Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MAKUNDI YA WANAWAKE NA MITAZAMO YAO KWA WANAUME KATIKA MAPENZI

MAKUNDI YA WANAWAKE NA MITAZAMO YAO KWA WANAUME KATIKA MAPENZI

Ninachozingatia hapa ni fikra katika makundi ambayo nayachambua hapa, vigezo vyao kwa wanaume vipo kimtazamo zaidi.
Fikra zao ndizo zimetengeneza mtazamo kwa namna ambayo wao wamepima maslahi yao kwa wanaume. Maisha yanavyosogea mbele ndivyo binadamu wanavyojihisi wana akili na maarifa zaidi. Sasa wanajiona wana uwanja mpana zaidi wa kuchanganua, kuchambua na kuchagua.
Wakati miaka ya nyuma kila mwanamke ndoto yake kuu ilikuwa kuolewa ili apate mume wa kutulia naye, hivi sasa mambo yamebadilika. Makundi ni mengi, hata hilo ambalo linaundwa na wale wanaoteswa na kupata waume lipo lakini halitambi, linabezwa.
Sababu ya kundi hilo kubezwa ni mtazamo uliopo kwenye makundi mengine mawili kuwa watu wanaoota kupata wanaume wa kuwaoa, mawazo yao ni ya kale. Kwamba hayajitoshelezi kwa kizazi cha sasa ambacho kimeegemea teknolojia na utandawazi.
Tamaa ya fedha na kupanuka kwa sanaa, video zinazowaonesha mastaa wa Marekani na Ulaya pamoja na mitindo yao ya maisha, kumechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya baadhi ya wanawake kutengeneza mitazamo yao ya kupenda.
 KUNDI LA KWANZA
Mara nyingi linaundwa na wasichana wadogo na hata wanawake wakubwa wenye fikra ambazo ni rahisi kuziita changa. Hawa hupenda wanaume kutokana na muonekano wao. Inawezekana ikawa ni mtindo wa mavazi au umbile lake.
Katika kundi hili, ni rahisi kukuta mwanamke ameangukia kwa mwanaume asiye na malengo yoyote ya maisha. Matokeo yake, mwanamke huyo ndiye anageuka mlezi wa mwanaume husika, akimhudumia kila kitu.
Mathalan, anavutiwa na urefu, atafanya juu chini mpaka ahakikishe amemtia kwenye himaya yake. Hata kama hana ujasiri wa kusimama mbele ya mwanaume na kuwasilisha hisia za moyo wake lakini namna atakavyokuwa anaonesha kupagawa, itatosha kufikisha ujumbe.
Inawezekana pia ikawa kwa umbo lake lililojengeka kimazoezi. Ipo mifano ya mabaunsa wengi tu mjini ambao kimuonekano tu, ipo wazi kuwa wana nguvu za kutosha ambazo wangezitumia katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Ajabu ni kuwa misuli na nguvu zao havina faida, kwani wanalelewa tu na wanawake.
Hata mavazi, jinsi mwanaume anavyobadili mavazi, inaweza kumsababishia mwanamke kuingia kichwakichwa. Sura nayo ni kielelezo pamoja na sifa nyingine ambazo huonekana wazi katika mwili wa binadamu. Ongezea rangi, mpangilio wa meno, anaweza kupenda mwanya tu!
Yupo mwanamke ambaye anaweza kudondoka kwenye penzi kwa sababu mwanaume mwenyewe huwa anavaa miwani.
Hata utembeaji na mikogo yake, sauti na jinsi mtu anavyoongea, vinaweza kushawishi wanawake ndani ya kundi hili. Kimsingi, wanawake ndani ya kundi hili, huvutiwa kimapenzi kwa wanaume kutokana na muonekano wao au msemo wa kisasa ni kuwa swaga za mtu ndizo ambazo zinaweza kumpa alama ya kupendwa au kupotezewa.
TATHMINI KIMAPENZI
Wanawake wa kundi hili huwa na rangi mbili. Ya kwanza ni kwamba wanazo alama nyingi za kupenda. Anapompata yule anayemmulika, humpa mapenzi yote na kila kitu ambacho mwanaume atakuwa anakihitaji. Rangi ya pili ni kuwa kama mwanamke mwenyewe ni mapepe, basi anaweza kuhamisha upendo kutokana kwa mwanaume mmoja hadi mwingine.
Kama alimpendea urefu, warefu wapo wengi, ikiwa ni mavazi, wavaaji wamejaa kila kona, vivyo hivyo kwa sifa nyinginezo. Mwanaume anapaswa kutathmini mwanamke wake yupo vipi.
Utulivu wake unaweza kuwa kichocheo cha penzi la kudumu, umapepe ni kielelezo hatarishi katika uaminifu. Ukweli ni kwamba wale watulivu huwa na mapenzi ya kweli lakini kasoro yake ni kuwa dunia inageuka, kama alikupendea gari, kuna siku unaweza usiwe nalo, hapo atakuacha. Kama ni sura, basi unaweza kupata ajali, ile ‘baby face’ iliyomvuta haitakuwepo tena.
BAHATI MBAYA
Wanawake wa kundi hili huwa na bahati mbaya moja kubwa ambayo ni  usalitiwa na wanaume. Sababu ni kuwa wanaum hao mara nyingi hutawaliwa na kiburi kwamba wao ni wazuri na wanapendwa, kwa hiyo hukosa msimamo na utulivu wa kweli. Kwa vile hupenda kulelewa, hutoka na wanawake wengine ambao wataonekana wana fedha zaidi. Kadhalika, hujiona wao ni tabaka maalum sana, kwa hiyo huwa wanataka wanyenyekewe hata kama ni kwa jambo ambalo linawahitaji kunyenyekea.
Wenye tabia ya kupenda wanaume kutokana na muonekano wapo wengi, kwa hiyo unaweza kupenda kesho yake asubuhi mwingine naye akamtaka mwanaume huyohuyo wa kwako, hivyo kuleta ushindani wa kimaslahi kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
Kwa kumalizia uchambuzi wa kundi la kwanza ambalo nilieleza kuwa linaundwa na wanawake wenye umri mdogo ambao hupenda wanaume kutokana na muonekano, vema nitaje bahati mbaya ambazo wanaweza kukutana nazo.Wanawake wa kundi hili huwa na bahati mbaya moja kubwa ambayo ni kusalitiwa na wanaume.
Sababu ni kuwa wanaume hao mara nyingi hutawaliwa na kiburi kwamba wao ni wazuri na wanapendwa, kwa hiyo hukosa msimamo na utulivu wa kweli.
Kwa vile hupenda kulelewa, hutoka na wanawake wengine ambao wataonekana wana fedha zaidi. Kadhalika, hujiona wao ni tabaka maalum sana, kwa hiyo huwa wanataka wanyenyekewe hata kama ni kwa jambo ambalo linawahitaji kunyenyekea.
Wenye tabia ya kupenda wanaume kutokana na muonekano wapo wengi, kwa hiyo unaweza kupenda kesho yake asubuhi mwingine naye akamtaka mwanaume huyohuyo wa kwako, hivyo kuleta ushindani wa kimaslahi kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
Tafsiri ya jumla ni kwamba wanaume ambao humulikwa na wanawake wa kundi hili, aghalabu huwa siyo waaminifu. Kutokana na hali hiyo, wanawake hao mara nyingi husumbuliwa na mateso ya mapenzi, wakilalamikia jinsi wanavyotendwa au wasivyo na bahati ya kupendwa.

KUNDI LA PILI
Kwa kawaida, kundi hili halina tabaka la umri. Wanaounda kundi hili wanaweza kuwa wasichana wadogo au hata wanawake watu wazima. Kipaumbele chao siku zote huwa ni kupata wanaume ambao watawalea, yaani watakaokidhi haja zao.
Wanaweza kuangukia hata kwa wanaume wasiowapenda ilimradi wapate unafuu wa kuishi vizuri. Wao huwa hawana kile kitu kinachoitwa ‘mapenzi ya dhati kutoka moyoni’, isipokuwa hujenga mazoea mpaka huhisi wanapenda au wanapendwa.
Kutokana na ukweli huo kwamba huwa hawazingatii mapenzi ya dhati kutoka moyoni, wanawake wanaounda kundi hili huwa hawachagui umri wa wanaume. Iwe ni kwa vijana wadogo mpaka wazee wenye umri sawa na vikongwe.
Mrembo mwenye umri wa miaka 24, anapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mzee mwenye umri wa miaka 70 ambaye kiuhalisia ni babu yake, hilo haliwezi kuwa jambo geni, isipokuwa kilichozingatiwa na mwanamke husika ni unafuu wa kuishi.
Wanawake wa kundi hili, hushawishika kutokana na jinsi wanavyopokelewa na wanaume. Namna ambavyo mwanaume anavyowajibika katika utoaji wa huduma za kimsingi na hata za ziada kwa mwanamke wa kundi hili, humfanya apate alama nyingi za ushindi.
Kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa na mwanamke ni lazima kusoma tabia. Makala haya kusudio lake ni kuyabainisha makundi ya wanawake na tabia zao, lengo likiwa moja tu, kukuwezesha wewe kutambua mahali pa kushika, vilevile wao wenyewe kujitambua ili kama wapo kwenye mstari mbaya, basi wajikosoe.
Wiki iliyopita, nilikomea kundi la pili. Na nikaanza kubainisha bahati mbaya zinazojiri nyuma ya wanawake wanaounda kundi hilo. Kwa kifupi ni kuwa wanawake wa kundi hili hupoteza mvuto wao mapema, kwani hawataonekana wana jipya.
Kwa vile ujanja wao upo kitandani, taratibu mapenzi ya wanaume hupungua kadiri wanavyozoeana.
Mwisho humuona wa kawaida kwani hisia ni zilezile, mguso ni uleule na mapenzi ni yaleyale.
Huonekana mzigo hasa pale wanaume wao wanapokuwa wanakabiliana na matatizo ya kiuchumi.
Kwa kawaida, mume anapoona mambo magumu, huhitaji mwanamke ambaye anaweza kuisoma hali na kudhibiti matumizi.
Kadhalika, mwanaume hutaka kuwa na mwanamke ambaye anaweza kumpa kazi ya kugharamia chakula na matumizi madogomadogo ya nyumbani. Inapotokea mwanamke anakuwa hawezi kuingiza chochote, humtia kasoro katika harakati za maendeleo ya kimaisha.
Tatizo lingine ni kwamba inawezekana mwanamke akawa anajishughulisha lakini kwa sababu yeye anapenda kuhudumiwa, atahakikisha kipato chake anakibania ili aweze kutumia rasilimali za mwanaume peke yake. Baadaye mwanaume anaposhtuka humuona mwanamke ni mnyonyaji.
Jambo lingine baya ni kuwa wanawake wa kundi hili ni wanyonge sana mbele ya wanaume.
Hufanya hivyo ili wasipeperushe ndege. Imani yao ni kwamba wanapokuwa wapole ndivyo huongeza mvuto kwa wanaume wao.
Kwa mantiki hiyo ni ngumu hata kutambua hisia zao, huogopa kuzionesha kwa kuhofia kuachwa.
Hali hiyo hutoa mwanya kwa wanaume wa kundi hili (hasa wale wasio waaminifu), kuanzisha uhusiano na wanawake wa pembeni. Mke akisikia taarifa za usaliti wa mumewe, huogopa hata kuuliza.
KUNDI LA TATU
Aghalabu, kundi hili huundwa zaidi na wanawake wenye umri uliopevuka. Kwao pesa ni kila kitu.
Mwanaume ajitokeze mbele yake lakini kama hana fedha, asitegemee kupata penzi lenye angalau chembechembe ya mahaba. Uzuri ni kwamba ni rahisi kuwatambua kwa maana huwa hawafichi kipaumbele chao.
Ukianza naye uhusiano wa kimapenzi leo, hazitapita wiki mbili kabla hajakuonesha kile anachokitaka.
Atakuomba fedha tu na ukimpa kwa haraka, hapo unakuwa umefungulia njia.
Iwe kwa shida ndogo au kubwa, kimbilio lake ni wewe. Atakugeuza Automated Teller Machine (ATM) mpaka utajiuliza: “Hivi kabla ya kuwa na mimi alikuwa anaishije?”
Endapo siku ya kwanza akikuomba fedha utamjibu huna, unakuwa umejiwekea doa ndani ya moyo wake.
Ataendelea kubuni vitu vya hapa na pale kusudi avune pesa kutoka kwenye mfuko wako. Hata kama hana shida hasa, husisitiza mahitaji yake mpaka umpe, vinginevyo atanuna, atasusa na kukusema vibaya.


Wale wenye vipato vidogo au wanaume wachumi, hawakubaliki kwa wanawake wanaounda kundi hili. Mara nyingi wanawake wa kundi hili huwa hawaivi na wanaume werevu, wenye kupenda kujiuliza mara mbilimbili kwa kila jambo.
Kwa kawaida, wanaume werevu hutaka zaidi kuwekeza mapenzi yao kwa wanawake wasiosukumwa na kitu ndiyo wapende. Kwa maana hiyo, mabadiliko ya mwanamke kipindi cha fedha na pale zinapokata, huwashtua, hivyo kuwatia kasoro.
Mara nyingi huachana, zaidi wanaume ndiyo huacha, mara chache wanawake hukimbia. Kama wewe unadhani chako ni chenu na chake ni chenu, utakuwa umeambulia sifuri.
Tambua kuwa chako ni chenu na chake ni chake, kama unabisha hebu mjaribu kumuomba fedha uone kama atakupa. Akikupa lazima ataandika deni.
Na atakuwa anakudai mpaka umlipe hata kama fedha zenyewe alizitoa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Hata kama yeye ndiye atakuwa na
kipato kikubwa zaidi, bado hawezi kukubali kuhudumia familia wakati wewe upo.
Bora fedha zake ziende kununua nguo na kufanya mambo
mengine binafsi lakini familia lazima ihudumiwe na wewe.

TATHMINI YAO KIMAPENZI
Kuwa na mwanamke wa kundi hili ni kujitafutia maradhi ya moyo. Kwa maana tafsiri ya mapenzi ya dhati wao huichakachua kutoka kwenye uhalisia mpaka kusomeka “fedha ndiyo mapenzi.” Hata ukiwa nazo na ukajitwisha mzigo kumuoa na kumweka ndani, kuna siku utajuta, utalia machozi. Vilevile yanaweza yasikutokee lakini moyoni ikawa mateso.
Umeshawahi kuona mateso ya mtu anayeumia kwa ajili ya mapenzi? Hebu omba uendelee kusimuliwa yasikukute.
Ila ukitaka nawe uwe mfano wa wanaume wanaolia mchana kweupe, jiweke kwa mwanamke
wa kundi hili halafu thubutu kuwekeza moyo wako wote. Utakonda bila kuumwa, utapoteza hamu ya kula ilhali tumboni hakuna kitu.
Leo utakuwa na fedha na unampa, atakupenda sana.
Kesho ukiishiwa utapata matokeo matatu ambayo yote ni mabaya mno kufanyiwa na umpendaye.
Mosi; anaweza kukukimbia na kutua kwa mwanaume mwingine anayeonekana ana fedha zaidi.
Hawezi kuendelea na wewe, atakwenda kuchuma kule zinapopatikana kwa urahisi. Pili; kama mmeshaoana, atakunyanyasa ndani ya nyumba.
Anaweza kutoka nyumbani bila kukutaarifu ratiba zake, vilevile atarudi muda autakao.
Akifanya hivyo ni bora ukae kimya, kwa maana ukimuuliza au kumkosoa unaweza kukumbana na majibu ya kuumiza sana. Usishangae akakuuliza: “Katika wanaume na wewe umo?” Kabisa, tena atakapokuuliza hivyo atakuwa anajiona yupo sahihi kwa asilimia 100.
Hawezi kujiona anakosea kwa sababu tafsiri yake ndiyo inamuongoza hivyo. Anaamini ili uwe mwanaume timilifu, sharti uwe na fedha, tena zisiishie mfukoni kwako, badala yake muwe ‘mnashea’. Zako ni zenu, zake ni zake, tena usithubutu kufikiri zake ni zenu.
Tatu; atakuingiza kwenye madeni. Atakufanya ukope ili kumtimizia mahitaji yake. Naye atakopa halafu atakuhimiza ulipe. Maisha yako hayatakuwa na amani. Kwa vile muda wote anawaza fedha, atatoka nje ya ndoa wakati wowote.
 Yeyote atakayejitokeza mbele yake ambaye atamfanya awe na fedha, hatasita kumpa kilichopo ndani ya mwili wake.
Anaweza kuutoa mwili wake kwa muuza duka au genge kwa sababu hupata mahitaji bure, hivyo kuweka kibindoni fedha ambazo humwachia za matumizi nyumbani.
Wanawake wa kundi hili ni hatari mno, kwani unawezakupona maradhi ya moyo kutokana na usugu wako kihisia lakini ukapata maambukizi ya magonjwa zinaa, kwa maana hawachagui pa kujiweka.





 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa