Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label taarifa. Show all posts
Showing posts with label taarifa. Show all posts

TAARIFA TOKA BODI YA MIKOPO TANZANIA KWA WAOMBAJI

TAARIFA KWA UMMA
KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja hadi Julai 31, 2013.

Pamoja na nyongeza hii ya muda, Bodi inasisitiza waombaji kujaza fomu za maombi ya kwa njia ya mtandao (OLAS) kwa usahihi na kuzingatia muda wa maombi uliowekwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. 
Waombaji wa mara ya kwanza wahakikishe wanajaza kwa ufasaha na kuweka viambatanisho vyote muhimu ili kufanikisha mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo. 

Kundi la kwanza la wanafunzi waliopangwa kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamemaliza mafunzo hayo mwezi Juni, 2013 wanapaswa kutumia fursa hii kujaza fomu za maombi ya mikopo bila kukosa. 
Aidha, kundi la pili la wanafunzi wanaotegemea kuanza mafunzo hayo mwezi Julai, 2013 walitakiwa wawe wameshaomba mikopo kati ya tarehe 1 Mei, 2013 na 30 Juni, 2013 lakini endapo kuna wachache ambao hawakuweza kufanya hivyo basi nao watumie muda huu wa nyongeza kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao wakiwa huko huko JKT.
Endapo mwombaji yeyote atakabiliana na matatizo wakati wa kujaza fomu yake anashauriwa kupiga simu kwenye dawati la huduma kwa wateja kwa namba 022 550 7910 kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 2.00 usiku siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 10.00 jioni siku za Jumamosi.

Ikumbukwe kwamba Bodi haitaongeza muda wa ziada baada ya Julai 31, 2013 ili kutoa nafasi kwa Bodi kuendelea na mchakato wa uchambuzi na upangaji mikopo. 
 
IMETOLEWA NA: 
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

AWAMU YA PILI YA MAJINA YA WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA NA KAMBI ZA JKT WALIZOPANGIWA...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 JUNI MWAKA HUU

JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YA RUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT WWW.JKT.GO.TZ. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAURU KWA DIVISIONI, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa