Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » WANAWAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KULEWA MUDA KA KAZI

WANAWAKE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KULEWA MUDA KA KAZI


Washitakiwa wakipelekwa kizimbani.

Wakisubiri kusomewa mashitaka.
WAREMBO wanne jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar es Salaam kwa kosa la kunywa pombe za kienyeji muda wa kazi.
Warembo hao walinaswa maeneo ya Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Baada ya kufikishwa mahakamani hapo na kukana mashitaka hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Timothy Lyon, aliwawekea wazi dhamana kwa kumtaka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja. Sharti hilo la dhamana lilikuwa gumu kwa warembo hao ambao walipandishwa karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka tarehe 15 mwezi ujao.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa