Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » WAKATI NANDO AKIHANGAIKA NA GONJWA LA ZINAA ALOPEWA, FEZA NAYE AMETANGAZA NIA YAKE YA KUZALISHWA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER

WAKATI NANDO AKIHANGAIKA NA GONJWA LA ZINAA ALOPEWA, FEZA NAYE AMETANGAZA NIA YAKE YA KUZALISHWA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Huenda Jay (mtoto wa kiume wa Feza Kessy) anaweza kupata wadogo zake wa kucheza nao soon. Hiyo ni kutokana na mama yake anayeiwakilisha Tanzania mwaka huu kwenye shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ kumwambia mchumba wake raia wa Botswana, Oneal kuwa angependa azae naye watoto.


Wapenzi hao waliopo Ruby House walikuwa wakiongea mipango kuhusu uhusiano wao kwenye chumba cha Rendezvous mjengoni humo.
 
“Please put a little thought into your answers,” anasikika Oneal akimwambia Feza.
 
“Natamani tungekuwa na mazungumzo haya bila kamera zozote zinazotuzunguka,” Feza alimjibu Oneal.

Lakini baadaye alimjibu, “Nataka furaha na wewe, future, nataka mahaba, nataka watoto, nataka maisha na wewe.” 

Hata hivyo Feza amekisema kitu kinachomkwaza toka kwa Mbotswana huyo anayefanya kazi ya UDJ nchini mwao kuwa wanapokorofishana yeye huondoka bila kuyamaliza japo amesema atajaribu kumwelewa.
 
“I know I am a complex man, I don’t even understand myself at times,” alikiri Oneal.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa