Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Showing posts with label je wajua. Show all posts
Showing posts with label je wajua. Show all posts

HUYU NDIYE MWANAUME WA KWANZA AMBAYE HAJAWAI KUOGA WALA KUKATA NYWELE ZAKE ZAIDI YA MIAKA 37

Mr Singh na Mkewe  
Hakika haya tunaweza kuyaita mafanikio ya ajabu kwa mzee huyu kutokana maamuzi yake.Labda tumite Mr Adui wa Maji ila jina lake kamili ni Mr Kailash Singh akiwa na ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu anayenuka zaidi kutokana na kutokuoga kwa zaidi ya miaka 37 sasa.
Mr Singh, 65, hajaoga na hata kukata nywele zake zenye urefu wa futi 6 toka mwaka 1974, mda mfupi mara baada ya kutoka kuoa.

Akielezea juu ya uamuzi wake wakushangaza, Mr Singh anasema mchungaji alimuahidi zawadi ya mtoto wa kiume kama atafata ushauri.

Licha ya majirani kuwa wanamtania na kumdhihaki jamaa huyo walishindwa kubadili maamuzi yake na namna ya kipekee alifanikiwa kumshawishi mke wake, ila cha ajabu zaidi ni pale ambapo imani yake imeonekana kumdanganya kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike

JE WAJUA..? MADHARA YA KUTOFANYA MAPENZI KWA MUDA MREFU.

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
• kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
• Kusahausahau,
• Kupendelea story za mapenzi,

• Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
• Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
• Kuumwa na kichwa,
• Kukakamaa mgongo (wanaume),
• Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
• Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
• Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
• Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala kama ulevi n.k.
 

MWANAUME WA KWANZA DUNIANI KUBEBA MIMBA AJIFUNGUA MTOTO WAKE SALAMA

Yule mwanamke-mwanaume wa Marekani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya picha yake akiwa na mimba huku akiwa na midevu kusambaa duniani amerudi tena kwenye vichwa vya habari mwaka huu baada ya kujifungua mtoto wa pili. Thomas Beatie, au maarufu kama 'Mwanaume Mjamzito' amerudi tena kwenye vichwa vya habari vya magazeti baada kujifungua kwa mara ya pili mtoto wa kiume jana asubuhi.

Picha za Thomas akiwa na madevu kibao huku akiwa na tumbo kubwa la ujauzito zilikuwa maarufu sana duniani mwaka jana kiasi cha kumfanya Thomas atajwe kama mwanaume wa kwanza kupata ujauzito.

Thomas anaishi na mkewe Nancy ambaye ndiye atakayekuwa akimnyonyesha mtoto wao mpya kama alivyofanya kwa mtoto wao wa kwanza wa kike anayeitwa Susan Juliette aliyezaliwa mwezi juni mwaka jana.

Thomas alizaliwa kama mwanamke lakini baadae alibadilisha jinsia kuwa mwanaume na kufanya upasuaji wa kuondoa matiti yake huku akitumia madawa ya homone za kiume yaliyomfanya awe na madevu kama mwanaume.

Thomas hakufanya upasuaji wa kuondoa uke wake hali ambayo ilimwezesha kupata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza baada ya kupandikizwa mbegu za kiume.

Thomas ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 35 alisema kuwa aliamua kuzaa mtoto baada ya mke wake Nancy mwenye umri wa miaka 45 kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito.

"Kuwa na mtoto hakuangalii kuwa wewe ni mwanamke au mwanamme, mimi pia ni binadamu na ninahitaji kuwa na mtoto" alisema Thomas.

WATALII WAAMUA KUTEMBEA UCHI WA MNYAMA WAKIANGALIA VIVUTIO

DUNIANI kuna mambo! Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada  ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama.
Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma. 

Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja  ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha  afungwe ni kutemba uchi wa nyama hadharani.
Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.
Gough alikiri kosa hilo na hakujitetea na jaji akamfunga miezi kumi na moja jela.

MSICHANA WA MIAKA 25 ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAUME 5,000

Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni. Wakati wapo wanawake ambao hawapati salamu barabarani, Nikki Lee, 25 amevunja rekodi baada ya kutimiza idadi ya wanaume 5,000 aliofanya nao ngono.

Nikki ambaye aliibukia katika fani ya urembo anasema alifanya vitendo hivyo kwa muda wa miaka tisa sehemu mbalimbali alizokuwa akitembelea.

Anasema alikuwa anafanya ngono katika klabu za usiku, ndani ya ndege, mbuga za wanyama, sehemu za kupaki magari, ndani ya gari, sinema na disko.

Anasema kwamba alianza kufanya hivyo tangu alipotolewa bikira yake akiwa na umri wa miaka 16.

Anasema aliweza kufanya ngono na wanaume wawili kwa siku. "Nilikuwa nasikia raha  ya ajabu na ndiyo maana nilipenda kufanya ngono wakati wote," anasema Nikki. Alipokuwa na miaka 21 alifikisha idadi ya wapenzi 2,289 ambao alikuwa amewaandika katika kitabu chake chekundu.

"Hakuna mwanaume aliyepita mbele yangu asinitamani kwa waliotaka kufanya nami mapenzi nilifanya hivyo, kwa sasa nimeathirika na ngono," anasema Nikki.

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU "BRIAN DEACON" AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.

Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.
  Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.


Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.


watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.



Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.


Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.



kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.


Makala hii kwa msaada wa mtandao....

HIKI NDICHO KIASI CHA PESA ALICHOMINGIZA DIAMOND MWEZI JUNE NA JULY

Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi.


Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.
Show ya nchini Comoro 22 June
Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38.
Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June
Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15.
Show ya Tigo Mwanza 30 June
Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10.
Kili Music Tour 2013
Tulipata taarifa kuwa Diamond atafanya show kwenye mikoa minne na kwamba amelipwa shilingi milioni 50 kwa show zote.
Show ya Matumaini 7 July
 kwenye hii show diamond ana zaid ya mil.10

Show ya Kenya 27 July
Kwenye show hii Diamond atashare stage na mastaa wa Nigeria, Ice Prince na Davido na hapa kama alivyosema kuwa katika show za nje ya nchi huwa hachukui chini ya dola 15,000. Kuna uwezekano hapa akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 20.
Kama una calculator basi unaweza ukapiga hesabu mwenyewe ni kiasi gani ameingiza kwa show za June na July. Kumbuka pia kuwa show zote hata za July tayari ameshasaini mkataba na ameshalipwa chake tayari. Kitu kama milioni 140 na usheee!!
Pia kumbuka ni balozi wa Cocacola na hulipwa kila mwezi kwa shughuli zinazohusiana na deal hiyo. Katikati wa mwezi July pia kuna uwezekano akawa na show zingine kibao.
“Siku zote ishi ukikumbuka, Maisha ni Vita, vita ambayo mwisho wake ni siku ya wewe kuingia kaburini, hivyo haupaswi kuchoka wala kukata tamaa.Heshima, Juhudi na Maombi ndio nguzo pekee zitazokusaidia wewe kushinda Vita hii… tambua Mwenyezi Mungu ndiye Muweza na Mpaganga wa yote,” anasema Diamond.

WASICHANA WATENGENEZA JENERETA INAYOTUMIA "MKOJO" BADALA YA MAFUTA

WASICHANA wanne kutoka Nigeria wamegundua jinsi ambacyo mkojo unaweza kutumika kama mafuta ya kusukuma jenereta. Wasichana hao, Duro-Aina Adebola,Akindele Abiola, Faleke Oluwatoyin na Bello Eniola, wote wenye umri wa miaka 14 wamefanya maonyesho ya jenereta hilo na limeonekana kufanya kazi.

Genereta hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k, Sasa genereta hilo linafanyaje kazi?

Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo kiitwacho electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen. Kisha hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji kwaajili ya kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.

Hiyo gas cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa, liquid borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi.

FACEBOOK UATHIRI WATU KISAIKOLOJIA-"KIVIPI SOMA HAPA"

Facebook, mitandao mingine ya kijamii pamoja na huduma ya ‘blackberry mesenger’ maarufu kama BBM huathiri watu kisaikolojia, husababisha ndoa kuvunjika pamoja na usaliti katika uhusiano, wanasayansi wamebaini.
Utafiti huo uliofanywa mwaka 2012 na wanasayansi wa nchini Israel umebaini kuwa kwa wastani, wanawake wanatumia dakika 81 katika mitandao ya kijamii kwa siku ukilinganisha na wanaume ambao hutumia dakika 64, huku watu wasio na elimu wakionekana kuathirika zaidi na mitandao hiyo.
Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv walihusisha matukio kadhaa ya kisaikolojia kati ya watu walioathirika na mtandao na udanganyifu uliosababishwa na uhusiano unayoanzishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Utafiti huo ulibaini kuwa wote waliohusishwa walikuwa na tatizo la upweke, ingawa hakuna aliyekuwa na historia ya matumizi ya dawa za kulevya au matatizo ya kisaikolojia.
Watu wenye upweke walionekana kupendelea kutafuta uhusiano kupitia mitandao, jambo linaloelezwa kusababisha kuwaumiza watu hao na kuhisi kusalitiwa.
Kiongozi wa utafiti huo Dk Uri Nitzan kutoka Chuo Kikuu cha Sackler mchepuo wa Tiba na Afya ya Akili, Shalvata Mental Health Care Centre alisema: “Kama ilivyo matumizi ya mtandao yanazidi kuwa makubwa. Vivyo hivyo inavyozidi kuhusiana na masuala ya saikolojia. Mawasiliano ya kompyuta kama Facebook na makundi ya mawasiliano yaliyopo ndani ni sehemu muhimu ya habari hii.”
Utafiti huo awali ulihusisha wagonjwa watatu ambapo Dk Nitzan anasema kuwa utafiti wao ulibaini kuwapo na mawasiliano kati ya saikolojia za wagonjwa hao na mawasiliano ya mitandao ikiwemo Facebook. Dk Nitzan anasema kuwa wagonjwa wote watatu waliachana na maisha ya upweke na kupata furaha baada ya kupata wapenzi wapya kupitia mitandao.
Anasema: “Ingawa uhusiano wau huwa na mtazamo chanya awali, lakini huishia kuwa na mawazo ya kuumizwa, kusalitiwa na uvamizi wa faragha. Watu hawa walibadilishana mawazo, ikiwamo upweke na mazingira magumu katika hasira au kutengana na watu waliowapenda awali, kutokana na teknolojia hawakuwa na historia ya kunyanyaswa,” anasema na kuongeza:
“Katika kila kesi, kulikuwa na uhusiano baina ya kuwapo na maendeleo ya taratibu na ongezeko la dalili za kuathirika kisaikolojia, pamoja na udanganyifu, wasiwasi, kuchanganyikiwa na matumizi yaliyozidi ya mawasiliano ya kompyuta.
”Dk Nitzan anasema kuwa tatizo kubwa la mitandao ni watu kuanzisha uhusiano kabla ya kuonana ana kwa ana, tatizo ambalo husababisha mtu kumwona mwenzake anamfaa, huku hali ikiwa ni tofauti pindi wawili hao wanapokutana. Aliongeza kuwa wataalamu wa afya ya akili lazima waache ushawishi wa matumizi ya mitandao ya kijamii wanapozungumza na wagonjwa.
“Unapowauliza watu kuhusu maisha yao ya kijamii ni busara zaidi kuwauliza juu ya matumizi ya Facebook na mitandao mingine ya kijamii, kama matumizi ya mitandao,”anasema.
Anaongeza: “Utafiti wetu unaonyesha, wakati teknolojia kama Facebook ikiwa na faida nyingi, baadhi ya watu wamekuwa wakiathirika na mitandao hii ya kijamii, huku ikiwavutia walio wapweke au walio katika mazingira magumu katika maisha yao ya kila siku, wakati wengine wakilazimisha tabia zisizo zao.”
Wataalamu Dar
Mwanasaikolojia na Mkurugenzi wa Kliniki ya NEHOTA inayotoa huduma ya ushauri iliyopo Makongo Juu jijini, Dk Bonaventura Mutayoba Balige anasema kuwa tatizo kubwa linalowafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuathirika kisaikolojia ni uhusiano unayoanzishwa kupitia mitandao hiyo. Uhusiano unaoanzishwa katika mitandao ya kijamii hata ukiwa na matokeo chanya na kuanzisha ndoa, mara nyingi wanandoa hao huhisi kuumizwa au kusalitiwa muda wowote, jambo linalosababisha migogoro ya mara kwa mara.
“Unapokuwa na mume au mke mliyekutana Facebook, kisha akaendelea kutumia mtandao huo, bila shaka anapokuwa bize mtandaoni muda mwingi, mwenzake huanza kuathirika kisaikolojia kwani huanza kuumia kwa kuhisi kusalitiwa na mweza wake,” anasema mwanasaikolojia huyo.
Dk Balige anasema kuwa licha ya kuwepo watu wanaoathirika kwa kuwa mitandaoni muda wote, bado idadi ya watu wanaoanzisha uhusiano kwenye mitandao hiyo wakiwa kwenye hatari ya kuathirika zaidi, hasa kutokana na udanganyifu uliopo.
“Picha hazisemi kweli; wapo watu wakipiga picha haitoki kama alivyo. Hivyo mwanamke au mwanamume akianzisha uhusiano kwa kutegemea picha aliyoiona Facebook, bila shaka anaweza asitamani kuendelea na uhusiano huo atakapokutana na mtu husika ana kwa ana,” anasema Dr Balige.
Tafiti nyingine
Machi 8, 2011 wanasheria nchini Marekani walitoa ripoti yao kuwa mtandao wa Facebook ni chanzo cha migogoro katika uhusiano. Pia husababisha ndoa nyingi kuvunjika, hali inayosababisha kuongezeka kwa kesi za kudai talaka mahakamani.
Wanasheria hao walisema chanzo cha talaka nyingi ni mtandao wa Facebook ikiwamo ‘Blackberry messenger’ (BBM), huku ‘My Space’ ikichangia kwa asilimia 15 na Twitter kwa asilimia 5.
Mwanasaikolojia na mshauri wa ndoa kutoka Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Loyola, Chicago Dk Steven Kimmons amewahi kusema: “Nimepokea kesi nyingi, mojawapo ni mwanamume aliyekutana na mwanamke aliyesoma naye kwenye mtandao wa Facebook na kuanza uhusiano, huku akiwa ameshaoa. Ni tatizo kubwa.”
Mikasa ya Facebook
Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Henry anasema kuwa aliwahi kufungua akaunti ya Facebook na barua pepe feki vyote vikiwa na jina la msichana. Aliombwa urafiki na wanaume wengi, ambao walimtongoza na baadaye aliamua kumkubali mmoja aliyemfahamu, akiwa pia mtu wake wa karibu bila mtu huyo kumgundua.
“Nilianza kuchati naye, alinipenda kupitia picha niliyoiweka kwenye ukurasa wangu. Alinitumia barua pepe pia, baada ya miezi miwili alihitaji kuniona niliamua kufunga akaunti hiyo baadaye,” anasema Henry aliyebainisha kuwa mwanaume huyo alikuwa ni mume wa mtu.
Rahel Simon (si jina lake halisi) anasema kuwa alikutana na mume wake mwaka 2009 kwenye mtandao wa Facebook. Walipendana na kwa kuwa wote waliishi jijini Dar es Salaam ilikuwa rahisi kuonana.
“Wakati huo mtandao ulikuwa hauna watu wengi kama ilivyo sasa. Tulijuana na kufunga ndoa, ila nina wasiwasi wa kusalitiwa, muda mwingi mume wangu anapokuwa akichati na marafiki zake kupitia mtandao huo. Yaani kuna wakati huwa najilaumu na kutamani kama tungekutana kanisani, huwa nahisi kama alivyokutana na mimi ipo siku ataisaliti ndoa,” anasema Rahel.
Mwingine aliyejitaja kwa jina moja la Janet anasema: “Sitaki kusikia uhusiano wa kwenye mtandao.
Nilikutana na wanaume kadhaa, nikajiingiza katika uhusiano nao, baada ya kunitumia waliniacha, sidhani kama kuna mwanamume aliye tayari na mwanamke anayekutana naye kwenye hii mitandao ni waharibifu tu,” anasema kwa jazba.

Mwathirika mwingine (Hamis) aliyekuwa akitafuta mchumba kupitia Facebook anasema kuwa alikutana na msichana mmoja kupitia mtandao huo baada ya kuona picha alizoweka binti huyo kwenye ukurasa wake, zikiwa na staili mbalimbali na kumpenda, akamtongoza na wakakubaliana kuonana. “Tulipanga kuonana Ukonga jijini Dar es Salaam. Wakati wote tuliwasiliana kupitia simu. Aliniambia angefika kwa usafiri wa daladala nilimsubiri kituoni.
Alipofika alinipigia simu, nilimuuliza umevaaje akaniambia nguo za kitenge. Nilitupa jicho ila nilipomwona sikuamini, nilizima simu kwa kuwa alikuwa mbali ili asijue kama ni mimi na kutokomea. Alikuwa ni tofauti na nilivyomwona Facebook alikuwa mbaya,” anasema Hamis.
Dondoo muhimu
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Gothenberg uligundua kwamba watu wenye kipato cha chini na wenye elimu ndogo wanatumia muda mwingi katika mtandao wa Facebook.
Katika kundi hili, wengi wanaotumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii hawana furaha na wametawaliwa hali ya chini katika maisha yao.
Utafiti unaonyesha zaidi ya asilimia 85 ya watumiaji wa Facebook huingia katika mitandao hiyo kila siku. Asilimia 26 ya kundi hilo huona ni jambo la kawaida kwa wao kutoingia mara kwa mara.

MFAHAMU KIJANA WA KIKENYA ALIYETENGENEZA HELIKOPTA


Onesmus Mwangi

Kijana mfanyakazi wa shambani ambaye ameunda ndege aina ya 'helikopta’ sasa anaitaka Serikali kumsaidia kufanikisha ndoto yake ya kupeperusha angani badala ya kumzima.
Bw Onesmus Mwangi, mwenye umri wa miaka 20, amekosa kifaa kimoja tu na kibali cha serikali kwa ndege yake kupaa angani.


Aidha, anahitaji cheti cha wasimamizi wa safari za ndege kupata idhini ya kupeperusha kifaa chake katika anga ya Kenya.
Ni ndoto ambayo imebakia padogo kutimia kwa kijana huyo aliyekatiza masomo kwa sababu ya umaskini. Alikosa kuendelea zaidi ya darasa la sita kwa kukosa karo.
Aidha, mamake alimkazia mara kwa mara kuunda vitu kama hivyo. Asitake mwanawe kukwama njiani na kufedheheka kwa kukosa ufadhili wa kununua vifaa alivyohitaji.
“Imewahi kupaa japo mara moja tu na hata mwenyewe sikubaini. Nilikuwa nikifanya majaribio kama kawaida nikagundua niko juu naona tu mabati ya nyumba,” aliambia Taifa Leo pia sisi tulipofika kushuhudia.
Ni ubunifu uliovutia mamia ya wakazi katika boma la tajiri wake Esther Wanjeri eneo la Magomano mjini Githunguri kijana alipowaita watu kujionea mradi wake ukifanyika halisi.
Ilibidi bikizee huyo kuwaita maafisa wa utawala kwa woga kwamba ujuzi wa kijana huyo umepita mipaka. Aidha, alihofia umati uliofurika bomani kwake kwani walifurika hadi nje na kufunga barabara.
Ni hatua hiyo iliyomfanya kuwa maarufu kwani ndege hiyo kwa sasa imepelekwa katika ofisi za mkuu wa wilaya.
Ilimchukua Mwangi miezi minane kuunda kifaa hicho – tangu Agosti mwaka jana. Hana mafunzo yoyote ya kiufundi. Kisomo chake cha darasa la sita hakijamfaa.
Ndege hiyo sio ubunifu wa kwanza, asema. Ameunda simu lakini vifaa vikamkosa. “Mamangu pia alinizuia kuunda vitu kama hivi akisema hana pesa za kuninunulia vifaa nilivyohitaji,” alideleza.
Ni mtoto wa sita kati ya watoto 12 katika familia ambayo mamake ndiye mlezi pekee.
Aliamua kutoka kwao Nyandarua kuja tafuta kazi ya kuchunga ng’ombe na ndipo akakutana na bikizee Wanderi. Kumbe alikuwa na mengine kapuni. Bi Wanderi amekuwa wa msaada sana kumtia moyo na kumadisia senti zilipomkosa.
Injini
Ni ndege iliyo na sehemu zote za kimsingi: mtaimbo endeshi, vyuma vya kusimama chini, injini japo ni ya kawaida ya gari , na yatumia mafuta ya dizeli kuguruma.
Lakini ni hilo tu aweza kufanya—kugurumisha, kwani amepewa onyo kali dhidi ya kuipeperusha angani hadi ikaguliwe na wataalamu wa serikali na kupata kibali cha mamlaka ya safari za ndege ili kufanyiwa 'majaribio’.
Kwa jumla ametumia takriban Sh57,000 hadi sasa ambazo zimekuwa ni mshahara wake tangu kuajiriwa na Bi Wanjeri.
Bidii yake ya kazi ilimtoa Sh2,000 kwa mwezi hadi Sh3,000 sasa. Alizihifadhi kwa simu kupitia Mpesa hadi zilipofika Sh10,000 zikawa mtaji wake.
“Nilianza kwa kununua vifaa vya kimsingi kama mabati, vyuma na misumari nikaunda bodi kwanza kisha nikanunua injini,” alisema kando ya ndege yake.
Anatumia mabati mepesi na vyuma vya pua: “sikuwa na pesa za kununua vyuma vya alumini.”
Anatumai wafadhili watavutiwa na ubunifu wake na kumwezesha kupata vifaa bora ili ndege yake itoshane na zile za kisasa. Yahitaji viti ndani, taa, bodi ya kisasa, mashine za kusoma mwendo na kuonyesha vipimo vingine na kadhalika.
Ukosefu wa fedha, asema hata hivyo, halitamzuia kubuni vifaa vingine. “Sasa nataka kuunda vitu vitakavyofaa watu wengi kwa pamoja,” alisema bila kufafanua.
Naam, ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

KWA STAILI HII YA KUSACHI KWA SECURITY!! WEWE UNAONAJE!

Hivi ndivyo inavyokuwa nigeria , kutokana na kundi la boko haramu kufanya mauaji kwa mabomu .angalia hawa wasichana jinsi wanavyosachiwa je ilikuwa ni muhimu kwa wadada hawa kuweka mikono yake sehemu za siri, tena kwa wakati huu wa sayansi na technolojia huu ni uzalilishaji. 

Ninafahamu kuna vifaa vya ulinzi vya bei rahisi kabisa vya kusachi namna hii bila kumbughuzi mtu hapo ndipo ninaposhangaa  kwa nini walinzi wanafanya mikono yao kuwa vifaa vya ulinzi? ni kweli mikono inaweza kuhisi bomu lililofichwa?

JE WAJUA SABABU KUU ZA WANAWAKE WENGI KUVAA NUSU UCHI?

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo. Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao.

 Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.



Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa. 

Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao
HUU NI MTAZAMO TUU!! wewe ksomaje unaonaje tuandikie hapo chini

SEMA KITU KUHUSU HII KITU



JE WAJUA:UHURU KENYATTA NDIE RAISI ANAEONGOZA KWA UTAJIRI AFRIKA

Uhuru_M_Kenyatta_685841119
Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta ndio rais tajiri zaidi barani Afrika. Kenyatta alikamata nafasi ya 26 mwaka 2011 kwenye orodha ya watu matajiri zaidi barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 500.

Mtoto huyo wa rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta ni mrithi wa mali kibao zilizopo Kenya. Anamiliki ardhi yenye ukubwa wa acre 500,000 katika maeneo mbalimbali nchini humo. Ardhi hiyo ilikuwa ya baba yake aliyoipata miaka ya 1960s na 1970s baada ya serikali ya kikoloni ya Uingereza na benki ya dunia kuwezesha maofisa wa serikali wa Kenya na matajiri kupata ardhi kutoka kwa waingereza kwa bei chee.
Uhuru na familia yake wanamiliki kampuni ya Brookside Dairies ambayo ni kubwa zaidi nchini Kenya kwa utengenezaji wa maziwa na pia ana hisa nyingi kwenye kituo cha TV cha K24 pamoja na benki moja kubwa ya biashara jijini Nairobi. Pia ana miradi mingine kibao.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa