Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » KILICHOJIRI MAHAKAMANI JANA KUHUSU LADY JAY DEE

KILICHOJIRI MAHAKAMANI JANA KUHUSU LADY JAY DEE

              Jide na Mumewe wakiwasili mahakamani jana.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee(Pichani)  muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa
  akiongea katika jukwaa la wasanii, 
alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika 
alikabidhiwa hati  hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa