Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » SNURA AKANA KUHUSIKA NA BIASHARA YA KUUZA MADADA POA KWA MAPEDESHEE

SNURA AKANA KUHUSIKA NA BIASHARA YA KUUZA MADADA POA KWA MAPEDESHEE

Snura 'Majanga', Baada ya kukaa na maumivu moyoni kwa muda mrefu hatimaye leo hii ameamua kufunguka na kusema kuwa anaumizwa sana moyo na wale wote wanaomhusisha ama kumtuhumu kuwa njia yake kubwa ya kujipatia pesa ni kujiuza kwa watu wenye pesa mjini na pia kuuza wasichana wengine.

Snura amesema kuwa kutokana na watu kumhusisha na mambo haya, kwa upande wake yeye binafsi kuna mtu ambaye aliwahi kutumia picha yake kwenda kumnadi kwa wenye pesa zao, lakini mwisho wa siku alishindwa kukamilisha mpango wa kumuuza kwasababu hakuweza kumfuata na kumueleza kuwa anahitajika kwaajili ya mpango huo.

Snura ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja, amesema kuwa, Pesa alizonazo sasa zinatokana na yeye kuhangaika kwa njia ambazo ni halali na zinafahamika na watu na anakasirishwa sana na wale woote ambao wanamhusisha na mambo ya kujiuza.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa