FUNGUKA:FAHAMU MENGI KUHUSU CATHY
Wiki mbili zilizopita tulimleta kwenu mwigizaji na mcheza filamu za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambaye mlimuuliza maswali hivyo wiki hii anajibu na kufafanua kile mlichohitaji kujua kuhusu maisha yake, shuka nayo.
NINI SIRI YA KUDUMU KWENYE NDOA?
Dada Cathy samahani, naomba unipe siri ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka kumi. Juma Ramadhani, Moro, 0716110028
CATHY: Siri kubwa ni uvumilivu tu kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika. Nilimsoma mume wangu naye akanisoma hivyo tunajuana vyema.
PONGEZI
Hongera sana kwa uigizaji wako kwani unatufundisha sisi wanajamii kiujumla. Prosper Mallya, 0658565860
CATHY: Nashukuru sana Mungu akubariki.
KAZI NYINGINE?
Tofauti na kucheza filamu unajishughulisha na nini? Ivody, Iringa, 0764608330
CATHY: Mimi ni mjasiriamali.
SIMU YA KICHINA?
Tunakuona kama simu ya Kichina ambayo haidumu mbona hutoi filamu hata watu hawakushirikishi au umeishiwa swaga? Msomaji, 0754021962
CATHY: Umechelewa sana, tafuta muvi zangu madukani zipo nyingi sana za kwangu mwenyewe na za kushirikishwa.
HISTORIA
Dada Cathy nataka kujua historia yako kwa ufupi. Ester, Morogoro, 0654502305
CATHY: Mimi ni mtoto wa saba kati ya watoto 12 tuliozaliwa katika familia yetu, nina watoto watatu, kabila langu ni Mpare wa Lembeni, Kilimanjaro na sanaa nilianza mwaka 1997.
PONGEZI
Hongera dada Cathy kwa kazi yako nzuri nakufahamu tangu enzi za Mambo Hayo hadi sasa kwenye filamu hauna skendo kama mastaa wengine, upo juu dada kaza buti. Maimuna Dammbaya, Dar, 0658878793
CATHY: Nashukuru sana.
NDUGU YAKE
Eti dada Cathy ni kweli una undugu na mke wa Championi Keko? Natamani kuwa kama wewe. Msomaji, 0719058681
CATHY: Ni ndugu yangu tumetoka sehemu moja, kuhusu kuwa kama mimi nitafute.
USHAURI
Cathy ni mwanamke unayejiamini, hujivuni na unampenda kila mtu ila tunaomba ujikite zaidi kwenye filamu. Aggrey, Dar, 0712316278
CATHY: Asante kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi.
IDADI YA WATOTO
Dada Cathy nataka kujua una watoto wangapi? Baby Fay, Handeni, 0772274232
CATHY: Nina watoto watatu.
WATOTO WAKE?
Eti Jamila na Sophia ni watoto wako? Jamila, Kisarawe, 0716093981
CATHY: Ni watoto wa rafiki yangu ninawapenda na wao wananipenda sana kama mama yao.
ANAMUELEZEA
Cathy nimesoma na wewe jina lako unaitwa Lina John, tulisoma Shule ya Kaili uliacha darasa la tano ukakimbilia Tanga, sijui huko aliendelea au la mko mapacha mwenzako anaitwa Lilian. Celine, 0753485724
CATHY: Umekosea kidogo, mimi nilihamia Tanga nikiwa darasa la saba ambapo nilienda kuanza tena darasa la sita, ni kweli tuko mapacha.
KABLA YA SANAA
Kwa kawaida watu wengi maarufu kabla ya kupata umaarufu kupitia kazi fulani huwa kuna kitu ambacho walikuwa wakifanya. Wewe je, ulikuwa ukifanya kazi gani? Andrew Peter, Dar, 0717570873
CATHY: Nimefanya kazi nyingi sana kama biashara, mfanyakazi kwenye maduka ya watu na saluni na huko kote nilikuwa nahangaika kutafuta maisha.
HUYU ANAMFAHAMU SANA
Nakufahamu Cathy Issaya, kwenu ni Lembeni, Mwanga, una dada yako anaitwa Rozi ndugu zako ni kina Naomi na baba mkubwa wako ni Mzee Kivatiro. Msomaji, 0755699959
CATHY: Kweli unanifahamu.