Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.
Zoezi litaanza kwa kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya zoezi la kuzima simu kuanza ili kuhakikisha kuwa wananchi hawaathiriwi na zoezi hilo.
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
CREDIT:Bongo5