Sospeter alifikia uamuzi huo juzikati baada ya mkewe kumchoma kisu kutokana na wivu wa kimapenzi kisha kutimkia kusikojulikana hivyo kumtumia talaka hukohuko aliko baada ya kuona siyo mwanamke sahihi kwake.“Tumeishi kwa miaka takribani mitano yaani ugomvi kila siku hauishi, sitaki kwenda mahakamani wala kumshtaki kwani mtoto wangu Rick atapata shida ila namtumia talaka hukohuko aliko, simtaki tena asije akaniua bure siku nyingine,’’ alisema Martin.

