Ongezeko la makahaba mjini Dodoma limeendelea kuwa kero kwa chuo kikuu cha Dodoma na wanafunzi wake kwa ujumla....
Kero hiyo imekuwa ikisababishwa na baadhi ya makahaba hao kujifanya wanafunzi wa chuo hicho kwa lengo la kujiimarisha kibiashara...
Takribani miezi mitatu iliyopita, kahaba mmoja alinasawa na polisi mjini Dodoma akijiuza kwa kujinadi kuwa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili chuo kikuu cha Dodoma ..
Baada ya mahojiano ya kina na Polisi Central, ilibainika kuwa kahaba huyo hakuwa Mtanzania na hakuwa mwanafunzi wa chuo chochote hapa nchini na badala yake alikuwa ni raia wa Malawi.
Upekuzi wa polisi ulifanikiwa kunasa ARVs za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI toka kwa mwanamke huyo aliyekuwa akiendesha maisha yake kwa kuuza mwili wake maeneo ya Uhindini mkoani humo.
Mbali na ushahidi huo, mtandao huu umefanikiwa kumnasa binti mwingine anayejiita SECHE MAUTAMU...
Seche ni binti aliyeamua kujiuza kupitia mtandao wa facebook kwa kuwalaghai wanaume kwamba yeye ni mwanafunzi wa UDOM....
Hata katika profile yake, binti huyo ameweka wazi kuwa yeye ni mwanafunzi wa UDOM huku ukurasa wake ukipambwa na picha kadhaa za uchi.....
Kinachotia shaka ni kwamba, picha zote 25 zilizowekwa hazithibitishi moja kwa moja kwamba Seche ni mwanafunzi ama wa UDOM au chuo chochote cha Tanzania...
Picha zilizowekwa ni za gheto lake akiwa UCHI, hali inayotia shaka kubwa ya kukubaliana na uanafunzi wake wa UDOM....
Ili kuupata ukweli wa mambo, mtandao huu ulizungumza na wanafunzi 10 toka chuoni hapo kwa nyakati tofauti..
Miongoni mwa wanafunzi tulioongea nao ni wale waliomaliza mwaka 2013, 2012 na 2011. Wanafunzi wote 10 wameshindwa kumtambua Seche na kudai kuwa huyo ni kahaba aliyeamua kuwachafua....
"Huyo siyo mwanafunzi, ni kahaba ambaye ameamua kutuchafua. Kama kweli ni mwanafunzi, mwambieni aweke japo picha moja tu akiwa katika mazingira ya chuo cha UDOM"...Alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkoa wa Dodoma umekubwa na ongezeko kubwa la MALAYA wanaoishi kwa kuuza miili yao..
Maeneo makubwa yaliyoathiriwa na makahaba hao ni Chako ni chako, Uhindini,eneo la ofisi za hood karibu na club moja ya usiku na maeneo ya ukumbi wa 84.
Cha kushangaza ni kwamba malaya wote hujiita wanafunzi wa UDOM.Wakiulizwa kozi wanazosoma huishia kujiuma na kuwa wakali .
KWA PICHA ZAIDI, TEMBELEA UKURASA WAKE WA FACEBOOK