Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » SHARABARO ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUINGIA KANISANI AKIVUTA 'FEGI'

SHARABARO ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUINGIA KANISANI AKIVUTA 'FEGI'


JAMAA ‘sharobaro’ ambaye jina halikupatikana amezua kizaazaa baada ya kula kichapo akidaiwa kuingia kanisani akivuta sigara.
Tukio hilo lilijiri katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mviringo lililopo Magomeni, Dar hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, kijana huyo aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30 na 35 aliingia ndani ya kanisa hilo akivuta ‘fegi’ na kutafuna big g ambapo watu waliokuwa kwenye ibada walipigwa butwaa na wengine kuliona tukio hilo kama kituko wakihoji ujasiri wa sharobaro huyo kuingia kwenye nyumba ya Mungu na sigara.

Baada ya kushtukiwa alibebwa msobemsobe na kutolewa nje kisha kupokea kichapo na alipobanwa alidai kuwa alikuwa ametumwa na kundi fulani la watu.
Hadi naondoka eneo la tukio, kijana huyo alikuwa chini ya ulinzi mkali.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa