MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefanyiwa oparesheni ya haraka kwa ajili ya kuondolewa uvimbe tumboni.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe huo siku nyingi pasipo kujijua hadi alipougua ghafla wakiwa katika mizunguko ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe, alisema staa huyo anaendelea vizuri.

