Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » SHILOLE ACHEZEA KICHAPO NA KUHAMA MTAA KWA SABABU YA MADENI

SHILOLE ACHEZEA KICHAPO NA KUHAMA MTAA KWA SABABU YA MADENI

Msanii nyota kwenye kiwanda cha filamu za kibongo nchini Zuwena Mohamed “ Shilole”
 mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina 
dada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.

Habari za uhakika zilizothibitishwa na mmoja wa wakina dada hao waliokuwa wanamdai 
 zilisema kuwa wanawake hao waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya
 kupata taarifa kuwa siku hiyo alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao “ Ishu ilikuwa
 hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga sana 
na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na deni letu ndio
 maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba hifadhi ya jina lake.
 
Dada huyo aliendelea kufunguka mengi kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara
 zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa
 na tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa
 akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa 
staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wane na kushushia kipigo” 
Alisema dada huyo
Baada ya taarifa hizo Xdeejayz ilimtafuta Shilole kupita simu yake ya mkononi pamoja na
 kupita kwenye makoloni yake lakini hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali 
walikili kutokea kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa mwanamuziki huyo.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa