Tumemsikia  Mwazani Said leo katika leo tena akituelezea namna alivyonusurika  katika ajali ya gari iliyopelekea wasanii 13 ya band ya taarab ya 5stars  kupoteza maisha.Ajali hiyo ilitokea tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka  2011.Mwazani alisafiri na band kama mcheza show lakini yeye ilikuwa ni  mara ya kwanza.Rafiki yake ambae alikufa kwenye band ndio alimwambia  kuna kazi ya kucheza mikoani ambayo atatoka na pesa kidogo kuliko kukaa  bure.

Wakasafiri  na kuzuru mikoa mitano na yeye akafanya kazi yake ambayo alilipwa Tsh  100,000.Siku mbili kabla ya kurejea Dar wasanii waliopoteza maisha  walikuwa wakiona vitu vya mauza uza.Msanii Issa Kijoti na mwimbaji  mwingine wa kike walitokewa na mtu aliyevaa nguo nyeupe.Wakawaambia  wenzao juu ya hilo wakawafanyia kisomo na dua ili waweze kukaa sawa.
Pia  kulizuka ugomvi mkubwa ambao wasanii walikuwa wakigombana wao kwa wao  mpaka Sheba Juma ambae ni marehemu alitaka kuondoka mwenyewe kurudi  Dar.Lakini Ali J ambae yu hai alinusurika alisuluhisha ugomvi huo wakawa  sawa.

Katika  ajali hiyo wakiwa kwenye basi mwazani alikuwa amelala.Alikaa siti moja  na marehemu Sheba Juma akamuomba wabadilishane siti ili yeye Mwazani  alale maana alikuwa na usingizi.Alipolala alikuja kuzinduka baada ya  siku 5 na kujikuta yupo hospital mkono umepooza na mguu umefanyiwa  upasuaji na kuwekewa vyuma.Akamuuliza mama yake kumetokea nini mbona  yupo hospital mama hakumjibu.Baba ndio akamletea gazeti akasoma na kuona  kilichotokea na yule shosti wake aliyemuita wakacheze alipoteza maisha.

Baada  ya ajali ile mpaka sasa mkono wake wa kushoto umepooza na mguu wa  kushoto pia unavyuma bado.Walilipwa pesa ambazo yeye alizinunulia eneokanyumba kadogo kakuishi.

 Wakati  ananunua hapa sio yeye alikuja kununua.Kuna ndugu yake alikuja  kupanunua lakini hakukuwa na choo.Ni mwaka sasa amekuwa akitumia choo  cha jirani na kwa sasa amepigwa marufuku kutumia choo cha wenyewe.Baada  ya kupigwa marufuku akarudi kwa baba yake ambae amepanga chumba na  sebule.Baba na mama wanalala chumbani yeye analala sebuleni.

Sebule katika nyumba yake hiyo ambayo ipo Yombo dovya.


Huyu ndio jirani mwenye choo chake lakini amepigwa marufuku

Hapa ni chumbani kwake.
Kama  ambavyo amesikika kwenye leo tena Mwazani anaomba kusaidiwa pesa ili  aweze kujenga choo.Iwapo uliguswa na matatizo yake mchangie kwa namba  0759 789863 na 0657 795654.

