Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MAINDA AFANYIZIWA

MAINDA AFANYIZIWA

Ruth Suka ‘Mainda’.
Kwa mujibu wa sosi wetu, tukio hilo lilimtokea Mainda juzikati akiwa nyumbani kwa msanii mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ huko Mbezi-Beach jijini Dar.
Habari zilinyetisha kuwa Mainda alikwenda kuipumzisha akili kwa msanii huyo anayemuita wifi kutokana na ukaribu wake na aliyekuwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Ilisemekana kuwa Mainda alichukua mapumziko hayo kufuatia tafrani iliyoibuka hivi karibuni kati ya wasanii Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans kisa kikielezwa kuwa ni penzi la Ray.
Sosi huyo alidai kuwa, akiwa nyumbani hapo, Mainda alikuwa akichaji simu yake ambayo pia huitumia kutunzia siri zake kati yake na mpenzi wake zikiwemo meseji alizokuwa akitumiana na Chuchu.
Simu hiyo ikaibwa katika mazingira ya kutatanisha, jambo ambalo limesababisha achanganyikiwe.
“Siku hiyo Mainda alichanganyikiwa vibaya kwani hakutarajia kama simu hiyo ingeibwa kwani alikuwa anaitegemea sana,” alisema sosi huyo.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa mbali na simu ya Mainda ‘kuyeya’ pia kulikuwa na vitu vingine vilivyoibwa nyumbani hapo.
Inasemekana kuwa, baada ya Mainda kuchanganyikiwa alimua kuondoka nyumbani kwa Davina na kukimbilia nje ya Jiji la Dar kwa rafiki yake ambaye jina halikupatikana.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo tulimwendea hewani Davina ambaye alikiri kutokea kwa wizi nyumbani kwake lakini akasema asingependa habari hiyo iandikwe kwani kitendo kilichotokea hakukifurahia kwa kuwa kimemtokea rafiki yake huyo.
Alisema: “Naomba sana msiiandike hiyo habari, kwanza nashangaa kusikia habari zimewafikia, kweli duniani kuna wambeya, unadhani Mainda atanichukuliaje mimi? Naomba sana msinichonganishe na wifi yangu, kwanza hakuibiwa peke yake, kwa nini hilo la kwake ndiyo mnalishikilia?”
Kwa upande wake Mainda alipopigiwa simu aliipokea na alipoambiwa anazungumza na mwandishi wetu alijibu kwa harakaharaka kuwa yeye ni mdogo wake Mainda amempokelea simu, hivyo apigiwe baadaye.
Hata hivyo, baadaye alipopigiwa hakupokea. Waandishi wetu walijaribu kwenda nyumbani kwake, Kijitonyama, Ally-Maua, Dar lakini hawakumkuta.

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa