Wema akiwa na Penny.
SIRI ya Mtangazaji wa Televisheni ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kumpindua Wema Isaac Sepetu kwa mwanamuziki Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ imevuja huku Wema mwenyewe akidaiwa kuchangia.
Alisema, Wema na Penny walikuwa marafiki (picha ukurasa wa nyuma zinathibitisha) na kwamba Wema alikuwa akimringishia mwenzake jinsi Diamond anavyojua kubembeleza na kumjali mwanamke na hapo ndipo mtangazaji huyo akafanya mapinduzi.
“Wema alikuwa akimsifia Diamond kuwa anajua mapenzi na wanawake wengine wakishaambiwa hivyo huwa wanafanya wawezavyo kumnasa mwanaume huyo.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Wema kuzungumzia madai hayo lakini hakupatikana huku simu ya Penny ikiwa haipatikani.
Wema na Diamond wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu lakini katika siku za hivi karibuni Diamond amehamia kwa Penny.
