Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » VIDEO YA HOTUBA YA RAISI UHURU KENYATA BAADA YA WESTGATE KUOKOLEWA NA MAGAIDI KUUWAWA

VIDEO YA HOTUBA YA RAISI UHURU KENYATA BAADA YA WESTGATE KUOKOLEWA NA MAGAIDI KUUWAWA

Rais Uhuru Kenyata ametangaza siku tatu za maaombolezo kufuatia tukio la Ugaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Jumla ya watu 72 wameuawa katika tukio hilo huku wanajeshi sita wa Kenya wakiwa wamepoteza maisha wakati walipokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya watu anaoshikiliwa mateka na magaidi wa al Shabab katika jumba lenye maduka la Wastgate jijini Nairobi.

Askari wengine 8 wanaripotiwa kuwa mahututi baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo yanayoendelea hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) Jenerali Julius Karangi.

Duru za Kenya zinaripoti kuwa hadi sasa watu 72 wakiwemo raia sita wa nchi za nje wamethibitishwa kuwa wameuawa pamoja na magaidi kadhaa wamekamatwa na wanahojiwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusiana na tukio hilo katika jengo la maduka la Westgate nchini Kenya.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohammed amesema kuwa Wamarekani wawili au watatu na Mwingereza mmoja wamehusika katika shambulizi lililofanywa na magaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi. 

Balozi Amina Mohammed amesema washambuliaji hao walikuwa wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa ajili ya kuua watu mwishoni mwa wiki mjini Nairobi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya amesisitiza kuwa shambulizi la sasa mjini Nairobi limefanyika kitaalamu.

cheki video ya hotuba yake hapo chini...
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa