Katika kile kinachoonekana kukerwa na vitendo vya vyombo vingi vya habari hususani magazeti ya kadhaa ya udaku yanoyochapisha habari za uongo kuhusu wasanii wa bongo movies kwa ajili ya kuuza magazeti yao, hatimaye msanii Elizabeth Michael “lulu”naye ameamua kuyaweka wazi ya moyoni mwake bila kuficha baada ya gazeti moja pendwa (Jina tunalihifadhi) kuchapisha habari iliyopew kichwa kisemacho “Lulu, wema, Diamond afya mgogoro”ambayo imeonekana dhahiri kumkera mrembo huyu na kuamua kaundika haya yafuatayo kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii.
“..Imekuwa ni kawaida ya mtu kujisikia kusema chochote...muda mwingine mnaweza mkahisi hatuoni au mkahisi kukaa kwetu kimya ni wajinga!!mm kama mm napenda kuwajulisha kuwa LULU mliyekuwa mnamjua sio LULU wa ss...msitegemee kusikia nabisha au kupigizana kelele...fanyeni kazi yenu lakini sio kuchafuana na kuipotosha jamii....!!!nadhani kimya changu kina majibu mengi...''
Lulu anakuwa msanii wa pili kwa kipindi cha wiki mbili kukasirika hadharani baada ya mwanadada Batuli kulaani kitendo cha gazeti moja la udaku kuandika habari za uongo kuhusu yeye....
Home
»
skendo mastaa
»
KAULI YA LULU BAADA YA KUSAMBAA MAGAZETINI 'LULU,DIAMOND NA WEMA AFYA MGOGORO'