Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label msiba. Show all posts
Showing posts with label msiba. Show all posts

HIVI NDIVYO MTANGAZAJI "JULIUS NYAISANGA" ALIVYOTESEKA....APIGANIA UHAI WAKE KWA SIKU 1460

NYOTA katika utangazaji Bongo, Julius Nyaisangah aliyefariki dunia Oktoba 20, mwaka huu katika Hospitali ya Mazimbu mjini hapa,  amepitia kipindi cha mateso cha takribani siku 1460 katika kupigania uhai wake.

Akizungumza , Jumatatu nyumbani kwake, Kihonda kulipokuwa na shughuli ya kumuaga marehemu Nyaisangah, mke wa marehemu, Bi. Leah Nyaisangah alisema mumewe alianza kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari tangu mwaka 2009.
“Kama alikuwa nayo kabla hatujui lakini tuligundua kuwa mume wangu mpenzi ana sukari mwaka 2009 na baadaye ikagundulika pia alikuwa na shinikizo la damu, tangu hapo amekuwa akiteseka sana,” alieleza mama huyo akijitahidi kuzuia machozi.
 
Marehemu Nyaisangah enzi za uhai wake.
Alisema, licha ya kuugua mumewe alikuwa hodari wa kufanya kazi na kuendelea na majukumu yake muda wote katika Kampuni ya Abood Media aliyokuwa akifanya kazi mpaka mauti yalipomkuta.
“Kwakweli alijitahidi sana, alikuwa baba bora kwa familia yetu lakini Mungu amempenda zaidi. Namuombea makazi mema,” alisema.

MIEZI MITATU YA MATESO
Bi. Leah alisema, mumewe alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali mjini hapa na kuendelea na dawa lakini miezi mitatu iliyopita hali ilikuwa mbaya zaidi na alipumzika kwenda kazini kwa kipindi chote cha miezi mitatu.

“Lakini alipata nafuu na kurudi kazini, hadi wiki iliyopita alikuwa kazini kama kawaida ila sasa sukari ikapanda tena ghafla, halafu na presha nayo ikawa juu huku akiwa na malaria, ndipo akafariki,” alisema kwa uchungu.

RATIBA YABADILIKA
Awali, ratiba ilikuwa aangwe mjini hapa jana Jumanne kisha wasafari kwenda Tarime kwa  maziko yaliyotarajiwa kufanyika leo Jumatano lakini ilibadilika baada ya serikali kuomba mwili wake upelekwe Dar kwa ajili ya kuagwa na viongozi wa serikali pamoja na jamaa zake wa Dar.

Ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ulioagizwa na Naibu Waziri, Amos Makalla ulifika nyumbani kwa marehemu na kueleza nia ya wizara ambapo ulikubaliwa baada ya kushauriana na bosi wa Nyaisangah, Aziz Abood, ambaye pia ni Mbunge wa Morogoro Mjini.

MAMIA WAMUAGA MORO
Baada ya makubaliano hayo ambayo yalipata baraka kutoka kwa kamati ya mazishi, ililazimika kubadilisha ratiba haraka ambapo mwili ulichukuliwa Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa ajili ya kuagwa ili usafirishwe kwenda Dar.

Wakazi wa Morogoro na vitongoji vyake walijitokeza kwa wingi juzi Jumatatu nyumbani kwa marehemu Kihonda na kutoa heshima zao za mwisho kabla ya safari ya kwenda Dar ambako mwili ulifikishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

DAR VILIO TUPU
Jijini Dar es Salaam, jana Jumanne, umati wa watu ulifurika kumuaga marehemu Nyaisangah, kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda Tarime kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika leo.

Nyaisanga ameacha mjane, Leah na watoto watatu ambao ni Samuel, Noela na Beatrice.

TAZAMA PICHA ZA WANANCHI WALIVYOJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA JULIUS NYAISANGA



Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara




Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu


Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara




Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders muda huu






Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakisubiria Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kabla haujasafirishwa kupelekwa Kwao Tarime Mkoani Mara.

MWILI WA JULIUS NYAISANGAH 'ANCLE J' KUAGWA LEO KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB..

 
Marehemu Julius Nyaisangah (katikati) akiwa katika pozi na Meneja Mkuu wa GPL Abdallah Mrisho (kushoto)
Mwili wa mtangazaji mkongwe, Julius Masyaga Nyaisanga maarufu kama ‘Uncle J’ (53), aliyefariki dunia Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro, unatarajiwa kuletwa leo jijini Dar es Salaam na baadaye kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders’ Club.
Meneja Matangazo wa Kituo cha Abood Media, Abeid Dogoli alisema mwili wa Nyaisanga uliagwa jana jioni mjini Morogoro na leo alfajiri unasafirishwa kuja Dar es Salaam.
“Mwili wa marehemu utaagwa kesho (leo) kwenye Viwanja vya Leaders, na shughuli zitaanza saa 4 asubuhi baada ya kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili,” alisema rafiki wa karibu wa marehemu, Aboubakar Liongo.
Liongo aliyewahi kufanya kazi pamoja na Nyaisanga wakati huo ikijulikana kama Radio Tanzania (RTD) na baadaye Radio One, alisema baada ya shughuli ya kuaga, mwili wake utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Mara kwa mazishi.
Mkoani Morogoro, mwili uliagwa nyumbani kwake eneo la Kihonda Viwandani, na mke wake Leah Nyaisanga alisema wamepanga kuondoka Jumanne kwenda Tarime.
Nyaisanga alifariki dunia katika Hospitali ya Mazimbu inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), siku moja baada ya kufikishwa na kulazwa kutokana na maradhi ya ugonjwa wa kisukari.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Nyaisanga.
Nyaisanga pia aliyewahi kufanya kazi Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo hivi sasa ni TBC Taifa na katika Kampuni ya IPP, ambako alikuwa Mkurugenzi wa Radio One.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa kutokana na kifo cha mtangazaji maarufu na mkongwe hapa nchini katika Tasnia ya Habari hususan upande wa Utangazaji, Julius Nyaisanga kwani kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa katika Tasnia hiyo”, alisema Rais Kikwete katika salamu zake.
Nyaisanga aliyekuwa Mkurugenzi wa Radio Abood, ameacha mjane na watoto wawili wa kike, Boke na Nyange.

HII NDO HISTORIA FUPI YA MAISHA YA MAREHEMU JULIUS NYAISANGAH "ANKO J" ALIYEFARIKI JANA...

Nyaisanga( wakwanza kushoto) akiwa na wanamuziki wa Sikinde na MK Sound
Jina la Julius Nyaisanga hakika litabaki kutajwa katika historia ya muziki Tanzania. Mtangazaji huyu ambaye alitokea Kenya na kuja kujiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam, alikuja na aina mpya ya utangazaji ambayo ilimfanya apate nafasi ya pekee katika nyoyo za wasikilizaji wa RTD kwa miaka yote aliyokuweko huko. Julius ambaye mwenyewe alisema alitengeneza staili yake ya utangazaji kwa kumuiga mtangazaji maarufu wa KBC Leonard Mambo Mbotela aliyejulikana sana kwa kipindi chake 'Je huu ni uungwana?' alikuja na utangazaji uliochangamsha sana kumsikiliza. Nyaisanga alikuwa Producer wa mamia ya nyimbo za bendi zilizorekodiwa na bendi mbalimbali katika studio za RTD miaka ya 80. Nilipata bahati ya kufanya nae kazi wakati nilienda kurekodi nikiwa katika bendi tatu tofauti, Orchestra Mambo Bado, Tancut Almasi Orchestra, na  Vijana Jazz Band. Alishauri vizuri na matokeo yake ni nyimbo nyingi zilizopitia mikononi mwake zingali zinapendwa mpaka leo.
Pamoja na utangazaji, na u producer wa muziki, Nyaisanga alipenda muziki na wanamuziki, alikuwa rafiki wa wanamuziki wengi sana, alikuwa na tabia ya kutembelea bendi zinapopiga na aliweza hata kutembelea bendi nne au tano kwa usiku mmoja. Na hasa kama bendi iko katika ratiba ya kurekodiwa. Aliwahi hata kufika Iringa kutembelea tancut Almasi Orchestra kabla ya kurekodi toleo lao lililokuwa naule wimbo usiochosha Masafa Marefu. Nyaisanga alipita kwenye bendi kadhaa kututaarifu kuhusu kuanza kwa radio mpya ambayo ingekuwa katika masafa ya FM, na ndipo muda si mrefu Radio One ikaingia hewani wakati huo ikiwa pale katika jengo la NASACO ambalo lilikuja kuungua na baada ya kukarabatiwa sasa linaitwa Waterfront. Pia akiwa Radio One Nyaisanga aliendelea kuwa Nyaisanga, japo sera za Radio One hakika zilikuwa tofauti na zile za RTD, lakini pia huko mchango wake katika muziki ulikuwa mkubwa sana. Hatimae Nyaisanga alihamia Abood Radio Morogoro ambako amekuweko mpaka hatimae usiku wa kuamkia leo 20 October 2013, umauti umemkuta katika hospitali ya Mazimbu Morogoro kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na Kisukari.
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI UNCLE J

TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA MAZISHI YA MWANAFUNZI WA IFM, ALIYEZAMA BAHARINI.

CONTINUE READING:

















Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw akiongea nenoa.


Askofu Mkuu wa KKKT. Ask.Dr. Alex Malasusa akitoa salamu za Kanisa.









Ni vilio tu kwa waombolezaji



Rachel Fute na Vaileth Lwendo ambao ni Dada wa Marehemu wakipita
Mama wa Marehemu akisaidiwa kutoa heshima kwa Binti yake.

Baba wa Marehemu, Mchungaji Habakuki Lwendo akimuaga Binti yake.





Vilio vilitawala kanisani


Sanduku lililouhifadhi mwili wa Marehemu Wende likiwa tayari kushushwa kaburini.



Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wameungana na Familia ya Mchungaji, Habakuki Lwendo na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mazishi ya Binti yao Wende Lwendo aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Uhandisi Kompyuta katika mazishi yaliyofanyika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wende alifariki Ijumaa ya Julai 12, 2013 wakati akijumuika na rafiki zake kuogelea Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Kipepeo Kigamboni kilometa chache kutoka eneo alilokuwa akishi.
Mazishi hayo mbali na wanafamilia na wanafunzi wa IFM kuhudhuria pia yalihudhuriwa na Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu, Dk Alex Malasusa, Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw pamoja na wachungaji mbalimbali na Wafanyakazi wa Chuo cha Makumira anakofanyia kazi Mchungaji, Habakuki Lwendo ambaye ni baba wa Marehemu Wende.
Picha na Jestina George
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa