Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » IMEBUMA!

IMEBUMA!




KUTOKANA na kudaiwa kwamba baadhi ya watu hupeleka maiti na kuzihifadhi katika hospitali za serikali bila kufuata taratibu zilizowekwa, hivi karibuni mapaparazi wetu waliamua kutengeneza mtego ili kuthibitisha hilo.
 
Paparazi akijiaandaa kushusha 'maiti' kutoka kwenye gari.
Timu ya waandishi  iliweka mtego wake wa kujaribu kuingiza maiti mochwari kinyemela ili kuwanasa kwa rushwa wafanyakazi wa Hospitali ya Mwanyamala, jijini Dar.
Lengo lilikuwa ni kuwanasa wafanyakazi wa hospitali hiyo wakipokea rushwa wakati wakijiandaa kupokea maiti feki iliyoandaliwa na kisha kuwafotoa kwa kamera maalum walizokuwa wameziandaa.
HATUA YA KWANZA
Sanda ilinunuliwa na kumfunika mmoja wao na kumpakiza kwenye gari maalum kisha kumpeleka katika hospitali hiyo wakidai kuwa amefariki dunia ghafla hivyo wanaomba kuhifadhi mwili.
HATUA YA PILI
Mapaparazi walitinga katika hospitali hiyo na kushuhudia geti la mochwari likiwa limepigwa kufuli, ikawabidi kupanga mkakati mpya wakiwa na maiti yao feki ndani ya gari.
 
Geti la mochwari likiwa limepigwa kufuli.
HATUA YA TATU
Mapaparazi wawili walikwenda getini kwa lengo la kutaka kuzungumza na walinzi pamoja na manesi wa hospitali hiyo ili waweze kukubali kuihifadhi maiti mochwari hapo hadi kesho yake asubuhi bila ya kujiandikisha.
MPANGO WABUMA
Dalili za kugonga mwamba kwa zoezi hilo zilionekana pale mapaparzi hao walipowaona askari getini, hata hivyo, wakaamua kuongea nao dili kwa kuamini kuwa nao watashawishika.
“Kaka zangu kama mna maiti ileteni hapa, iwekeni pale, (akionesha machela) kisha daktari atakuja kuichoma sindano na kuipima, wala hakuna maongezi mengi,” alisema mlinzi mmoja wa kike.
Pamoja na mapaparazi hao kubembeleza kama kuna uwezekano wa kufunguliwa geti la mochwari ili waingize maiti kisha wazungumze kwa herufi kubwa, askari na wahudumu hao walikataa katakata.
 
'Maiti' ikiwa kwenye gari.
“Kwanza ufunguo wa mochwari huwa unakabidhiwa utawala saa 12:00 jioni na kuchukuliwa saa 12:00 asubuhi ‘so’ si rahisi kufanya hivyo mnavyotaka. Fuateni tu utaratibu maana tunaogopa kupata kashfa,” alisisitiza huku akiwaonesha waandishi manesi watakaokagua maiti kisha wamuite daktari wa kuichoma sindano.
  Tunawapa pongezi wafanyakazi hao wa Hospitali ya Mwananyamala pamoja na viongozi wao kwa jumla kwa kutegua mtego ambao ungewachafua kwa kashfa nzito.


 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa