Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » JOKETI ANENA YA MOYONI JUU YA PENZI JIPYA LA DIAMOND NA PENNY

JOKETI ANENA YA MOYONI JUU YA PENZI JIPYA LA DIAMOND NA PENNY



BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.

 
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake, Jokate Mwegelo.
Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
 
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na demu wake mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa