KAMPUNI ya Proin Promotions imewasilisha filamu yake iliyopewa jina la “Foolish Age” kwa Bodi ya Filamu Tanzania kwa ajili ya ukaguzi ambapo baada ya kufanyiwa marekebisho filamu hiyo inaweza kuruhusiwa katika uzinduzi wa Kampuni hiyo hivi karibuni.
.
.
Lulu akiwa na Katibu wa Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Bi. Joyce Fisso na mwanasheria wa Proin Promotion Bi. Gift Msuya wakiwa katika majadiliano ya filamu ya Foolish Age.
Lulu akisaini makubaliano na bodi.
Katika majadiliano hayo Bodi ya Filamu iliwakumbusha wahusika hao kufanya baadhi ya marekebisho katika filamu hiyo ili iweze kuwa kivutio kwa umma, pia Bodi ya Filamu iliwakumbusha juu ya umuhimu wa kuzingatia kifungu cha 14 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ambacho kinaipa Bodi mamlaka ya kukagua filamu, matangazo na maelezo yote na kile cha 24 (1) (d, n na t) cha Kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kinachofafanua mambo yanayotakiwa na yale yasiyotakiwa katika filamu ambayo filamu hiyo imekwenda kinyume.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Bi. Gift Msuya alikubaliana na ushauri uliotolewa na Bodi ya Filamu na aliiomba Bodi itoe muda kwao kwa ajili ya kufanyia marekebisho katika filamu hiyo.
.
Lulu akibadilishana mawazo na katibu wa Bodi Bi. Fissoo.
Moja ya picha ya siku nyingi ya Lulu akiwa katika pozi .
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Fissoo alimalizia kwa kuishauri Kampuni hiyo kutotumia filamu hiyo katika uzinduzi wa kampuni yao hadi hapo watakapofanyia marekebisho katika baadhi ya maeneo muhimu ndani ya filamu hiyo.
Proin Promotions ni Kampuni inayojikita katika kuandaa na kutengeneza filamu za kitanzania na kuzisambaza nchini, pia ni kampuni inayotarajiwa kutoa ushindani mkubwa katika tasnia ya filamu. Kampuni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya maandalizi rasmi kukamilika.

