Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito kuhusiana na mirathi ya marehemu Steven Kanumba kwani taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa, hakuna kitu kilichofanyika mpaka sasa kutokana na mvutano uliokuwepo ndani ya familia.
Akizungumza hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
