Na Bryceson Mathias, Morogoro.
WANDISHI waandamizi wa Vyombo vya Habari nchini,Wamemshutumu moja kwa moja Spika wa Bunge, Anne Makinda, wakimtuhumu kuwa kuwa anaongoza kudhalilisha Utu wa Wandishi na Vyombo wa Habari.
Wakizungumza katika mahojiano ya Jicho letu ndani ya habari Julai 13, 2013 kujadili Rasimu ya Katiba, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Deodatus Balile alisema,
“Mimi Simung'unyi Maneno, Spika Makinda anaongoza kwa kuvidhalilisha Vyombo vya habari na Utu wa Wandishi”.alisema Balile.
Upande wake, Allan Lawa, wa Baraza Habari Tanzania (MCT) alisema, Spika anafanya hivyo akijua fika kuwa aliwahi kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu akishugulikia Habari’
Walidai, wanamshangaa Makinda kudhalilisha Wandishi na Vyombo vya habari na kuwaita Wanahongwa na Wabunge ili wawaandike vizuri, lakini amesahau kuwa wakati wa Mchakato wa Ubunge wake na kinyang’anyiro cha U-Spika, vilimsaidia na hakusema vinahongwa!.
Mtangazaji Dotto Bulendu aliongoza majadiliano Startv-Mwanza na wageni Balile na Lawa, na Stumai Gerge alikuwa na Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Ayub Rioba na Pili Mtambalike wa MCT,
Rioba alisema, ziko Demokrasia za aina Mbili ya kuletwa ambayo katika utekelezaji wake huwa na maslahi kwa walioileta, na ile iliyoibuliwa na wananchi (created) utekelezaji wake una faida kwa wahusika, na kusema Rasimu haikuandika na Jaji Joseph Warioba pekee, ila wajumbe wote 30, akihofu vitu vilipitishwa Warioba akiwa hayupo .
Aidha, Pili Mtambalike (MCT), akihojiwa na Stumai alisema, kuna maeneo ya Rasimu katika Uhuru wa Habari lazima yapitiwa upya; ili tusirudi tena nyuma kwenye Sheria gandamizi kwa wandishi na ugumu wa kupata habari, “tunakwenda mbele haturudi nyuma”.alisema Mtambalike!
Mbali ya waandishi kusema ukikiandika Chama tawala mwandishi unaonekana Mchochezi na kupendelea Upinzani, na ukikiandika Chama pinzani unaonekana Mzalendo, Wachangiaji nchini pia walipigilia Msumari wakiwaunga Mkono wandishi wakidai, habari zao kamaa Waajiri zinapuuzwa, wanasia ambao ni waajiriwa ni kipaumbele kwa watawala.