Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » SPIKA WA BUNGE ATOA AGIZO KUKAMATWA NA POLISI KWA MBUNGE YOYOTE ATAKAYE TUKANA BUNGENI

SPIKA WA BUNGE ATOA AGIZO KUKAMATWA NA POLISI KWA MBUNGE YOYOTE ATAKAYE TUKANA BUNGENI


Akiongea kwa uchungu , Spika wa Bunge bi Anne Makinda amewashambulia wabunge  leo asubuhi na kuwaambia suti zao walizovaa haziendani na matusi  yanatoka  katika vinywa vyao  ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana kwa  madai  kuwa mdomo  wake hauwezi kutamka matusi hayo.....
Makinda amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala katika midomo ya wawakilishi hao na kuacha hoja inayojadiliwa hewani....
 
Spika wa bunge amekwenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge hao kwamba hataangalia chama endapo mbunge atavunja kanuni za bunge kwa kuwa kanuni za bunge zinampa nafasi ya kuita polisi na kuja kumchukua mbunge huyo kwa hatua za kisheria.

Makinda  amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.
 
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa