Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » DIDA APATA GONJWA LA MARALIA 250 LATAKA KUMPELEKA KABURINI.....

DIDA APATA GONJWA LA MARALIA 250 LATAKA KUMPELEKA KABURINI.....

Khadija Shaibu ‘Dida’.
MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefungua kinywa chake na kusema ugonjwa wa malaria uliompata hivi karibuni ulimfanya alichungulie kaburi kwani alihisi mauti yanamkuta. 
Akizungumza na paparazi wetu mapema wiki hii katika Hospitali ya Muhimbili, jijini Dar, Dida alisema kitendo cha kukutwa na malaria 250 katika mwili wake kilikuwa hatari sana kwani ingeweza kumuondoa uhai kabisa.
“Nilichungulia kaburi mwenzenu maana hali niliyokuwa naisikia siku ile ya kwanza ilikuwa ni nusu duniani, nusu akhera. Nilikuwa wa leo au wa kesho ila namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri,”
alisema Dida.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Dida alipandwa na malaria kali, akakimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa