.
Skendo zinazidi kuiandama hospital hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa hospital ya rufaa hivi karibuni ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top redio ya mkoani hapa Edward Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimwizwa kwenye hospital hiyo imeilalamikia hospital hiyo kwakumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi ya masaa matano na kuradhimika kuondoka kwenye hospital hiyo ya serikali na kwenda kutibiwa hospital za watu binafsi.
Mtandao huu umeibuka Skendo nyingine ndani ya hospital hiyo baada ya kushuhudia waunguzi wa hospital hiyo wakipokeza kuwashikia madripu ya dawa wagonjwa waliolazwa chini ya sakafu baada ya hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
Juzikati hospital hiyo ilivamiwa na majeruhi zaidi ya 60 waliopoteza fahamu baada ya kiwanda cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na shoti ya umeme na kukimbizwa kwenye hospital hiyo,hivyo uongozi wa hospital hiyo baada ya kuelemewa na wingi wa majeruhi hao uliradhimia kutoa magodolo stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kufuatia hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
" Hii ni aibu kubwa kwa hospital ya rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba wagonjwa wamekuja kwa mkupua hospital inapopewa hadhi ya rufaa inamaana inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi zaidi ya mia watakaofikisha kwa mkupua kwenye hospital hiyo"alisema Bi Asha Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao.
Vile vile mwandishi wa matandao huu mbali ya kushudia wauguzi hao wakipokeza kuwashikia madripu wagonjwa hao pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kupita juu ya wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo
Ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo Mtandao huu ulimsaka Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo kwa zaidi ya siku tano na kufanikiwa kumpata leo asubuhi ambapo alipotakiwa kueleza hali hiyo Mganga huyo mfawidhi Bi Rita Lyamuya alikuwa na haya ya kusema
" Nikweli siku ile ya tukio la kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya majeruhi kiukweli kwa ishu kama ile tulikosa namna ya kukabiliana nayo kwani walikuja kwa mkupua zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya tuliwapokea na baadhi kuwaradha chini na kuwapatia hudumu ya kwanza huku kukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza"alisema Dr Rita

