Mwanamke Mtanzania aliyekamatwa na dawa za kulevya Dubai baada ya kutiwa nguvuni.
*Yana thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3
*Yana thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3
*Adai mzigo huo ni wa rafiki wa mumewe aliyempatia amletee Tanzania
*Alikuwa anatoka nchini Brazil kwa mapumziko ya miezi mitatuMwanamke mmoja ambaye ametambulika kuwa ni Mtanzania amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege Dubai akiwa na kilo tatu za dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3. Mwanamke huyo aliyekuwa anatoka nchini Brazil kwa mapumziko kuja Tanzania baada ya kuhojiwa na maofisa wa polisi alidai kuwa rafiki wa mumewe ndiye aliyempa mzigo huo na kumuomba amletee Tanzania.
Alieleza kuwa mumewe ndiye aliyemponza baada ya kumuandalia safari ya Brazil kwa mapumziko ya miezi mitatu ndipo rafiki wa mumewe akamuomba amletee mizigo yake hiyo ambayo imemtia hatiani.