Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » » MUIGIZAJI WA PRISON BREAK "MICHAEL SCOFIELD" ATHIBITISHA KUWA SHOGA

MUIGIZAJI WA PRISON BREAK "MICHAEL SCOFIELD" ATHIBITISHA KUWA SHOGA

                    Wentworth Miller maarufu kama Michael Scofield.
STAA wa Filamu ya Prison Break, Wentworth Miller maarufu kama Michael Scofield, amethibitisha kuwa yeye ni shoga.
Wentworth Miller amethibitisha hilo wakati akijibu barua ya mwaliko kutoka nchini Urusi alipoalikwa kwenye tamasha la filamu. 
Akimwandikia barua Maria Averbakh, ambaye ni Mkurugenzi wa St. Petersburg International Film Festival, Scofield alikuwa na haya ya kusema: "Asante kwa mwaliko wenu wa upendo.
"Kwa mtu ambaye nimewahi kutembelea Urusi katika siku za nyuma na kufurahia asili ya nchi hiyo, ningeweza kukubali mwaliko huu.
Lakini kwa kuwa nashiriki katika mahusiano ya jinsia moja (Ushoga), lazima nionyeshe kutoridhika na hali hii.
Nasikitishwa sana na jinsi watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaume kwa wanawake wanavyonyanyaswa na serikali ya Urusi.
"Hali hii haikubaliki, na mimi siwezi kushiriki katika tamasha la nchi ambapo watu kama mimi wananyimwa haki yao ya msingi ya kuishi na upendo waziwazi."
"Kama hali hii ikiboreshwa, nitakuwa tayari kubadili maamuzi yangu ".
Alieleza katika barua hiyo iliyowekwa katika tovuti ya GLAAD.
 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa