonard Nyaoga lililazimika kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi waliopandwa na hasira waliotaka kufukua kaburi ili kuona kilichokuwa ndani.
Afande Nyaoga aliwaambia wananchi hao kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi na kuwaeleza kuwa chombo chenye uwezo wa kutoa kibali cha kufukua kaburi ni mahakama peke yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Pudensiana Protas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kufanya utaratibu wa kumpima DNA kijana huyo ili kujiridhisha kama kweli ndiye Mgonda aliyefariki dunia mwaka jana.
Hili ni tukio la tatu kutokea mkoani Geita katika kipindi kisichozidi miaka mitano iliyopita.
Aprili 12, 2013 katika Kijiji cha Kasamwa wilayani Geita, Flora Onesmo (45) aliyefariki dunia Februari 28, 2008 aliibuka akiwa hai.
Septemba 28, mwaka huu aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mwatulole mjini Geita, Shaban Maulid (16) aliyefariki dunia Januari 1, 2011 naye aliibukia Mtaa wa Mbugani jirani na nyumbani kwao, Kata ya 14, Kambarage mjini Geita.
Kufuatia matukio hayo yenye dalili za ushirikina, Askofu wa Kanisa la Zion Assemblies of God Geita, Edward Osako alisema katika maandiko hakuna binadamu aliyewahi kufa kisha akafufuka zaidi ya Lazaro aliyefufuliwa na Yesu akiwa kaburini.
“Haya matukio ya watu kufa na kuonekana wakiwa hai baada ya miaka kadhaa ni nguvu za giza ambapo hata kwenye Biblia yameandikwa,” alisema Askofu Osako.

HIVI NDIVYO BOSI NSSF ALIVYOCHINJWA KINYAMA...
BOSI wa NSSF aliyeuawa kikatili kwa kuchinjwa eneo la Moshono jijini Arusha, Regina Mushi amezikwa rasmi kijijini kwao Karansi, Kitongoji cha Ashengai,Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Jumamosi wiki iliyopita.
Akizungumza wakati wa mazishi hayo baba mzazi wa marehemu, Damas Mushi alilaani tukio la kuuawa kikatili kwa binti yake huyo ambaye miaka michache iliyopita alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuajiriwa katika Taasisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo alifanya kazi miaka miwili hadi kifo kilipomkumba Oktoba 14, mwaka huu nyumbani alipokuwa akiishi Moshono, jijini Arusha.
Regina aliuawa kinyama chumbani kwake kwa kuchinjwa na kukatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake na hadi sasa haijafahamika sababu ya kufanyiwa unyama huo.
“Siku chache kabla ya kifo cha mwanangu aliniambia kuwa ana mpango wa kuendelea kusoma kwa kiwango cha shahada ya pili lakini bahati mbaya ameuawa kikatili ni jambo la kusikitisha sana,” alisema mzazi huyo.
Ametoa wito kwa jeshi la polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo ili kuwabaini na kuwatia mbaroni waliofanya unyama huo.
Naye baba mdogo wa marehemu, Wakili Cornelius Kariwa amesema mauaji hayo ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha kishetani.
“Ukatili wa namna hiyo wa kumchoma mtu visu ni wa hali ya juu kwani ulisababisha kutapakaa na kujaa damu kitandani, ni ukatili uliopitiliza ambapo hata angekuwa na kosa marehemu asingepaswa kupata adhabu ya aina hiyo na kwamba kitendo hicho ni cha kulaaniwa katika jamii,” alisema wakili huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo,” alisema kamanda huyo.

HIVI NDIVYO VYUO 10 VYA TANZANIA VILIVYOFUTWA NA SERIKALI....ANGALIA USIJE UKADANGANYWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imevifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) .
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.
Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote vya Dar es Salaam.
Vingine ni Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values Training Institute na Information Technology Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.
Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea kujaza fomu za mikopo.

HURUMA SANA...!! TAZAMA PICHA ZA MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEAJILIWA KAMA MFANYAKAZI ZA NDANI ANAECHEZEA KIPIGO KAMA PUNDA..!
Huko Ubungo maziwa kuna ukatili wa kijinsia unaoendelea.
Yaani huwa kuna imani kuwa vitendo vingi vya ukatili vinafanywa na wanaume, ila la hasha hata wanawake nao ni balaa. Sababu kubwa ya kuamini hivyo ni ile hali ya kuchukulia unaujua uchungu wa kuzaa, unajua hata wewe hutapenda mwanao afanyiwe vitendo ambavyo sio vizuri, nimekutana na mama huko Ubungo maziwa akiwa amemuajiri mtoto mdogo wa miaka 8 kama house girl na mbaya zaidi anampiga vipigo sana sana mpaka kumkata kata na mtoto ana makovu ya vipigo.
Haya yote utayapata ndani ya kipindi cha Joyce Kiria Wanawake Live ndani ya EATV.
Huyu ni mtoto aliyeajiriwa kama mfanyakazi wa ndani na mtoto aliyembeba ni moja ya kazi zake za kulea huyu mtoto.
Huyu ndiye mama mwenye nyumba aliyemuajiri huyo mtoto na huwa anampiga sana.
Hapa nikiwa na hawa watoto
majirani na watu mbalimbali walikuwepo eneo la tukio.
Unaweza ukafikiria hawa wanaishi vizuri, Ila huyu mama anampiga sana huyu mtoto....