Pata Habari Motomoto kwa kuandika E-mail yako hapo chini.


Home » , » MGANDA AMUUA MKEWE KISA WIVU WA MAPENZI

MGANDA AMUUA MKEWE KISA WIVU WA MAPENZI

Jumuiya ya Waganda nchini Uingereza imekumbwa na simanzi baada ya mwenzao, anayeitwa David Kikaawa kumuua mkewe, mwenye asili ya Rwanda, anayeitwa Linah Keza.

Inasemekana David amemuua Linah mida ya alfajiri baada ya kumshuku kwamba alikua anamsaliti na kutoka na mwanaume mwingine kinyemela.

David alitoweka na kujificha baada ya kufanya kitendo hicho, na baadaye mwili wake ulikutwa katika Club 791, inayomilikiwa na kaka yake.

Ingawa polisi hawajatoa rasmi chanzo cha kifo chake, inaaaminika kuwa David amejitoa uhai mwenyewe.

Wawili hao walikua wakiishi kaskazini ya London, na walikua na mtoto mmoja (pichani katikati.) Taarifa zinasema kuwa David alishamtishia kumuua Linah mara kadhaa kama hataacha kumsaliti.

kutoka: investigator.co.ug

 

Copyright © 2009. MCHAMBUZI - Haki zote zimehifadhiwa