Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label agness masogange. Show all posts
Showing posts with label agness masogange. Show all posts

"ALIENITUMA MZIGO WA MADAWA SOUTH AFRIKA ITABAKI KUWA SIRI YANGU MPAKA KUFA "...MASOGANGE

VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ alitarajiwa kutua nchini juzi Jumatano akitokea Afrika Kusini huku siri nzito ya mzigo aliodakwa nao ikitawala, Amani linakujuza.
Masogange anakuja Bongo baada ya kumaliza kulipa deni lote la randi 30,000 (shilingi milioni 4.8) alizoamriwa kulipa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuingiza kemikali haramu, Julai 5, mwaka huu.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Masogange anarejea na Melisa Edward ambaye alikamatwa naye lakini mahakama ikamwona hana hatia.



SIRI NZITO
Ujio wa Masogange bado una siri nzito kwani licha ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa faini au kifungo cha miezi thelathini jela, lakini bado serikali ya Tanzania inahaha kutaka kujua mzigo aliodakwa nao alitumwa na nani!
“Masogange ameahidi kutowataja watu waliompa mzigo akidai kuwa itaendelea kuwa siri yake mpaka anakufa,” kilipasha chanzo chetu.



WATOTO WA VIGOGO
Watoto wa vigogo ndiyo wamekuwa wakitajwa zaidi kuhusika na kumtuma Masogange ingawa hakuna jina la moja kwa moja la mtoto yeyote wa kigogo lililowahi kutajwa.
ANAYEMJUA MWAKYEMBE
Mpaka sasa, Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe iliwahi kumtaja kijana aitwaye Mangunga ambaye ndiye anadaiwa kuwa na Masogange ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.



Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Afrika Kusini ikisema unga huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni kemikali haramu.
KAMATI YA MAPOKEZI YAMWANDALIA PATI YA MAMILIONI
Habari za kifukunyuku zinadai kuwa, jijini Dar baadhi ya mastaa wameunda kamati ya mapokezi ya Masogange, Jacqueline Wolper Massawe akiwa mwenyekiti wake, katibu na wajumbe hawakupatikana majina.
KAZI YA KAMATI
Kazi ya kamati hiyo inadaiwa ni kukusanya mamilioni kutoka kwa mapedeshee wa mjini ili kuwezesha kufanyika kwa pati ya nguvu ya kumshukuru Mungu kwa kumsaidia staa huyo kutoka jela na kurudi Bongo.
“Kamati iko chini ya uenyekiti wa Wolper, si unajua huyu dada hata hivi karibuni alimfanyia birthday Masogange japo mwenyewe hakuwepo?
“Sherehe itaandaliwa kwenye ukumbi mmoja uliopo ufukweni mwa Bahari ya Hindi lakini kwa sasa sitautaja ili kuepuka wazamiaji,” kilisema chanzo chetu.


NZOWA: HIYO PATI ITAFANYIKIA WAPI, SINZA KWA DADA’KE AU?
Kufuatia kuwepo kwa madai kwamba, Masogange akitua tu Bongo atadakwa na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, juzi Amani lilimsaka kamanda wa kikosi hicho, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo.
Amani: Afande, naomba unisaidie mawili matatu. Yule msanii Masogange aliyekamatwa na madawa ya kulevya na kuhukumiwa Afrika Kusini anarejea nchini kesho Jumatano (jana) Je, ninyi mna mpango wowote wa kumkamata akitua?
Nzowa: Sisi hatuna shida naye tena. Alishahukumiwa kule, sasa tumkamate huku kwa sheria gani?
Amani: Basi kuna habari kwamba mmepanga kumkamata maana tumeambiwa na chanzo chetu kuwa atafanyiwa pati ya kumshukuru Mungu kwa kumtoa katika mazito.
Nzowa: Hiyo pati ataifanyia wapi, Sinza kwa dada’ke au?
Amani: Bado hawajaweka wazi.
Nzowa: Sisi hatuna shida naye.
WOLPER ASAKWA KUULIZWA
Juzi asubuhi, Amani lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumuuliza ukweli wa kuwepo kwa kamati ya sherehe ya mapokezi ya Masogange ambapo  alijibu:
“Nipo shooting (narekodi) Arusha, nitawatafuta baadaye kuhusu hilo suala kama lipo au halipo.”
MASOGANGE NAYE
Juzi Jumanne, Amani lilimpigia simu Masogange akiwa Afrika Kusini na kumuuliza kuhusu ujio wake wa jana.
Masogange: Ni kweli narudi huko (Bongo) Jumatano, mipango yote ya safari tayari, namshukuru Mungu kwa yote.
WENGINE WANASOTA!
Wakati Masogange akiwa ameponea tundu la sindano, mrembo mwingine wa Bongo Fleva, Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ anateseka gerezani huko China alipofungwa kwa miaka mitatu kwa msala wa madawa ya kulevywa wakati Saada Kilongo yuko mahabusu Bongo kwa kesi ya aina hiyohiyo.

AGNESS MASOGANGE AMETUA BONGO KUTOKA AFRIKA KUSINI ..PICHA AKIWA AIRPORT

Ikiwa ni wiki chache toka kesi ya video vixen Agnes Gerald a.k.a Masogange ya kutuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kuisha kwa kulipa faini nchini Afrika Kusini na kuwa mtu huru, hatimaye jana Jumanne amerejea nyumbani Tanzania.

Masogange

Kupitia Instagram jana Agnes alipost picha (hapo juu) akiwa uwanja wa ndege na kuandika “am cmng homeeeeeeeee”.

Mwishoni mwa mwezi uliopita (September) mrembo huyo aliachiwa huru pamoja na mdogo wake Melissa Edward ambaye mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini ilimuachia huru baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani.

PICHA ZA MUONEKANO WA AGNESS MASOGANGE BAADA YA KUMALIZA KESI YAKE YA MADAWA YA KULEVYA SOUTH AFRIKA

Pichani juu ni taswira mbalimbali za muonekano mpya wa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye kwa sasa yupo uraiani baada ya kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

MCHUMBA WA MASOGANGE ADAI AKITUA BONGO TU ATAMUO MASOGANGE



MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza  hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.

Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.

-GPL

HUKUMU YA MASOGANGE....KUNA MCHEZO UMECHEZEKA!



“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?”
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati akionyesha picha ya Masogange kwa wanahabari.
Stori:  Waandishi Wetu
VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8, lakini baadhi ya wadau nchini wanasema kuna mchezo umechezwa, Ijumaa Wikienda limebaini mambo ya kushangaza nyuma ya pazia.
Masogange na Melissa walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo. Wawili hao wameishi mahabusu kwa saa 1824.
MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA
Uhuru wa Masogange ni baada ya Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg kumtia hatiani kwa kuingiza kemikali hatari nchini humo, akatakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela.
Melissa yeye hakukutwa na hatia kwa vile ilibainika mizigo aliyokutwa nayo aliombwa na Masogange amsaidie kubeba baada ya kukutana ndani ya ndege ya Shirika la South Africa Airlines.

KUMBE SI CRYSTAL MATHAMPHETAMINE
Habari kutoka nchini humo zinasema mdhamini wa Masogange (jina halijapatikana) alipigana kuhakikisha staa huyo na nduguye ambaye amezaliwa naye kwa mama mkubwa wanakuwa huru na kurejea Bongo.
Katika kupigana huko, mdhamini huyo alifurahia matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa serikali ya nchi hiyo kuyaona madawa hayo kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi.
Kwa Bongo madawa hayohayo ni unga na tayari watu wengi wapo korokoroni kwa kukamatwa nayo akiwemo aliyekuwa rafiki wa marehemu Steven Kanumba, Saada Ally.
Katika hilo, mtu anayekamatwa na madawa hayo nchini humo hushtakiwa kwa kosa la kuingiza kemikali hatari. Serikali ya Afrika Kusini ilipiga marufuku kuingizwa nchini humo kwa madawa hayo na adhabu yake iko wazi.
“Yule mdhamini alipojua mkemia mkuu amesema yale si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine aliitumia nafasi hiyo kucheza na mwanasheria ambapo kifungo chake kinajulikana,” alisema mtoa habari wetu mmoja.
 
Mangunga.
MSEMAJI WA ‘TRA’ YA SAUZ AINGIA SHAKA
Habari zinasema kuwa, kufuatia taarifa za mahakama kwamba mzigo huo si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini (SARS), Marika Muller alisema kuwa timu yake ina uhakika wa asilimia mia moja kwamba, mzigo wote wa Masogange na Melissa walioukamatwa  nao ni madawa ya kulevya aina ya Crystal Meth.
Muller akatoa la moyoni akisema kwamba, kama mahakama imekubaliana na matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa nchi hiyo, yeye hana la kusema kwa kuwa uamuzi wa korti ni wa mwisho.
KAMANDA NZOWA ANYOOSHA MIKONO
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa ambapo alipoulizwa juzi kama serikali ina mpango wa kumkamata Masogange atakaporejea nchini ili awataje waliomtuma, alisema:
“Sasa kama wameachiwa kule, sisi tutawakamataje? Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kesi ilisikilizwa kule mahakama ikafikia ilipofikia, basi tena! Ila tutafuatilia chini kwa chini mtandao huo.”
 
Melissa Edward.
MCHEZO UMECHEZWA
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya wasomaji walipozungumza  juzi walitilia shaka kuwepo kwa mazingira ya kuchakachuliwa kwa madawa hayo.
Walisema kuwa, ilikuwaje SARS iwakamate akina Masogange na kugundua walibeba Crystal Meth (unga) halafu mahakama iseme ni Ephedrine (kemikali hatari)?
“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?” alihoji msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Aunt Elizabeth, mkazi wa Mbezi Beach, Dar.
Wengine walitupia kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na Twitter wakidai hivyohivyo kwamba kuna mchezo umechezwa.
“Kwanza wamekamatwa Julai 5, mwaka huu. Kesi imeisha katikati ya wiki iliyopita, hata miezi mitatu haikufika. Hapa Bongo, yule mama Leila (Mwanaidi Mfundo) na wenzake walikamatwa 2011 kwa unga huohuo, kesi yao bado ipo Mahakama Kuu, Dar hadi leo,” alisema Samuel Msalanda wa Ilala, Dar.
Wengi walionesha kutilia shaka hukumu hiyo kutokana na mitazamo yao lakini Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg, Afrika Kusini ndivyo ilivyoamua.
MASWALI TATA
Ukiachana na mitazamo na ukweli ulivyo, bado kuna maswali tata ambayo utatuzi wake unakuwa mgumu kulingana na kesi yenyewe kuanzia kutajwa, kusikilizwa hadi hukumu ilikuwa nje ya Tanzania.
Je, mwenyewe Masogange alipokuwa akisafirisha dawa hizo alijua ni kemikali hatari ambayo ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
Iwe ni kemikali au la! Alitoa wapi mali ghafi hiyo na alikuwa akimpelekea nani kule Afrika Kusini?
Ni kigogo au mtu gani aliyeratibu safari hiyo mpaka Masogange akafanikiwa kupita kwenda Afrika Kusini?
Nani alimpeleka Masogange hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)?
Kituo cha kwanza cha Masogange kuondokea kwenda JNIA kilikuwa wapi? Inawezekana ni nyumbani kwake ambapo alilala na mizigo yote ile?
Kama mahakama imebaini Masogange hakuingia Afrika Kusini  na unga, vipi kuhusu wale  wafanyakazi wa  JNIA walioachishwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwa kuzembea Masogange akapita na ule mzigo?
Yupo wapi Nassoro Mangunga aliyetajwa na Dk. Mwakyembe kuwa alifanikiwa kutoroka na mabegi matatu ya unga kule Sauzi?
-PGL

POLISI SASA KUFUATILIA NYENDO ZA AGNESS MASOGANGE NA MELISA..


Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, kimewataja Agnes Gerald, maarufu Masogange, na Melissa Edward kuwa watafuatiliwa nyendo zao kwa umakini.

Hatua hiyo iliyotangazwa na Kamishna Mkuu wa kitengo hicho, Geofrey Nzowa, imekuja siku moja baada ya Watanzania hao, Masogange na Melissa kuachiwa huru na Mahakama ya Kempton Park ya Afrika Kusini.
Nzowa alizungumza jana na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu, kuwa watu hao wataangaliwa kwa umakini watakapokuwa wakisafiri nje ya nchi.
Vilevile, alisema wataimarisha ukaguzi kwa Watanzania wengine, wenye historia ya kubeba dawa za kulevya wanaposafiri kwenda nje ya nchi.
“Masogange na Melissa tutawaangalia kwa jicho la umakini zaidi watu hawa,lakini siyo hao tu hata Watanzania wengine kwa sababu umdhaniaye siye kumbe ndiye,” alisema Nzowa.
Nzowa alisema Watanzania watakaokamatwa na dawa za kulevya nchini au nje na wataadhibiwa kulingana na sheria kama Masogange alivyoadhibiwa.
Hata hivyo, juzi Nzowa alionyesha kushangazwa na hukumu waliyopewa Masogange na Melissa akisema kuwa ni ndogo ukilinganisha na kiasi kikubwa cha kemikali walizobeba.
Hapa jijini Johannesburg, Masogange na Melissa jana walionekana wakitembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo ikiwamo madukani wakifanya ununuzi na katika saluni za urembo.
Mtu wa karibu na watu hao alisema, Watanzania hao hawana hofu ya kufanya chochote kwa sababu mahakama imegundua kuwa hawana hatia.
Waogope kutembea barabarani kwa sababu gani wakati wameachiwa huru? Mahakama imefanya kazi yake na wao wana haki,” alisema mtu huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Julai 5 mwaka huu, Masogange na Melissa walikamatwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Oliver Tambo Afrika Kusini wakiwa wamebeba kilo 150 za dawa za kulevya aina ya crystal methamphetamine (Tik).
Hata hivyo, baada ya kukaa mahubusu kwa takriban miezi mitatu, mahakama ya Kempton inayoshughulikia makosa ya jinai, ilibaini kuwa Watanzania hao hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya aina ya ephedrine.

AGNESS MASOGANGE AACHIWA HURU BAADA YA KULIPA FAINI YA SH. MILIONI 4.8

Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya. 
 
Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
 

Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
 

Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.
 

“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
 

Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
 

Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
 

Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.
 

Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
 

Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya

Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
 

Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.
 
“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.
 
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
 
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.
 
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
 
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.
 
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.
 
“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.
 
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.
 
Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.
 
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
 
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani

Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
 
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.
 
Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
 
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
 
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

HUU NI USHAHIDI KUWA AGNESS MASOGANGE YUKO HURU ...CHEKI PICHA HIZI 3

Picha  hizi  zinatosha  kuthibitisha  kwamba  Agness  Masogange  ambaye  siku  hizi  anajiita  Agness MATAKO yuko  huru  mtaani.....

Agness alikamatwa  na  madawa  ya  kulevya  nchini  Afrika  Kusini  na  vyombo  vya  habari  vya  nchi  hiyo  viliripoti  hivyo....

Mapema wiki  hii, taarifa  zilibadilishwa  na  kuripotiwa  kuwa  madawa  aliyokamatwa  nayo  si  ya  kulevya...

Picha hizi Amezipiga akiwa Gym leo asubuhi zinazidi kutoa ushahidi kuwa yupo Mtaani ...au jela za South Mambo ndio hivi ? We unasemaje?

MASOGANGE AINGIZWA CHUMBA CHA MATESO ILI WAWATAJE WALIO WATUMA


EVUJA! Staa muuza nyago kwenye video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu za Kibongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.
Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.





























MATESO SAA 24
Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.
USHUHUDA
“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.
“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.
“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.
“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.
“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.
“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.
“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.
“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.
WALIOWATUMA
“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.
MTOTO WA KIGOGO ATAJWA
Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).
Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.
Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.
i lilipozungumza na Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba  kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.
ULINZI KAMA SHEHE PONDA
Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.
WAPANDISHWA TENA KORTINI
Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.
Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.

UREMBO NDIO ULIMPONZA MASOGANGE HADI KUKAMATWA NA MADAWA SOUTH...HII NDIO STORY NZIMA






























Imebainika kwamba, Baada ya mpango madhubuti uliosukwa na wauza madawa ya kulevya hapa nchini wakishirikiana na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wa kuwasafirisha watuhumiwa hao Agnes Gerald maarufu kwa jina la Masogange na mwenzake Melisa Edward, mtandao huo ulikuwa pia umejipanga vyema nchini Afrika Kusini kuwapitisha watuhumiwa hao bila kukamatwa.
Kilichomponza Masogange kukamwatwa ni pale alipochelewa kutoka uwanjani hapo kutokana na kujiremba, kitu ambacho kilisababisha kufanyiwa upekuzi wa dharura na askari ambaye hakujua kuhusu mpango huo.
Taarifa zinabainisha kwamba, baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, mwenzake waliyesafiri pamoja aliyetajwa kwa jina la Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 za madawa hayo ya kulevya bila kujulikana.
Kilichomponza Masogange ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine, bali ulikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na Polisi. Nadhani huyu Askari aliyewashika hakujua kuhusu mpango huo.” kilisema chanzo kimoja ndani ya jeshi la Polisi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania Daima la Tarehe 17/8/2013

HUU NDIO MCHEZO ULIO FANYIKA UWANJA WA NDEGE KUMPITISHA "AGNESS MASOGANGE NA MELISSA" WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA

 
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana alikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa picha ya namna mchezo wa usafirishaji wa madawa ya kulevya unavyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Dr. Mwakyembe akionesha picha ya Masogange aliyoipost Instagram ikimuonesha ameshika lundo kubwa la hela

Mwakyembe alisema kamera za CCTV, zilizowekwa uwanjani hapo zinaonesha mchezo mzima ulivyokuwa.

Alisema majira ya saa 10:15 walionekana Agnes ‘Masogange’ Gerald akiwa na mdogo wake Melisa Edward walionekana wakiwa na mfanyabiashara mmoja katika eneo la kuingilia abiria huku wakiwa na mizigo na mabegi tisa yaliyofanana.

Alisema kamera zilimwonyesha askari polisi akihangaika kuwasaidia abiria mbalimbali kuweka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi, kazi ambayo alieleza kuwa haikuwa yake.

“Mbeba mizigo anayetuhumiwa kuwa katika mtandao huo alionekana akiwasaidia vijana hao watatu (Agnes, Melisa na mfanyabiashara) kupeleka mizigo yao kwenye mashine ya ukaguzi na baadaye kuyazungushia mabegi hayo katarasi za nailoni na kuyafikisha kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini,” alisema.

Alisema kamera hizo zilimnasa ofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA akimwondoa katika kiti cha ukaguzi wa mizigo mfanyakazi mwenzake, na kukaa yeye ikiwa ni dakika chache kabla ya mabegi tisa ya vijana hao hayajaingia katika mashine ya ukaguzi.

“Kinyume na taratibu ofisa huyo hakujiandikisha kwenye kitabu cha wakaguzi (Screener’s logbook), saa 10:16 akaanza kupitisha mabegi hayo tisa mpaka saa 10:22. Alipomaliza kupitisha mizigo hiyo kwa dakika sita akamwachia ofisa aliyekuwa katika eneo hilo na kuondoka.”

Dr Mwakyembe alidai ofisa huyo baada ya kuondoka katika kiti hicho alizungumza kwa dakika kadhaa na askari polisi anayedaiwa kuwa katika mtandao huo na kurejea tena sehemu aliyokaa ofisa mwenzake wa TAA na kumnong’oneza jambo fulani.

“Baada ya hapo akaelekea ukumbi wa abiria huku akiongea na simu, mambo hayo yote yalifanyika huku kiongozi wa sehemu ya ukaguzi akiwa hapohapo bila kushtuka.”

Alisema baada ya mizigo hiyo kupita katika mashine ya ukaguzi (baggage screening machine), vijana wale watatu wakahamia na mizigo yao kwenye kaunta ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

“Mabegi matatu ya kilo 20 kila moja yalipitishwa yakabaki mabegi sita ambayo yalitakiwa yalipiwe malipo ya uzito wa ziada. Kwa taratibu za shirika hilo kila kilo moja inayoongezeka hulipiwa dola 5 (Sh8,000), vijana wale walitakiwa kulipia dola 600, lakini walitozwa dola 94 tu ambazo zinathibitishwa na risiti tuliyonayo,” alisema.
Alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia gharama ya dola 60 (Sh96,000) ili kupata tiketi.

“Kutokana na hali hiyo mhakiki wa nyaraka za safari nje ya ukumbi wa abiria siku hiyo, hakupaswa kumruhusu mfanyabiashara kuingia ndani ya ukumbi bila tiketi ya siku hiyo,” alisema na kuongeza; “Kwa hali ya kawaida mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa, lakini siku hiyo mbwa walichelewa na walikuja kutumika baadaye ikiwa ni baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.”

Alisema siku ya tukio saa 9:28 kamera hizo za usalama zilimwonyesha mbeba mizigo wa uwanja huo akiwa anazungukazunguka eneo la kuingilia abiria kama mtu ambaye ana ahadi na kukutana na mtu fulani.

“Kamera pia zilimnasa ofisa mwingine wa TAA kwa mara kadhaa akitoka na kuingia ndani ya jengo la abiria huku akizungumza na simu, kitendo ambacho hakiruhusiwi kabisa kwa wafanyakazi wa eneo la ukaguzi wa abiria,” alisema na kuongeza;

“Wakati huohuo, kamera zilikuwa zinamwonyesha askari polisi anayetuhumiwa kuhusika katika mpango huo akiwa anarandaranda eneo la uhakiki wa hati za kusafiria kama vile anasubiri kitu fulani.”

Kutokana na hali hiyo, Dr. Mwakyembe ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kuwasaidia Masogange na mwenzake kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini, “Akamatwe na kuunganishwa na kesi inayowakabili Watanzania hao wawili.”

Alisema TAA inatakiwa kuwafukuza kazi mara moja wafanyakazi wake wanne waliohusika katika mpango huo, kuwakamata na kuwaunganisha katika mashtaka yanayowakabili.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa