Showing posts with label anti ezekiel. Show all posts
Showing posts with label anti ezekiel. Show all posts
AUNT EZEKIELI AMUHENYESHA MBAYA WAKE ..YULE ALIMPIGA NA CHUPA CLUB KISA MWANAUME
' Yvonne Maximilian(22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa Aunt Ezekiel.'
Hatimaye yule mbaya wa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel aitwaye Yvonne Maximilian (22) amenaswa na kuhenyeshwa kortini kisa kikiwa ni kumpiga chupa mwigizaji huyo.
Yvonne aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kukamatwa maeneo ya nyumbani kwake Kinondoni-Manyanya.
Habari za ndani kutoka kortini zilieleza kuwa awali kesi hiyo ilikuwa isikilizwe na hakimu Agustino Mbando lakini baadaye kulitokea mabadiliko ambapo ilisomwa na Fundi Fimbo.
Akiwa mahakamani hapo huku Aunt naye akihudhuria kama mlalamikaji, Yvonne alishuhudiwa akipelekwa puta na polisi.
Hata hivyo, baada ya kesi hiyo kusomwa iliahirishwa hadi Oktoba 17, mwaka huu, itakaposikilizwa tena.
Agosti 26, mwaka huu, Yvonne anadaiwa kumjeruhi Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar.

Yvonne Maximilian katika pozi
HALI YA KIDONDA CA AUNT EZEKIELI CHA KUTOBOLEWA NA CHUPA CLUB CHAANZA KUOZA
INASIKITISHA! Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la chupa alilolipata hivi karibuni.
Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.
Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.
ALIKATISHA DOZI
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.
Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.
“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.
ASAFISHWA UPYATukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.
Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.
ALIKATISHA DOZI
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.
Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.
“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.
Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.
MKONO ULIANZA KUOZA
Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.
“Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.
CHANZO CHA UGOMVI NI NINI?
Licha ya kuhusishwa na ugomvi wa kimapenzi baina yake na mpenzi wa Yvonne anayejulikana kwa jina la Joff, Aunt alisema ugomvi wao uliisha zamani na kila mmoja ana maisha yake.
“Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu,” alisema Aunt.
Wakati huohuo, taarifa ambazo Amani limezipata kuhusu mtuhumiwa wa Aunt, Yvonne ambaye alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar siku ya tukio, anahaha kukwepa kifungo kwani uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani kisha gerezani.
MUME WA MTU NDIO CHANZO ZA ANT EZEKIEL KUJERUHIWA NA HUYU DADA "IVONY"....CHECK PICHA MBALIMBALI ZA IVONY
Chanzo nini?
Baada ya kufuatilia kwa karibu na kuichunguza habari hii tumegundua kuwa chanzo kilikuwa ni ‘beef’ la kugombania mwanaume ambaye anasadikika ni mume wa mtu kati ya mwanadada huyo (Ivony) na Aunty Ezekiel
Ilikuaje?
Mpashaji wa habari hii anasema kuwa wanadada hao walikuwa ukumbini hapo na ghafla mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Sunday alitokea ukumbini hapo na ndipo patashika hilo likazuka kila mmoja akidai kuwa jamaa huyo ni wa kwake.
Baada ya vuta nikuvute ndipo uzalendo ukamshinda mwanadada ivony na kuanza kuzichapa na Aunty kabla ya kuamua kuchukua chupa na kumpiga nayo na kumjeruhi maeneo ya mkononi
PICHA ZA IVONY HAPA CHINI...

AUNT EZEKIEL APIGWA CHUPA USIKU AKIWA CLUB

Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema.

“Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo.
Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan, Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.
Baada ya taarifa hizo, juzi mchana, mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.
“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”
mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza.

Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.
Source:Risasi
AUNT EZEKIEL AJERUHIWA VIBAYA NA CHUPA AKIWA CLUB. ...HIZI PICHA ZAKE
Actress Aunt Ezekiel amechimbwa na kitu chenye ncha kali kinachodaiwa kuwa chupa katika mkono wake wa kushoto. Tukio hilo lilitokea juzi katika ukumbi wa Club Billicanas wakati Wema Sepetu akitambulisha wasanii wapya wa Bongofleva. Habari ambazo bado sio rasmi ni kuwa huenda muigizaji huyo alikumbwa na tukio hilo hatari kutokana na issue za kimapenzi yaani kugombea mwanaume siku za nyuma au sasa. Tutakujuza zaidi kinachoendelea. Ugua pole Aunt. Angalia picha chini jinsi actress huyo alivyojeruhiwa.......
![]() |
| Mkono uliojeruhiwa kabla ya kufungwa |
![]() |
| Aunty akiwa hospital baada ya kupatiwa matibabu. |
HII NDIO HISTORIA FUPI YA MAISHA YA ANTI EZEKIEL ALIKO ANZIA MPAKA SASA.....
JINA la Aunt Ezekiel siyo geni kwa wadau mbalimbali wa burudani hapa nchini, ni staa ambaye hivi sasa ana jina kubwa kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka sita iliyopita.
Japokuwa kwa sasa ni staa, amepitia mambo mengi magumu katika safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipo hivi sasa.
Aunt alizaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam, baba yake akijulikana kama Ezekiel Grayson’ Jujuman’ ambaye alikuwa ni mchezaji hodari sana wa timu ya Simba. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alienda kumalizia darasa la saba katika Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Kisarawe, mkoani Pwani.
Vipi maisha yalikuwaje baada ya kumaliza shule?
“Kwa kweli maisha yalikuwa ni magumu mno kwa maana nilipomaliza shule tu, alijitokeza mwanaume na kutaka kunioa kitu ambacho mimi sikukipenda kabisa lakini baba yangu alitaka hivyo kwa vile uwezo wa kunisomesha hakuwa nao tena na maisha yalikuwa ni magumu sana.
“Baada ya kuona mambo ya mimi kuolewa yanapamba moto huku yule mwanaume akizidi kuihudumia familia yangu, nikaona nikichelewa nitabebwa mzobemzobe, hivyo niliamua kutoroka alfajiri na mpaka natoroka, sikuwa najua naelekea wapi.
“Baada ya kutoroka, asubuhi ile nilienda mpaka Ukonga, sehemu moja inaitwa Mazizini, nikagonga nyumba moja ya mtu na kumwambia natafuta kazi za ndani, bila kuchelewa yule dada aliniambia hata yeye anatafuta msichana, hivyo nilianza kufanya kazi nikawa namlea mtoto na kufanya kazi zote za ndani huku nyumbani kwetu wakinitafuta bila mafanikio.
“Baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu, niliamua kumpigia simu baba yangu ambapo aliposikia sauti yangu alifurahi sana na kuniambia kuwa nirudi nyumbani wala hawataweza kuniozesha tena, hivyo niliamua kumuaga tajiri wangu na kumwambia narudi nyumbani kwetu.
“Niliporudi nyumbani bado nilimkuta yule mchumba lakini nilimwambia kama anataka kunioa anisubiri nisome, hivyo nilienda Iringa katika Shule ya Sekondari Kawawa na kuanza kidato cha kwanza mpaka cha pili, nikarudi Dar na kumalizia katika Shule ya Sekondari Makongo mwaka 2004.
“Baada ya kumaliza sekondari, nilijiunga na mambo ya computer pale Amana, lakini baadaye niliamua kushiriki mambo ya urembo ambapo niliibuka kuwa Miss Mwanza 2006 na kuingia katika shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania lakini sikufanya vizuri na hapo ndipo nilipoingia kwenye uigizaji wa filamu ambapo filamu yangu ya kwanza kabisa ilikuwa ni Miss Bongo, iliyokuwa ya William Mtitu.
“Ilipofika mwaka 2007 nilifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara maarufu Jack Pemba. Yule mchumba aliyekuwa akinisubiri mwanzo alikuwa ameshakata tamaa na kuendelea na maisha yake, hivyo nilianza kuishi na Jack kama mke na mume huku akinisaidia katika mambo yangu ya sanaa.
“Baadaye alinizuia kwani alikuwa hapendi nitoke nyumbani na baada ya muda nilipata ujauzito wake kitu ambacho kilimfurahisha sana na kunizawadia vito vya dhahabu vyenye uzito wa kilo moja, lakini kwa bahati mbaya ilipofika miezi saba nilijifungua mtoto akafariki.
“Ndoa ilikuwa ni nzuri, nilikuwa napata kila kitu ambacho nataka na kutembelea gari za kifahari lakini kitu ambacho nilikishindwa ndani ya ndoa hiyo ni kipigo kikali nilichokuwa nakipata, kwani nakumbuka kuna siku alinipiga kiasi ambacho mashuka meupe yalikuwa kama yamepakwa rangi nyekundu, hivyo bibi yangu alikuja kunichukua na kuondoka moja kwa moja.
“Baada ya kuondoka kwa Jack, nilianza kupigana katika maisha na niliingia kwenye uhusiano na mtu mwingine na nikaanza kuingia kwenye kucheza filamu ambapo huko jina langu lilizidi kukua siku hadi siku, hivyo nikawa naweza kuyaendesha maisha yangu ya kila siku, mpaka nilipokutana na mume wangu wa sasa, Sunday Demonte ambaye alinioa mwishoni mwa mwaka jana.
“Unajua kazi yangu kubwa mimi ni uigizaji ambapo huku Tanzania ndiyo kila kitu, sasa nikisema nikae Dubai muda wote ni lazima kipaji changu kitapotea, hivyo nafanya kazi zangu kwa kutengeneza filamu kama tatu, kisha narudi Dubai kidogo kukaa na mume wangu.
“Siku zote naumia sana kuwapoteza wazazi wangu wawili, yaani baba na mama, nilitamani sana mpaka leo wawepo na waione kazi yangu na nilifurahi sana siku ambayo nilifunga ndoa yangu ya pili na Sunday Demonte,” anaeleza Aunt.
AUNT EZEKIELI GONJWANI....AFANYIWA OPERATION YA HARAKA...
MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefanyiwa oparesheni ya haraka kwa ajili ya kuondolewa uvimbe tumboni.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe huo siku nyingi pasipo kujijua hadi alipougua ghafla wakiwa katika mizunguko ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe, alisema staa huyo anaendelea vizuri.
PICHA ZA MPAMBANO WA NGUMI WA ESTER BULAYA VS AUNT EZEKIEL
Aunt Ezekiel na Ester Bulaya wakizichapa ulingoni.
Mhe. Ester Bulaya ndani ya ulingo.
SERIKALI YAMKALIA KOONI AUNT EZEKIEL
Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili.
“Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.
Kabla ya paparazi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee. “Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
Alipotafutwa Aunt kuhusiana na suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo, badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha Ukatoliki.

MSAANII WA BONGO MOVIE "AUNT EZEKIEL" AJITABARIA KIFO
WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa hawezi kuishi miaka mingi, atakufa mapema.
“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.