Kiongozi na mwimbaji mkongwe wa bendi ya 'Twanga Pepeta' luiza Mbutu amefunguka na kuonyesha kukerwa kwake na tabia ya baadhi ya wasanii wa filamu na bongofleva wanaojihusisha na skendo za kimapenzi na kuamua kuwafunda ka kuwapa somo kali.Akizungumza na mwandishi wetu kwenye hivi karibuni luiza alidai kwamba wasanii wa fani zote ni kioo cha jamii hivyo kitendo cha baadhi ya wasanii kujihusisha na mambo yasio kubalika kwenye jamii wakati wao ni kioo cha jamii ni sawa na kuipotosha jamii hiyo inayowatazama.
mfano lshu ya Diamond na Uwoya kunaswa hotelini na mapaparazi jamii inayowatazama inawasomaje kimaisha wakati sisi wasanii ni kioo cha jamii siku hizi watu wako bize na na maisha na sio mambo hayo ya kitoto kwani dunia ya sasa magonjwa ni mengi hivyo kitendo cha kubadilisha wapenzi kila kukicha ni hatari pia kwa afya yako mimi natoa soma kwa wasanii wenzangu tujiheshimu ili tuheshimike"alisema Mbutu kwa hisia kali.huku akiongeza kusema
" Nashukuru kwa upande wetu wa sanii wa muziki wa dani sekendo hizo za ngono sio kubwa kama ilivyo kwa wenzetu wa bongofleva na bongomovie"alisema luiza ambaye kiukweli licha ya kuwepo kwenye fani hiyo ya muziki wa danisi kwa muda mrefu hajaingia kwenye skendo yoyote mbaya pia Ruiza ni miongoni mwa wanamuziki wachache wasio na tamaa ya kuhama hama bendi kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wengine jambo lililopeleka kudumu kwenye cheo chake cha ukiranja mkuu wa bendi hiyo kwa muda mrefu sasa.
Siku za hivi karibuni msanii kiwango cha juu kwa sasa Afrika Mashariki na kati Nasibu Abdul'Diamond Platnumz' alinaswa hotel usiku wa manane na mapaparazi wa kampuni wa Global Publishers akiwa na mwigizaji nyota wa filam za kibongo lrene Uwoya ambaye ni mke wa mtu wakila raha ndani ya hotel hiyo iliyopo kando kando ya ufukwe wa bahari ya hindi jijini Dar es salaam.